burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

31 Okt 2017

WhatsApp yaruhusu kufuta ujumbe/picha kwa mtu uliyemtumia kimakosa


Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo.

WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa.



Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia.

Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart  ndani ya mwaka huu.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makubwa manne ndani ya mwaka huu ambayo yataifanya programu ya WhatsApp kuwa ya kisasa zaidi.

Twambie wewe mtumiaji wa programu pendwa ya WhatsApp umeyapokeaji mabadiliko haya.

29 Okt 2017

Ruby ajibu kuhusu kolabo na Yemi Alade


Msanii wa muziki Bongo, Ruby amefunguka kuhusu tetesi za ujio wa kolabo yake na msanii wa Nigeria, Yemi Alade.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa hawezi kuweka sana hilo wazi kwani mipango yake sasa ni kuvunja ukimya wake kwa upande nyumbani.

“Siwezi nikasema tayari kila kitu kimemalizika lakini vitu vipo, sitaki kusema kabisa kwenye kolabo za kimataifa natamani iwa surprise kwa sababu nimekaa muda mrefu kimya I need talk about home kwanza” amesema Ruby.

NEW VIDEO | Qboy Msafi Ft Mr blue (Byser) - Kamoyo | Watch


NEW VIDEO | Barakah The Prince – Sometimes | Watch


25 Okt 2017

Darassa kuamsha dude la kufungia mwaka


Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Darassa amezungumzia ujio wake mpya.

Rapper huyo ambaye mara mwisho alisikika na ngoma ‘Hasara Roho’ ameiambia Dj Show ya Radio One yupo katika maandalizi ya kufanya hivyo ila kwa sasa asingependa kulizungumzia sana kwani yeye siku zote siyo muongeaji zaidi ya kazi.

“Kwenye single mpya watu wananijua mimi siyo mtu wa kuongea ongea kama sina kitu cha kuongea mara nyingi huwa nakuja kuongea nikiwa na kitu, kwa sasa naandaa project ambazo naamini nitakuja kufunga nazo mwaka watu wakae tayari tunakuja tuko poa kabisa” amesema Darassa.

Mwishoni mwa mwaka jana Darassa alifunga mwaka na ngoma Muziki ambayo alimshirikisha Ben Pol ambayo inatajwa kuwa ndio ngoma pekee kuwa hit ya kutisha kutoka kipindi hicho hadi mwaka huu.

NEW VIDEO | SQUEEZER ( SKWIZA) - SITAMANI | Watch


NEW VIDEO | Lameck Ditto - Nabembea | Watch

23 Okt 2017

Yamoto Band Imeshakufa Kila Msanii Anasimama Kivyake - Beka Flavour


Msanii wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa hayupo tayari kurudi kwenye kundi la Yamoto Band na kudai ukweli ni kwamba kundi hili lilishakufa na kila msanii sasa anasimama kivyake.

Beka alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa wakati wanaondoka kwenye kundi hilo hawakuwa na pesa zozote zile kwani enzi zao wakati wanafanya show mbalimbali walikuwa wanapewa fedha za matumizi tu na wao walipendekeza kwa uongozi fedha zinapopatikana wafanyiwe mambo kadhaa ikiwa pamoja na kujengewe nyumba.

"Mimi saizi ukisema nitoke kwenye uongozi wangu mpya nirudi Yamoto Band sidhani kama itawezekana unajua watu hawajui tu lile kundi ndiyo limeshakufa kwa sababu saizi kila msanii yupo na uongozi wake, sidhani kama wanaweza kukubaliana watoke walipo na kurudi kule" alisema Beka Flavour

Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi kuwa anafurahi kuona Aslay msanii ambaye alikuwa naye kwenye kundi moja na yeye saizi anakuwa ni kati ya wasanii wanaozungumziwa sana kwa kazi nzuri.

