burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Jan 2017

Tegemeeni kitu kizuri kutoka kwangu - Gbros De Voice

Picha ya Gbros De Voice
Msanii alietamba na kibao cha bye bye hivi sasa kafunguka kwamba kuwaambia mashabiki wake kuwa tegemeeni kitu kizuri kutoka kwake kwa kuwa yupo katika kuitimiza ahadi yake ya kufanya kazi nzuri ya kupendwa na kila rika

Msanii akiongea na G.LOVETZ amesema kuwa kuhusu kichupa kitakuwa kikari sana pia atabirii mafanikio baada ya kuachiwa hivo video yake mpya iangawa hakutaka kuweka wazi hio nyimbo itatoka lini ila kasema ni kazi nzuri ya kupendwa na kila mtu na rika pia
kumsikiliza na kudownload pia mahojiano ya  Gbros De Voice akiongea na G.LOVETZ
gusa HAPA.

VIDEO | Dayna Nyange Ft. Billnass - Komela | Watch


VIDEO | Meda Feat Timbulo - Sidhani | Watch



VIDEO | Linah - Kosa Sina | Watch

Tunda Man aweka wazi ratiba ya muziki wake ndani ya mwaka 2017


Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amedai tayari ameshafanya maandalizi ya kutosha kwajili ya mashabiki wa muziki wake ndani ya mwaka 2017.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Tunda Man amedai ndani ya mwaka huu ataachia nyimbo 5 pamoja na video zake.

“Namshukuru Mungu mwaka umenza vizuri na ratiba yangu ya mwaka au kalenda yangu imepangika vizuri. Nitaachia nyimbo tano pamoja na video zake, sitaki mwaka huu kutoa ngoma chache kwa sababu muziki wa sasa umebadilika mashabiki wanataka kazi nyingi zaidi,” alisema Tunda Man.

Aliongeza, “Kwa hiyo kazi zipo nyingi, kuna ngoma nimefanya na Yamoto Band, kuna wimbo nimefanya na Jaguar wa Kenya, yaani kuna kazi nyingi Mungu akitujalia ngoma tano zitatoka mwaka huu,”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Debe Tupu’ ambao aliuachia January mwaka huu.

Walter Chilambo ataja mabadiliko aliyoyaona tangu alipoingia kwenye muziki wa injili


Walter Chilambo amefunguka mabadiliko aliyonayo kwa sasa tangu alipotangaza kuingia katika tasnia ya muziki wa injili.

Kupitia kipindi cha V-Mix cha Channel 10 cha Mwaka The Boy, Walter amesema, “Nimebadilika vingi japo kama mwanadamu kimuonekano bado nipo vile vile lakini ndani yangu nimebadilika vingi sana. Nimekuwa na amani zaidi na nimekuwa najua nipo huru zaidi tofauti na nilivyokuwa mwanzo.”

“Sijawahi kuona Bongo Fleva ngumu na wala sijawahi kuona ugumu wowote kwangu na kama ingekuwa ngumu nisingekuwa na mafanikio ambayo tayari nilikuwa nimeyapata,” ameongeza.

Mpaka sasa Walter ameshaachia nyimbo mbili za muziki wa injili ikiwemo ‘Asante’ na ‘Merry Christmas’ tangu alipotangaza rasmi mwaka mwishoni kuingia kwenye muziki huo.

Video ya Mazoea imekula pesa nyingi sana – Billnass

Msanii wa muziki wa hip hop Billnass amedai uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Mazoea’ ndio kitu ambacho kimeufanya wimbo huo kupokelewa kwa kasi zaidi.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa video ya wimbo huo ni moja kati ya video zake alizowekeza pesa nyingi zaidi.

“Mamshukuru mungu ‘Mazoea’ inaenda vizuri na tayari kuna simu za show ambazo nimeanza kupigiwa ili kurudisha kile tulichokiwekeza kwa sababu Mazoea ni moja kati ya video zangu ambayo imekula pesa nyingi sana,” alisema Billnass.

Bill amewashukuru mastaa mbalimbali pamoja na mashabiki wake ambao wameonyesha kuusupport wimbo huo aliomshirikisha rapper mkongwe, Mwana FA.

Belle 9 aelezea umaskini ulivyomfanya mpenzi wake aporwe na mtu aliyekuwa akimfahamu


Wimbo, Sumu ya Penzi uliomtoa Belle 9, ulikuwa ni true story.
Aliuandika baada ya mpenzi wake kummwaga na kuanzisha uhusiano na mtu aliyekuwa akimfahamu.
“Ilinichukua muda sana kuzoea ile hali,” Belle 9 alisema kwenye mahojiano na Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

“Kwasababu kitu ambacho kilichokuwa kinaniuma ilikuwa katoka kwangu halafu kaenda kwa mtu ambaye namfahamu kabisa, na yule mtu maisha ya kwao na maisha ya nyumbani ni tofauti. Yule alikuwa hata siku tukienda kwenye mpira kila siku anabadilisha six, anabadilisha jezi, sisi ndio tulikuwa wale watu ambao tunarudia hizo hizo kila siku,” aliongeza.

“So akawa anapita naye maskani ambapo sisi tunakaa sababu yeye alikuwa anakaa mtaa wa juu, sasa kuna barabara pale nyumbani ilikuwa inapita kwenda chini kuna ukumbi fulani ambao ndio tulikuwa tunaimbaimba, kuna kama karestaurant fulani, so wakawa wanapita maskani pale wanaenda kule, wameshikana mkono, wameshikana viuno, halafu mchizi anasimama anasalimia sasa, ni kitu ambacho kiliniuma sana.”

