burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Sep 2017

Madee amchana Dudu Baya, ‘hatusikii kazi tunasikia maneno’


Msanii wa muziki Bongo, Madee amemjibu msanii Dudu Baya aliyedai kuwa wimbo ‘Sikila’ si mzuri.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sema’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anachukulia hayo ni kama maoni yake binafsi kwani hakuna ambaye anafanya kitu bila kupingwa na msanii hawezi kutoa ngoma kila mtu akaikubali.

“Hatusikii kazi tunasikia maneno, kwa hiyo hivyo ni vitu ambayo kwangu mimi huwa navipisha tu, ukitaka kubishana nakuonyesha kazi yangu hii hapa, nadhani huo ndio msingi bora ambao tunatakiwa tuwaelekeze wezentu wanaojaribu kutoka nje ya mistari,” amesema Madee.

“Wengi ambao nilikuwa nao, nilianza nao miaka hiyo 17 ndio ambao sasa hatuwasiki zaidi utawasikia wanaongea hiki na kile lakini still Madee bado anatoa ngoma watu wanapokea na show zinafanyika na maisha yanaendelea vizuri tu,” amesema.

Ngoma Sikila ambayo Madee amemshirikisha Tekno kutoka nchini Nigeria alifanya video katika mtindo wa katuni (animation) kitu ambacho Dudu Baya alieleza kuwa hakiendani na Madee aliyemfahamu hapo awali.

Diamond awasha taa nyekundu Instagram


Diamond anazidi kufurahia mafanikio anayoendelea kuyapata kila kukicha.

Msanii huyo kutoka WCB amekuwa staa wa kwanza Bongo kufikisha followers milioni 4 kwenye mtandao wa Instagram.



Furaha hiyo ya Diamond inasindikizwa na bashasha la kuona wimbo wake mpya aliouachia kwa kushtukiza ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha kundi la Morgan Heritage kutoka Jamaica, kufanikiwa kutazamwa zaidi ya mara laki sita kabla ya masaa 24 tangu alipouachia.

Jibu la Ommy Dimpoz iwapo alimkimbiza Barakah The Prince RockStar4000


Msanii wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz amesema si kweli kwamba yeye kuingia RockStar4000 ndio sababu ya Barakah The Prince kuondoka katika menejimenti hiyo.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa kwanza hawana beef na walifahamiana miaka mingi hivyo hawezi kujua kilichomuondoa Barakah RockStar4000.

“Kwanza mimi na yeye tunafanya muziki tofauti hakuna sehemu tunaweza kusema unaweza ukatokea mkwaruzano na tunaheshiana na ninaamini ni moja ya wasanii wenye talent kubwa hapa Tanzania,” Dimpoz ameiambia Bongo5.

“Kwa hiyo kilichomfanya aondoke RockStar siwezi kukizungumzia wala kujua nini kilitokea yeye na RockStar ndio wana majibu zaidi,” ameongeza.

Alipoulizwa iwapo RockStar4000 imepata pengo baada ya Barakah kuondoka alisema hawezi kusemea hilo au kujua kwa sababu wakati Barakah yupo RockStar4000 yeye hakuwepo.

NEW VIDEO | Madee Ft. Nandy - Sema | Watch


NEW VIDEO | Diamond Platnumz Ft. Morgan Heritage - Hallelujah | Watch


21 Sep 2017

NEW VIDEO | Nikki Wa II Ft. Chinbees - Kihasara | Watch

Nikki Wa II Ft. Chinbees - Kihasara

Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie – Shamfa Ford


Wakati moto ukiendelea kuwaka Hamisa Mobetto kujulikana kuzaaDiamond Platnumz wakati akiwa na mhusiano na mpenzi wake Zari. Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka na kuwafunda wanawake kwa kusema kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.

Shamsa Ford ambaye ni mke wa halali wa Chid Mapenzi, mashabiki wameibua mzozo katika mtandao wa Instagram ambao baadhi ya mashabiki wamedai kuwa anamuonea wivu Hamisa.

Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.haitakuja kutokea kamwe wanawake tukapendana.mwanamke ndo huwa mstari wa mbele kumuumiza na kumdhalilisha mwanamke mwenzie.kabla ya kumuumiza mwanamke mwenzio jaribu kuvaa viatu vyake ingekuwa wewe ungefanyaje..wanawake sisi daaa####TUNAHITAJI MAOMBI

Shamsa amekuwa akiutumia ukurasa wake wa instagram kuwandika mambo mbalimbali ya kushauri wanawake na watu ambao bado hawajaingia kwenye ndoa.

20 Sep 2017

NEW AUDIO | Chege Ft. Billnass & Rich Mavoko - Wanakupenda | Download

Enika, Farida, Stara Thomas na Makamua wampa ‘upweke’ Dayna Nyange


Msanii wa Bongo Flava Dayna Nyange ametaja orodha ya wasanii wa zamani ambao anatamani kuwasikia tena katika muziki.

Hitmaker huyo wa Komela ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’ amewatajawa wasanii hao kuwa ni Enika, Farida, Stara Thomas na Makamua.

“Wapo wengi kwa haraka haraka kuna Makamua alikuwa akiimba vizuri, Stara Thomas nilikuwa napenda ile sauti yake nzito lakini unaweza ukawa unafeel,” Dayna ameiambia Bongo5.

“Enika na Farida ni wasanii waliokuwa wakiimba vizuri na nilikuwa nawasikia nikawanajiuliza wao wanawezaje kipindi hicho narap huniambii kitu na nilikuwa nashagaa wanawezaje kuimba hivi,” ameongeza.

Pia amesema kupotea kwa wasanii hao si kwamba wameshindwa muziki bali ni kubadilika kwa mtindo wa maisha, iwe kwenye muziki au kwao binafsi.

NEW VIDEO | Barnaba - Mapenzi Jeneza | Watch


Young Killer na Dogo Janja ni kama vifaranga vyangu – Young Dee


Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amefunguka kwa kudai kuwa Young Killer na Dogo Janja anawachukulia kama vifaranga vyake hivyo anaweza kuvimiliki na kuvifanya vyovyote anavyotaka.

Rapa huyo ameiambia ThePlaylist ya Times FM kuwa yeye hawezi kushindana na wasanii hao kwa kuwa ni wadogo zake ambao amewaona wakati wanakuwa.

Kupitia taarifa hiyo, mkali huyo wa Utani Utani, amemuita Dogo Janja na Young Killer ni vifaranga vyake na wala hawamsumbui chochote kwenye muziki, na hata akialikwa kwenye shoo ambayo wote kwa pamoja wapo itahitaji dau kubwa sana ili aweze perfom shoo kama hiyo, kwani yeye ni mkali na ana thamani kubwa sana, na kasema ni ngumu sana kumfananisha yeye na wao.

Rapa huyo baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Bongo Bahati Mbaya’ ameachia video ya wimbo wake mpya Utani Utani ambayo inafanya vizuri katika baadhi ya vituo vya redio na runinga.

18 Sep 2017

NEW AUDIO I NACY MASOUND - MPENZI I DOWNLOAD

Image may contain: 2 people, people smiling

Bob Junior Awapa Makavu Wanaoingilia Beef Lake na Diamondi Asema Awajui Undani wa Tatizo

Bob Junior Awapa Makavu Wanaoingilia Beef Lake na Diamondi Asema Awajui Undani wa Tatizo
Aliyekuwa producer wa Diamond Platnumz ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava, Bob Junior amewataka mashabiki kuliacha kama lilivyo suala lake na Diamond kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Give Me’ ameiambia Bongo Dot Home ya Times Fm kuwa mashabiki wanaingilia kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho si sawa.

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwa sababu wakati tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kwa kuingilia vitu ambavyo huvijui.

“Mimi na yeye tulikuwa tunafahamiana wakati tupo chumbani, katika chumba cha studio lakini bada ya hapo tukawa wakubwa, sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? au unanijua mimi?, au mimi na yeye ndio tunajuana zaidi?,” amesema.

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo wewe unaingia kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unaanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hatuwafamu”.

Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza kuwa kuna kolabo ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji na anapomtafuta ili kuzungumzia hilo amekuwa akimpuuza.