"Mimi nazidi kumuombea kwani mwenzangu saizi amekuwa ni kati ya wasanii ambao
wanazungumziwa sana kutokana na kazi zake, lakini napenda kuwaambia Watanzania kuwa wasanii ambao tulikuwa tunaunda kundi la Yamoto Band Mungu alitupa kitu ndani yetu hivyo muda si mrefu mtakuja kuona haya nayosema kwani kila mmoja ana upekee wake katika kazi zake" alisisitiza Beka

Birdman Kutua Tanzania


Mmiliki wa lebo ya Cash Money, Birdman amethibitisha mpango wake wa  kutua nchini mapema mwakani ikiwa ni sehemu ya ziara kwenye nchi tano za Afrika.

Rapa huyo wa  Marekani, mapema wiki hii ameandika katika akaunti yake ya Instagram kuwa atafanya ziara licha ya kutoeleza ni kwa ajili ya muziki au la!

Mkongwe huyo wa Hip Hop amesifu upendo na mapokezi makubwa wanayopata kutoka nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.

Mbali na Tanzania amezitaja nchi nne ikiwamo Nigeria, Gambia, Ghana na Kenya na kuandika “Nitatembelea kwenye nchi hizi kuanzia Februari.

Birdman ameingia katika mzozo na rapa, Lil Wayne ambaye amekuwa akimtuhumu bosi huyo kuchelewesha kutoa albamu yake “Tha Carter V”.

Bifu hilo limeendelea kuwa kubwa huku baadhi ya mastaa akiwamo Rick Ross kumtaka Birdman amlipe fedha Lil Wayne licha ya meneja huyo kuwa mbogo.

Msanii wa TZ Anayelipwa Kenya na Mtandao Milioni 20 Kwa Siku



Mtangazaji maarufu wa Classic 105 ya nchini Kenya, Maina Kageni amefunguka kwa kusema kuwa kuna msanii mmoja wa Tanzania analipwa na mtandao wa simu milioni 20 kwa siku kutokana na nyimbo zake.

Mtangazaji huyo amedai hawezi kumtaja msanii huyo lakini alibainisha ni kati ya Alikiba na Diamond. Alisema hakuna msanii mwingine wa Kenya au Tanzania anayelipwa pesa nyingi kama hizo kwa siku.

Irene Uwoya Afunguka na Kusema "Naombeni Mniache"


Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya ambaye ndoa yake na mchezaji mpira Ndikumana Katauti wa Rwanda iliingia katika mgogoro mzito na kupelekea kila mtu kuishi peke yake amefunguka na kuwataka watu wasimuingilie katika malezi ya mtoto wake.

Irene Uwoya ambaye alibahatika kupata mtoto mmoja na mume wake huyo kabla ya migogoro yao, ameonyesha kukasirishwa na maneno ya baadhi ya watu kusema kuwa anamlea mtoto wake huyo kizembe zembe huku wengine wakienda mbali na kumtabiria mambo mtoto huyo kutokana na makuzi yake, ndipo hapo Uwoya alipocharuka na kuwataka wasimuombee mambo ya ajabu mtoto wake.

"Wale mnaosema namlea kizembe naombeni sana mniache, namlea navyoweza mimi na mwanangu bado mdogo sana anahitaji mapenzi ya Mama.  Hakuna hata mmoja wenu amewahi kuchangia ata mia ...sipendi kuongea sababu siyo swaga zangu, mimi mpole sana ila kwa mwanangu sina masihara. Sijawahi sema kitu ila leo nimeona niseme na sitarudia tena kusema, mwenye maskio na asikie na mwenye macho aoneee! yale mambo ya laaana mnayo mtabiria mwanangu yashindwe na MUNGU awasamehe sababu hamjui mlitendalo" alisisitiza Irene Uwoya.

NEW AUDIO I CAT P - IN LOVE I DOWNLOAD


21 Okt 2017

E. Mbasha atupa shutuma nzito kwa Flora, ‘anachokifanya siyo kizuri’


Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amemshutumu mzazi mwenzie, Madam Flora kwa kumzuia kuonana na mtoto wake.

