Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
26 Apr 2017
RAY KIGOSI ACHOSHWA NA WATANZANIA; AMFANANISHA KANUMBA NA DIAMOND PLATNUMZ
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Ray ameamua kuwachana watanzania ambao hawana jambo la kufanya zaidi ya kuwakatisha tamaa wale watu wanaojituma kwenye kazi zao badala ya kuwafariji na kuwashauri .
Ray akitolea mfano wa Marehemu Steven Kanumba na Diamond Platnumz amesema awali Kanumba alishawahi kukatishwa tamaa na watanzania kwa kuambiwa kuwa ni Freemanson na wengine kumtabiria kuwa hatafika mbali kwenye sanaa yake lakini leo anashangaa wale wale watanzania waliokuwa wanamponda ndiyo hao wanaomsifia leo kuwa haitatokea muigizaji mkali kama Kanumba.
“1.Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza !!,2.Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba !,3.Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho,and alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba”.Ameandika Ray Vicent Kigosi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Ray aliendelea kutoa mifano na kwenda mbali zaidi zaidi kwa kumfananisha Kanumba na Diamond Platnumz kwa kusema hata Diamond pia kuna kipindi baadhi ya watanzania na waandishi wa habari walikuwa wanamwambia ni Freemanson hata mganga wao wanamjua na ilifikia pahala walimtabiria kuwa atadondoka kwenye muziki lakini yeye hakujali aliendelea kupiga kazi na tumeona kila kukicha anazidi kupanda juu.
“Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema .
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.”Aliendelea kuandika kwa kusema
“Kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwasababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.“Ameandika Ray kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Amemaliza kwa kusema watanzania tuwe wepesi wa kuvipa vitu vyetu dhamani kwanza hata japo kidogo kwani leo hii kanumba aliyekuwa anaonekana hajui Kiingereza na Filamu zake mbovu leo inaonekana filamu zake ni bora sana wakati walimbeza hao hao watanzania.
“Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao
Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nyeupe !!
Tukosoe penye tija na tutoe appreciation“Amemaliza kwa kuandika hivyo.
STEVE NYERERE AWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE NA WEMA SEPETU KWA SASA
Muigizaji na Mchekeshaji maarufu kutoka Tanzania Steve Nyerere amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na Wema Sepetu hawana tatizo lolote na kudai yule ni dada yake hivyo wanaheshimiana na kuendelea kuishi kama zamani licha ya Wema Sepetu kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Steve Nyerere ni kweli kulikuwa na matatizo hapo nyuma lakini matatizo hayo siyo sababu wao kuharibu undugu wao na urafiki wao, hivyo ule ulikuwa ni upepo na umepita kwa sasa wanaendelea kuishi kama zamani.
“Mimi ni niwe muwazi tu,Wema hawezi kuwa adui yangu Wema ni rafiki yangu, Wema ni ndugu yangu hivyo yeye kuhama chama na kuhamia CHADEMA si kubadilisha urafiki, na kuhusu matatizo na Mama Wema yule ni mama yangu kwa hiyo yaliyopita si ndwele tugange yajayo, mimi na wewe ni ndugu yangu kabisa na tumeshakutana mara kwa mara baada ya yale kutokea na maisha yanaendelea. Wema na mama yake ni ndugu zangu wale siwezi kuwatupa sijakosana na mtu Wema ni dada yangu, rafiki yangu kipenzi na mama ni mama yangu mzazi yale yalipita ule ni upepo tu” Alisema Steve Nyerere kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.
Nay amtambulisha msanii wa kwanza wa label yake
Label ya ‘Free Nation 966’ ya rapa Nay wa Mitego imemtambulisha msanii wake wa kwanza aitwae ‘B Gway’.
Rapa huyo amedai huyo ni msanii wake wa kwanza wa kurap kwani siku chache zijazo atamtambulisha msanii wake wa kuimba.
Nay amedai msanii huyo ataachia wimbo wake wa kwanza uitwao ‘Sijachukia’ ambao umetayarishwa na Yogo Beat.
“Leo label yangu ya ‘Free Nation 966’ imemtambulisha kijana wake wa kwanza ‘B Gway’,” alisema Nay. “Ni msanii mkali sana, sikutaka kumchukua msanii ambaye anatanisumbua, tena wimbo wake wa kwanza ‘Sijachukua’ amenishirikisha,”
Aliongeza, “Kwahiyo ningependa kuwaambia mashabiki wasubirie mambo mazuri kutoka ‘Free Nation 966’. Pia siku chache zijazo tutamtangaza msanii mwingine wa kuimba,”
Wimbo wa msanii huyo kuachiwa Jumatano hii kupitia redio na runinga pamoja na mitandaoni.
