burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Okt 2016

OFA OFA OFA YA UKWELI AISEEE!!!! PENDEZESHA MGUU WAKO SASA


 Ebhana eeehhh!!! hili ni bonge la ofaa hebu tufanye kweli aisee wasiliana na uongozi wa blog hii upate maelekezo zaidi 0684016994 mzigo wote huu upo kwa ajili yako changamkia ofaa hii ni yako sasa































NARUDIA TENA
mzigo huu wote upo kwa ajili yako

Jokate azitetea ‘blunder’ za shindano la Miss Tanzania

Kwa miaka mingi mfululizo, haijawa rahisi kwa shindano la Miss Tanzania kumalizika bila malalamiko, lawama au kashfa. Awamu hii pia, yamekuwepo malalamiko kadhaa kuhusiana na maandalizi yake na jinsi shindano lilivyofanyika huku kukiwepo kasoro kadhaa.
14582260_1609371272700665_1583891794536431616_n
Lakini mrembo aliyewahi kushiriki shindano hilo miaka ya nyuma, Jokate Mwegelo, ameyatetea mashindano hayo akisema kuwa waandaji wamefanya kazi nzuri na wanastahili pongezi. Haya ni maelezo yake aliyoandika kupitia Twitter.
Fainali za mashindano ya Miss Tanzania zitafanyika Mwanza kwa miaka mitatu zaidi. Brilliant idea. I support this move. Open up mikoa zaidi. Ukiacha mapungufu fainali za Miss Tz ni shindano pekee la urembo ambalo huwezi kusikia mshindi amedhulumiwa zawadi yake au show ikapwaya.
Show ya Mwanza ilifanyika nje viingilio 100k,50k,20k na ilijaa watu licha ya mapungufu ya production. Nilikuwepo so najua ninachoongea.
Wadada wawili walipewa jukumu la kusimamia fainali hizi. Hao wadada wanakaa mkoani Mwanza. Nawapongeza kwa kufanikisha licha ya changamoto.
Kamati just needs to perfect the craft of moulding contestants to be competitive and of coarse giving us the ideal winner who will thrive. Ni rahisi sana kuchambua na kukosoa mashindano haya humu ila ukilinganisha na mashindano mengine ya urembo nchini angalau wanafanya vizuri.
Wanafanya vizuri kufikia warembo wengi kupitia mikoa mbalimbali na sio DSM tu au mikoa ya karibu. Vipaji vinatoka sehemu mbalimbali.
We need a sole company to deal na production. Creative themes and execution. Sio tu kwenye show za urembo na kwenye matamasha mengine.

Amini akisema mimi nimepotea kwenye muziki yeye mwenyewe yupo wapi – Linah

 Image result for amini na linah
Baada ya Amini kudai msanii mwenzake Linah Sanga amebadilika na kupoteza ule uimbaji wake wakuvutia, Linah amefunguka na kuizungumzia kauli hiyo.
 Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Ole Themba’ amesema kwa sasa yeye yupo juu zaidi ya Amini.
“Unajua soko letu lilivyo linabadilika badilika na hii ni biashara kusema nifuate ‘Ulinah’ sana naweza nikapotea kwa sababu watu walianza kuongea toka kwenye ‘Ole Themba’ lakini ‘Ole Themba’ ni wimbo ambao uliniweka sehemu nzuri sana,” alisema Linah. “Hii hali ya kusema nataka kubaki pale pale inatuangusha sana sisi wasanii ambao tumekuwa pamoja. Yaani tumejiwekea sisi ni wahivi hivi, hapana tunatakiwa tujichanganye ili tubadilike. Kwa sababu mbona yeye bado yupo kule kule lakini yupo wapi?. Usiseme mimi nimepotea yeye mwenyewe yupo wapi? na tukisema kwenye kupotea yeye na mimi nani amepotea?,”
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ amewataka wasanii wenzake kubadilika ili kukabiliana ushindani iliyopo kwenye game.

TID na Bill Nas waingia studio kuandaa wimbo

Msanii mkongwe wa muziki TID pamoja na rapa Bill Nas wameingia studio kuandaa project mpya ambayo bado hawajaweka wazi ni project ya namna gani.
bil-nas
Miezi kadhaa iliyopita, TID alilalamika kuwa Bill ni mtu mwenye tamaa na asiye na shukrani baada ya kuondoka Radar Entertainment licha ya kumlea na kumfikisha pahali.
Kwa sasa wawili hao wapo pamoja na wanaonyesha ushirikiano katika mambo yao ya muziki.
Alhamisi hii Bill Nas alipost picha instagram akiwa na TID na kuandika:

#inthekitchen with @tidmusic !! #NENGA #itsbeenawhile Yo! 2ko Around Mazeee
Bill Nas aliwahi kumshirikisha TID kwenye wimbo ‘Ligi Ndogo’ ambao ulifanya vizuri.

