burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Mac 2017

Shigongo amuonya Diamond, amlaumu kutoza milioni 100 show za ndani ‘ukimya wake bila shoo nyumbani utamzamisha’


Eric Shigongo, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amelalamika kitendo cha Diamond kuwatoza mapromota wa nyumbani kiwango kile kile anachowatandika wale wa nje.

Shigongo ni mmoja wa waandaji wakubwa wa matamasha kupitia ukumbi wake wa Dar Live na huenda miaka ya hivi karibuni ameshindwa kuzimudu gharama za kumchukua kutumbuiza. Kupitia Instagram, haya ndio mambo aliyoandika:

Kama nilivyosema wakati naanza kwamba ninampenda sana Diamond kwa sababu amekuwa mtu wa kujituma, aliyeng’ang’ania kutoka kwenye umasikini mpaka kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo. Ieleweke kwamba sipo kwa ajili ya kumsema, kumponda, hapana, nipo kwa ajili ya kumshauri kama mdogo wangu, rafiki yangu kwa hiyo naomba nisieleweke vibaya.

Diamond Platnumz kwao ni Tanzania, ni mwanamuziki wa Kitanzania na hata wapenzi wake wengi wanaomsapoti kwa nguvu nyingi ni Watanzania ambao asilimia kubwa vipato vyao ni vya chini mno. Wengi wanatamani kumuona akifanya shoo katika ardhi yake ya nyumbani, lakini badala yake wamekuwa wakimuona mara nyingi akifanya shoo Marekani, Ulaya, Nigeria, Afrika Kusini, kwenye Mashindano ya Afcon na sehemu nyingine nyingi ambazo ni nje ya Tanzania, mahali alipozaliwa na kuthaminiwa, mahali ambapo aliweza kujijazia mashabiki wengi.

Mashabiki zake wanahitaji shoo, kumsoma kwamba amejenga nyumba, amenunua au amepata watoto na Zari si kitu ambacho mashabiki wanakihitaji zaidi kutoka kwake, wanachohitaji ni kuona shoo zake kwa wingi kama kilivyokuwa kipindi cha Moyo Wangu, Kamwambie na nyimbo nyingine.

Ni kweli ana jina kubwa, ana mashabiki wengi, amepambana sana kufika alipokuwa lakini kwa upande mwingine anatakiwa kuangalia gharama za shoo zake hasa anapofanya nchini Tanzania, kwa watu ambao walimfanya leo kujulikana zaidi kama Diamond na si Naseeb Abdul. Leo, Diamond anafanya shoo kwa dola 55,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100. Hii inamaanisha kwamba kwa mtu kama mimi, nikimchukua Diamond kwa gharama hiyo inamaana kwamba nitataka niingize kiasi kikubwa kama faida, kwa hiyo badala ya kufanya shoo Dar Live, Diamond Jubilee au sehemu nyingine, nitaihamishia shoo yangu Mlimani City na kufanya kiingilio cha shilingi elfu hamsini.

Swali la kujiuliza, je, yule bodaboda anayepiga sana nyimbo za Diamond ataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini? Yule kijana anayatafuta riziki kwa kuingiza nyimbo za Diamond kwenye simu za wateja ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Je, yule kijana wa Tandale, Temeke, Mbagala mwenye fulana kubwa iliyoandikwa WCB ataweza kuingia kwa gharama hiyo? Jibu rahisi ni kwamba hatoweza.

Ni lazima afikirie ajue kwamba gharama anazotoza sehemu nyingine ziwe tofauti na Tanzania, au azifanyie gharama hizo kampuni kubwa za mitandao ya simu na vinywaji lakini si mtu binafsi.

Mara nyingi amekuwa akisema huko nje analipwa zaidi ya milioni mia moja, je, ni halali hata kwa Watanzania wenzake waliomfanya kuwa hapo alipo kuwatoza kiasi hicho cha fedha huku huyo anayemchukua akitarajia shoo yake iingiwe na watu wa hali ya chini wenye kiu ya kumuona?

Labda Naseeb Abdul mwenyewe ndiye aliyelazimisha ada hii, kama si yeye bali ni mameneja wake (Salam na Tale) basi wanamshauri vibaya na matokeo yake kutofanya shoo nyumbani kwake (Tanzania) kutamfanya apoteze kupendwa na mashabiki sababu ya umbali alioutengeneza. Ikumbukwe kwamba watu hununua bidhaa ya mtu wanayempenda, mtu akichukiwa na bidhaa zake hususiwa.
Diamond na WCB ni biashara ya Naseeb Abdul, hivyo basi Naseeb Abdul hatakiwi kuthamini sana fedha na kusahau mashabiki zake waliomfanya kuwa hapo alipo. Kifike kipindi awaeleze mameneja wake “HAPANA! TANZANIA NI NYUMBANI NA HAWA NI NDUGU ZANGU”

Basi kama waandaaji watashindwa kumudu gharama zake sababu Naseeb ni mfanyabiashara kama mimi, basi afanye shoo ya kujitolea (Charity show) kama tuliyofanya naye huko Tandale huko Mwanza, Kigoma, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro kwenye viwanja kwa kiingilio cha shilingi 3000 na kisha fedha hizo azipeleke kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na hiyo itamfanya kupendwa na mashabiki na kumfanya kwenda juu kimuziki.