Belle amedai kuwa hadi sasa msichana huyo anajutia kitendo alichomfanyia.

Sinaga Swagga ya Young Killer ipo kwenye playlist ya Fid Q


Wiki iliyopita mcee mkongwe nchini, Fid Q alizua maswali mengi baada ya kuonesha kuupa heko wimbo mpya wa Joh Makini,Waya, mkali ambaye tulikuwa tukiamini kuwa wana tofauti.
Sasa mbali na ngoma hiyo ya Joh Makini,Fid Q ameitaja ngoma ya Sinaga Swagga ya Young Killer kuwa ni ngoma ambayo ameisikiliza sana pia.

“Nimeiskia Sina Swagga ya Young Killer,nimeipenda, nimependa jinsi ambavyo amejaribu kuwa yeye,” Fid kwenye mahojiano nami kupiti Kings FM.

Kwa muda mfupi wimbo huo wa Young Killer ulisababisha headlines kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuwachana rappers wenzake wakiwemo Joh Makini, Young Dee na Dogo Janja.

Mrisho Mpoto awataka wasanii kuwa kitu kimoja ‘tusiwe wasanii wa bila hit song maisha hayaendi’


Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii kuondoa makundi yaliyopo kwenye muziki na kuanza kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa wengi.
Muimbaji huyo amedai kila msanii anafanya kazi kivyake hali ambayo inawanyima zaidi wasanii fursa za kibiashara.

“Kwa muda mrefu sasa wasanii wa Tanzania wamekua wakifanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi, lakini kila mtu anacheza karata yake kivyake kutokana na network na nguvu yake,” Mpoto alitoa taarifa hiyo Instagram. “Nadhani sasa wakati umefika kuondoa tofauti zetu, makundi, tukawa team moja tukae tuone tunawezaje kusaidiana kwenye nyanja za kibiashara,”

Aliongeza, “Kuwa kama wasanii wa Taifa la Tanzania wenye muelekeo mmoja bila kuingilia fani ya mtu wala maisha binafsi, Wazo langu tusitawanyike ikawa kila mtu anaenda kivyake, ukiotea hit basi ndiyo unapata hela, najaribu tu kuwaza kwa sauti kama wazo lina mashiko, #teamtanzania,”

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao wanapiga deal nyingi nje ya muziki ukiachia mbali deal za ubalozi za makumpuni mbalimbali alizopewa.

Kumbe Dogo Janja ndiye amemrudisha Madee kurap kwenye Hela!


Unashangaa kusikia kuwa Dogo Janja ndio amemrudisha Madee kwenye kuchana? Ni muda mrefu tumekuwa tukimsikia Madee akiwa anaimba kwenye nyimbo zake kabla ya kuachia ‘Hela’ hivi karibuni.
Akiongea katika kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM ya Dodoma na mtangazaji Silver Touchez, rapper huyo amedai kuwa alimshauri Madee arudi kwenye kurap kwa kuwa anamkubali zaidi akifanya hivyo kuliko anapoimba.

“Madee hapa katikati kawapeleka sana watu mchaka mchaka ukiangalia ‘Tema Mate’, ‘Migulu Pande’, ‘Pombe Yangu’ nikamwambia mzee rudi kidogo kwenye kurap. Mimi nampenda Mdee wa kurap sana kwa sababu anamaneno fulani ya mtaani. Kw hiyo mshua akapiga dude la ‘Hela’,” amesema Dogo Janja.

Janjaro ameongeza kwa kutaja kitu ambacho akipendi kwenye muziki, “Mimi sipendi kushindanisha nyimbo zangu mimi kama mimi. Mfano nyimbo yangu ikianza kutoka kwenye Top 10 nianze kuwa na stress kiasi kwamba nipiganie kuingiza mkwaju mwengine, kitu ambacho sikiwezi kabisa. Huwa napenda kuzipa nafasi nyimbo zangu, sipendi kuwa na muziki wa Big G yaani naachia leo baada ya miezi miwili au mitatu naachia tena, no. Napenda kuwa kwenye challenge fulani kafanya ngoma kali na mimi nafanyaje ili kuweza kufanya zaidi ya pale.

Aunt Ezekiel adai matendo machafu ya wasanii yamechangia kuporomoka kwa soko la filamu


Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja Aunt Ezekel amedai matendo machafu ya wasanii wa filamu ni moja kati ya vitu ambavyo zimechangia kushuka kwa soko la filamu nchini.

Muigizaji huyo ambaye kwa sasa yuko kwenye mahusiano ya kudumu na dansa wa WCB, Mose Iyobo amedai wasanii wengi wa filamu wameendekeza starehe kuliko kasi.

“Kipindi hiki filamu zimepoteza mvuto na watu wamekuwa wakizungumza mengi ila ninachoona mimi ni matendo yetu machafu yanachangia,” Aunt aliliambia gazeti la Mtanzania. “Mbona wasanii kama kina King Majuto bado wanafanya vizuri? Skendo zinayumbisha soko la filamu na siyo kitu kingine,”

Kati ya skendo ambazo zinatajwa zaidi kuwatikisa wasanii wa kike wa filamu ni kutoka na waumume wa watu, kuolewa na kuachika pamoja na kubadilisha mabwana mara kwa mara.