Beyonce kuwasomesha wanafunzi wa kike
Beyonce ameamua kuanzisha “Formation Scholars,” ambayo itasaidia kuwalipia ada wasichana,kwa ajili ya kupata elimu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hilo limewekwa wazi na muimbaji huyo katika kusherekea mwaka mmoja tangu alipoachia albamu yake ya ‘Lemonade’. Kupitia tovuti yake Queen Bey amethibitisha kwa kuandika, “To add to the celebration of the one-year anniversary of LEMONADE, BeyoncĂ© Knowles-Carter announces the establishment of Formation Scholars awards for the 2017-2018 academic year, to encourage and support young women who are unafraid to think outside the box and are bold, creative, conscious and confident.”
“Four scholarships will be awarded, one per college, to female incoming, current or graduate students pursuing studies in creative arts, music, literature or African-American studies. The schools selected for participation are Berklee College of Music, Howard University, Parsons School of Design and Spelman College. All details and application deadlines are available directly from the colleges,” ameongeza.
Wakati huo huo mapema mwaka huu, Beyonce alitajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 256 kupitia ziara yake ya Formation iliyoanza April 27 na kumalizika Oct. 7, huku akiwa ameuza tiketi zaidi ya milioni 2.2.
Antonio Conte wa Chelsea amekiri kikosi chake kimekutana na magumu.
Meneja wa klabu ya Chelsea,Antonio Conte, amekiri michezo miwili waliocheza siku za hivi karibuni yamekua michezo migumu kwa upande wao na imekua muhimu kuhakikisha wanapata alama tatu zitakazowasaidia kujikuta kileleni mwa ligi hiyo ya Epl.
Conte ambaye ni raia wa Italia, amewasifia wachezaji wake kwa kupambana hadi kuhakikisha wanachomoza na ushindi huo Mnono wa magoli 4 kwa 2 mbele ya kikosi cha Southampton, na anaamini kuwa wachezaji wake watapambana na kuhakikisha wana nyakua Ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwa Msimu huu.
Meneja huyo mwenye Mizuka pindi timu yake inapopata ushindi, amesema kuwa anahitaji kukipumzisha kikosi chake baada ya Michezo hiyo migumu waliokutana nayo wiki hii.
Aliyekuwa Mwiba katika mchezo huo uliopigwa hapo jana ni nyota wa timu, Eden Hazard aliyeanza kuiandikia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 5 ya mchezo. Katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, beki Gary Cahill alifunga bao la pili.
Katika kipindi cha pili mshambuliaji mahiri wa Chelsea, Diego Costa aliongeza mabao mawili, huku mabao ya Southampton yalifungwa na kiungo Oriol Romeu na beki Ryan Bertrand.
The Blues wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 78 wakiwa wamecheza michezo 33 huku Tottenham ikiwa katika nafasi ya pili kwa alama 71 wakiwa nyuma ya Chelsea kwa mchezo mmoja.
Majogoo wa London, klabu ya Liverpool, inashikilia nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 66 huku matajiri wa Uingereza Manchester City, wakishikilia nafasi ya 4 wakiwa na alama zao 64 nyuma ya klanbu ya Mashetani wekundu Manchester United inayoshikilia nafasi ya 5 na alama zao 63 wakiwa nyuma kwa alama 1 dhidi ya City.
Sijui chochote kuhusu kuibiwa kwa nyimbo ya ‘Show Me’ – Ray C
Wiki iliyopita, kuliibuka mazito kuhusu wimbo wa Harmonize ft Rich Mavko uitwao ‘Show Me’. Wimbo huo unadaiwa kuibiwa kutoka kwa msanii PCK anayeishi Uingereza, huku Ray C akitajwa kama shahidi namba moja, kwa kuwa alikuwepo studio wakati msanii huyo chipukizi anarekodi.
Baada ya kupata maneno kutoka kwa Hamonize na mtayarishaji wa ngoma hiyo kutoka Wasafi Records, Laizer, sasa G.LOVETZ imefanikiwa kuongea na Ray C kuhus sakata hilo.
Ray C amegoma kuongelea lolote kuhusu hicho kinachoendelea kwa kusema, “Aisee siwezi kuongea hizo vitu hazinihusu mimi, simjui.”
Katika mahojiano tuliyofanya na Harmonize alikataa kuzungumzia hilo kwa madai kuwa mambo hayo tayari yapo chini ya uongozi wao wa WCB, lakini Laizer alidai kuwa hamfahamu msanii huyo na wala hajawahi kusikia jina kama hilo na kuongeza kuwa, kama aliwahi kurekodi katika studio zao basi lazima atakuwa amepewa risiti kwa hiyo anaweza kuionyesha kama ni kweli.
Ujio wa Tumbo bandia kuwasaidia watoto Njiti duniani
Wanasayansi kutokea nchini Marekani hatimaye wamebuni tumbo bandia, ambalo linategemewa kuja kutumika kuhifadhia watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (Njiti).
