burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

19 Nov 2016

Ruge adai Ruby hawezi kushuka kimuziki, amshauri haya ili afike mbali zaidi (Audio)


Mwanzilishi wa THT na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, amesema licha ya Ruby kuwa na tofauti naye na kujiondoa kutoka kwenye usimamizi wake, hawezi kushuka kimuziki sababu ana kipaji cha hali ya juu.
Miezi miwili iliyopita, Ruby alijiondoa kwenye usimamizi wa THT na kukataa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta hali iliyotafsiriwa kuwa hilo linaweza kuwa anguko lake. Hata hivyo bado muimbaji huyo anaendelea kuwika ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa ambako amejinyakulia sifa za kutosha.
Akiongea na mtangazaji wa Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny, Ruge amesema kipaji cha Ruby ni ‘unstoppable’ na kwamba kama akipata waandishi wengine wazuri atafika matawi ya mbali.
“Mimi naamini Ruby ana kipaji sana. Binafsi ana kipaji cha ukweli kabisa wala sio uongo,” alisema Ruge. “Kama atashuka labda itakuwa ni mambo yake tu mwenyewe lakini sidhani kama kuna namna kipaji chake kitashuka,” aliongeza na kumshauri kuwa apate watunzi wengine wazuri wa kumsaidia. Anadai kuwa nyimbo zake tatu, Na Yule, Forever na Sijutii, ziliandikwa na yeye akishirikiana na Amini na Barnaba.
Kwa upande mwingine, Ruge amesema haoni kama kuna tatizo Ruby kuondoka THT kwakuwa tofauti na wengine wanavyodhani, THT si label bali ni kama chuo ambacho wasanii mbalimbali hunolewa.
“Yeye ameona yuko tayari kivyake kwenda kwenye sehemu anayoweza kupata maslahi zaidi, ndio hivyo tu, kwahiyo sioni kama kuna shinda,” amesisitiza Ruge.
Pia amedai kuwa muda wowote ambao muimbaji huyo atahitaji ushauri kutoka kwake, milango iko wazi kwakuwa bado ataendelea kumchukulia kama mdogo wake

Jokate aja na biashara mpya kupitia brand yake ya Kidoti

Super business woman, Jokate Mwegelo amezidi kujitengenezea njia nzuri za kibiashara kupitia brand yake ya Kidoti na kumfanya kuwa miongoni mwa vijana wenye umri mdogo wa Tanzania wanaoingiza fedha nyingi. Sasa amekuletea biashara yake mpya ya mabegi ya mgongoni yenye brand yake ya Kidoti.
14374059_178671149206962_327093865_n
Kwenye moja ya picha alizoweka kwenye mtandao wa Instagram, Kidoti ameandika:
Safari huanza na hatua mmoja na safari mmoja huanzisha nyingine. It was awesome bringing this concept to life with my brother @raqey_allaraqya and his entire team from @iviewstudios thank you and so sorry if I was too demanding, I can’t help myself 😁😝😷. Cc @kidotibags #BeKidotified #ThisBagContainsMyStory #Kidoti
Hizi ni baadhi ya piucha za mabegi hayo.
15101716_649030521944032_5082186521629425664_n
15034519_323911414643965_2919796231850950656_n
13827478_911059349024882_8817537725197451264_n
15034723_106160673202751_1442060408075583488_n

New Audio I KIONJO- DIAMOND PLATNUMZ x NEYO - I Will Marry You[KIONJO] I DOWNLOAD

dia

New Audio I Timbulo Ft Baraka Da Prince - Usisahau I DOWNLOAD

New Audio I walter Chilambo - Asante I DOWNLOAD


New Audio I Cyrill Kamikaze - Nipe Mugongo I DOWNLOAD

New Audio I G.LOVE - NIMEKUONA I DOWNLOAD