Baba na mama yangu ndio couple ninayoikubali zaidi – Belle 9

Ni couple gani ambayo unailewa zaidi hapa Bongo? Ni swali ambalo mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy alimuuliza Belle 9.
“Wananivutia kwasababu nyumbani maisha ni ya kawaida lakini still baba yuko na mama halafu mara zote ambazo nimekuwa nyumbani, sijawahi kuona mama yangu anagombana na baba. Mimi nimekaa sana nyumbani kwa muda mrefu, lakini mara ya kwanza naona kama wanashikanashikana hivi ilikuwa mimi ndio chanzo, yaani mama alikuwa ananitetea mimi kwasababu baba alikuwa ananinyoosha sana sasa mama alikuwa kama anaingia hivi, lakini haukuwa ugomvi,” ameongeza.
“Kiukwezi ni best couple kwangu mimi, najifunza mengi kupitia pale, inanipa nguvu nikirudi nyumbani baba yupo, mama yupo nikitoka hapo nami nakuwa nipo fast kila kitu.”

Kwa upande wa couple ambayo haielewi ni ile ya Kanye West na Kim Kardashian.

Video: Ice Boy Ft Nandy – Binadamu

Wastara ataja mambo 5 ambayo hatayasahau katika maisha yake

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma ametaja mambo matano ambayo hatakuja kuyasahau katika maisha yake.
Muigizaji huo amekiambia kipindi cha FNL cha EATV, jambo la kwanza ambalo hata kuja kulisahau maishani mwake kifo cha wazazi wake wote wawili na jambo la pili ni ajali ambayo ilimsababishia ulemavu mpaka sasa hivi.

Jambo la tatu ambalo Wastara ameongeza hatalisahau ni kifo cha mumewe Sajuki na jambo jingine ambalo linamuumiza na hatalisahau wakati alipotumia vyombo vya habari kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya mumewe Sajuki ambaye baadaye alifariki dunia.

Wastara ameweka wazi jambo la tano ambalo linamuumiza zaidi kichwa ni kitendo cha mashabiki wake kumchukulia tofauti na alivyo kiuhalisia.

Tunaweza kupata album ya Mwana FA iwapo mipango hii ikienda sawa


Nani asiyependa kumiliki album mpya ya mmoja wa waandishi wakali wa mashairi ya hip hop wa muda wote kutoka Tanzania – Hamis ‘Mwana FA’ Mwinjuma? Kama wewe ni mmoja wa mashabiki damu damu na Binamu, basi tuombe Mungu mipango iliyopo mezani mwake ifanikiwe ili tupatiwe fursa hiyo adimu kwenye muziki wa leo.
“Tuna muziki mwingi ndani, kama kutotolewa kwa album kutaendelea, inawezekana kuna nyimbo hazitokaa zisikike maisha yote,” FA ameiambia Bongo5.
FA amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakitafuta utaratibu ambao wanaweza kuanza kutoa album tena lakini kila anayehusika ikamlipa.
“Kwahiyo utaratibu kama tunataka kuufanya hivi,” anasema. “Kuna mwekezaji mmoja ametokea hivi anataka kama kuinvest kwenye haya masuala. Bado tunajadiliana naye, sisemi kwamba tumekubaliana tutatoa album, lakini tupo kwenye mazungumzo na yanakwenda vizuri. Pengine siku chache hizi kama atakuwa ameturudia, tutajua kama album inaweza kutoka mwaka huu. Album kwasababu ipo tayari ni vichache tu vimesalia, namna ya kuziunganisha nyimbo, sehemu ambapo zinakutana, theme ya album, covers na vitu vidogo vidogo,”ameongeza.

Hii ndio tarehe ambayo album ya Fid Q ‘Kitaaolojia’ itatoka


Ni mwaka wa tatu sasa tumekuwa tukisubiri album ya tatu ya Fid Q, Kitaaolojia.
Kwanini haitoki, ama nayo inataka kuwa kama Detox ya Dr Dre? Habari njema ni kuwa, album hiyo mwaka huu lazima iingie mtaani ili kusambaza hiyo elimu ya mtaa, iliyobeba jina lake.

“Kitaaolojia ni kweli ina miaka mitatu imekuwa kama Detox na nini, lakini unajua mimi ni perfectionist, natakaa itokee kweli konki,” Fareed ameiambia Bongo5.

“Na idea zimekuwa zikibadilika mara kwa mara, lakini so far sasa hivi nimeshaipatia direction, na kuna uhakika ninaweza nikawaguarantee kabisa kwamba August 13 ya mwaka huu panapo majaliwa Kitaalojia itakuwa mtaani,” amesisitiza.

Fid ameshatoa album mbili hadi sasa, Vina Mwanzo Kati na Mwisho na Propaganda.

Vanessa Mdee apata shavu nchini Nigeria


Mwaka 2017 bado unaendelea kuwa wa mafanikio kwa Vanessa Mdee. Muimbaji huyo amepata dili jingine nchini Nigeria.
Hitmaker huyo wa Cash Madame amefanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wachache ambao watasikika katika mixtape ya watayarishaji wa muziki wa Nigeria ambao wanafanya kazi zao nchini Uingereza, Legendury Beatz.

Mixtape hiyo imepewa jina la ‘Legendury Beatz’. Kupitia mtandao wao wa Instagram, wathibitisha hilo kwa kuandika, “Of course the sexy @vanessamdee all the way from Tanzania, came through saucin on the #Afropop101 😉certainly certified!!! 🙌🏽🙌🏽🙌🏽✅ #LegenduryBeatz.”

Wasanii wengine watakaosikika katika mixtape hiyo ni pamoja na Mr Eazi, Simi, Niniola, Timaya na Wizkid (wote kutoka Nigeria) na R2Bees (Ghana).