Watafiti katika hospitali ya watoto mjini Philadephia, wanasema kuwa lengo lao ni kuweka mazingira salama kwa watoto wanaozaliwa kabla muda wao kutimia.
Kifaa hicho maalumi chenye muonekano wa tumbo kimejaribiwa kwa kubebea mimba ya kondoo. Kitatumiaka kubebea Njiti iliwanaweza kukuza viungo vyao vya mwilini kama vile mapafu na viungo vyengine.
Wanasayansi wanaamini mfuko huo ama tumbo hilo bandia linaweza kua tayari kwa majaribio ya binadamu kuanzia miaka mitatu mpaka mitano kuanzia sasa. Kifaa hicho kimetengezwa na wanasayansi kwa kutumia mifuko ya plastiki
Takwimu za shirika la afya dunaini zinaonyesha wastani wa watoto milioni 15 huzaliwa njiti ulimwenguni kote.
Kuzaliwa kabla ya muda ni tatizo linalochangia na kusababisha vifo vya watoto wachanga na inakadiriwa kufikia asilimia 27 ya vifo hivyo kwa Tanzania. Vifo hivyo husababishwa na kuzaliwa njiti, magonjwa ya vimelea vya bakteria, matatizo ya kupumua na kuvuja damu.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imekuwa mfano katika kutekeleza mpango wa kangaroo wa kusaidia watoto wanaozaliwa njiti.
Tottenham haitauza wachezaji -Mauricio Pochettino
Meneja wa klabu ya Tottenham hotspurs, Mauricio Pochettino, amesema, klabu yake kamwe haitauza wachezaji wake tegemezi katika kipindi hiki cha majira ya Joto na badala yake watakaouzwa ni wale watakaoonekana hawana umuhimu ndani ya klabu hiyo.
Kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza nyuma ya klabu ya Chelsea inaahidi kulinda wachezaji wake wasije wakachukuliwa na klabu nyingine zilizoanza kunyemelea katika kikosi hiko.
Pochettino amesema kua ana mahusiano mazuri na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy ambae amemuhakikishia klabu hiyo haitauza wachezaji wake na kamwe haina haja na fedha, na kuongeza, wachezaji wao watasalia ndani ya klabu amesema.
Beki wa kikosi hiko, Kyle Walker na Danny Rose pamoja na viungo wa kati Christian Eriksen na Dele Alli ni miongoni mwa wachezaji wanaosemekana kukikacha kikosi hiko cha White Hart Lane, suala ambalo liawaumiza vichwa uongozi wa klabu hiyo.
Meneja huyo amesema kua ,wanadhani kuwa wanafanya mambo mazuri na ndio sababu klabu nyingi zenye uwezo zinawatolea macho wachezaji wao wenye vipaji vikubwa.
Billnass aeleza wakati wake mgumu katika muziki
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Billnass amefunguka kwa kudai kuwa siku mbaya katika maisha yake ya muziki ni siku ambayo anaachia wimbo mpya.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mazoea’ akiwa amemshirikisha Mwana FA, ameiambia G.LOVETZ kuwa siku hiyo huwa na wasiwasi juu ya kile anachokipeleka kwa mashabiki wake.
“Siku ambayo huwa inanisumbua ni siku ambayo naachia wimbo mpya na ni siku moja tu,” alisema Billnass. “Huwa nakuwa na wasiwasi kuhusu kazi yangu mpya lakini baada ya muda tu hali inabadilika na pia hali hii inanikuta katika nyimbo zangu nyingi,”
Rapa huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Posta, amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa kazi zake mpya.
Ray C Foundation imewekwa pembeni – Ray C
Muimbaji Rehema Chalamila aka Ray C amedai taasisi yake ya kupambana na dawa za kulevya ‘Ray C Foundation’ ameamua kuiweka pembeni kwa muda ili afanye kwanza muziki.
Miaka miwili iliyopita muimbaji huyo aliianzisha foundation hiyo, kwaajili ya kuwasaidaia watu walioathirika na dawa za kulevya baada ya yeye mwenyewe kusaidiwa na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii kuhusu taasisi hiyo, Ray C amedai kwa sasa ameamua kujikita kwanza kwenye muziki ili kuijenga upya brand yake.
“Foundation kwa sasa nimeamua niiweke pembeni kidogo kwa sasa kwa sababu siwezi kushika mambo mawili kwa sasa. Sasa hivi nataka nguvu yangu kubwa niiweke kwenye kazi, kazi yangu ambayo iko kwenye damu kwa sababu muziki ni maisha yangu,” alisema Ray C.
Muimbaji huyo amedai mambo yake ya muziki yakikaa sawa ndipo atakaporudi kuanza kufanya vitu vingine.