TOFAUTI NA HAPA, MBELE YAKE KUNA SHIMO, UKIMYA WAKE BILA SHOO NYUMBANI UTAMZAMISHA!!

NEW AUDIO | Yamoto Band - BASI | Download

Yamoto Bandi Safi


NEW VIDEO | Wakazi – Tanganyika | Watch


NEW VIDEO | BIBI CHEKA - NALIA | Watch

BIBI CHEKA - NALIA

The Rock na Vin Diesel bado hawapikiki chungu kimoja


Uhasama kati ya mafahari wawili wa filamu ya Fast and Furious, The Rock na Vin Diesel bado unaendelea, imeripotiwa.

Chanzo kimeuambia mtandao wa The Hollywood Reporter kuwa wawili hao wanatenganishwa kwenye matukio ya kuitangaza filamu yao ijayo na hata kuwa kwenye chumba kimoja. Hii imekuja kama surprise kwakuwa wawili hao waliwahi kusuluhishwa.

The Fate of the Furious itaingia kwenye majumba ya sinema April 14, 2017.

FIFA yakubali kuwepo timu 48 kombe la dunia


Baada ya Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino kutaka kuwepo kwa timu 48 ambayo ilikua ni moja ya ahadi zake katika kampeni.

Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.

FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.

Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.

Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.

Mapendekezo hayo yapo hivi

Afrika – 9 kutoka timu za awali 5

Asia – 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya – 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean – 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania – 1 kutoka timu 1 ya awali

Amerika ya Kaskazini – 6 kutoka timu 4 za awali

Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.

Serengeti Boys yapata ushindi dhidi ya vijana wenzao wa Burundi


Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepata ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi jana katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na fainali za vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Mtanzania, mwenye beji ya FIFA, Deonisya Rukyaa.

Mabao ya vijana wa Tanzania yalifungwa na kiungo Muhsin Makame na beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyepanda kusaidia mashambulizi.

Makame alifunga dakika ya 19 akimalizia pasi ya Israel Mwenda kutoka upande wa kulia, wakati Kibabage alifunga dakika ya 38 baada ya kupanda na mpira upande wa kushoto na kuingia nao ndani kabla ya kumtungua kipa Djuma Bitiyaweho.

Pamoja na wenyeji kurudi vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0, lakini timu hizo zilishambuliana kwa zamu na ila uimara wa safu ya ulinzi ya Tanzania iliwafanya Burundi wasipate hata goli moja, bao la tatu, lililofungwa na Nahodha Kevin Nashon Naftali dakika ya 72.

Timu hizo zitarudiana Jumamosi Uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu

Bill Nass akiri kuwa chorus ya Nazizi kwenye Raha ndio ilimweka kwenye ramani ya muziki


Rapper Bill Nass hawezi kusahau mchango mkubwa wa Nazizi na TID kwenye maisha yake ya muziki.

Wawili hao waliufanya wimbo wake uliomtoa, Raha uwe na mvuto mkubwa.

Akimpongeza Nazizi kwenye siku yake ya kuzaliwa wiki hii, Bill ameielezea chorus iliyofanywa na muimbaji huyo wa kundi la Necessary Noise kuwa ndio ilikuwa kila kitu.

“Nakutakia maisha maref miaka mobb momma wa taifa,” aliandika Bill Nenga.

“U know I love u….!!have a blast chorus yako ndo imefanya leo wananiita Nenga mara Mzungu Mzee nabado nakomaa tuu….hope ur very proud too….hbd @nazizihirji.

Raha ndio wimbo uliomfanya rapper huyo atajwe kuwania tuzo za KTMA kwenye kipengele msanii bora chipukizi miaka miwili iliyopita.

Lady Jaydee leo kuzindua album ya ‘Woman’ King Solomon Hall, Dar


Lady Jaydee leo atafanya uzinduzi wa album yake mpya na ya saba, Woman.
Ametangaza kubadilisha ukumbi wa awali na sasa utafanyika King Solomon Hall.

“Naomba kuwafahamisha mabadiliko ya Venue Ijumaa Woman Album Launch Itafanyika ukumbi wa King Solomon Hall , karibu na Best Bite (Ada Estate- Kinondoni) Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” ameandika Jide kwenye Instagram.

Album hiyo itakuwa na nyimbo kama Kamoba alioshirikiana na Hamoba wa Zambia, Together Remix akiwa na Spicy, Rosella akiwa na H_Art the Band, Unanichanganya akiwa na Naava wa Uganda na zingine.

Hawa ni wasanii wa kike wa Bongo Jay Moe anawakubali + rappers wa anaoamini wana uwezo wa kuwakalisha wakongwe


Jay Moe amewataja Vanessa Mdee, Lady Jaydee na Aika wa Navy Kenzo kuwa ndio wasanii wa kike anaowakubali zaidi kwa sasa na ambao angependa kuja kuwashirikisha siku moja kwenye kazi zake.

“Hao ni katika wachache ambao naona wanaipeperusha bendera yetu ya Tanzania,” alisema Jay Moe kwenye mahojiano na kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Watu kama akina Dayna Nyange pia natamani nifanye nao sababu nakubali anachofanya sababu niliona tangu anaanza mpaka leo alipofikia kwahiyo niko proud pia ikitokea kufanya kazi na mtu kama huyo,” alieleza rapper huyo.
Kwa upande mwingine Jay Moe alitaja baadhi ya rappers ambao anaamini wana uwezo mkubwa kuzidi wakongwe kibao.