Kuachana na Hasheem Thabeet huenda kilikuwa kitu kibaya zaidi kuwahi kutokea kwa Jokate

Hasheem Thabeet kwa mujibu wa Jokate Mwegelo, alikuwa ni ‘first love’ na huenda kuachana naye kilikuwa ni kitu kibaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake.
epdh_fa2
Mrembo huyo alikuwa akijibu swali la PapiChulo_Chuly kwenye Twitter aliyeuliza, “Ni tukio gani baya huwezi sahau maishani?”
“Kumwacha mtu ambaye nilikuwa nishapanga vitu vingi sana nae kichwani. Very very disappointing but it’s life,” alijibu Jokate.
October 2013, kwenye jarida la Vibetz, alifunguka kuwa japo uhusiano wake na Hasheem ulidumu kwa miaka mitatu, walifanikiwa kuufanya usijulikane sana kwa wengi na walikuwa wakipendana sana.
“With Hasheem, I think it was more than love. He was my first real love,” aliliambia jarida hilo.
“Siku zote nilidhani he was my soulmate. Kiukweli nilimpenda sana. He is like the only guy I would drop anything at anytime for. Nilikuwa tayari kufanya lolote kwaajili yake, that’s how deep I loved that guy,” aliongeza.
“Nilimpenda kiukweli Hasheem, and yes kama mwanamke mwenye kutaka kufanikiwa I’m drawn to ambitious/successful men, you know the go getters but my family haikunilea katika maadili ya kujenga mahusiano yoyote katika mhimili wa fedha,” Jokate alieleza kujibu swali kama aliamua kuwa na Hasheem kwasababu ya fedha zake. “I had never wanted to use Hasheem, all I wanted was to love him.”
Jokate alidai kuishi mbali na Hasheem ni moja ya sababu iliyochangia kuvunjika kwa uhusiano wao.
“Yes kuishi mbalimbali pia inaweza kuwa sababu japo ndogo iliyochangia kuvunjika mahusiano yetu cause sometimes I would hear a lot of stuff and that would upset me. Nilikuwa naogopa sana kumpoteza, I ended up doing vitu vya kijinga kama dating Diamond. I had issues with Hasheem na Diamond came in picture. It was a very frustrating time for me. I was super confused. I cried for a whole year. Like every night I would just cry like crazy.”
Kwa sasa Jokate ana uhusiano na Alikiba.

Nay wa Mitego adai Wema Sepetu ndiye aliyemfilisi Idris Sultan

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego ameanza kuitupia madogo kambi ya malkia wa filamu Wema Sepetu kwa kudai mwigizaji huyo ambaye zamani alikuwa mpenzi wa Idris Sultan ndiye aliyemfilisi mshindi huyo wa BBA 2014.
Wema na Idris
Wema na Idris kipindi cha nyuma
Rapa huyo ambaye yupo kimya kwa sasa, alipost video katika mtandao wake wa instagram akieleza ni kwanini mshindi huyo wa BBA 2014 alifilika.
“Huwa najiuliza kitu kimoja ni mwanamke gani amemaliza mahela ya Idris?,” aliuliza Nay kupitia video hiyo. “Ni yule Msouth au madam (Wema). Mimi nadhani atakuwa madam maana madamu ni mtu wakukwarua mahela mengi, tena kabla hajatua Tanzania walimwambi, huku nyumbani kuna wanawake wacheza sinema maharamia wakikukamata na hizo hela utajikuta huna hata mia,”
Kambi ya malkia huyo wa filamu haijajibu chochote juu ya tuhuma hizo.


Wema Sepetu amuandikia ujumbe mzito Aunty Ezekiel kwenye birthday yake

Mastaa wawili wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Aunty Ezekiel, wameonekana kutokuwa na tatizo baada ya Wema kuweka mfululizo wa picha akiwa na shoga yake huyo.
14712253_1761811674037709_6603918272398098432_n
Picha na ujumbe wa Wema kwa Aunty unafungua ukurasa mpya wa urafiki wao ulioonekana kuvunjika miezi kadhaa iliyopita. Baada ya kuweka picha takriban 30 kwenye Instagram za kumpongeza kwa kuzaliwa, Wema aliandika ujumbe mrefu:


Okay…. i think imetosha na mapicha picha na hapo bado ninazo nyingine kama Mia… Tusisahau kwenye simu ya Tiake pia zipo… Maana tungeamua kuweka zote tungekesha…. We come a long way my love… Na kila siku tumekuwa tukikorofishwa na maneno ya huku na kule… Mi na wewe hakuna wa kutuingilia, Nadhani ndo tunachosemaga kila siku… I miss you, And I know u miss me too… Nakupenda everyday… Maneno Kitu simple, kajisemea Chafu pozi…😂😂 But wat matters is the heart… Na ndani ya moyo wangu jua kwamba nakupenda sana…. No matter wat… You know Better… On this special day nataka nikwambie, maybe Sometimes watu wanatuweza kweli kweli na inaweza tokea tuka kechi wote na tununiane na tusisemeshane, BUT You will forever have a special place in my Heart Tiake…. Navyokupenda ni vile vile kama nilivyokuwa nakupenda juzi na jana… Nothing has changed…. Happy Birthday my love… My Best friend…. Usikechi basi ukaanza kulia maana nakujua….… Love you alot… And this comes from ndani kabisa ya moyo wangu”…. @auntyezekiel ….❤️
wema
wema2


Huu unaweza kuwa ujio mzito na mpya wa Ray C kimuziki

Rehema Chalamila, how I wish arudi tena kwenye chati kama zamani. Ray C – kama unavyomjua zaidi, amepitia mapito mengi, na tena yaliyojaa njia yenye mbigili ibakishayo maumivu mguuni.
Miaka minne iliyopita, kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu alimkatia tamaa kuwa ndio basi tena ameshatumbukia kwenye shimo waliloshindwa kutoka vijana wengi. Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuongezea jina la uteja lililolifunika jina lake la utani ‘kiuno bila mfupa.’ Rehema, msichana mrembo aliyekuwa ndoto ya wanaume wengi, akapoteza thamani yake.
Jina lake likapotea kwenye ramani ya muziki na akawa mtu wa kuonewa huruma. Na kwa jinsi madawa ya kulevya yalivyo, humnyong’onyeza mtumiaji, humpunguzia utimamu wake kiakili, humpa utegemezi unaotesa yasipotumiwa na ikawa wakati mwingi Rehema akawa wa kukutwa amezima! Maskini wa Mungu Ray C akaingia kwenye dimbwi la maji ya moto ya uteja, nani wa kumuokoa?
Kwa alama aliyoiweka kwenye muziki wa Tanzania kwa nyimbo kibao zilizofanya vizuri, Ray C akapata msaada kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa zaidi nchini, Rais Jakaya Kikwete. Alijitolea kumpeleka rehab, kumsadia kwa hali na mali hadi hali yake ikarudi kwenye mstari – walau kwa muda huo. Aliingia kwenye mpango wa kutumia methadone aliodumu nao kwa takriban miaka mitatu.
Katika kipindi hicho, Ray C akageuka kuwa kinara wa vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya. Alianzisha pia taasisi yake, The Ray C Foundation kwaajili ya kampeni za kukemea ubwiaji unga. Katika kipindi hicho, Rehema, alijaribu tena kurejea kwenye muziki kwa kuachia wimbo mmoja ‘Mshum Mshum’, ambao hata hivyo haukufanikiwa kumrudisha pale alipokuwa ameishia.
Haikuwa rahisi kuishinda vita hiyo na mwaka huu alionekana kuweka silaha chini kwa kudaiwa kurejea tena kwenye matumizi ya madawa hayo. Video iliyosambaa mtandaoni akionekana akiwa kwenye mvurugano wa akili, akilia na kutaka kujichoma kisu, ilirejesha tena hofu kwa wapenzi wa muziki kuwa amerudi kwenye jela ya uteja.
RAY C ANARUDI
Peleka mbele hadi wiki moja iliyopita, Ray C anaonekana kupata chaji ya muziki inayompeleka hadi kwenye studio za kisasa za Wanene Entertainment. Kwanza nimefurahi kuona amebadilika mno kutoka yule msichana aliyenenepa hadi kuupoteza utambulisho wake. Amerudisha umbo lake la zamani linalompa matumaini ya kulikomboa jina la jukwaani – kiuno bila mfupa.
14717437_193840194391121_4773183368646885376_n
Uhakika nimeupata kwenye video alizoziweka Instagram zikimuonesha akiwa kwenye mazoezi makali ya kucheza huku kiuno chake kikifuata vyema maagizo kinayopewa. Huu unaweza kuwa urejeo wenye nguvu zaidi wa muimbaji huyu na namuomba Mungu amsaidie kukaa tena kwenye nafasi yake.
14676582_1467445509939009_6886310319115730944_n
Kutoka Kushoto: Anna Peter wa East Africa Radio, Ray C na Mamy Baby wa Clouds FM
Muziki wa Tanzania unamhitaji Ray C hasa kwakuwa kuna upungufu wa wasanii wakubwa wa kike. Inanipa moyo kuona mahaba yake ya muziki yamerudi kwa kasi ya ajabu. Napata amani nikimuona anavyofurahia mchakato wa kutengeneza nyimbo mpya. Nafarijika kuona kuwa amezungukwa na watu wanaotaka arudi kwenye chati.
Atakachohitaji baada ya hapo ni kuungwa mkono na vituo vyote vya redio nchini na pia mashabiki wakitimiza wajibu wao. Yapaswa kukumbuka kuwa muziki pekee ndio unaweza kuwa mkombozi kwake na unaoweza kumpa nafasi ya pili – nafasi ya kung’ara tena.
Naamini anarekodi nyimbo nyingi na katika hizo lazima kutakuwa na nyimbo kubwa. Pamoja na matatizo yote aliyoyapita, sijawahi kuwa na shaka na kipaji chake. Nasubiri kwa hamu kusikia kile alichotuandalia.