Siasa ni chanzo cha Bongo Movie kusambaratika – Steve Nyerere
Msanii wa filamu nchini, Steve Nyerere ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, amedai kitendo cha waigizaji kujiingiza kwenye siasa ni chanzo cha tasnia ya filamu nchini kupoteza mvuto.
Amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu kufanyika maandamano ya baadhi ya wasanii wa filamu kuishinikiza serikali kuwaondolea kodi katika filamu zao au kuhakikisha inakusanya pia kodi za filamu za nje ambazo zinakuwa zinapakuliwa katika mitandao kitu kinachopelekea kuua soko la ndani la filamu za Bongo.
“Mimi naomba niongee ukweli leo, kilichotuawa Bongo Movie ni siasa. Kipindi tupo kwenye uchaguzi mkuu kulikuwa na makundi mawili ya siasa ambayo yalikuwa yanawasapoti wagombea tofauti ndani ya tasnia ya filamu,” Steve Nyerere alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Aliongeza, “Lakini cha kushangaza uchaguzi tumeumaliza vizuri ila badala ya kuendelea na kazi zetu za uzalishaji wa filamu bado tunaendeleza kazi za watu ambazo hatuna hata utaalamu nazo,”
Pamoja na hayo Steve Nyerere ameongeza wapo wasanii wa filamu ambao wameweza kutenganisha siasa na filamu na kwamba hao ni wale ambao wamebahatika kuvaa kofia hizo mbili ndio maana wametumia busara zao kutotumika kwenye maandano ya watu wachache.
“Unajua pamoja na siasa kuna watu pale Bongo Movie wana kofia mbili mbili mfano mimi niliwahi kugombea Ubunge wa Kinondoni kwa hiyo lazima najua nini nafanya, Irene Uwoya ni Mbunge pale na anayo nafasi yake ndani ya chama ikitokea bahati mbaya mbunge wa viti maalumu akaanguka yeye ndiye atakayeziba pengo au Wema Sepetu na harakati aliozonazo sasa hivi na ndio maana hata ukiangalia kwenye maandamano watu waliyoyafanya wao walikaa pembeni siyo kwamba siyo wasanii , hapana ni wasanii ambao wamejitambua na hawataki kutumika kwa maslahi ya watu wachache,” Steve alifafanua.
Ray C afunguka ujio wa albamu na jinsi Diamond alivyoamua kumbeba
Msanii mkongwe wa muziki, Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kuhusu ujio wake mpya baada ya misukosuko ya maisha pamoja na ishu ya kusaini, Wasafi.Com ya Diamond Platnumz.
Muimbaji huyo ambaye ana mashabiki wengi amepambana kwa muda mrefu kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii akiwa mwenye siha njema na muonekano wa kuvutia, Ray C amedai kwa sasa amerudi upya kwenye muziki akiwa amejipanga na kazi nyingi pamoja albamu mpya.
“Kazi nimeanza upya natengeneza albamu, mpaka sasa hivi na nyimbo kama kumi,” alisema Ray C. “Nimependa kwa sababu nimekaa muda mrefu kimya bila kutoa kazi yoyote kwahiyo hiyo ni kama zawadi kwa mashabiki wangu. Lakini pia tumeanza na wimbo ‘Unanimaliza’ na umepokelewa vizuri sana na mashabiki na kuna mambo ya video yanakuja yaani ni back to back huu mwaka ni kwaajili kazi,”
Muimbaji huyo alisema amesaini mkataba mpya na Wasafi.Com kwaajili ya kumsambazia kazi zake mpya za muziki.
“Kuhumu ukaribu wangu na Diamond ni kwa sababu tuna mahusiano ya kikazi. Wasafi.Com iko chini ya Diamond na ni kampuni kwahiyo mimi kazi zangu zote zitakuwa zinauzwa kupitia kampuni hiyo. Nipo chini ya Wasafi.Com siyo WCB ingawa Wasafi.Com ndio Wasafi WCB. kwahiyo kazi zangu zote zitakuwa zinauzwa kupitia Wasafi.Com.
Dj Khaled aongeza nguvu kwenye albamu yake mpya
Dj Khaled amezidi kuipa nguvu albamu yake mpya ‘Grateful’.
Rapper huyo ameamua kuwaongeza mastaa wengine wawili, katika albamu hiyo, wakiwemo muimbaji Rihanna na Rapper Nas. Khaled amesema hayo mjini Los Angeles, katika Power 106 ambapo kwa msanii Rihanna, itakuwa mara yake ya kwanza kushirikishwa na DJ Khaled katika nyimbo, huku Nas akiwa tayari alishasikika katika albamu yake iliyopita ya ‘Major Keys’.