“Nakutana nao, kuna wimbo mimi natakiwa nifanye na One The Incredible,” anasema. “One ni kati ya vijana ambao wamekuja zama za sasa hivi ambaye inaniuma ninavyoona hawi kama vile mimi ninataka awe kwasababu uwezo wake ni mkubwa sana hata ukifananisha na wasanii nilioanza nao mimi zama zangu, kuna wengine kibao ambao kiukweli kwa ushairi na nini hawamwezi. Napenda kwasababu anaweza kufanya kwa Kiswahili vizuri, kwa Kiingereza vile vizuri na ukiacha hivyo, unampenda mtu pia kutokana na tabia yake na anavyokurespect. Ndio maana hata kwenye interview nyingi nakuwa nataja mtu kama Bill Nass kutokana na respect yake na ile passion yake aliyokuwa nayo kwenye muziki. One the Incredible ni mmoja wapo ambao nawish kesho nimuone akiwa kwenye nafasi ya juu kabisa,” alifafanua Jay Moe.

“Songa, napenda anachokifanya, napenda anavyousoma mchezo, tulimuona Songa wa kabla ya Mwendo Tu na wa kwenye Mwendo tu, unaweza kuona kabisa huyu jamaa akifanya Mwendo tu tatu nne atakuwa yuko mbali. Napenda pia hiyo passion ya hip hop na presentation ambayo wanafanya watu wengine, Wakazi bado anafanya vizuri kwenye ile side ambayo watu wanataka ile hardcore hip hop na ile rap ambao kuna ushairi, silabi na nomino za kutosha Nikki Mbishi bado yupo kwenye hiyo nafasi pia.”

Shilole apanga kufanya makubwa kwenye 40 ya mtoto wa Nuh Mziwanda

Shilole aka Shishi Trump ni mzungu. Amesema hana kinyongo na ex wake Nuh Mziwanda na ndio maana mwaliko wa 40 ya mtoto wa kike wa Nuh na mke wake Nawal ukihusika, ataenda kufanya makubwa.

“Mimi sinaga shobo ujue,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni.

“Mimi naenda kwa moyo wangu kwamba ntaenda kama msanii mwenzangu kwamba hongera kwa kupata mtoto vizawadi hivi kama vibeseni, si unajua tena mama yake mkubwa wa zamani lazima naye.. sina tatizo,” aliongeza.

Alipoulizwa kwanini hakumpa mtoto Nuh kwenye uhusiano wao, staa huyo alijibu, ‘hatukujaaliwa tu.’ Shilole amesisitiza kuwa bado yupo single kwa sasa.

Nay wa Mitego akutana na Dkt Mwakyembe Dodoma


Rapper Nay wa Mitego, Alhamis hii aliitikia wito wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kukutana naye mjini Dodoma kwaajili ya kuzungumza namna ya kuuboresha wimbo wake Wapo ambao licha ya kuikosoa vikali serikali pamoja na Rais Dkt John Magufuli umepokelewa kwa mikono miwili.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais Magufuli kuamuru kuachiwa huru kwa Nay ambaye alikuwa amekamatwa na polisi na wimbo wake kufungiwa na BASATA. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Dkt Mwakyembe alisema wasanii wana nafasi kubwa katika kuisaidia serikali kukemea mambo maovu.

Amewataka vijana kutambua kuwa Tanzania ni nchi inayozingatia utawala wa sheria na kwamba wana uhuru wa kukosoa bila kutukana au kwenda nje ya maadili. “Na ndio maana tukasema kwa wimbo wa Nay hapana, hebu ngoja tuusikie, mbona ni wimbo mzuri tu,” alisema Mwakyembe.


Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haiwezi kuwanyima watu uhuru wa kujieleza ilimradi tu wasivuke mipaka.

Kwa upande wake Nay alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwa mwelewa, kitu ambacho hakuwa ametegemea huku pia akiwatetea polisi waliomkamata kwa kueleza kuwa walikuwa wakifanya kazi yao.

Nay anatarajiwa kukutana na Rais Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Barakah The Prince: Uhasama wa Alikiba na Diamond ulikuwa na athari kwenye Nisamehe


Barakah The Prince amedai kuwa kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake Nisamehe kulikuwa na changamoto hasa kutokana na mvutano uliopo kati ya Team Kiba na Team Diamond.

“Ujue Alikiba ni brand kubwa na ni brand ambayo ina mvutano na vitu vingi, kwahiyo unavyofavya collabo na Alikiba kuna mawili hapo, kuna nyimbo kufanya vizuri na kuna nyimbo kufanya vizuri wastani, wa kawaida kwasababu ya ule mvutano wa kibiashara ambao upo kati yake na timu nyingine,” Barakah alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.

Hata hivyo amesema hakutegemea kama wimbo huo ungekuja kufanya vizuri kama ngoma zake zingine.