Linah: Sikua Nimejipanga Kupata Mtoto Kama Kipindi Nilichokua Ninauhitaji Nikawa Najaribu Haiingii


Msanii wa bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai hakuwa amejipanga kwa kipindi hiki kuwa na mtoto ila anamuomba Mungu isiwe kigezo cha yeye kupotea katika muziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii wenzake wa kike wanaogopa kubebea ujauzito.

Linah amebainisha hayo kupitia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' kutoka EATV baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu wakidai msanii akioa, akiolewa hata akijifungua na mtoto mara nyingi hawezi kuendelea kufanya vizuri katika kazi zake kwa kuwa majukumu ya ulezi yanaongezeka na kupelekea kupotea katika 'industrial' ya muziki.

"Nina muomba Mungu usiku na mchana nisije kupotea katika 'game' kwa sababu ya uzazi, ili iwe mfano hata kwa wengine ambao watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa kufikiri watapotea. Ila mimi nafikiri ni jinsi mtu mwenyewe anavyoishi na mashabiki zake", amesema Linah.

Pamoja na hayo, Linah ameendelea kwa kusema "Sikuwa nimejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila nilikuwa na-wish nipate ujauzito nizae lakini sikufahamu ni lini itanitokea hivyo. 'So' kipindi kile nilichokuwa na-wish nikawa kila nikijaribu haingii, nikajisahau na kujikuta imekuja hata sikutarajia, lakini kwa kuwa nilikuwa nina uhitaji nikasema hakuna neno. Japo nilishauriwa vitu vingi sana mwanzoni lakini nikasema hapana kwa kuwa nimetaka kuzaa acha nifanye hivyo", amesisitiza Linah.

Kwa upande mwingine, Linah amesema kwa anajipa mapumziko katika kufanya kazi zake na kuwataka mashabiki zake wamvumilie mpaka mwakani (2018) katika miezi ya mwanzoni ndipo atakapoachia kazi yake mpya.

Picha ya Inayoaminika ni Diamond Platnumz na Hamisa Kitandani Yavuja Mtandaoni, Pia Jina La Mtoto wa Hamisa



Miongoni mwa stori kubwa katika burudani na udaku Tanzania ni Picha inayoaminika ni Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto wakiwa kitandani imesambaa mtandaoni saa chache baada ya kuisha kwa 40 ya mtoto wa kiume wa Hamisa anayetajwa kuwa ni mtoto wa Diamond.

Ikiwa ilitegemewa Hamisa atamuonyesha mtoto wake 17 September 2017, staa huyu hajafanya hivyo pakiwa na tetesi kuwa Diamond amekataa jambo hilo kufanyika mpaka aweke mambo sawa.

Jambo lingine ambalo limekuwa gumzo mtandaoni nikubadilika kwa jina la mtoto huyu , Tetesi zinasema Prince Abdul Naseeb kwa sasa anaitwa Prince Abdul Latif.

New VIDEO: Mafikizolo – Love Potion

New VIDEO: Flavour Ft. Phyno – Loose Guard

NEW VIDEO | Jay Moe Ft. Ke Miller - Me & You (Mii Na Wee) | Watch


NEW VIDEO | MAN FONGO - SIO POA | Watch


NEW VIDEO | Eric Omondi – Zilitemwa | Watch

Eric Omondi – Zilitemwa

NEW VIDEO | Hemedy Phd - Mkimbie | Watch


15 Sep 2017

Wema Sepetu Aandika Ujumbe Huu Baada ya Manji Kutua Uraiani


Baada ya mfanyabiashara, Yusuf Manji kuachiwa huru Mahakama ya Kisutu leo, Malkia wa Bongo movie,Wema Sepetu ameonyeshwa kufurahishwa mfanya biashara huyo kurudi uraiani.

