burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

17 Feb 2018

WILLY PAUL ATOA SABABU ZA KUMTUMIA LYNN WA KWETU KWENYE VIDEO YAKE MPYA


Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Wilson Abubakar Radido ‘Willy Paul’ ameachia kazi yake mpya chini ya lebo yake ya ‘Saldido Records’, iliyotayarishwa na Prodyuza Teddy B na ametoa sababu za kwanini amemtumia Mrembo na Video Vixen ‘Lynn’ kutoka Tanzania katika video ya wimbo huo.

Akipiga stori na g.lovetz Willy Paul amesema kuwa, siku zote kitu kikubwa anchozingatia katika kazi zake ni kufanya kazi nzuri na kubwa yenye viwango vya kupimwa kimataifa na moja ya sababu ya kumshirikisha Lynn kama video Queen kwenye video ya wimbo wake huo mpya ni ‘Urembo’ aliobairikiwa nao binti huyo.

“Asante sana kwa Support ninayopata kutoka kwa mashabiki na wadau wa music kwa huko Tz coz wana mchango wa mimi kufika hapa, on my new Project. I am very proud of Lynn wa kwetu kushiriki katika video yangu and what I can say about her ni mrembo na pia hiyo ni one of my reasons mimi kufanya naye kazi” Amesema Willy Paul.

Video ya wimbo huo iliongozwa na Director Hanscana kutoka Tanzania na imeshootiwa mjini Mombasa, Kenya.

NEW VIDEO | Bonge la nyau Ft. Beka Flavour - NAJIONA MBALI | Watch

NEW VIDEO | Linah Ft. Rachel - Same boy | Watch

New VIDEO: Willy Paul Msafi – Malingo

15 Feb 2018

Fid Q aeleza sababu ya kuweka wazi mahusiano yake kwa sasa


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ameeleza ni kwanini sasa hivi ameamua kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi tofauti na hapo awali.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Fresh’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kwa sasa amempata mtu ambaye wanaendana sawa kimtazamo hasa katika maongezi yao.

“Sikuwa na hiyo picha kwamba nakuja kuwa wa kwake, sema nilikuwa navutiwa na maongezi yake, yaani naongea na mtu ambaye anajua vitu vingi ambayo na mimi navijua,” amesema Fid Q.

“Unajua kuna vitu fulani unakuwa unaongea na watu, kuna watu wanakuwa wanakuona kama chizi na kuna mtu mwingine ikitokea unaongea naye na anakuelewa, labda vitu vya kisaikolojia na anakuelewa unaona inanoga, kwa hiyo hicho ndio kitu kilivutia zaidi,” ameongeza.

Rapper huyo ameongeza kuwa baada ya mazungumzo ya hapa na pale na mrembo huyo amegundua kuwa wapishana siku moja katika kuzaliwa (birthday), Fid Q amezaliwa, August 13 na mpenzie August 14.

New VIDEO: Juma Kakere – HAPPY


New VIDEO: Nyashinski – Bebi Bebi

Wabongo wampongeza Zari kwa maamuzi yake ya kuachana na Diamond

Picha inayohusiana
Baada ya Zari kutangaza rasmi kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mzazi mwenzie, Diamond Platnumz imeonekana hatua hiyo kupokelewa kwa mtazamo chanya na baadhi ya mashabiki wa Diamond Platnumz hususani wanawake.

Watu wengi ambao walikuwa wanawafuatilia wawili hao wameonekana wakitoa maoni ya kumpongeza kwa maamuzi aliyoyachukua ya kumuacha Diamond Platnumz.

Baadhi ya maoni ambayo yametolewa kwenye posti ya Zari kwenye mtandao wa Instagram, yamempongeza Zari kwa kumwambia kuwa yeye ni mwanamke jasiri na anayejitambua.

iam_golden_heartIt’s awise decision darling though it’s not easy. I salute you mum Tee
queen_godlistenAsante @zarithebossladyu have to be Your self cause hakuna namna ma dear and I appreciate Ur Opinions always
hamisi_wa_instarHongera sana @zarithebosslady umefanya maamuzi sahihi kabisa
selestina.makwega84😪😪😪Maamuzi magumu sana, MUNGU akutie nguvu.
karen.kamauyu r strong woman ever known.Love love love salute…
chivixhbMungu atakuongoza zaidi.mwache awe anavyotaka yy.
evelynnyamigishaI love your confidence and the fact that you don’t compromise with any piece of nonsense.. Go on boss lady, this life is too short to waste time on people who don’t know what they want @zarithebosslady
minacollection_znzNice strong women my dear wowow 😍❤ww nimwanamke unaye jiamini kila siku hivo ndo anavo takiwa mwanamke @zarithebosslady
Hata hivyo sio mashabiki wote wamempongeza Zari wapo baadhi yao wamemkosoa kwa maamuzi hayo kwa kumwambia kuwa amekurupuka na amefanya maamuzi kwa hasira.