30 Mac 2017

NEW AUDIO I Gbros De Voice - KALE I DOWNLOAD

Image may contain: 1 person

NEW AUDIO | J.I - Sijatosheka | Download

NEW VIDEO | M2the P Ft. Mr Blue - Nakuhonga | Watch


NEW VIDEO | SAM WA UKWELI - KISIKI | Watch

SAM WA UKWELI - KISIKI

NEW VIDEO | WEUSI - YA KULEVYA DANCE | Watch


NEW VIDEO | J.I - Sijatosheka | Watch


NEW VIDEO | Nuh Mziwanda - Anameremeta | Watch

Nuh Mziwanda - Anameremeta

Tusipoangalia Siasa itauzidi nguvu muziki nasi tupotee kama Bongo Movie – Nay wa Mitego


Nay wa Mitego amedai kuwa kama wasanii wa Bongo Flava wasiposimama kidete kuupigania muziki wao, kuna hatari ukapotezwa na siasa.
Amedai kuwa siku za hivi karibuni mashabiki wamekuwa wakifuatilia zaidi mambo ya siasa kuliko wanavyofuatilia muziki, na anasema hiyo ni hatari.

“Watu walikuwa wanasikiliza siasa zaidi kwamba leo nini kinaendelea, leo kiongozi gani ameongea kitu fulani, nafikiri sasa ni time ya sisi kupambana kuurudisha muziki wetu kwenye line, kuurudisha muziki wetu watu wausikilize muziki, siasa na vitu vingine ambavyo vinaendelea, skendo, kiki, viwe vya baadaye,” rapper huyo amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

Nay ameonya kuwa kama wasanii wa muziki wasipokomaa, wanaweza kujikuta wakipumulia mashine kama wenzao wa bongo movie ambao soko lao linazidi kuporomoka.

Kwa upande mwingine Nay amedai kuwa wimbo wake Wapo umefanya muziki uanze kusikilizwa tena. Ijumaa hii rapper huyo anakutana na Rais Dkt John Magufuli baada ya kuitwa Ikulu kufuatia wimbo wake Wapo uliokosoa serikali.

Maneno ya Lionel Messi baada ya kufungiwa na FIFA kwa kumtukana refa


Baada ya Lionel Messi kufungiwa mechi nne na shirikisho la soka la kimataifa (Fifa) baada ya kudaiwa kumtukana muamuzi wa pembeni.

Wakati wa mchezo dhidi ya Chile uliyochezwa March 24 2017, baada ya kufungiwa Lionel Messi mtandao wa bleacherreport ulimtafuta Lionel Messi na haya ndio yalikuwa maneno yake.

“Maneno yangu hayakuwa yamemlenga moja kwa moja muamuzi msaidizi, kuna maneno ambayo yalikuwa yamesemwa kwangu mimi nilijisemea tu” >>> Lionel Messi

Chelsea waanza kumfukuzia Alexis Sanchez


Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte ana malengo ya kumsajili mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez majira ya joto kwa mujibu wa habari kutoka The Guardian.

Muitaliano huyo ambaye kwa sasa anafanya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake na ameshafanya mjadala kuhusu maswala ya uhamisho na uongozi wa klabu ya Chelsea, hivyo kuwa mstari wa mbele kumpata mchezaji huyo raia wa Chile anayetaka kuondoka Emirates majira ya joto.

Alexis amekerwa na kikosi cha Arsenal kisicho na maendeleo, pia anatakiwa na PSG, Juventus na Inter Milan.

Brazil timu ya kwanza kufuzu kombe la Dunia 2018 Russia


Timu ya taifa ya Brazil alfajiri ya leo imekuwa ni timu ya kwanza kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 Russia, baada ya kuifunga timu ya taifa ya Paraguay kwa magoli 3-0.

Magoli ya Brazil yalifungwa na Coutinho alifunga goli la kwanza na la pili lilifungwa na Neymar na goli la mwisho lilikuwa katika dakika tano za mwisho ambapo Coutinho alicheza vyema kwa muuganiko na Marcelo, ambao walipeleka pasi kwa Paulinho aliyekuwa amepanda mbele na akauunganisha mpira kwa kisigino ukakuta Marcelo aliyekuwa anakimbia na kufunga kwa urahisi.

Brazil katika kundi lake yupo na timua za Uruguay, Peru na Paraguay.

Nyota Ndogo awajibu wanaoteta kwanini hazeeki


Staa wa kike wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Kenya maarufu kama Nyota Ndogo, amewajibu watu wanaoonekana kumfUatilia maisha yake binafsi.
Nyota ambaye alizaliwa mwaka 1981, amekuwa kwa game ya muziki tangia mwaka wa 2004 ambapo tokea hapo amekuwa akitoa hits za muziki kila anapoingia studioni kurekodi.

Muziki kwake umekuwa kila kitu, na si mara moja amekuwa akihoji kwenye vituo vya habari kuwa hata nyumba anayoishi kwa sasa imejengwa na pesa za muziki pamoja na biashara nyingine ambazo zinazidi kumtilia kipato cha kila siku.

Nyota ni baadhi ya mastaa wa muziki wa nchini Kenya wanaoheshimika sana, na pia amekuwa katika mstari wa mbele katika wale mastaa wakongwe nchini Kenya ambao hawakosi show kila wakati.

Hata hivyo mbali na mafanikio hayo, Nyota Ndogo katika maisha yake ya kawaida hakosi kupitia changamoto za kimaisha kama staa wengine Afrika. Leo kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyota ametupia ujumbe unaonekana kuwasuta watu fulani wenye kupenda kumdadisi maisha yake binafsi hadi kufikia kiwango cha kumuuliza kwanini yeye hazeeki.

