Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
21 Des 2017
19 Nov 2017
15 Nov 2017
14 Nov 2017
Ndikumana afariki dunia ghafla baada ya mazoezi
Mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda na beki wa zamani wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla.
Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza kuwa Hamad Kataut kabla ya kufikwa na umauti alikuwa mazoezini jana asubuhi.
Katauti alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, enzi za uhai wake na aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus.
Ndikumana alikuja nchini siku ya Simba Day Agosti 8 mwaka huu akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kufungwa bao 1-0.
Mchezaji Ndikumana Hamad amewahi kuwa mume wa muigizaji filam maarufu nchini, Irene Uwoya.
10 Nov 2017
Bright awashangaa wanaomfananisha na Belle 9
Msanii wa Muziki Bongo Bright amesema kuna utofauti mkubwa kati yake na Belle 9.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ni Wewe’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wapo wanaowafanisha lakini kiuhalisia hawafanani na walishafanya hata ngoma pamoja ili mashabiki kuona utofauti wao.
“Hapana, mimi nimeingia studio kwa mara kwanza mwaka 2006 sidhani kama Belle 9 alikuwa amefahamika lakini kutokana amefahamika na mimi nimekuja kufahamika baadaye yeye ameshapata nafasi lazima mtu awe anaongea hivyo” amesema Bright.
Ameongeza kuwa kutokana na watu kuwafananisha ndio sababu ya kufanya kazi kwenye menejiment moja kipindi cha nyuma ambapo hata uongozi wao ulikuwa unawafanisha lakini kila mmoja ana kitu chake.
Kesi ya Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond Platnumz yafutwa na Mahakama
Dar es salaam, Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
2 Nov 2017
1 Nov 2017
Barakah The Prince alia kufanyiwa hujuma akose views YouTube
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Barakah The Prince amedai kuwa YouTube account yake inafanyiwa mchezo mchafu ili ishusha idadi ya views.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sometimes’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa views za ngoma yake hiyo zimekuwa zikishuka na kupanda na hata muda mwingine comment kufutwa.
“Kwa upande wa YouTube kuna mchezo mchafu unafanyika kwa sasa hivi, kwa mfano wimbo wangu kama jana ulikuwa ni namba saba kwenye trending ukiangalia video za watu wengine ni namba 40 lakini views wake ni milioni 4.4, nyingine inasoma namba 10 ukiangalia views zake ni laki 5.8 lakini mimi ambayo nina views elfu 20 ninasoma namba saba kwa nini iwe hivyo?” alihoji.
“Kuna mchezo mchafu unafanyika wa ku-block views wangu hata Mx kaniambia kuna mchezo mchafu unafanyika” ameongeza.
Amesema kuwa kuna baadhi ya nchini ikiwemo China mashabiki wake wamekuwa wakilalamika haiwapati video yake lakini video za wa wasanii wengine zinapatikana.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa watu wenye access ya kuendesha account yake hiyo ni Mx Carter na Seven Mosha wa RockStar4000 kutokana na makubaliano ya hapo awali, pia ameeleza kuwa yupo katika utaratibu wa kufuta account hiyo na kufungua nyingine.
Ngoma ya Barakah ‘Sometimes’ video yake ilitoka October 28 mwaka huu lakini hivi sasa haipatikani YouTube (imeondolewa).
Anachojivunia Feza Kessy kwa sasa
Msanii wa muziki Bongo na Mtangazaji wa Choice Fm, Feza Kessy amefunguka anachojivunia kwa sasa ni mafanikio yaliyofikiwa na ngoma yake ‘Kaa Kijanja’ ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili.
Muimbaji huyo amesema ngoma hiyo imeweza kumpeleka katika hatua nyingine kabisa ukilinganisha na hapo awali.
“Nafikiri imeniweka katika position nzuri kama female artist wa Tanzania, so I thanks my supporter, am very happy, am very great full kwa sababu imenitoa from one level to another, sasa hivi nipo kwenye level nzuri naweza kusema kwa sababu ya Kakaa Kijanja” amesema Feza.