Mastaa hao wataungana na wasanii wengine katika albam hiyo ya ‘Grateful’ wakiwemo Chance The Rapper, Travis Scott, Mariah Carey, Bryson Tiller, Future, Alicia Keys, Lil Wayne, Justin Bieber na wengine.
Wakati huo huo Jay Z na BeyoncĂ© ni sauti nyingine zitakazo sikika kwenye albamu hiyo ambapo tayari walishirikishwa kwenye wimbo wa ‘Shinning’ uliotoka mwezi Februari mwaka huu, ambao nao utakuwemo kwenye albamu hiyo.
Naanza muziki upya na Spidoch Band – Beka
Msanii wa muziki, Beka Ibrozama, ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Tumaini’, amejipanga na ujio wa bendi yake mpya iitwayo ‘Spidoch Band’.
Muimbaji huyo alikuwa kimya kwa kipindi cha miaka 3 akiandaa bendi yake hiyo, ambayo itazinduliwa Aprili 29 katika ukumbi wa Next Door, Masaki Jijini Dar es salaam.
Akiongea na G.LOVETZ kuhusu ujio huo, Beka amedai alipokuwa nje ya muziki alipata nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitaboresha style ya muziki wake.
“ Mimi Beka nimerudi upya kwenye muziki,tena kwa miguu miwili. Nimejifunza vingi, na kubwa zaidi ni ujio wa bendi yangu mpya, ambayo nitaizindua hivi karibuni. Ni bendi ya muziki ambayo inaendana na hadhi ya kimataifa kwa hiyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya muziki mzuri,” alisema Beka.
Beka amesema alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda wake wote kwaajili ya kuandaa bendi yake na kwa sasa amerudi rasmi na kilichobaki ni mashabiki zake wasubiri kupata mziki mzuri kutoka kwake.
Wafahamu viumbe wanaopatikana nje ya sayari yetu
Wataalamu wa masuala ya sayansi wanaotafuta maisha nje ya sayari hii, katika anga za juu watahitajika kusubiri zaidi, kwani kuna dalili ya uwepo wa viumbe katika anga za juu wajulikanao kama Aliens.
Mradi wa kutafuta viumbe hao una gharama za zaidi ya dola milioni 100, lakini bado mpaka sasa bado haujapata chochote tangu uzinduliwe,mwaka mmoja uliopita. Shughuli ya kutafuta viumbe hao wa ajabu zinafanywa kwa kutumia darubini kubwa zaidi ambayo inasikiliza dalili yoyote ya kuwepo kwa viumbe aina ya ‘Aliens’ na wengineo.
Darubini hiyo iliyopo West Virginia, Marekani, ni moja ya darubini zenye nguvu zaidi duniani, zenye uwezo wa kutafuta dalili za kuwepo kwa teknolojia ambayo iliundwa na viumbe vilivyo nje ya sayari ya dunia.
Mwaka uliopita mradi huo ulifuatilia nyota lilioenda kwa jina Tabby, ambayo ilikuwa na tabia iliyosababisha watu kufikiri kuwa ilikuwa na viumbe vyenye maisha ndani yake.
‘Mazoea’ imeniingizia hela kuliko nyimbo zangu zote – Billnass
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka label ya LFLG, Billnass amedai wimbo wake ‘Mazoea’ ambao bado unafanya vizuri ndio wimbo uliomwingizia hela nyingi kuliko nyimbo zake zote.
Wimbo huyo aliomshirikisha rapa Mwana FA, umeangaliwa mara 877,121 kupitia mtandao wa YouTube kwa kipindi cha miezi 4.
Akiongea na G.LOVETZ, Billnass amedai ameingiza hela nyingi kupitia shows, ringtone pamoja YouTube.
“Mungu ni mwema sana, ‘Mazoea’ imefanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, na ni wimbo ambao umeniingizia hela nyingi sana kuliko nyimbo zangu zote,” alisema Billnass.
Aliongeza, “Mauzo ya mitandaoni yamekuwa makubwa sana, shows nyingi ambazo nimekuwa nikifanya nalipwa vizuri, YouTube. Yaani huu wimbo umekuwa kama baraka katika miasha yangu. Siwezi kusema nimeingiza kiasi gani lakini ni hela nyingi sana,”
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya ambao amedai utakuwa na surprises nyingi.
Diamond ataja sababu ya kumshirikisha Young Killer kwenye wimbo wake mpya
Diamond amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kumshirikisha Young Killer katika wimbo wake mpya ambao bado haujatoka.
Ni mara nyingi hitmaker huyo wa Marry You, ameonekana kushindwa kuzizuia hisia zake za kumkubali Msodoki huku mara kadhaa akionekana kutumia mistari ya rapper huyo katika kuandika katika mitandao yake ya kijamii.