Naye mwanadada huyu, hajasita kuwajibu wanaouliza maswali kama haya kwa kuuandika ujumbe ulioambatana na picha yenye kumuonyesha akiwa na tabasamu kubwa kwenye kipaji chake cha uso…nikinukuu, Nyota ameandika: Wanasema why uzeeki nyota nawajibu nakubali matokeo and I smile all the time, sijui kukasirika kwa mda mrefu ila ikifikia hapo basi umeniumiza sana.”

Cristiano Ronaldo ndio mcheza soka anae ingiza mkwanja mrefu


Mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa ni mchezaji aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani na jarida la France Football, huku Messi akiwa katika nafasi ya pili kwa msimu wa 2016-17.

Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12.



Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo na Ronaldo anaonekana amepanda haraka baada ya kushinda Ballond’Or.

Mchezaji mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid.

Hii ndio list ya wachezaji watano wanao ingiza pesa nyingi zaidi

Cristiano Ronaldo, Real Madrid, Pauni 75.62m
Lionel Messi, Barcelona, Pauni 66.12m
Neymar, Barcelona, Pauni 47.97m
Gareth Bale, Real Madrid, Pauni 35.4m
Ezequiel Lavezzi, Hebei China, Pauni 24.63m

Nicki Minaj apata dili jipya la mitindo

Nicki Minaj amepata shavu jipya – rapper huyo amesaini mkataba na kampuni ya mitindo ya Wilhelmina.

Rapper huyo amethibitisha kupata dili hilo kupitia mtandao wa Vogue.“I love the synergy between my music and how it inspires my fashion,” amesema Minaj.

“My message is always celebrating your own style. I’m thrilled and honored to have signed with Wilhelmina—they get me,” ameongeza.

Kwa sasa Nicki atakuwa anafanya kazi na mastaa wengine kama Nick Jonas, Demi Lovato, na Shawn Mendes kwenye kampuni hiyo.

Sijasanda kuichana serikali, ila tu mimi si mtu wa kutabirika – Roma

Roma amekanusha madai ya mashabiki wa muziki kuwa ameufyata mkia na kuacha kuichana serikali kwenye nyimbo zake kama zamani kutokana na serikali ya awamu ya tano kuto’entertain’ mambo hayo!

Rapper huyo amedai kuwa muziki anaofanya sasa hautabiriki na ataendelea kuwashtukiza mashabiki kwa nyimbo wasizotarajia kutoka kwake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Extra Fleva cha Uplands Fm, Roma amedai kuwa si mara ya kwanza mashabiki kusema ameufyata. “2012 ile ndio ilikuwa noma, kwasababu ndio nakumbuka ndio nilikuwa nimeachia Mathematics halafu tukachukua tuzo mbili halafu nikakaa kimya mwaka na miezi nane,” amesema.

“Ndani ya kipindi hicho zilitokea sana kuliko hata zinazotokea sasa hivi ‘yaani huyu Roma ndio hawezi kufanya chochote, ameshapewa hela, Roma ametishiwa, Roma amepelekwa polisi, Roma amepelekwa ikulu’ yaani ziliongelewa sana halafu siku isiyokuwa na jina wakasikia 2030 watu wakasahau yote waliyoyasema,” ameongeza.

“Baada ya mwaka mambo yote yakapita wakasahau, wakarudia tena kuongea, siku isiyokuwa na jina wakaja wakasikia Viva Roma.”

Kazi za hivi karibuni za Roma zimeonekana kuwa na mrengo tofauti ukilinganisha na zile alizokuwa akizitoa miaka ya nyuma. Kwa sasa nyimbo zake zinazofanya vizuri ni Usimsahau Mchizi akiwa na Moni Central Zone na K aliyoshirikiana na Baghdad.

Shigongo adai Diamond anaelekea shimoni, awataja mameneja wake kama chanzo


Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameandika barua yenye ujumbe mzito kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Shigongo ameandika:

Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.
Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.

Nitaendelea kesho.

Unadhani kwanini Shigongo anahisi Sallam na Babutale wanampoteza Diamond?

Hii ndio sababu ya show ya Drake ya Amsterdam kuvunjika


Drake alilazimika kuivunja show yake ya mjini Amsterdam Jumatatu hii baada ya kudaiwa kuugua ghafla. Kumbe rapper huyo alikula chakula chenye sumu!

Mtu wa karibu wa rapper huyo ameuambia mtandao wa TMZ kuwa rapper huyo alikula chakula hicho chenye sumu muda mfupi kabla ya kufanyika kwa show hiyo.

Drake alikimbizwa hospitali ndipo madaktari walipomshahauri kutofanya show hiyo. Mashabiki walimsubiri rapper huyo katika ukumbi wa Ziggo Dome kwaajili ya kutumbuiza kwa muda wa dakika 75 kabla ya kutangaziwa kuvunjika kwa show hiyo.

Hata hivyo show hiyo inatarajiwa kufanyika tena Jumatano hii katka ukumbi huo.