Napenda kufanya kazi nje ya matarajio ya wengi – Joh Makini

Joh Makini anataka kuweka kitu kimoja ‘very clear’ kuwa hupenda kufanya kazi nje ya matarajio ya wengi.
Kauli yake inakuwa jibu kwa baadhi ya mashabiki walio na mtazamo tofauti na kazi yake mpya, Waya.
“Siku zote kwenye sanaa, lazima uwe mtu tofauti na usiyetabirika kwamba unakuja vipi,” Joh alimuambia mtangazaji, Eddy Msafi kupitia kipindi cha Full Charge cha Pride FM ya Mtwara.
“Kwa maana hiyo nimeona Waya ni wimbo mzuri na mkali na unaweza kufanya vizuri sehemu yoyote duniani na utakuwa ni msimu mzuri ukitoka wakati watu wanaelekea Valentine’s,” ameongeza.

Joh hakusita pia kukumbusha kuwa Waya kwa sasa ndio video inayotrend katika nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa Youtube.

Miss Tanzania 2010, Genevieve aachia ngoma yake ‘Nana’ ni fireeee

Alikiba, yazingatie malalamiko ya mashabiki wako


Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.
Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda.

Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi kwenye soko la muziki barani Afrika.

Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.

Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February.

Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.

Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.

21 Jan 2017

Fid Q kaona kilichoandikwa na Paul Makonda, kamuandikia na yeye


Kwenye ile orodha ya mashabiki wa damu wa Mwanahiphop Fid Q inabidi umuongeze na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ambaye January 20 alitumia time yake kupost kipande cha video ya Fid Q na kuandika>>’Hakika umetubeba hakuna bingwa na mbabe ktk anga hizi kama wewe, huna mbwembwe na ujumbe unafika’ #Mzikimgum‘
Image result for poul makonda
Baada ya Fid Q kuiona hiyo post amemshukuru Paul Makonda kwa kuandika >>> ‘Shukrani sana Mheshimiwa mwenye DAR yake @paulmakonda – kiukweli tunajivunia kuwa na kiongozi kijana na mchapakazi kama wewe’

‘Kinachotukosha zaidi ni vile unavyoutumia muda wako wa mapumziko vyema kwa kufuatilia na kusapoti kazi za sanaa za vijana wa taifa letu kama mimi’ – Fid Q

 ‘Ubarikiwe zaidi bro.. 🙏🏿 Na kama utapata muda usisahau kuclick kwenye ile LINK iliyopo kwenye BIO yangu.. kuna NGUMU nyingine mpya inaitwa ‘ KEMOSABE ‘ nimeiweka jana.. yote na yote mkuu.. Asante sana kwa #loveyahelayote 🙏🏿 😇’.

Ay kaandika ‘Ndugu zangu Wasanii nimeona sio vibaya kuwaambia hili’



Ay ambaye ni staa wa smash hit ya ‘zigo’ na kwasasa akiwa ana brand new single na Nyasinski amechukua time yake na kuwaandikia Wasanii wenzake yafuatayo >>>> ‘Ndugu zangu Wasanii wa kibongo, Wadau na Mashabiki wa muziki nimeona sio vibaya kuwashirikisha na nyie jambo hili‘

‘Ili Producers wa Kibongo waweze kubadilisha Tunes kwa beats zao na waendelee kutisha KULIKO JANA nawaomba wasanii wenzangu muweke utaratibu wa kusafiri nao mnavyotoka nje ya Afrika Mashariki wakienda, wakiona, wakijifunza na kujiongeza LAZIMA TUTATISHA SANA‘ – AY

‘Nimeona sana Afrika Magharibi wana hesabu hizo ndio maana wana Tunes za kila aina,Tuna Producers wazuri sana ila wanahitaji kusafiri zaidi,Mfano mzuri ni @majani187 @nahreel@hermyb na @marcochali wamepata exposure ndio maana wana Tunes Unique‬ all the time #ZEE – @AyTanzania kwenye Instagram

Maneno ya Naibu Waziri wa Afya shabiki namba 1 wa Fid Q


Muziki wa Bongofleva unaendelea kufanya vizuri na sasa hivi imekua sio ajabu sana kuona viongozi mbalimbali wa Tanzania wakitoa saluti za kutosha kwa vijana wa Kitanzania waliojiajiri kwenye sanaa.

Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamis Kigwangalla hajaficha ushabiki wake kwa kusema yeye ni miongoni mwa wanaomfatilia kwa sana mwanahiphop Fid Q na mistari yake iliyo deep.

Naibu Waziri Kigwangala.

Kupitia Twitter page yake Kigwangalla ameonyesha kuielewa pia ngoma mpya ya Fid Q aliyoachia leo, akaandika >>>‘Huwa nasikiliza wasanii wachache sana wa Bongofleva, FidQ ni mmojawao sababu anajua kutunga mistari na ana attitude ya hip-hop!‘

Kwenye tweet nyingine akaandika sehemu ya mistari ya ngoma mpya ya Fareed >>’wengi wana-cheat na kuwaudhi wachache wanao-play fair!” @FidQ nimeiba mstari huo kwenye ukurasa wa Makonda kule IG, nimeielewa hii namba’ baada ya maneno hayo akaweka alama ya kunyoosha mikono juu.

‘Sijutii kile ambacho nimekifanya kwa sababu sijakosea’-Madee

kupita XXL ya clouds FM, Soudy Brown ametuletea U Heard inayomhusu Madee na mama Makavaka baada ya pande hizo mbili kuwepo kwenye mgogoro uliopelekea mpaka Madee kuchukua simu ya mama huyu,  Madee alipozungumza na Soudy, ameyasema haya…..