Feza kwa sasa ametajwa kuwania tuzo za Afrima katika kipengele cha Best Female Artiste in Eastern Africa, tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 10 hadi 12 mwaka huu Lagos nchini Nigeria.
Nyomi la mashabiki la kwamisha mazoezi Al Ahly
Timu ya Al Ahly ya Misri hapo jana imeshindwa kufanya mazoezi katika makao makuu ya klabu hiyo huko Cairo baada ya mashabiki kujaa Uwanjani.
Mamia ya mashabiki waliingia Uwanjani kuitazama timu hiyo hali iliyosababisha wachezaji kushindwa kufanya mazoezi na hivyo kughairishwa.
Wamisri wanatazamia kuweka rekodi ya kutwaa kombe la Afrika mara ya tisa endapo wataifunga timu ya Wydad Casablanca siku ya Jumamosi huko Morocco.
Katika mchezo wa awali uliyofanyika Alexandria timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Ahly itahitaji kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wao wa nyumbani kabla ya kusafiri siku ya Jumatano kuifuata Wydad Casablanca huko Morocco.
Ahly wamekutana na klabu hiyo ya Afrika Kaskazini 2006 kwenye mechi ya CAF Super Cup.
Timu hizo zimekutana mara nne kwenye michuano hii awali. Wydad wakiing’ang’ania Ahly kwa sare ya 3-3 mnamo 2011 mjini Cairo na 1-1 mjini Casablanca na 2016 sare ya bila kufungana mjini Alexandria na hatimaye Ahly kushinda 1-0 Morocco, kabla kukutana tena na nakutoka sare ya 1-1 Alexandria mwaka huu.
Msimu huu timu zote zilikuwa kwenye kundi moja, kila moja ikishinda 2-0.
Al Ahly ambao wanatafuta ubingwa wa tisa, waliifunga Etoile du Sahel 7-2 nyumbani na ugenini kutinga fainali.
Licha ya kupata kipigo cha 2-1 Sousse, Mashetani Wekundu walibadilika katika ardhi ya nyumbani kwao Misri na kushinda 6-2. Walid Azaro akifunga hat-trick kwa timu hiyo ikiwa nyumbani.
Kwa upande wa Wydad, walishinda 3-1 mjini Casablanca baada ya sare waliyopata mjini Algers dhidi ya USM Alger, katika harakati zao za kutwaa ubingwa wa pili Ligi ya Mabingwa tangu waliposhinda 1992.
Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani milioni 2.5 na atapata tiketi kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa duniani mwezi Disemba falme za kiarabu.
Baada ya Jux, Vanessa Mdee atua kwa Cassper Nyovest
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee amezidi kuonyesha uwezo wake kwa upande wa ‘video queen’ mara baada ya kuonekana katika video ya rapper Cassper Nyovest kutoka nchini Afrika Kusini.
Hii si mara kwanza kwa Vanessa kufanya hivyo, utakumbuka January 2015 alitokea kwenye video ya Jux katika ngoma ‘Sisikii’, baada ya hapo waliweza kutoka ngoma ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu.
Hata hivyo kuna uwezekana mkubwa Cassper Nyovest akapita katika nyayo za Jux kwa kuja kuachia ngoma na Vanessa. Akizungumza na Dj Show ya Radio One Vanessa amesema kuna muendelezo wa kazi kati yake na rapper huyo.
“Ni project endelevu tumeanza kwanza na video yake ya ‘Baby Girl’ ambayo nimecheza, so next msubirie kidogo itakuja very soon” amesema Vanessa.
Sunderland yamtimua kazi kocha wake Simon Grayson
Meneja wa klabu ya Sunderland muingereza, Simon Grayson ameachishwa kazi baada ya kuihudumia timu hiyo katika michezo 18 pekee toka kuteuliwa kwake.
Grayson ametangazwa kuachishwa kazi dakika 17 tu kupita baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bolton Wanderersdraw.