28 Mac 2017

NEW AUDIO | Wagosi Wa kaya - Dereva | Download

Wagosi Wa kaya - Dereva

NEW AUDIO | Diamond Platnumz Ft. Ne-Yo – Marry You (Violin Cover) | Download

Diamond Platnumz Ft. Ne-Yo – Marry You

Harmonize – Niambie (Behind The Scene Part 1 & 2) Watch



PART 1

PART 2

Mastaa wanne wa muziki waliojiunga na siasa Kenya


Wakati uchaguzi mkuu nchini Kenya ukiwa umebakiza miezi minne pekee, joto la kisiasa nchini Kenya limezidi huku kila upande wa vyama vya kisiasa ukipiga kifua kuchukua hatamu za uongozi.

Kulingana na katiba ya nchini Kenya, uaniaji wa nafasi za ungozi uliongezeka kwani sasa kuna nafasi za Useneta na Ugavana kinyume na ilivyokuwa kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2002, ambapo wakenya waliwachagua madiwani (MCA Member of county Assembly kwa sasa), Mbunge, na Rais. Kwa sasa wakenya kulingana na katiba wanatakiwa kuchagua MCA, Wawakilishi wakinamama, mbunge, Seneta, Gavana na Rais akiwa na makamu wake. Kutokana na hivi, nimekusogezea wasanii wakali kutoka Kenya wenye kumezea nafasi tofauti za kisiasa kwenye uchaguzi ujao wa Agosti 8 2017.

1. Jaguar

Kwa sasa anatamba na ngoma African Warrior aliyomshirikisha msanii EL kutoka nchini Ghana. Jaguar ameamua kupigania kiti cha eneo bunge la starehe Jijini Nairobi ambacho kwa sasa kinakaliwa na mwanasiasa nguli Maina Kamanda. Tayari Jaguar majuma kadhaa yaliyopita, alijiuzulu kama mmoja wa ma directors wa NACADA ili kuanza rasmi kazi ya kupiga kampeni ya kuwania kiti hicho.

2. Prince Adio

Ni mmoja ya legendary katika muziki wa kizazi kipya ni nikimweka kundi moja na Nyota Ndogo, waliowahi kufungulia njia mastaa wanaoibuka nchini Kenya. Alitamba na vibao kama Nikiwa Ndani, Natamani, Sikitiko na vingine vingi. Pia ni muigizaji ambaye amewahi kuonekana kwenye tamthilia zinazorushwa hewani na televisheni nchini Kenya kama vile tamthilia ya Udhalimu na nyinginezo. Kwa sasa anawania kiti cha MCA wadi ya Frere Town Mombasa mjini.

3. Cannibal

Ni rapper mkali kutoka Mombasa ambaye wengi watakuwa wanamkubali kwa jinsi anavyofoka. Cannibal aliwika na ngoma aliyomshirikisha rapper mwenzake Sharam enzi hizo na kutoa hit kama Street Hustler, Bouncing, Kichwa Kibovu na nyinginezo. Kwa sasa pia anajiunga na mastaa kama Jaguar katika mtanange wa kisiasa na kupigania kiti cha MCA wadi ya Mtopanga Mombasa mjini.

4. Frasha

Kutoka kundi maarufu la muziki la P-UNIT, Frasha ambaye ni staa wa muziki kutoka hapa nchini Kenya, pia hajaachwa nyuma. Ameweka wazi kuwa atapigania kiti cha MCA wadi ya Athi River Township, huku tayari akiwa ametangaza rasmi chama cha kisiasa atakachokitumia katika mtanage huo na chama chenyewe ni chama cha Maendeleo Chap Chap kinachoongozwa na Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutia.

Man city yakumbana na rungu la FA


Klabu ya Manchester City wamepigwa faini ya Pauni 35,000 na chama cha soka cha England FA kwa kosa la kushindwa
kuwadhibiti wachezaji wake kwenye mchezo dhidi ya Liverpool Machi,19,2017 ulio chezwa katika uwanja wa Etihad.

Wachezaji wa City walionekana kumzonga mwamuzi Michael Oliver katika dakika ya 50 ya mchezo baada ya kuwapatia Liverpool Penati.

Liverpool walipata penati hiyo kufuatia Roberto Firmino kuchezewa madhambi na Gael Clichy katika eneo la hatari ,na ikawekwa kimiani na James Milner kabla ya Sergio Aguero kusawazisha dakika ya 69 mechi ikiisha kwa sare ya 1-1.

Kim Kardashian afikiria kuongeza mtoto wa tatu


Kim Kardashian anafikiria kuwapa North na Saint West mdogo wao. Ndio, staa huyo wa Keeping Up With The Kardashians na mke wa rapper Kanye West, ana mpango wa kuongeza mtoto wa tatu.

Kwenye episode mpya ya kipindi chao cha TV, mrembo huyo ameonesha nia ya kuendelea kuipanua familia yake licha ya ujauzito uliopita kumletea shida. Kupitia kipande kifupi cha video toka kwenye episode mpya, Kim anasikika akisema, “I’m going to try to have one more baby.”

Hata hivyo Kim amedai kuwa madaktari wake wamemshauri kutofikiria kupata mtoto mwingine kwa sasa.

FIFA kumlipa mshahara Coleman kwa kuvunjwa mguu


Shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuwa litamlipa mshahara beki wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland na klabu ya Everton Seamus Coleman kwa kipindi chote atakachokuwa anauguza mguu wake.