Wawili hao ambao wote ni waimbaji ndoa yao ilishavunjika na Madam Flora kuolewa. Akizungumza na TBC Fm amedai kitu anachokifanya siyo kizuri na amekuwa akifanya jitihada za kuonana mwanaye ila imeshindikana.

“Kiukweli mtoto sijaonana naye muda, yeye mwenyewe hajataka kunipa mimi mtoto, nimeshafanya jitihada na anajua na hata kama sasa hivi anasikia anajua mtoto ameninyima na kitu anachokifanya siyo kizuri kwa mtoto” amesema Mbasha.

“Ni muda mrefu, mara mwisho nimeona naye (mtoto) mahakamani, muda mrefu kipindi wanakaribia kufunga harusi. Inaniumiza sana ni mtoto wa kipekee, ni mtoto ambaye nampenda na nimeishi naye kipindi chote tangu mdogo”

New Video: Mr. P – Cool It Down I Warch

NEW AUDIO | G Nako - Seduce Me (Cover) | Download

NEW VIDEO | Harmonize - Nishachoka | Watch


19 Okt 2017

Alikiba, Diamond, Nay, Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini wachanwa na Rayvanny

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Rayvanny ameachia ngoma mpya ‘Tabia’ ambayo amewachana wasanii wengi kuhusu tabia zao.


Ngoma hiyo ambayo Rayvanny amerap, baadhi ya wasanii waliopitiwa na punch line zake ni Diamond, Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini Juma Nature na wengineo kibao. Hapa chini ni baadhi lines hizo.

Ila Juma Nature muda mwingi yupo tungi, Alikiba wa Kariakoo yeye ni shisha na Mirungi/

Diamond akiongea kidogo katukana, Love Boy hupenda wasichana/

Ommy Dimpoz kwa vijembe huyo bwana hachoki, dogo mtoboa siri ni Young Killer Msodoki/

Ukikutana na FA kama hakujui haongei, yuko bize na simu kama Bongo Movie Ray/

Nay wa Mitego yeye ni bifu na kuchonga, utasikia yule mtoto bishoo nitamgonga/

Wanao-act kishua Gosby na Young Dee, wasiogopa wajua mengi Kimbunga na Nash Mc/

Shilole, Shishi mitusi kwa mkupuo, sijui stajini ana sweat maana sizioni nguo/

Nikki wa Pili ha-act kiki-crazy, ila kaka yake Joh anamkopi Jay Z/

Unaweza kuisikiliza ngoma hiyo hapa: TABIA

Hii ni ngoma ya pili Rayvanny kuitoa akirap chini ya WCB baada ya ile ‘Sugu’ ambayo alirudia chorus ya ngoma ya Mr II ‘Sugu’.

Harmonize achekelea support ya Wolper

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulala’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anafurahi kuona anapata support ya Wolper katika muziki wake.

“Nadhani mwanzo ilikuwa hasira tu, nashukuru kuona support ya Wolper, namchukulia kama shabiki yangu tu” amesema Harmonize.

Hiyo juzi katika mtandao wa Instagram Jacqueline Wolper aliposti video mbili zikimuonyesha akifurahia kusikiliza ngoma hiyo ambayo Harmonize amemshirikisha Korede Bello.

AY aupa kisogo muziki?, afungua bucha la nyama

Bila haka siku moja ungependa kuhudumiwa na staa unayemhusudu. Taarifa zikufikie kwamba msanii Ambwene Yessaya maarufu kama AY amefungua bucha la kuuza nyama na unaambiwa yeye ndio muuzaji.

 Picha hii hapa juu inaonesha mazingira ya bucha hilo ambayo hadi sasa bado hatujajua inapatikana maeneo gani. Mkali huyo wa Bongo Fleva ameonekana kuimudu vyema kazi yake mpya na anaifurahia, tunamtafuta AY kwa mahojiano zaidi na tutayaleta kwako ili kufahamu zaidi kazi hii mpya aliyoamua kuifanya.