22 Okt 2016

Msanii Chidy Stress afanyiwa mapokezi mazito na Mheshimiwa.........


Msanii wa kizazi kipya hivi karibuni alifanyiwa mapokezi mazito na Mbunge wa wilaya ya kilindi Mheshimiwa Omar Kigua hata hivo mheshimiwa huyo alijawa na furaha kwa kumuona huyu msanii Chidy Stress
Chidy Stress aliyasema hayo wakati akiongea na G.lovetz kwamba mengi wameyazungumza na mheshimiwa huyo ikiwemo na kusukuma gurudumu la maendeleo pia wote waliafikiana kufanya kazi kwa kujituma alisema msanii huyo
Pia hakutaka kuweka wazi kuhusu kazi mpya inayokuja ila alisema kazi mpya inakuja soon na watu wangu wategemee kitu kizuri kutoka kwangu na location tayari tumeshaingia na ni kazi nzuri sana ambayo kila mtu akiiona lazima ataipenda kwa sasa namalizia michakato yangu ili nikiachia ngoma iniweke mahali pazuri,amaliza Stress

MTVMAMA2016: Tanzania yatoka kapa, hii ni orodha nzima ya washindi

Tanzania imetoka kapa kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 zilizofanyika usiku wa Jumamosi hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, Raymond, Navy Kenzo na Yamoto Band walikuwa wametajwa kuwania tuzo hizo.
cvz5ptjxgaakzly
Wizkid alikuwa man of the night
Ulikuwa ni mwaka wa Wizkid aliyeibuka na tuzo nyingi zaidi, ikiwemo ya msanii bora wa mwaka. Diamond na Alikiba walikuwa miongoni ma wasanii waliotumbuiza.
“Shukran sana sana kwa Kura na support Kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pia S/O kwa my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kuingia tunwengi kwenye MtvAwards ni Ushindi tosha kwa Tanzania…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award… my hommie @jahprayzah and @wizkidayo ya’ll deserve the Trophies,” ameongeza.
Alikiba amepost picha ya Sauti Sol na kuandika: Congratulations to my brothers @sautisol for The MTV Best Group Winner. You have had a great year and you deserve it.”
Naye Vanessa Mdee amepost picha ya Yemi Alade aliyekuwa akishindana naye kwenye kipengele cha msanii bora wa kike na kuandika: Congratulations to my lady love @yemialade ðŸ’œ na bado tunaenda #Juu and ALL the winners tonight. Thankyou @mtvbaseafrica for the recognition and your continued efforts to elevate Afrikan Music.Now lets get back to work kids.”
Kwa upande wao, Navy Kenzo wamewapongeza Sauti Sol kwa kuandika: With a Great pleasure we Thank God and all Fans, family, friends and all of our teams,Thank you Everyone for voting and it was a great exposure motivation and challenge towards major Goal…! We also Give thanks to @mtvbaseafrica @mtvbaseafrica For the Nomination and recognition we are very happy with a Great Gratitude. Until next Year. EAST AFRICA #KENYA AND AFRICA AT LARGE LET’S STAND TOGETHER AND SAY CONGRATULATIONS @sautisol @sautisol
@sautisol @sautisol #BESTGROUP #AFRICA.”
Hii ni orodha kamili ya washindi.
cvzwptgwyaaxlqr
1
cvzpyyfwcaavr-1
cvzsgfwwyaa1sdf
cvzbjdswaaanki6
cvzehd_wyaadw5a
cvzfoxdwyaaep98
cvzh0vhxgaaaaft
cvzirevwyaane6y
cvzkawnwgaafbgm
cvzlvjjwgaej5hp
cvzmqxwwgaa8djt
cvzo2txwiaaxiwb
cvzufrawgaabrkh
cvzwwu0wyaaf9c1
cvzxrurxeael16c
cvzyqtmxgaegra9