‘Mama alikuwa anamteta mwanae, sijaona kama ni kosa mama kumtetea mwanae kwa sababu ni utamaduni wa mama wa kiafrika, ila jana nimeshaongea naye nimemuomba msamaha sehemu ambayo nimemkosea japo mimi sijutii na kile ambacho nimekifanya kwa sababu sijakosea nilichokifanya ni kutaka haki yangu, haki yangu nimeipata’

Usichokijua kwenye remix ijayo ya Aje ya Alikiba

Aje ni wimbo wa Alikiba uliompa mafanikio makubwa mwaka jana ikiwemo tuzo kadhaa za video bora ya mwaka ikiwemo ile ya Soundcity MVP Awards.
Baada ya kuwepo version yenye verse toka kwa rapper Jude ‘M.I’ Abaga aka Mr Chairman wa Nigeria iliyovuja hata kabla ya official video, mashabiki walikuwa wamekaa tamaa kuwa hakutokuwepo na official remix yake.

Habari njema ni kuwa, Alikiba anaileta remix official ya Aje. Na tena itakuwa ni video.

“Ndio, remix inayokuja ndio ambayo yuko M.I na ina utofauti than the one that leaked,” meneja wa Alikiba, Seven ameiambia Bongo5. Seven amewataka mashabiki wawe tayari muda wote sababu remix hiyo itaachiwa kwa kushtukiza.

“He will just release it when it’s ready,” ameongeza. “Hatutoi official release date. It will drop unexpectedly.”

NEW VIDEO | Madee - Hela | Watch


VIDEO | Diamond Platnumz Live performance at AFCON 2017 GABON | Watch

Full Show Diamond Platnumz Live performance at AFCON 2017 GABON

NEW AUDIO I Young Romance - MOYO I DOWNLOAD

Picha ya Nasibu Mussa

VIDEO | Roma & Moni - Usimsahau Mchizi | Watch


VIDEO | Isha Mashauzi & Mashauzi Classic - Kismet | Watch


VIDEO | BillNass Ft. MwanaFA - Mazoea | Watch


2017: Rappers Bongo wanateka agenda za mazungumzo redioni, mtaani na mtandaoni

Wakati muziki wa kizazi kipya umeanza, ni rappers ndio walikuwa waasisi na waliojenga msingi mkuu wa Bongo Flava ya leo.
Wasanii wote wakubwa wa zamani walikuwa wachanaji. Hits zote za zamani zilifanywa na wasanii wa hip hop. Watu wa kwanza kulipwa fedha za show, walikuwa watemaji wa rhymes.

Waimbaji waliofanikiwa miaka hiyo wengi walikuwa wanawake, wakiwemo Lady Jaydee, Ray C, na Stara Thomas. Mambo yalikuja kubadilika tu miaka kama mitano iliyopita, na waimbaji wakaibuka kuwa wasanii wakubwa kiasi cha kuvuka zaidi border.

Upepo huo ndio uliosababisha kuwepo majina makubwa sasa ya wasanii kama Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, Ben Pol, Ommy Dimpoz, Rich Mavoko, Navy Kenzo na wengine. Pia kizazi cha miaka ya hivi karibuni kama vile Raymond, Harmonize, Barakah The Prince na wengine.

Ukafika muda, wasanii wa kuimba wakateka agenda katika mazungumzo ya kila siku ya muziki wa Bongo Flava. Hiyo ilisababishwa na uthubutu wao katika kuwekeza fedha nyingi kwenye kazi zao ikiwemo kufanya video kubwa. Hiyo ndio sababu wasanii wa kuimba wakawa kitovu cha mazungumzo kwenye vyombo vya habari, mtaani na kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu rappers wameonekana kutaka kurudisha ubabe wao. Ni wazi kuwa rap sasa imetawala zaidi agenda za muziki wa Tanzania. Hits nyingi sasa hivi ni za wasanii wanaorap. Ukianza na anthem ya Darassa, Muziki, ambayo imemweka kwenye daraja la aina yake kwenye rap ya Bongo, hits kama Dume Suruali ya FA, Roho ya Fid Q, Pesa ya Madafu, Perfect Combo ya Joh Makini, ziliufunga mwaka 2016 kwa kishindo.

Na ukiangalia hits nyingi kwenye rotation ya muziki sasa, ni za wasanii wanaorap. Ngoma kama Umeniweza ya The Amazing, Sijiwezi ya Nay wa Mitego, Hela ya Madee, Mazoea ya Bill Nas na Mwana FA, Sinaga Swagga ya Young Killer, Usimsahau Mchizi ya Roma na Moni na zingine zinafanya vizuri kuzidi ngoma kibao za wasanii wa kuimba.

Collabo za kimataifa kama ile ya AY na Nyashinski, More and More na zingine zinazosubiriwa kuja ikiwemo ya Young Killer na Khaligraph, zinarudisha heshima ya rap Tanzania. Na ukiangalia video za ngoma hizo, utagundua kuwa rappers hawataki tena ubahili kwenye kazi zao kama walivyokuwa mwanzo.

Mabishano na majigambo ya wasanii wa Bongo kwa sasa yametawaliwa zaidi na rappers na hata vituo vya redio vimeonesha kuicheza zaidi ngoma yao. Mistari tata kama ya Young Killer dhidi ya Joh Makini, Young Dee na Dogo Janja au ile ya Madee dhidi ya Nay wa Mitego, imezalisha mijadala mirefu na kuipa favor rap.

Nadhani hamasa kama hiyo ilikuwa ikihitajika zaidi kwa sasa kwenye muziki wa Bongo ili kuwapa chaji wasanii wa rap waliokuwa wamefunikiwa kimafanikio katika macho ya mashabiki wa muziki. 2017 ni mwaka tutakaoshuhudia mengi makubwa kwenye muziki huo.