Coleman alivunjika mguu wake wa kulia ijumaa iliyopita katika mechi dhidi ya Wales baada ya kuchezewa rafu mbaya na beki Neil Taylor, mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0.

Siku ya jumamosi Coleman alifanikiwa kufanyiwa upasuaji na sasa anataraji kukaa nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi 6 akijiuguza.

FIFA kupitia (Fifa Club Protection Programme) wamethibitisha watakuwa wanamlipa mchezaji huyo kwa kipindi hicho chote atakachokuwa nje ya uwanja. Mshahara wake ambao kwa wiki ni Pauni 50,000.

Bill Nass afunguka sababu ya kutoweka wazi mahusiano yake


Je unajua sababu inayomfanya Bill Nass awe msiri katika mahusiano yake?

Rapper huyo amefunguka sababu inayomfanya awe hivyo. Akiongea na kipindi cha Bongo Dot Com cha Times FM, hitmaker huyo wa Mazoea amesema alishawahi kuwa katika mahusiano mengi ambayo ambayo hakuwa na bahati nayo.

“Nimekuwa kwenye mahusiano mengi ambayo sikuwa na bahati nayo pia inaweza kukutengeneza kisaikolojia kutokana na mambo ambayo nayaona kwa rafiki zangu. Nina bahati ya kuona hivyo vitu kwa hiyo sijui huko mbele mahusiano ni suala la feelings,” amesema rapper huyo.

Bill ameongeza kwa sasa hana mahusiao na mrembo yoyote wala hajawahi kufikiria kuoa hivi karibuni.

Nay wa Mitego aalikwa Ikulu na Rais Magufuli Ijumaa hii


Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameitwa Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Nay amepata mwaliko huo ikiwa ni sasa chache baada ya kuachiwa huru na Jeshi la Polisi lililokuwa likimshikilia tangu Jumapili.

Akiongea na G.LOVETZ Jumanne hii, Nay wa Mitego alikiri kupata mwaliko huo jana na kusema kuwa ameambiwa aende siku ya Ijumaa.

“Yeah ni kweli jana nilipa mwaliko lakini nimeambiwa niende Ijumaa kwa sababu kuna ugeni unakuja kwahiyo na mimi nimealikwa kuhudhuria,” alisema Nay wa Mitego.

Rapa huyo amedai bado nafikiria nini cha kuongea na Rais endapo atapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye.

Nay alikamatwa na polisi Jumapili iliyopita mkoani Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga wimbo wenye maudhui yanayoikashifu Serikali.

Mapema jana mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.

Wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi – BASATA


Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kama kazi yake ikibainika kuwa na kosa la jinai.

“Tulifanya mazungumzo na wenzetu jeshi la polisi waliokua wanamhoji msanii Nay wa Mitego na kuchunguza jinai katika wimbo wake wa Wapo,” Basata walitweet.

Aliongeza, “Baada ya ushauri kutoka kwa Waziri Mwakyembe na baadaye taarifa ya jeshi la polisi na mazungumzo na msanii Nay kituo cha kati cha polisi.Tunaruhusu wimbo wa ‘Wapo’ wa msanii Nay kuchezwa katika vyombo vya habari. Kama taarifa yetu ilivyoeleza, ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi,”

Rapa huyo aliachiwa jana jioni na jeshi la polisi kwa kauli ya Rais Magufuli baada ya kushikiliwa kwa siku mbili.

Samatta kuikosa Burundi leo


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” leo atakuwa na jaribio jingine la kuwakabili Burundi ‘Intamba Murugamba’ katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA.

Mchezo huo utakuwa ni wa Pili kwa kocha Mayanga ambaye Jumamosi iliyopita alianza vizuri kibarua chake kwa kuifunga Botswana mabao 2-0 kwenye mechi ya Kirafiki.

Burundi tayari wamewasili Dar es Salaam jumapili mchana wakiwa na kikosi chao kamili kikiongizwa na Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo.

Kocha Mayanga katika mchezo wake wa leo atakosa huduma ya Mshambuliaji wake Mbwana Samatta anayoichezea KRC Genk ya Ubelgiji ambaye alifunga mabao yote mawili kwenye mchezo uliopita.

Mayanga amesema amemruhusu Samatta kuondoka ili kutumia kikosi chake cha wachezaji wanacheza ligi ya ndani, lengo ni kuiandaa timu ambayo itashiriki fainali za CHAN ambazo zinashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwao.

Mayanga amesema maandalizi yote kuelekea mchezo wa kesho yamekamilika na anatarajia kupata ushindi mwingine kutokana na uelewano mzuri waliokuwa nao wachezaji wake.

“Najua utakuwa mchezo mzuri wenye ushindani kwa kuwa Burundi ni majirani zetu, tunajuana lakini naamini tutashinda kutokana na maandalizi mazuri tuliyokuwa nayo kuelekea mchezo huo,” amesema Mayanga.

Kocha huyo amesema kutokuwepo kwa Samatta kwenye mchezo huo hakutaiathiri timu yake kwani kuna wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza nafasi yake.

Amesema kwenye nafasi hiyo anaweza kumtumia Abrahmani Mussa wa Ruvu Shooting kucheza sambamba na Ibrahim Ajibu na anaamini atafanya vizuri kutokana na uwezo aliokuwa nao mchezaji huyo.