Simon Grayson raia wa Uingereza alichukua mikoba ya David Moyes mwezi Juni wakati akitua Sunderland.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema “Sunderland AFC jioni ya leo kwa kushirikiana na meneja Simon Grayson, imeamua kuachana nae na kumpatia shukrani yeye na benchi lake la ufundi kwa jitihada zao kubwa walizofanya katika klabu hii.” Imesema taarifa kutoka Sunderland.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu toka akabidhiwe nafasi hiyo.
Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Glynn Snodin alishaondoka bila klabu hiyo kutoa maelezo ya nani atarithi nafasi yake wakati ikikabiliwa na mchezo wa derby siku ya Jumapili dhidi ya Middlesbrough.
Baada ya mapenzi kung’oa warembo MJ Records, Idris na Wema watajwa
Wakati mjadala ukiendelea baada ya wasanii wawili wa kike, Haitham Kim na Nini kutimuliwa katika label ya MJ Records na producer Daxo Chali, suala hilo limechukua sura mpya mara baada ya Idris Sultan na Wema Sepetu kutajwa.
Taarifa za awali zilieleza kuwa kutimuliwa kwa wasanii wao ni kutokana na mmoja wapo kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Nay wa Mitego kitu ambacho kilidaiwa kinaweza kuchafua brand ya label hiyo.
Hata hivyo Haitham Kim amefunguka mambo mengine kwa kile kilichokuwa kikidaiwa anatoka kimapenzi na Idris kitu kilichopelekea pia kutimuliwa MJ Records. Akizungumza na E-Newz ya EATV Haitham amesema jambo hilo halina ukweli wowote bali ni watu tu wanazusha.
“Ni watu tu wametengeneza kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya Haitham na Idris kwa sababu ukiangalia Wema pia ni mtu ambaye hakusapoti hiyo kazi ya Play Boy, so watu wanaendelea kujiuliza kwanini Wema hakusapoti, hivyo sababu inaweza kuwa ni hiyo lakini yule siyo sababu” amesema.
“Mimi nina mpenzi wangu na Idris ana maisha yake, so siwezi kumuingiza Idris kwenye maisha yangu ya mahusiano kwa sababu I have a boy friend, nishamposti hata kwenye social media fans wangu wanamjua” Haitham ameongeza.
Chini ya MJ Records Haitham ameweza kutoa ngoma mbili official, ya kwanza ikiwa ni ‘Fulani’ aliyomshirikisha Mwana FA na Play Boy ambayo sauti ya Wema Sepetu inasikika ndani yake.
31 Okt 2017
WhatsApp yaruhusu kufuta ujumbe/picha kwa mtu uliyemtumia kimakosa
Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo.
WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa.
Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia.
Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart ndani ya mwaka huu.
Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makubwa manne ndani ya mwaka huu ambayo yataifanya programu ya WhatsApp kuwa ya kisasa zaidi.
Twambie wewe mtumiaji wa programu pendwa ya WhatsApp umeyapokeaji mabadiliko haya.
29 Okt 2017
Ruby ajibu kuhusu kolabo na Yemi Alade
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amefunguka kuhusu tetesi za ujio wa kolabo yake na msanii wa Nigeria, Yemi Alade.
Muimbaji huyo ameeleza kuwa hawezi kuweka sana hilo wazi kwani mipango yake sasa ni kuvunja ukimya wake kwa upande nyumbani.
“Siwezi nikasema tayari kila kitu kimemalizika lakini vitu vipo, sitaki kusema kabisa kwenye kolabo za kimataifa natamani iwa surprise kwa sababu nimekaa muda mrefu kimya I need talk about home kwanza” amesema Ruby.
25 Okt 2017
Darassa kuamsha dude la kufungia mwaka
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Darassa amezungumzia ujio wake mpya.
Rapper huyo ambaye mara mwisho alisikika na ngoma ‘Hasara Roho’ ameiambia Dj Show ya Radio One yupo katika maandalizi ya kufanya hivyo ila kwa sasa asingependa kulizungumzia sana kwani yeye siku zote siyo muongeaji zaidi ya kazi.