Mtoto wa Ray, Jaden afuata nyayo za Tiffah na Nillan wa Diamond

Tiffah ni mtoto maarufu zaidi kwenye mtandao wa Instagram Afrika akiwa na followers zaidi ya milioni moja. Mdogo wake, Nillan naye anafuata nyayo zake akiwa na followers zaidi ya 99k sasa. Akaunti zao husimamiwa na mama yao, Zari na hutumia Kimombo.Na sasa mtoto mwingine wa mastaa wa Bongo, Jaden naye amejiunga kwenye kundi la watoto wa aina hiyo.
Jaden ni mtoto wa Ray Kigosi na Chuchu Hans aliyezaliwa wiki hii na tayari amefunguliwa akaunti kwenye mtandao huo. Yake inasimamiwa na mama yake na kama Tiffah na Nillan, amewafollow wazazi wake tu.
Katika kufurahia zawadi ya mtoto, Ray ameendelea kuweka wazi furaha yake kwa kuandika: Nikikuangalia Mwanangu Jaden Nakuwa Na Furaha Isiyo Kifani Na Kunipa Nguvu Ya Kupambana Na Maisha Ili Uishi Vizuri.. Mtoto ana Raha Yake Jamani asikwambie mtu Nyie Puyangeni Tu.

Fid Q asema yupo tayari kufanya kolabo na Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda aka Fid Q amedai yupo tayari kufanya kolabo na rapper Nay wa Mitego kwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa hip hip ambao wanafanya vizuri.
Alisema hayo baada ya hivi karibuni kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio, Nay wa Mitego amemtaja Fid Q kuwa miongoni mwa rappers anaowakubali zaidi Bongo na kusema kuwa hastahili kufananishwa naye sababu yeye ni rapper mwepesi.

Ijumaa hii akiwa katika kipindi cha Enewz cha EATV, Fid Q amedai yeye anaufuatilia muziki wa Nay wa Mitego huku akidai yupo tayari kufanya naye kolabo.

“Nimeipenda sana ngoma ya Nay wa Mitego ‘Sijiwezi’ hasa ile chorus, na niko tayari kufanya naye kolabo,” alisema rapper huyo.

Rapper huyo ambaye ameachia wimbo ‘Kemosabe’ hivi karibuni, amedai Nay wa Mitego siyo rapper mwepesi kama anavyojiona kwani ni mmoja kati ya marappers wenye uwezo mkubwa.

AIM ya Navy Kenzo yaingia online kwa kishindo

Baada ya kuachiwa kwa mfumo wa CD, album ya Navy Kenzo, Above In A Minute (AIM), imeingia online kwa kishindo.
Sasa watu wanaweza kustream album hiyo kupitia iTunes, Spotify, Tidal, Akazoo na Boom Player. Kupitia Boom Player unaweza kustream bure kabisa. Hii ni mara ya kwanza kwa album ya Tanzania kuingia mtandaoni kwa uzito huo.

Tangu itoke, AIM imepokea maoni chanya zaidi na kutajwa kuwa miongoni mwa album bora za Afrika kwa sasa. Kwenye album hiyo wasanii walioshirikishwa ni pamoja na Alikiba, Patoranking, R2Bees, Mr Eazi na Rosa Ree.

Mimi ni rapper mwepesi kufananishwa na Fid Q – Nay wa Mitego

Nay wa Mitego amesema yeye ni rapper mwepesi kufananishwa na Fid Q na in fact hukasirika kusikia Ngosha anafananishwa na rapper mwingine hapa Bongo.
Ni kwasababu Nay anaamini uwezo wa Fid kwenye hip hop ni wa sayari nyingine.

“Simfananishi na rapper yeyote Bongo, sitaki, huwa nakasirika nikisikia wanamshindanisha na fulani, sipendi, najua hana mwenzake sijui huko mbeleni, Fid Q,” Nay alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

“Simfananishagi na rapper yeyote wa Kibongo, nakasirikaga kusikia wanamfananisha na msanii mwepesi, rahisi kama mimi au kama nani hao, please. Sisi wengine tupo sababu ya biashara, tunafanya tuna mashabiki sawa lakini kuna watu ambao wanafanya muziki wao ambao waliamua kufanya ukawa huko na wana heshima zao. Msifanye hivyo, na tena nikisikia East Africa mnamfananisha Fid Q na msanii flani, kuna siku ntakuja kuandamana,” aliongeza.

Kwa upande wake Fid Q baada ya kusikia kauli ya Nay, aliandika kwenye Instagram, “wewe sio mwepesi kaka @naytrueboy – so yawezekana kabisa na wao wakawa na vigezo flani special vinavyowapelekea wadau kunilinganisha au hata kunipima nao.. yote na yote.. ubarikiwe sana na asante sana kwa #LoveYaHelaYote.”

Wasanii wengine aliowataja kuwakubali ni Sugu, Mr Blue, Mwana FA na yeye mwenyewe.

Black Rhyno kumshtaki Nay wa Mitego kisa beat? Sikia alichokisema

Kwenye playlist ya ngoma kali zilizotoka mwaka jana mwishoni, haziwezi kukosa sijiwezi ya Nay wa Mitego na Kama Movie ya Black Rhyno aliyompa shavu Jux.

Ngoma hizi zimezua utata kwani ni ngoma ambazo zina beat moja na zote zimetengenezwa na producer Mr T Touch.
Nimepiga story na Black Rhyno kwenye show yangu ya Supermega kupitia Kings Fm kutaka kufahamu kama atamshtaki Nay kwani ana haki miliki ya mdundo huo.
“Kuamua kumshtaki ni maamuzi yangu..mimi bado sijaamua kumshtaki,ila nikiamua kumshtaki basi nitamshtaki na itajulikana watu wote mtajua kama nimemshtaki,”amesema Black Rhyno.