Wema sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram ametumia ukurasa wake huo akiwa amempost mfanyabiashara huyo na kuandika “Alhamdulillah,”

Manji na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh. milioni 192.5 wameachiwa huru baada ya kesi yao kufutwa na Mahakama ya Kisutu

Baraka The Prince Akiri Kuponzwa na Mapenzi

Baraka The Prince akiri kuponzwa na mapenzi
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Baraka The Prince kwa mara ya kwanza amefunguka sababu ya kuondoka kwenye uongozi ulioanza kumsimamia kazi zake na kumtambulisha kwenye game Tetemesha Records, ambayo imemgharimu mpaka sasa.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Baraka amesema sababu kubwa iliyomtoa Tetemesha ni mahusiano ya kimapenzi na msanii wa filamu ambaye uongozi huo hawakutaka awe naye.

Akiendelea kupiga stori na Big Chawa Baraka The Prince amesema kwamba kwa sasa hawezi kumtaja muigizaji huyo, walisafiri na mpenzi wake huyo na baada ya uongozi kusikia taarifa hiyo, waliamua kumsimamisha kazi, na alipojaribu kukaa nao chini kuzungumza hawakumuelewa.

Jacquline Wolper: Hakuna wa Kumuamini Kwenye Mapenzi

Jacquline Wolper: Hakuna wa kumwamini
Muigizaji wa filamu na Mfanyabiashara, Jacquline Wolper amefunguka na kusema iwapo mpenzi wake wa sasa (Brown) akimtenda na kumuumiza kama waliopita ataamini kuwa hakuna wa kumwamini kwenye mapenzi na kwamba wanaume wote wana matendo ya kufanana.

Akizungumza na G.LOVETZ, Wolper ambaye miezi michache alitangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake (Msanii wa muziki) ma kisha kuweka wazi mahusiano yake na Mwanamitindo Brown amesema kutokana na kijana huyo pamoja na familia yake kuwa na imani ya dini anaamini hataweza kumuumiza ingawa binadamu wana mapungufu.

"Siamini kama BFF anaweza kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa. Namuamini sana kutokana na kuwa na hofu ya Mungu lakini bado sisi ni binadamu. Anaweza kunikosea kawaida au mimi nikamkosea kwa sababu sisi ni binadamu hiyo haitafanya nimchyukie lakini akifika huku pa kunifanya niumie kama nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuamini," Wolper.

Wolper amesema kuwa, Brown ni aina ya mwanaume ambaye alikuwa akimuhitaji katika maisha yake na hatimaye Mungu kasikia kilio chake.

Lady Jaydee ataja sababu za ku-rap kwenye ‘I Miss You’


Malkia wa Bongo Flava Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, amebainisha sababu zilizomfanya ku-rap katika ngoma yake mpya aliyoachia mapema  wiki hii.

Akiongea katika The Playlist ya Times Fm Jide, amesema kuwa kama msanii huwezi kufanya vitu vilevile kila ili watu wakuone mpya lazima ubadilike.

“Sababu ya kufanya rap ni kwa sababu huwezi kufanya vitu vilevile kila siku, ili watu wakuone ni mpya na wapende kitu kipya lazima ufanye kitu ambacho ni tofauti na ulichokuwa unakifanya,” amesema Jide.Pia akaongeza kuwa verse ya kwanza ya ngoma hiyo imeandikwa na rapper One The Incredible.

Video ya ‘I Miss You’ inatarajiwa kutoka hivi karibuni  na huu ni ujio wake mpya  wa mrembo huyi ikiwa ni baada ya kuachia albamu yake ya saba, iitwayo ‘Woman’ mwezi wa nne mwaka huu.

Wema Sepetu hakamatiki Instagram


Hakuna ubishi kuwa Wema Sepetu ni mmoja ya warembo wa Afrika Mashariki mwenye nguvu kubwa ya mashabiki. Umaarufu wake unazidi kuongozeka kiasi ambacho umemfanya afikishe followers milioni 3 kwenye mtandao wa Instagram.

Wema anaendelea kushikilia rekodi yake ya kuwa mrembo wa kwanza Bongo kuwa na idadi kubwa ya followers kwenye mtandao huo.

Umaarufu wa mrembo huyo umezidi kuteka vichwa vya habari kwa takribani miaka 11 tangu aliposhinda taji la Miss Tanzania mwaka 2016.

Lady Jaydee atangaza kutoa zawadi nono kwa mashabiki wake


Mlidhani amemaliza? Bado kidogo, Lady Jaydee ameandaa zawadi nono kwa mashabiki wake baada ya kimya cha takribani miezi mitano.