Amesema kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita mchezo wa kesho atatumia mfumo ule ule wa 4-4-2 kwa sababu wanataka kushambulia zaidi na kufunga mabao mengi.

Nahodha wa Burundi Mavugo amesema mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu Tanzania wanakikosi imara ambacho kinaundwa na wachezaji wengi vijana lakini ameahidi kupata ushindi kwenye mchezo huo.

“Tumekuja tukiwa na kikosi imara ambacho kina wachezaji wengi wenye uzoefu kwa hiyo pamoja na kucheza ugenini lakini naamini tutafanya vizuri,” amesema Mavugo.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa mwaka 2014 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Tanzania kufungwa mabao 3-1.

Huu ni ukweli kuhusu Kanye West na ujio mpya wa shindano la American Idol


Kanye West hayupo kwenye mazungumzo yoyote na NBC ama mtu mwingine kwaajili ya kujumuika kwenye ujio mpya wa shindano la American Idol.

Taarifa hiyo ya TMZ inakinzana na zile zilizokuwepo awali.
Kuna ripoti zinaenea kuwa NBC na watayarishaji wanataka kumleta Kanye West kama host, na kwamba mazungumzo yanaendelea.

Vyanzo vilivyopo karibu na Kanye vimesema, “There is no conversation with Kanye West to join ‘American Idol’ or any other show for that matter.”

Kumekuwepo na tetesi kuwa NBC inairudisha tena show hiyo baada ya kuisitisha.

Rapper Swae Lee amkatia tamaa mtoto wa Obama


Rapper Swae Lee amekata tamaa kumpata mtoto wa kwanza wa Obama, Malia.

Swae amefikia hatua hiyo baada ya kuonekana jitihada za kumpata mrembo huyo kuwa ngumu.

Akiongea na mtandao wa TMZ, rapper huyo mwenye miaka 21 amesema, “I give up. They’d probably pull up 20 black cars. man, I’d have to get my own secret service. I got, like, four I got my eyes on. Can’t tell you just yet.”
t.”

Serengeti Boys waweka kambi mkoani Kagera


Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeondoka kwenda mkoani Kagera wameenda na ndege ya (ATCL) kutoka Dar es Salaam, alfajiri ya Machi 26, mwaka huu kwa kambi ya wiki moja.

Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera. Michezo hiyo itafanyika Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.

Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

Timu itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon kwenye kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.

Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.

La ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.

Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego.

Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.

Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.

Washambuliaji: Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.

Benchi la Ufundi:

Bakari Shime (Kocha Mkuu)

Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)

Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)

Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)

Edward Evans (Mtunza Vifaa)

Shecky Mngazija (Daktari wa timu)

Diamond amwaga mamilioni kuisaidia jamii


Kumbe Diamond sio wa mchezo. Hivi ndio vitu ambavyo amejitolea kusaidi jamii mpaka sasa.

Hilo limekuja baada ya shabiki mmoja kuandika ujumbe ambao ulionekana kumgusa muimbaji huyo. “……100m Kwenye shingo…huku watu wana ishu nashida atleast wasaidie watu kwenye maeneo mabaya,” alicomment shabiki huyo kwenye picha hiyo hapo chini.



Naye Diamond alimjibu kwa kuandika, ““…..nimejenga nyumba 5 mwaka jana Iringa, misikiti miwili mmoja Morogoro pia nyingine Mtwara na madrasa Tegeta na nyumba ya Imamu mbali na sadaka mbali mbali sasa unataka nitoe hela zote sadaka nami nisifurahishe ebu niombe radhi kwa hilo.”

Hawa ndio mastaa watakaosikika kwenye albamu ya ‘The Heart Part 4’ ya Kendrick Lamar


Orodha ya nyimbo na wasanii watakaosikika kwenye albamu mpya ya Kendrick Lamar ‘The Heart Part 4’ imevuja.

Albamu hiyo yenye nyimbo 14 imeonekana kuwakutanisha wasanii kibao hatari akiwemo Kanye West, Swizz Beatz, Anderson .Paak na wengine.

Hii ndio orodha ya nyimbo na wasanii watakao sikika kwenye albamu hiyo.

1.Purple Hibiscus (prod. Sounwave & Terrace Martin)
2.Counterfeit (prod. Rahki & Taz Arnold)
3.Trust Everyone (prod. DJ Dahi, Terrace Martin & Thundercat)
4.Delusional (Like You Haven’t) (f. Anderson .Paak & Anna Wise, prod. Sounwave)
5.Product (f. Andre Benjamin, prod. Kanye West & Taz Arnold)
6.Richard Nixon (prod. LoveDragon)
7.None of Your Business (f. Anna Wise, Kanye West, & Q-Tip, prod. DJ Dahi, Kanye West & Sounwave)
8.Double Standards (prod. LoveDragon & Rahki)
9.If You Had Me, You Lost Me (Interlude) (prod. Flying Lotus & Mono/Poly)
10.Commercialized, Failed Experiments (prod. Alchemist, Cardo & Swizz Beatz)
11.Ten Steps (f. Bilal, D’Angelo, & Thundercat, prod. Sounwave & Terrace Martin)
12.Paranoia, Is Love Stronger Than Death? (prod. K.L. & LoveDragon)
13.Rest in Paradise (Interlude) (prod. Terrace Martin)
14.Swim with the Fishes (God Said) (prod. Sounwave & Terrace Martin)