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii, Diamond amesema,”Nilimuita Young Killer kuja studio, nikamwambia sijawahi kumshirikisha mtu katika muziki kipindi hiki na nikimshirikisha mtu ni wa WCB, kuna nyimbo yangu nataka nikushirikishe tufanye. Kwanza alipata shock kidogo, alipagawa kidogo”
“Nikamwambia usipagawe, hii nyimbo ukifanya verse mbovu nakufuta na hapa katika ofisi mimi ndio nimekupigania hili swala uingize verse kwa sababu kila mtu anashangaa kwanini Young Killer? Ile verse imeandikwa ndani ya siku hizi tatu, akanambia hii nyimbo angekuwa mtu mwingine ningeshamaliza. Katika intro ya kutafuta kuingilia alitafuta karibuni hata masaa sita, lakini mwisho wa siku amefanya verse kali sana sana, imeshaisha bado kushoot video ngoma itoke,” ameongeza.
Bosi huyo wa WCB amesisitiza, “Young Killer mtu ambaye masikini ya Mungu anajitahidi sana sana kufight na mtu ambaye anaandika, mimi napenda mtu anavyandika. Nikajua kwanza nikimchukua Young Killer, nitawaempower vijana wengine wengi wenye ndoto ya kufanya muziki kuona kwamba kumbe na sisi tunawezekana. Kwasababu wangejua Diamond angefanya ngoma labda na Fid Q na Joh, wao wanajua hizo ndio atafanya nao, lakini nimeonyesha kuwa yoyote ninaweza nikafanya naye nyimbo. Na Young Killer kiukweli anachokifanya ni kitu kikubwa na video tutashoot hapa hapa Tanzania na ngoma ni kali na yakinyamwezi.”
22 Apr 2017
M-RAP LION NA MISS RIZY WAFIKISHA MWAKA MMOJA NA UONGOZI WAO WA MAREKANI
Msanii wa hip hop Tanzania M Rap Lion ambae kwasasa anafanya vizuri kupitia wimbo wake wa ‘It’s not too late’ aliyoshirikiana na muimbaji Mayunga afifikisha mwaka mmoja wa kufanya kazi na uongozi wake Muki Intertational.
Kupitia ukurasa wa instagram wa uongozi huo wa Muki International amepost picha ya ya msanii wao M-Rap pamoja na Miss Rizy na kuandika “A year ago today #HappyOneYear #Anniversary @mraplion @Missrizy #Tanzania #Bongoflavourtotheworld #Bongoflavamusic #afrobeatsmusic”
Ni mara chache sana kwa baadhi ya wasanii wa Tanzania kudumu na menejimenti zao jambo ambalo limekuwa tofauti kwa M-Rap ambapo mwaka jana aliweza kupata uongozi wenye ofisi zake nchini Marekani ambao pia unamsimamia msanii mwenzake Miss Rizy
PRODUCER P. FUNK ‘MAJANI’ ATANGAZA UTARATIBU MPYA WA UFANYAJI WAKE WA KAZI.
Jina P. Funk ‘Majani’ ni moja kati ya majina makubwa kwenye ulimwengu wa muziki wa Bongo fleva ambao asili yake ni Tanzania,ukubwa wa jina la Majani linakuja pale ambapo muziki huu ulianza kusikilizwa na kupendwa na watu wengi baada ya mikono yake kuhusika kuzalisha hits nyingi za miaka ya nyuma.
Popote unapolisikia jina la Majani picha inayokuja ni haraka ni muziki mzuri ambao umeendelea kuishi ndani yake mpaka sasa,Majani ameamua kuchukua sekunde kadhaa kuelezea zaidi namna ambavyo amebadilisha utaratibu wa studio yake kwa wale watakaohitaji zaidi kwenda kurekodi au kufanya kazi nae.
Kwenye XXL ya Clouds FM,Majani amesema>>’Wewe unakua umerekodi studio yako nyingine ukitaka sauti uweke kwenye mic za Kimataifa zipitie kwenye mashine za Kimataifa na sikio la Kimataifa unalipa kiasi fulani,ukitaka mixing kama ni studio fulani naweza kwenda kwenye hiyo studio nikachukua hizo files’
‘Nikifanya hivyo haki zote ni zako wewe unanilipa kwa shughuli ya ngu kwa sababu mimi sijaunda huo muziki,lakini hii imekuja kutokana na mtu kuona amekulipa Milion moja,ukilipa Milion moja ni muda wa studio na Engineering ushanielewa’ – Majani.
MADEE AZIPA KISOGO KOLABO
Hivi unafahamu kwamba Msanii kutoka Tip top connection Madee ni moja kati ya wasanii wasiopenda kushirikishwa kwenye wimbo wowote na msanii yoyote? kama hujui kuhusu hilo ukweli wote ni huu hapa.