“Kwenye single mpya watu wananijua mimi siyo mtu wa kuongea ongea kama sina kitu cha kuongea mara nyingi huwa nakuja kuongea nikiwa na kitu, kwa sasa naandaa project ambazo naamini nitakuja kufunga nazo mwaka watu wakae tayari tunakuja tuko poa kabisa” amesema Darassa.
Mwishoni mwa mwaka jana Darassa alifunga mwaka na ngoma Muziki ambayo alimshirikisha Ben Pol ambayo inatajwa kuwa ndio ngoma pekee kuwa hit ya kutisha kutoka kipindi hicho hadi mwaka huu.
23 Okt 2017
Yamoto Band Imeshakufa Kila Msanii Anasimama Kivyake - Beka Flavour
Msanii wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa hayupo tayari kurudi kwenye kundi la Yamoto Band na kudai ukweli ni kwamba kundi hili lilishakufa na kila msanii sasa anasimama kivyake.
Beka alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa wakati wanaondoka kwenye kundi hilo hawakuwa na pesa zozote zile kwani enzi zao wakati wanafanya show mbalimbali walikuwa wanapewa fedha za matumizi tu na wao walipendekeza kwa uongozi fedha zinapopatikana wafanyiwe mambo kadhaa ikiwa pamoja na kujengewe nyumba.
"Mimi saizi ukisema nitoke kwenye uongozi wangu mpya nirudi Yamoto Band sidhani kama itawezekana unajua watu hawajui tu lile kundi ndiyo limeshakufa kwa sababu saizi kila msanii yupo na uongozi wake, sidhani kama wanaweza kukubaliana watoke walipo na kurudi kule" alisema Beka Flavour
Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi kuwa anafurahi kuona Aslay msanii ambaye alikuwa naye kwenye kundi moja na yeye saizi anakuwa ni kati ya wasanii wanaozungumziwa sana kwa kazi nzuri.
"Mimi nazidi kumuombea kwani mwenzangu saizi amekuwa ni kati ya wasanii ambao
wanazungumziwa sana kutokana na kazi zake, lakini napenda kuwaambia Watanzania kuwa wasanii ambao tulikuwa tunaunda kundi la Yamoto Band Mungu alitupa kitu ndani yetu hivyo muda si mrefu mtakuja kuona haya nayosema kwani kila mmoja ana upekee wake katika kazi zake" alisisitiza Beka
Birdman Kutua Tanzania
Mmiliki wa lebo ya Cash Money, Birdman amethibitisha mpango wake wa kutua nchini mapema mwakani ikiwa ni sehemu ya ziara kwenye nchi tano za Afrika.
Rapa huyo wa Marekani, mapema wiki hii ameandika katika akaunti yake ya Instagram kuwa atafanya ziara licha ya kutoeleza ni kwa ajili ya muziki au la!
Mkongwe huyo wa Hip Hop amesifu upendo na mapokezi makubwa wanayopata kutoka nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.
Mbali na Tanzania amezitaja nchi nne ikiwamo Nigeria, Gambia, Ghana na Kenya na kuandika “Nitatembelea kwenye nchi hizi kuanzia Februari.
Birdman ameingia katika mzozo na rapa, Lil Wayne ambaye amekuwa akimtuhumu bosi huyo kuchelewesha kutoa albamu yake “Tha Carter V”.
Bifu hilo limeendelea kuwa kubwa huku baadhi ya mastaa akiwamo Rick Ross kumtaka Birdman amlipe fedha Lil Wayne licha ya meneja huyo kuwa mbogo.
Msanii wa TZ Anayelipwa Kenya na Mtandao Milioni 20 Kwa Siku
Mtangazaji maarufu wa Classic 105 ya nchini Kenya, Maina Kageni amefunguka kwa kusema kuwa kuna msanii mmoja wa Tanzania analipwa na mtandao wa simu milioni 20 kwa siku kutokana na nyimbo zake.
Mtangazaji huyo amedai hawezi kumtaja msanii huyo lakini alibainisha ni kati ya Alikiba na Diamond. Alisema hakuna msanii mwingine wa Kenya au Tanzania anayelipwa pesa nyingi kama hizo kwa siku.