Chibu Perfume ya Diamond kuingia sokoni muda wowote


Chibu Perfume za mkali wa wimbo Salome, Diamond Platnumz zitaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa kwa mujibu wa Sallam, meneja wa masanii huyo.

Mwaka 2016 muimbaji huyo alionyesha sample ya perfume hizo hali ambayo ilileta shauku kumbwa kwa mshabiki wa muimbaji huyo.

Ijumaa hii meneja wa msanii huyo, kupitia ‘Insta Live’ amedai tayari mzigo wa perfume hizo umeshaingia mjini na utapatikana katika maduka mbalimbali nchini.

“Mzingo umeingia, utapatikana kila sehemu bado hatujapanga bei,” alisema Sallam huku akionyesha perfume hizo.

Meneja huyo alidai perfume hizo hazitapatikana kwa bei ya chini ya laki moja na huwenda bei ikaongezeka kutokana na ubora manukato hayo.

New Video: Fid Q – Kemosabe

Sallam atangaza ujio wa tamasha la Diamonds Are Forever 2017


Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK aka ‘Fundi Mitambo’ ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.
Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000 na 100,000 kwa VIP.

Sallam akizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Instagram (Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika uwanja wa Taifa.

“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” Sallam aliwaambia mashabiki.

Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuhudhuria.

Hata hivyo hakuweka wazi ni lini au mwezi gani tamasha hilo litafanyika.

Nay wa Mitego amsihi Raymond amwandikie Madee nyimbo

Nay wa Mitego ameuweka uhasimu wake na Madee kwa kumuomba Raymond amsaidie rais huyo wa Manzese kumwandikia nyimbo.
Nay alitoa ushauri huyo baada ya watangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, kumsikilizisha wimbo mpya wa Madee, Hela akiamini kuwa hauna kiwango cha kuridhisha.

“Nimeusikiliza, nimemuona Raymond anatakiwa kurudi sehemu kuwasaidia kaka zake,” alisema Nay.
Kwa muda sasa Nay na na Madee wamekuwa kwenye uhasama kimuziki.

Darassa ana fursa ya kuingiza mamilioni ya shilingi kwa show za Kenya


Akiwa anajitayarisha kutoa album yake mwaka huu wa 2017, rapper Darassa hivi sasa ana uwezo wa kujiunga na wanamuziki wa kuimba wa Bongo Flava nguli Diamond Platnumz, Rais CEO wa kampuni ya muziki Africa WCB na hasimu wake wajadi kimuziki si mwingine bali ni Mfalme wa Bongo Flava Africa Alikiba, kwa kuwachuna Wakenya mamilioni ya pesa kwa hiyari yao kupitia ufanisi wake kimuziki na umaarufu unaozidi kupanda kila uchao hapa nchini Kenya.

Nikianzia na mjini Mombasa uswahilini hapa, nakupatia hali halisi jinsi ilivyo. Nakutembeza katika mitaa kadha wa kadha ambapo mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wameupokea wimbo wa rapper Darassa ‘Muziki’ kwa taadhima na heshima kubwa. Kuanzia kitongoji cha Lights, Soko Mjinga, Kisauni, Mwandoni, Mtopanga, Bombolulu, Bamburi hadi kuvuka ng’ambo ya pili ya Ferry Likoni mpaka Ukunda nyimbo, ‘Muziki’ inatamba kwa kasi zaidi ya mawimbi mazito baharini.

Mbali na Pwani ya Kenya, sehemu za nyanda za juu na Ziwa Victoria hadi Kisumu na Kenya yote kwa jumla. Kituo cha redio maarufu zaidi nchini cha Citizen, kupitia kipindi cha Mambo Mseto kinachoendeshwa na mtangazaji anayependwa sana na vijana Afrika Mashariki Mzazi Willy M Tuva, huwa kipimo kamili cha ni mwanamuziki gani anayetamba kwa sana Afrika Mashariki katika msimu fulani kwa kupitia requests zinazotumwa na mashabiki kwa kuitisha nyimbo za wasanii wanaowakubali.

Msimu huu Darassa ameivunja rekodi kwa jinsi nyimbo yake ya Muziki inavyoombwa kwa sana si radio Citizen pekee bali hadi vituo vingine mbalimbali hata vile vinavyotangaza kwa lugha ya jamii fulani ama lugha ya mama hapa Kenya.

Kimtazamo mji wa Mombasa ndio kitovu cha mafanikio kwa wasanii wengi wa Bongo Flava kutamba nchi Kenya wanaobobea na waliobobea na kufifia kimuziki. Nikiwataja baadhi tu wakiwemo Mr Nice ‘’Mzee wa Fagilia, Mr. Blue jamaa la ‘Mapozi’, Ray C ‘Mrembo wa Wanifuatia nini’, Lady Jaydee ‘Dada wa Siku hazigandi’, Proffessor Jay ‘Nguli wa Zali la Mentali’, Ferooz ‘Kigogo wa Starehe.’ Alikiba, ‘Jamaa wa Cinderella’, Diamond Platnumz ‘Raisi wa Kamwambie’ Yamoto Band ‘Vijana wa Nitakupelepweta’ na wengine wengi.

