burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mac 2018

Sergio Ramos aonyesha ndinga yake mpya aliyozawadiwa kuelekea birthday yake, thamani yake ni …


Ikiwa zimebakia siku 21 kabla ya Sergio Ramos wa Real Madrid kusherehekea birthday yake, mchezaji huyo tayari ameshaanza kupokea zawadi za mamilioni.

Mchezaji huyo ameonyesha gari lake jipya aina ya Fiat 600 yenye rangi nyekundu ambayo amenunuliwa na kaka yake ainayeitwa RenΓ© Ramos. Gari hilo lina thamani ya dola 23,600 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 50 za Kitanzania.


Sergio Ramos (kushoto) akiwa na kaka yake Rene Ramos (kulia)

Ramos ameionyesha ndinga yake hiyo mpya kupitia mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka, “The classics never die. | Classic cars never die.πŸš—πŸ•΅♂ 6⃣0⃣0⃣ Birthday gifts that come forward. | Earthly birthday presents.πŸ’£πŸ’₯🎁 Thank you.”

Kufungiwa kwa nyimbo za Nay na Diamond, Papii Kocha afunguka


Wakati mjadala ukiendelea baada ya sekali kufungia baadhi ya nyimbo za wasanii ambazo zilionekana kwenda kinyume na maadili, Papii Kocha ametoa mtazamo wake kuhusuana na hilo.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Waambie’ ameunga mkono hatua hiyo na kusema kuwa msanii anapaswa kutunga muziki wenye kuelimisha.

“Msanii anatakiwa awe anaelimisha jamii sasa ukiandika vitu ambavyo vipo kinyume utakuwa unaharibu taifa na mataifa mengine ambayo yanapenda kusikiliza muziki wako,” Papii ameiambia Clouds TV.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.

3 Mac 2018

Nay kuachia remix ya wimbo ‘Mikono Juu’ baada ya wimbo huo kufungiwa


Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amewataka mashabiki wake wa muziki nchini kusubiria remix ya wimbo ‘Mikono Juu’ ambao umefungiwa na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza kwa kigezo cha maadili.

Rapa huyo mchana huu amewauliza mashabiki wake kama aachie remix ya wimbo huo au la!.

“Unadhani Tuachie Goma Lingine Au Tuache #MikonoJuu Iendelee Au Tufanye Remix,” aliandika Nay wa Mitego kupitia facebook.

Baada ya post hiyo mashabiki walionesha kuhitaji remix hiyo ndipo alipowaahidi mashabiki kwamba ataachia remix hiyo kwaajili ya mashabiki wake.

Rapa huyo mapema jana alidai kama angefungiwa na BASATA basi angeachana na kazi ya muziki na kujikita katika biashara zake.

NEW VIDEO | Matonya - Kiherehere | Watch