Irene Uwoya Afunguka na Kusema "Naombeni Mniache"
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya ambaye ndoa yake na mchezaji mpira Ndikumana Katauti wa Rwanda iliingia katika mgogoro mzito na kupelekea kila mtu kuishi peke yake amefunguka na kuwataka watu wasimuingilie katika malezi ya mtoto wake.
Irene Uwoya ambaye alibahatika kupata mtoto mmoja na mume wake huyo kabla ya migogoro yao, ameonyesha kukasirishwa na maneno ya baadhi ya watu kusema kuwa anamlea mtoto wake huyo kizembe zembe huku wengine wakienda mbali na kumtabiria mambo mtoto huyo kutokana na makuzi yake, ndipo hapo Uwoya alipocharuka na kuwataka wasimuombee mambo ya ajabu mtoto wake.
"Wale mnaosema namlea kizembe naombeni sana mniache, namlea navyoweza mimi na mwanangu bado mdogo sana anahitaji mapenzi ya Mama. Hakuna hata mmoja wenu amewahi kuchangia ata mia ...sipendi kuongea sababu siyo swaga zangu, mimi mpole sana ila kwa mwanangu sina masihara. Sijawahi sema kitu ila leo nimeona niseme na sitarudia tena kusema, mwenye maskio na asikie na mwenye macho aoneee! yale mambo ya laaana mnayo mtabiria mwanangu yashindwe na MUNGU awasamehe sababu hamjui mlitendalo" alisisitiza Irene Uwoya.
22 Okt 2017
21 Okt 2017
E. Mbasha atupa shutuma nzito kwa Flora, ‘anachokifanya siyo kizuri’
Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amemshutumu mzazi mwenzie, Madam Flora kwa kumzuia kuonana na mtoto wake.
Wawili hao ambao wote ni waimbaji ndoa yao ilishavunjika na Madam Flora kuolewa. Akizungumza na TBC Fm amedai kitu anachokifanya siyo kizuri na amekuwa akifanya jitihada za kuonana mwanaye ila imeshindikana.
“Kiukweli mtoto sijaonana naye muda, yeye mwenyewe hajataka kunipa mimi mtoto, nimeshafanya jitihada na anajua na hata kama sasa hivi anasikia anajua mtoto ameninyima na kitu anachokifanya siyo kizuri kwa mtoto” amesema Mbasha.
“Ni muda mrefu, mara mwisho nimeona naye (mtoto) mahakamani, muda mrefu kipindi wanakaribia kufunga harusi. Inaniumiza sana ni mtoto wa kipekee, ni mtoto ambaye nampenda na nimeishi naye kipindi chote tangu mdogo”
20 Okt 2017
19 Okt 2017
Alikiba, Diamond, Nay, Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini wachanwa na Rayvanny
Ngoma hiyo ambayo Rayvanny amerap, baadhi ya wasanii waliopitiwa na punch line zake ni Diamond, Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz, Young Dee, Shilole, Joh Makini Juma Nature na wengineo kibao. Hapa chini ni baadhi lines hizo.
Ila Juma Nature muda mwingi yupo tungi, Alikiba wa Kariakoo yeye ni shisha na Mirungi/
Diamond akiongea kidogo katukana, Love Boy hupenda wasichana/
Ommy Dimpoz kwa vijembe huyo bwana hachoki, dogo mtoboa siri ni Young Killer Msodoki/
Ukikutana na FA kama hakujui haongei, yuko bize na simu kama Bongo Movie Ray/
Nay wa Mitego yeye ni bifu na kuchonga, utasikia yule mtoto bishoo nitamgonga/
Wanao-act kishua Gosby na Young Dee, wasiogopa wajua mengi Kimbunga na Nash Mc/
Shilole, Shishi mitusi kwa mkupuo, sijui stajini ana sweat maana sizioni nguo/
Nikki wa Pili ha-act kiki-crazy, ila kaka yake Joh anamkopi Jay Z/
Unaweza kuisikiliza ngoma hiyo hapa: TABIA
Hii ni ngoma ya pili Rayvanny kuitoa akirap chini ya WCB baada ya ile ‘Sugu’ ambayo alirudia chorus ya ngoma ya Mr II ‘Sugu’.