Madee amefunguka kwamba mimi sitaki kushirikishwa na msanii yoyote iwe Tanzania au nje ya Tanzania , amesema kwa upande wake anaona hakuna umuhimu wa kushirikishwa ndo nilivyoamua na kama kuna mtu ana ndoto za kumshirikisha Madee kwenye wimbo wowote aondoe mawazo ayo
Ameongeza kuwa ata mimi kumshirikisha mtu sifanyi hivyo kwanza naona kila wimbo naona naenea mwenyewe na kama ukiona mimi nimemshirikisha mtu basi ujue kuna swala kubwa sana ndo nitamshirikisha msanii , kwanza ata album yangu naweza kuachia ngoma zote
nipo mwenyewe ila kwa sasa mpango ni kuachia compilation album mimi na dogo janja ambapo tarehe bado kutangaza,”Alisema Madee.
Mkali huyo kutoka Tip top connection kwa sasa anafanya vizuri sana na wimbo wake hela unaobamba na kushika chati kwenye radio na tv nyumbani na nje ya Tanzania
DIAMOND PLATNUMZ ATOA WITO KWA WASANII WA JINSI YA KUTUMIA UMAARUFU WAO
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ashauri kikubwa kwa wasanii mapema jana alipokuwa katika uzinduzi wa manukato yake(Chibu Perfume) uzinduzi uliofanyika GSM Mall barabara ya Pugu jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wadau na waandishi wa habari, Diamond amesema kuwa wasanii wanao wajibu mkubwa wa kutumia umaarufu wao katika vitu vyenye tija hivyo wasisite kujijenge katika mitazamo ya namna ya kuwa mchango kwa faida yao na jamii zao.
“nafikiri tutumie umaarufu wetu katika sehemu chanya yaani chanya kwa maana kwamba isiwe basi umaarufu au influence tuliyoipata tukaitumia katika mambo ambayo hayana maana na hayaleti tija katika jamii…mimi ni mtu ambaye sometimes sipendagi kusubiri eti mpaka wanasiasa wafanye lakini hata mimi kama msanii kama kitu naweza kukifanya basi niko radhi nikifanya ili kuonyesha kwamba unaweza kuwa msanii lakini ukafanya kitu ambacho kinaleta tija kwenye jamii” Alisema Diamond Platnumz.
Hata hivyo Diamond amesema hivyo kufuatia mambo kadhaa ambayo amekuwa akiyafanya ikiwa ni pamoja na kujenga msikiti, kama moja ya njia ya kuirudishia shukrani jamii iliyomfikisha nafasi aliyopo.
LIL WAYNE: JAY Z NI RAFIKI ANAYENISAIDIA KWENYE VITA YANGU NA CASH MONEY
Lil Wayne ameamua kutolea ufafanuzi tetesi za kuwa amejiunga na label ya Jay Z, Roc Nation. Kwenye mahojiano na Skip Bayless, rapper huyo amedai kuwa Jay Z amekuwa rafiki yake wa karibu anayetaka kumsaidia katika vita yake na Cash Money mahakamani.
“Jay ni mtu mzuri tu,” amesema Wayne. “Hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kitu kidogo tu. Rafiki kwa rafiki, nataka tu kukusaidia. Hivyo tu. Hivyo ndio ilikuwa. Nataka tu nikusaidie kwa lolote ninaloweza kufanya. Kwa sasa ataenda kunisaidia kwa vyovyote atakavyoweza.”
Bodi ya filamu yatoa taarifa juu ya sakata la filamu za nje
Bodi ya Filamu nchini imetoa taarifa juu ya habari zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu serikali kuzuia uingizaji, usambazaji na uuzaji wa filamu za kigeni nchini, kwa madai kuwa serikali ina lengo la kuwalazimisha wananchi kuziangalia filamu za ndani (bongo movie) kinyume na matakwa ya soko huria.
Hata hivyo bodi hiyo imekanusha taarifa hizo, kuwa sizo za kweli kupitia taarifa yake ifuatavyo;
Hayo yamebainishwa na mtayarishaji wa muziki kutokea studio za sharobaro, Hit Bits alipokuwa akiongea na G.LOVETZ kufuatia stori inayozunguka kuhusu kufungua studio yake maeneo ya kimara.
Mtayarishaji huyo amesema, uwepo wake hapo unampatia nafasi ya kufanya kazi zake kwa uhuru tofauti na studio zingine.
“Bado nipo sana, sharobaro na sina mpango wakuondoka na nitaendelea kutengeneza ngoma kali. Kwa sasa studio yetu ina project kali zinakuja kutoka kwa Bob mwenyewe na wasanii wengine kama Baraka da prince na chipukizi” amesema Hit Bits.