Je ni kweli maprodyuza wapya Bongo ni beat maker? Lamar ajibu


Producer ametoa ufafanuzi kauli kuwa baadhi ya prodyuza wa sasa ni beat maker tu.

“Yeah ni kweli beat maker wapo unajua kipindi cha nyuma watu walikuwa wana hustler kusoma zile fundamental za muziki, theory na practical watu wanaenda online wanaangalia jinsi ya kufanya vitu wanaenda shule, unakuta watu pia wana certificate za chuo” Lamar ameambia G.LOVETZ.

“Lakini sasa hivi mtu akiwa na laptop na yeye anatengeneza beat anasema ni prodyuza wakati kumix hawezi, kufanya mastering hawezi katika kiwango kile ambacho kinatakiwa” amesema.

Hata hivyo ameongeza kuwa katika media hamna kitu ambacho kinaweza kuchuja muziki ukoje ile kupata kitu kizuri hali ambayo inapelekea uwepo wa muziki ambao siyo.

11 Okt 2017

Dogo Janja Amzimia Vanessa Mdee


Mkali wa Ngoma ya Ngarenaro, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, amefunguka kuwa hakuna mwanamuziki wa kike Bongo anayemzimia kama Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kutokana na swagga zake.

Dogo Janja ambaye amekuwa akihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Uwoya madai ambayo ameyakana na kudai yeye ana mwanamke wake ambaye hayupo kabisa kwenye sanaa aliongeza kuwa, Vee humkosha zaidi na wakati mwingine anatamani mastaa wa kike Bongo wangekuwa wanavaa kama yeye.
“Kiukweli huwa nazimia sana swagga za Vee Money, anajua kupendeza na kuna wakati huwa natamani mastaa wa kike wote wavae na kutupia pamba kama yeye,” alisema Dogo Janja.

Diamond na Rick Ross waingia location kuandaa kitu kipya


Msanii wa muziki nchini ambaye anafanya vizuri kimatiafa, Diamond Platnumz Jumanne hii ameingia location kwaajili ya maandalizi ya kazi mpya akiwa na msanii mkubwa wa Hip Hip kutoka Marekani, Rick Ross.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Hallelujah ameonekana katika video na picha wakishoot Kazi hiyo ambayo haijajulikana ni kazi na namna gani.

Meneja wa kimataifa wa muimbaji huyo, Sallam amethibitisha kwamba wawili hao wameingia location kwaajili ya maandalizi ya Kazi hiyo.



“Diamond Platnumz x Rick Ross On set now somewhere in Miami #BlackBottleBoys and we never stop!!,” aliandika Instagram Sallam.

Rick Ross na Diamond wote ni mabalozi wa kinywaji cha Belaire ndio maana wanajiita BlackBottleBoys.

NEW AUDIO | Bright Ft. Nay Wa Mitego - Salio | Download

NEW VIDEO | KALA JEREMIAH - KIJANA | Watch



7 Okt 2017

NEW VIDEO | Z Anto - Kacheze unapochezaga | Watch


Ngoja nipite njia tofauti na Wasafi – Z Anto


Msanii wa mziki Bongo, Z Anto amesema si kwamba hawezi kufanya kazi na Diamond au label ya WCB bali anataka kupita njia yake ya tofauti.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kacheze Unapochezaga’ ameeleza sababu ya kutaka hivyo ni kutokana na kuwepo kwa team katika muziki.

“Sishindwi kufanya kazi na Diamond nina uwezo na muda wowote tunaweza kufanya kazi lakini pasipo mazingira ya u-team, hiyo inawezekana,” Z Anto ameiambia Bongo5.

“Nilishawahi kuongea na moja ya viongozi wa Wasafi lakini nikaomba ngoja nipite njia tofauti na wanayopita Wasafi, nilikuwa naongea na Tale,” ameongeza.