Hii inapelekewa na sababu ya kuwa watu wanaoishi katika pwani ya Kenya wengi wao hutumia Kiswahili na tokea jadi kabla ya muziki wa kizazi kipya kuiteka nyara anga ya muziki wa pwani nchini Kenya wamekuwa wakipenda sana muziki wa Taarabu ambao asili na chimbuko lake ni nchi ya Tanzania hivyo wa pwani wanajua utamu wa Bongo Flava kabla kusambaa sehemu zengine za nchi ya Kenya.

Kwa sasa wimbo, Muziki umekuwa kama wimbo wa taifa. Unaongoza kwa kuwa wimbo unaoitishwa na kuchezwa zaidi na Asilimia zaidi ya themanini ya vituo vya redio hapa nchini Kenya.
Unapoingia kwa matatu(Daladala), kuna msemao unaopewa abiria mwenye maneno mengi na utingo chambilecho pale mtu anapolalamikia nauli imepanda unajibiwa na mstari katika wimbo ‘Muziki’ (Acha maneno weka muziki). Kwakweli Darassa ametia watu wengi skuli(shule), sasa kazi ni kwake…mashabiki nchini Kenya wana kiu na hamu ya kumuona LIVE. Sasa kama soko limefunguka, kaka Darassa wangojani?

Ommy Dimpoz aeleza kwanini alisita kuingiza sokoni mavazi ya PKP


Kuna wakati Ommy Dimpoz aliwahi kuahidi kuwa angeingiza sokoni mavazi ya brand yake ya PKP na aliwahi kutengeneza hadi sample zake.
Lakini hadi sasa, hakuna dalili kuwa mavazi hayo yatazinduliwa rasmi.

Akiongea na Bongo5, Ommy amesema alisita kuingia kichwa kichwa kwenye biashara hiyo sababu aligundua atawanufaisha wajanja wachache.



“Kama kwa biashara ya kutaka sifa nionekane na brand ya vitu vyangu, sawa, lakini kama kwaajili ya kutengeneza pesa hii bado ni ngumu sababu ni kama unawafanyia promotion watu wengine,” amesema.

Ommy anadai kuwa kuna wafanyabiashara kibao ambao wanasubiri mastaa waanzishe brand zao na kisha kwao kwenda kutengeneza makontena ya mzigo China na kuuza kwa bei nafuu.

Ni AY ndiye aliyenibakisha kwenye tasnia ya burudani, nilikuwa bandarini huko – Sallam


Meneja wa WCB ya Diamond Platnumz ambaye pia ni meneja wa AY, Sallam SK aka ‘Fundi Mitambo’ amefunguka kwa kudai kuwa alitambulishwa na rapper AY kwenye tasnia ya burudani.
Sallam ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika jukumu la kumsimamia Diamond, alikuwa akijihusisha na biashara ya magari bandarini.

“Ni AY ndiye aliyenibakisha kwenye tasnia ya Burudani nilikuwa zangu huko bandarini na shughuli zangu huko,” Sallam alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Mapema mwaka 2016 Sallam alieleza furaha yake ya kufanya kazi na legendary ‘AY’ katika ukurasa wake wa Instagram huku AY akitupia comments zake juu ya meneja huyo mpya.

Billnas adai wimbo wake mpya ‘Mazoea’ aliurekodi miaka 3 iliyopita

Msanii wa muziki wa hip hop, Billnas amedai wimbo wake mpya ‘Mazoea’ aliyomshirikisha rapper Mwana FA aliurekodi toka mwaka 2014.
Rapper huyo ambaye yupo chini la label ya LFLG, amedai amekuwa na tabia ya kurekodi nyimbo nyingi na kuziweka kusubiria muda sahihi wa kuziachia.

“Nyimbo ya mazoea nilirekodi tangu mwaka 2014,” Billnas alikimbia kipindi cha Ubaoni cha EFM. “Unajua ukiwa na nyimbo nyingi ndani kuna utulivu fulani unakuja kwa msanii, kwa sababu tayari ndani una ngoma za kutosha ambazo zinasubiria muda wakutoka,”

Kuhusu wimbo wake wa ‘Mazoea’ rapper huyo amedai ameachia wimbo huo ili kuwataka watu kupunguza mazoea kwani mazoea hupunguza heshima.

“Mtu hawezi kutunza heshima kama akikuzoea sana,” alisema Billnass.

Changamoto ni nyingi sana lakini kila msanii ana changamoto zake asema SOUBER SNEARTZ katika interview na G.LOVETZ BLOGSPOT

Picha ya Souber Sneartz
Msanii anaekuja kwa kasi ya ajabu ameanza kuwa gumzo la mtaani kwa sasa na ngoma yake mpya ya sina raha amemweleza g.lovetz kuwa ana mpango wa kufanya makubwa katika mziki huu na kufika mbali
malengo yangu kufika mbali kimziki kila mtu ajue anijue na afahamu nafanya kitu gani,pia nawaambia mashabiki wangu wasapoti mziki wangu na video itakuja hivi karibuni

waweza kusikiliza na ku dawnload INTERVIEW  ya souber sneartz na G.LOVETZ gusa HAPA

13 Jan 2017

Akothee aweka wazi ratiba ya ziara yake katika bara la Ulaya mwaka huu


Ukiambiwa utaje wasanii wa kike wa Kenya wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye muziki, jina la Akothee hutaacha kulitaja.
Muimbaji huyo ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Madam Boss ameamua mwaka huu kuutangaza muziki wake zaidi katika bara la Ulaya kwa kuamua kufanya ziara katika nchi kadhaa za bara hilo.

Ziara hiyo ya Akothee inatarajiwa kuanza mwezi April mwaka huu, na nchi ambazo anatarajia kuzitembelea katika ziara yake hiyo ni Switzerland, Australia, Sweden, Ujerumani na Italia.