Hits ni maarufu kuatayarisha nyimbo kama vile chuku chuku ya Bob Junior,Nyamiela ya Nasiri na zingine za wasanii wachanga.
Chibu perfume ina asili ya Dubai – Diamond
Diamond Platnumz leo mchana amezindua rasmi perfume yake ya Chibu Perfume, hatua ambayo ni ya kihistoria.
Perfume hiyo yenye asili kutokea Dubai itauzwa kiasi cha Tsh 105,000. Diamond alisema “Inaaminika kuwa Dubai ndio sehemu kunakotoka manukato mazuri.
Diamond kujenga hospitali ya Moyo Tandale
Katika harakati za kurudisha kwa jamii kile anachokipata, mkali wa wimbo ‘Marry You’, Diamond Platnumz, ameweka wazi mpango wake wa kujenga hospitali ya moyo na magonjwa mengine katika mtaa aliozaliwa, Tandale Jijini Dar es salaam.
Muimbaji alisema tayari amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali na wamemuahidi kumpatia vifaa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii wakati akizindua perfume yake mpya ‘CHBU’, Diamond alisema hospitali hiyo itawasaidia Watanzania wa hali ya chini.
“Mafanikio yote tunayopata hatusahau kurudisha kwa jamii kile tunachokipata,” alisema Diamond. “Ukiachana na misikiti ambayo nimekuwa nikiijenga katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania habari nje kwa ndugu zangu wa Tandale ni kwamba nataka kuwajengea hospitali ambayo itakuwa inatoa huduma pale kwa bei nafuu,”
Aliongeza, “Kuna wadau wangu wanakaa nje, nimezungumza nao wameniambia nijenge tu nay wao kuna baadhi ya vifaa wataleta. Kwa hiyo nikaona hii ni fursa na tayari kuna baadhi ya mambo ya mwanzo tumeanza kuyashughulikia. Nataka ufike muda watu waache kwenda kusafiri nje kutibiwa magonjwa mbalimbali kama moyo na mengine ambayo yamekuwa akitufanya tusafiri nje kwa ajili ya matibabu,”
Perfume aliyozindua muimbaji huyo imeanza kuuzwa rasmi leo nchini kwa bei ya Tsh. 105000.
Chemical ateswa na video za ‘VIP’ na ‘Party’
Kwa sasa ukiachia wimbo bila ya kichupa, mashabiki wanakuwa hawakuelewi. Rapper wa kike Bongo, Chemical amewatoa wasiwasi mashabiki kuhusu nyimbo zake ambazo hajawahi kuzifanyia video.
Rapper huyo ameiambia G.LOVETZ kwamba bado yupo kwenye mipango ya kuachia video ya nyimbo ya ‘VIP’ na ‘Party’
“Tulisema hizo video tutaziachia bila ya kuangalia nimeachia project gani kwa sasa hivi, tutatoa hizo video. Nyimbo kama ‘VIP’ nimepata comments nyingi sana watu wanaomba, na pia madirector’s wanaiomba tuifanyie video na mashabiki wanatamani waione,” amesema.
“VIP is a huge song mpaka leo, na kwangu mimi hiyo ndio my favourite song na ninaamini by the time ambayo tutaiachia video, huo wimbo utarudi na watu wataujua vizuri,” ameongeza.
Hii ndio ratiba ya nusu fainali ya kombe la UEFA na Europa League
Hatimaye droo ya hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la UEFA na ligi ya Europa imepangwa Ijumaa hii.
Katika kombe la UEFA, mahasimu wa mji wa Madrid ambao ni Real madrid na Athletico Madrid wamepangiwa kukutana katika hatua hiyo huku nusu fainali ya pili ya kombe hilo likiwakutanisha Monaco dhidi ya Juventus. Mechi hizo zinartarajia kuchezwa Mei 2 na 3 huku mechi za marudiano zikitarajiwa kufanyiaka Mei 9 na 10.
Wakati huo huo katika Europa League Manchester United imepangwa kukutana na Celta de Vigo ya Hispania,nao Ajax watachuana dhidi ya Olympique Lyon.
Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 3 na 4 kwa michezo ya kwanza huku mechi za marudiano zikitarajiwa kurudiwa Alhamisi ya Mei 11.
21 Apr 2017
Marekani: Wasanii walivyosherehekea siku ya bangi, 4/20.
RIHHANA
Asap Rocky
snoop dogg
rick ross
Miley Cyrus
Soulja Boy
Juelz Santana
Tyga
420 ni namba za siri zinazotumika kuashiria desturi maalum maarufu kama Cannabis Culture nchini humo na baadhi ya maeneo duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wasanii hawa, nchini humo, wanajulikana zaidi kwa ku-enjoy kush mara kwa mara, na kutoona nishahi kupost katika mitandao yao ya kijamii.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)