Z Anto ameendelea kwa kusema suala la kusaini katika label ya Diamond ‘WCB’ ni kitu ambacho hajawahi kuwa na ndoto nacho.

Aslay aishusha ‘Hallelujah’ trending


Ikiwa siku moja imepita toka meneja wa msanii Aslay, Mx kutoa taarifa kuwa ngoma ya ‘Natamba’ imeripotiwa kushushwa katika mtandao wa YouTube hatimaye ngoma hiyo ilirejea hapo jana jioni na kushika namba mbili kama ilivyokuwa awali na hivi sasa imeshika nafasi ya kwanza katika trending ya YouTube.

Hii ni good news kwa mashabiki wa Aslay kwani ngoma hiyo imefanikiwa kushika namba moja katika mtandao wa YouTube kwa kuishusha ngoma ya Diamond Platnumz ft Morgan Heritage ‘Hallelujah’, iliyokuwa imeshika namba moja kwa takribani siku tano mfululizo.

‘Natamba’ ni ngoma nyingine kutoka kwa msanii huyo baada ya kuongeza meneja wake na ina watazamaji 446,213 mpaka sasa.

Kala Jeremiah aweka wazi siku atakayoachia ngoma mpya


Je unahamu ya kusikia ngoma mpya kutoka kwa Kala Jeremiah?

Baada ya kupita kwa takribani mwaka mmoja na miezi miwili bila ya kusikia ngoma mpya kutoka kwa msanii huyo, mwenyewe amethibitisha kuwa Jumanne ya Oktoba 10 ataachia wimbo wake uitwao ‘Kijana’ ambao amemshirikisha Fetty Kalumba.

Wimbo huo umetayarishwa na producer Zest. Kupitia mtandao wa Instagram Kala ameweka kava ya wimbo huo mpya anaotarajia kuuachia na kuandika, “TAREHE 10-10-2017 KWENYE REDIO YAKO NA TV YAKO WOTE MNAKARIBISHWA. #KIJANA @kijana_0444 @fettykalumbu.”

NEW AUDIO I Jobfire wa Melody - NAMPAGA COVER I DOWNLOAD


6 Okt 2017

Aslay Afunguka Sababu ya Kuachia Ngoma 'Bampa to Bampa'


Msanii wa muziki Bongo, Aslay ameeleza sababu ya kutoa nyimbo mfululizo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Natamba’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa anataka kuwa na nyimbo nyingi ila anapokuwa anafanya show zake asitumie nyimbo za Yamoto Band.

“Tangu nimetoka kwenye band nimekuwa nikifanya kazi peke yangu natengemea show zangu ziwe na nyimbo zangu tu siyo za Band ndio maana nafanya kutoa nyimbo nyingi ilimradi hata nikipata show niwe natumia nyimbo zangu,” amesema Aslay.

“Kingine natoa kazi nyingi kwa sababu ni nzuri, kazi nzuri ikikaa ndani huwa naogopa kwa sababu naogopa idea kugongana, kazi nuri ukitoa leo nyingine ukatoa kesho watu watapenda tu” ameongeza.

Kwa mwaka huu Aslay amefanya vizuri na ngoma kama Mhudumu, Baby, Angekuona, Tete, Pusha, Marioo, Likizo, Danga na nyinginezo.

NEW AUDIO I Carpoza ft Yank - WAMEWAKA I DOWNLOAD


NEW VIDEO: Juliana Kanyomozi – Wakajanja

wakanjanja-video

NEW VIDEO | G Nako - Energy | Watch


NEW VIDEO: Madada 6 ft Theophil – Usingoje

madada-6-usingoje

NEW VIDEO | Y TONY - KIBENTEN | Watch

Wolper afunguka salamu ya Harmonize na Brown kutohudhuria Party ya Diamond


Muigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameweka wazi juu ya salamu aliyosalimiana na  ex-boyfriend wake Harmonize katika private part ya Diamond siku ya tarehe 02/10/2017.

