Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
31 Mei 2018
30 Mei 2018
Baada ya kupata kigugumizi cha ndoa, Rayvanny anyoosha maneno
Baada ya Rayvanny kupata kigugumizi kuhusu kufunga ndoa na mpenzi wake Fahyma, sasa ameweka mambo wazi.
“Yeah, Mungu akijalia lakini kwa sasa siwezi kusema ni lini kwa sababu hivi vitu vinapangwa na familia, ndugu mkishapanga. ikishakuwa official kila mtu atajua,” alisema Rayvanny hivi karibuni kwenye uzinduzi wa filamu ya Aunty Ezekiel, Mama.
Habari njema kwa sasa, hit maker huyo wa Pochi Nene kupitia mtandao wa Instagram ameweka wazi kuwa ndoa yake itafanyika hivi karibuni tena na mama watoto wake Fahyma.
“🌸 @fahyvanny NDOA SOOOOOON can’t Wait,” ameandika Ray kwenye mtandao huo.
G Nako amtabiria makubwa Vanessa Mdee
Msanii wa muziki Bongo kutoka kundi la Weusi, G Nako amesema kolabo yake na Vanessa Mdee ‘Wet’ itafika mbali zaidi ya sasa.
Wakati G Nako akipiga stori na JJ wa Jembe FM amesema kuwa wimbo huo toka wakiurekodi walijua utakuja kufika mbali.
“Ni wimbo nzuri toka tulivyoureekodi, wakati albamu bado inaendelea kutengenezwa ilionyesha ni moja ya nyimbo zitakuja kufanya vizuri kwenye albamu,” amesema.
“So nafikiri mafanikio bado yataendelea kuwa makubwa na tunasubiri mafanikio mengine makubwa zaidi na mimi bado nashukuru kwa watu wote ambao wanaendelea ku-support,” amesisitiza.
Wet ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimetoka rasmi pamoja na video zake kutoka kwenye albamu ya kwanza ya Vanessa Mdee inayokwenda kwa jina la Money Mondays.
Kati ya Rihanna, Wizkid na Yemi Alade, mmoja wapo ana kolabo na Nandy
Msanii wa muziki Bongo, Nandy ametaja orodha ya wasanii wa kimataifa ambao anatamani kufanya nao kazi.
Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Ninogeshe’ amewataja wasanii hao kuwa ni Rihanna, Wizkid na Yeme Alade, huku akiweka wazi kuwa kazi na Yemi Alade ipo tayari.
“Wapo kama watatu Yeme Alade, kuna Wizkid and Rihanna, kila mtu ana wish, ipo kazi kwa mmoja; Yeme Alade,” Nandy ameiambia Hot90 Fm.
Katika hatua nyingine Nandy amesema kuwa katika maisha yake ya kimahusiano angetamani kujaliwa kupata watoto mapacha.
Diamond anafanya kazi, sijui hata kama huwa analala – Master J
Producer Mkongwe wa muziki Bongo, Master J amesema kuwa mafanikio ya Diamond Platnumz katika muziki ni kutokana na juhudi zake.
Master J amesema ambao wanaweza kumshangaa mafanikio anayopata kwa sasa pengine ni wale waliomjua hivi karibuni.
“Kwa wale ambao wanamjua kwa undani wanajua kwamba hivi vitu havijaja kwa urahisi, ni mtu ambaye anafanya kazi, sijui hata kama huwa analala, ana juhudi na ana bidii sana, kwa hiyo haya matunda tunaona leo ni matokeo kujitoa kwa miaka mingi sana,” amesema.
“Kwa hiyo mimi ninavyoona sasa hivi anaanza kupata matunda kusema kweli nafurahi sana na ninamshukuru Mungu,” Master J ameiambia Wasafi TV.
Licha ya kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava, Diamond ameingiza bidhaa zake sokoni ‘Chibu Perfume na Diamond Karanga’ na sasa amefungua Wasafi Media na hivi majuzi ameweka wazi kumiliki moja gari la kifahari.
1 Mei 2018
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)