Harmonize achekelea support ya Wolper
Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulala’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anafurahi kuona anapata support ya Wolper katika muziki wake.
“Nadhani mwanzo ilikuwa hasira tu, nashukuru kuona support ya Wolper, namchukulia kama shabiki yangu tu” amesema Harmonize.
Hiyo juzi katika mtandao wa Instagram Jacqueline Wolper aliposti video mbili zikimuonyesha akifurahia kusikiliza ngoma hiyo ambayo Harmonize amemshirikisha Korede Bello.
AY aupa kisogo muziki?, afungua bucha la nyama
Picha hii hapa juu inaonesha mazingira ya bucha hilo ambayo hadi sasa bado hatujajua inapatikana maeneo gani. Mkali huyo wa Bongo Fleva ameonekana kuimudu vyema kazi yake mpya na anaifurahia, tunamtafuta AY kwa mahojiano zaidi na tutayaleta kwako ili kufahamu zaidi kazi hii mpya aliyoamua kuifanya.
Je ni kweli maprodyuza wapya Bongo ni beat maker? Lamar ajibu
Producer ametoa ufafanuzi kauli kuwa baadhi ya prodyuza wa sasa ni beat maker tu.
“Yeah ni kweli beat maker wapo unajua kipindi cha nyuma watu walikuwa wana hustler kusoma zile fundamental za muziki, theory na practical watu wanaenda online wanaangalia jinsi ya kufanya vitu wanaenda shule, unakuta watu pia wana certificate za chuo” Lamar ameambia G.LOVETZ.
“Lakini sasa hivi mtu akiwa na laptop na yeye anatengeneza beat anasema ni prodyuza wakati kumix hawezi, kufanya mastering hawezi katika kiwango kile ambacho kinatakiwa” amesema.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika media hamna kitu ambacho kinaweza kuchuja muziki ukoje ile kupata kitu kizuri hali ambayo inapelekea uwepo wa muziki ambao siyo.
11 Okt 2017
Dogo Janja Amzimia Vanessa Mdee
Mkali wa Ngoma ya Ngarenaro, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, amefunguka kuwa hakuna mwanamuziki wa kike Bongo anayemzimia kama Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kutokana na swagga zake.
Dogo Janja ambaye amekuwa akihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Uwoya madai ambayo ameyakana na kudai yeye ana mwanamke wake ambaye hayupo kabisa kwenye sanaa aliongeza kuwa, Vee humkosha zaidi na wakati mwingine anatamani mastaa wa kike Bongo wangekuwa wanavaa kama yeye.
“Kiukweli huwa nazimia sana swagga za Vee Money, anajua kupendeza na kuna wakati huwa natamani mastaa wa kike wote wavae na kutupia pamba kama yeye,” alisema Dogo Janja.
Diamond na Rick Ross waingia location kuandaa kitu kipya
Msanii wa muziki nchini ambaye anafanya vizuri kimatiafa, Diamond Platnumz Jumanne hii ameingia location kwaajili ya maandalizi ya kazi mpya akiwa na msanii mkubwa wa Hip Hip kutoka Marekani, Rick Ross.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Hallelujah ameonekana katika video na picha wakishoot Kazi hiyo ambayo haijajulikana ni kazi na namna gani.
Meneja wa kimataifa wa muimbaji huyo, Sallam amethibitisha kwamba wawili hao wameingia location kwaajili ya maandalizi ya Kazi hiyo.
“Diamond Platnumz x Rick Ross On set now somewhere in Miami #BlackBottleBoys and we never stop!!,” aliandika Instagram Sallam.
Rick Ross na Diamond wote ni mabalozi wa kinywaji cha Belaire ndio maana wanajiita BlackBottleBoys.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)