Baada ya malkia huyo wa Bongo Flava kuachia ngoma mpya ‘I Miss You’ wiki hii huku akitarajia kuachia video Ijumaa hii, ameamua kutoa zawadi ya simu aina ya Tecno Camox CX kwa ajili ya mashabiki wake.



Jinsi ya kushiriki ili kushinda zawadi hiyo.

1. Pakua “I Miss You” kupitia app ya Boomplay Music
2. Chukua screenshot na post kwenye profile yako
3. Nitag mimi @jidejaydee na @boomplaymusic_tz
4. Usisahau kuweka hashtag #BoomJide

NEW AUDIO I WAMELODY CLASSIC FT JAMBO SQUAD - MIDATO I DOWNLOAD


NEW AUDIO | Jay Moe Feat. Ke'miller - Me & You (Mii Na Wee) | Download

NEW AUDIO | Alikiba X Patoranking – KATIKA (Leaked) | Download

New Comedy | Idris Sultan – Sio Habari | Kupanua Episode 1

NEW VIDEO | Rayvanny - Unaibiwa | Watch


NEW VIDEO | Quick Rocka - STILL | Watch


13 Sep 2017

KUMTUMIKIA MUNGU KUNA RAHA SANA HIO NDIO SIRI NINAYOKUPA - Walter Chilambo

Image result for Walter Chilambo siri
WALTE CHILAMBO afunguka na kusema kumtumikia MUNGU kuna raha sana pia amani ninayoipata ni kubwa isiyo ya kifani 

Ikumbukwe  pia WALTER CHILAMBO anasumbua na nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la SIRI hii apa


MTUMISHI HUYU HAKUISHIA  HAPO PIA WAWEZA ANAZIDI KUMSHUKURU MUNGU KWA KUSEMA ASANTE  HII ALIMAANISHA
WAWEZA KUICHEKI HAPA 





3 Sep 2017

TUMEJIPANGA KUHAKIKISHA UNATAPA BURUDANI YA UHAKIKA NA KWA WAKATI - G.LOVETZ



G.lovetzblogspot imejipanga kukuletea habari za wasanii mbali mbali wa ndani ya tanzania na nje ya tanzania utapata full stori kuhusu wasanii wengi duniani

pia utapata stori za kuelimisha na kuburudisha pia  tumepijanga kukuletea exclusive interview za wasanii mbali mbali wa nyimbo za injiri na bongo fleva wadogo na wakubwa pia ndani ya tanzania wa mikoani na wa hapa hapa bongo wote utawasikia hapa hapa ndani ya blog yako pendwa kabisaa ya g.lovetz

B Dozen atia neno mvutano wa Diamond na Alikiba, ‘ni kitu kizuri’


Host wa show ya XXL ya Clouds Fm, B Dozen amefunguka mambo machache kuhusu mvutano wa Diamond na Alikiba pamoja na team zao katika mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano na Times Fm kwenye kwenye uzinduzi wa viatu ‘SultanXforemen’ vya msanii wa filamu na mchekeshaji, Idris Sultan. B Dozen alisema ni kitu kizuri iwapo kitawaletea fedha.

“Ni game inasonga mbele, unaona kama kwenye wiki hizi mbili pamechangamka kweli, kumekuwa na team hii na team hii as long as hakuna ambacho kitatokea baada ya mabishano yanayondelea kwenye social media, radio station na Tv kwenye interview zao,” amesema.

“Ni kitu kizuri ilimradi kiwe kinawatengenezea hela isiwe ni tuwe na namba kubwa ya followers na like kwenye page zao na views kwenye YouTube bila ku-make money it won’t make sense lakini kama inatengeneza hela it very goog thing,” ameongeza.

Siku za hivi karibuni Diamond na Alikiba pamoja na mashabiki wao walikuwa na mchuano mkali katika mitandao ya kijamiii baaada ya kutoka ngoma ‘Seduce Me’ ya Alikiba na ‘Zilipendwa’ ya Diamond/WCB.

NEW VIDEO | OCHU SHEGGY - NISAMEHE BURE (Accapella) | Watch