Akiongea kupitia kU-Heard ya Clouds Fm, mrembo huyo ameeleza kuwa  jambo la yeye kumsalimiana na Harmonize halikuwa tatizo kwani salamu haikataliwa.

“Siwezi kumshangaa sasa kwa nini nimshangae, mimi siwezi kumshangaa bhana yeye si ndo kaja kunisalimia masikini, coz nilikuwa nimekaa na Aunty akaja akanisalimia sasa sijui kama salamu inakataliwa, hata ingekuwa wewe umesalimiwa ungekataa hata ingekuwa wewe ungekataa,” amesema mrembo huyo.

Pia Wolper akadai kuwa hakutokea na mpenzi wake huyo katika sherehe hiyo kwani w alikuwa anaumwa kwa takribani siku tano na kuhusu kufutwa kwa picha zake mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo amedai hafahamu kuhusu ilo kwani hajaingia katika mtandao huo.

Wadukuzi wa mitandao waiingilia ‘Natamba’ ya Aslay


Kwa sasa ukimtaja Aslay basi hautaacha kutaja uwezo wake aliyonao katika muziki wa Bongo Flava, kwani amesha toa hits kadhaa kwa kipindi kifupi ikiwemo ‘Natamba’ ambayo imezua kizaazaa katika mtandao wa YouTube.

Ngoma ya ‘Natamba’ ilikuwa namba mbili trending siku ya jana  YouTube, ila kutokana na hali ya sinto fahamu ngoma hiyo imepotea katika mtandao huo na kushuka kabisa katika nafasi iliyokuwepo.

Kwa mujibu wa meneja wake MX Carter ameripoti kusikitishwa na tukio hilo na amedai kuwa kuwepo kwa  watu  wasiopenda maendeleo ya msanii huyo na kuamua kuiripoti ‘Natamba’ ishuke Youtube.

“Naona wabaya wasiopenda maendeleo ya AslayIsiaka wamereport video ishuke YouTube… bahati nzuri team ya ufundi inajitaidi kuweka sawa,” ameandika Mx katika Twitter.

Akaongeza kuandika katika mtandao wa Instagram “Poleni kwa mnaopata usumbufu kuiona Video mpya ya AslayIsihaka kama ujumbe unavyoongea hapo juu tuko kwenye jitiada za kuirudisha popote ilipokuwa ikionekana haswa kwenye trending mungu akipenda. Video imekuwa reported na iko Undereview na Youtube na tunajitaidi kuiweka sawa! Ukitaka kuangalia video ya aslay for Now ingia kwenye Bio yake au Search on YouTube.”

Diamond atoa povu kwa wanaofuatilia mahusiano yake


Diamond Platnumz ameamua kutema cheche kutokana na watu kufuatilia mahusiano yake kwa ukaribu kila kukicha.

Kupitia mtandao wa Instagram, hit maker huyo wa ‘Hallelujah’ ameonekana kuumizwa na maneno yanayoendelea kuzungumzwa mitandaoni na kuamua kusema kuwa ikifika muda wa kuweka wazi atafanya hivyo kwani hakuna kitakacho mzuia.



Kupitia mtandao huo, Diamond ameandika:

Mara Diamond Kamla Huyu, mara sjui naskia anatembea na Huyu, Mara Ooh sjui inasemakana juzi alikuwa na Huyu…Yani kila Ukiamka limezuka jipya, Utazani yangu ina Sukari au Nakojoa dhahabu😏…..Hebu Niacheni kidogo, niko Busy nahangaika kuipeleka Bongo fleva yetu Duniani…. Sijamkaza yoyote, na Sina Mahusiano na Yoyote anaetajwa, na Siku pia Nikimaliza Mahusiano yangu na Alie South na nikawa na Mwengine na ikifikia kuliweka wazi ntaliweka wazi Mwenyewe, Maana hakuna kitachonizuia… ndio kwanza nna miaka 28, Sijaoa na Hata nikioa Naruhusiwa niwe na wake Wanne PERIOD!!!….