burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Nov 2016

New Video Darassa ft Ben Pol - Muziki ( Official Music Video )


Ben Pol adai hajawahi kufurahia kufanya video kama ilivyokuwa kwenye ‘Muziki’ ya Darassa

Kama umeitazama video ya wimbo mpya wa Darassa ‘Muziki’ aliomshirikisha Ben Pol, utakuwa umeona jinsi wanavyokula bata kiasi cha kukufanya uyatamani maisha yale.
15056795_322345568149424_1416941223125450752_n
Ben Pol amesema kuwa kinachoonekana ndicho kilichofanyika – walikuwa na muda mzuri kiasi cha kumfanya akiri kuwa hajawahi kufurahia kufanya video kama ilivyokuwa kwenye hiyo.
“Ni video ambayo nimefanya bila kuchoka. Kwasababu kwanza tulikuwa tunahave fun wamekuja akina Jux pale. Wale warembo pia waliwekuwepo, watu wako charming, wako very happ yaani,” anasema muimbaji huyo.
“Hata walinzi waliokuwepo pale pembeni walikuwa kama wanatutamani fulani, yaani tulikuwa kama tunahave fun kiukweli.”
Ben pia anasema aligundua kuwa Darassa ni mtu anayependwa na ni rahisi mtu yeyote kumzoea. “Naweza kusema Darassa ni mtu rahisi kufanya naye kazi.”

Mwana FA aonya kuhusu bifu zinazoendelea Bongo ‘tunakoelekea tutatoana macho’

Mwana FA ameonya kuhusu bifu zinazoendelea kwenye muziki wa Bongo Flava kwamba zinakoelekea, watu wanaweza kufanyiana vitu vya hatari zaidi.
15099330_914188058682108_8839950530995290112_n
Akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo, FA amesema busara zinahitajika kumaliza tofauti baina ya wasanii wanaohusika kwenye bifu hizo.
“Tufike mahali kwamba tujiwekee mipaka kama binadamu kwamba hivi vitu ambavyo tunaambiana kama ungekuwa unaambiwa wewe na familia yako ingekuwa sawa? Maana yake tunavyoelekea tutatoana macho hivi karibuni,” alisema rapper huyo.
“Watu pekee wanaoweza kufanya ni wao wenyewe wanaohusika. Nafikiri watu wawe humble, warudi chini kidogo, wanaelea sana juu, turudi chini kidogo, tujikumbuke sisi nani na kama malengo yetu ni kutoana roho ama kuendelea kufanya muziki tuweze kujitengenezea vipato,” amesisitiza.
Ushauri wa Mwana FA umekuja katika wakati ambao uhasama kati ya kambi ya Diamond na Alikiba unazidi kushika kasi.
Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Dume Suruali’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee.

Siku Lady Jaydee akitupa order tucheze nyimbo zake tutaanza kucheza – Ruge (Audio)

Ruge Mutahaba amesema siku Lady Jaydee akiwaambia waanze kucheza nyimbo zake watafanya hivyo.
Bosi huyo wa Clouds Media Group, ametoa kauli hiyo Ijumaa hii kwenye mahojiano na kipindi cha XXL cha kituo hicho. “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.
Ruge amesema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’
Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.
“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”
Mtazame hapo chini Ruge akizungumzia bifu ya Diamond na Alikiba, Clouds na yeye kulaumiwa, tofauti yake na Ruby pamoja na lawama za hivi karibuni za TID.


New Audio I Jobfire wa Melod-Ni sawa I DOWNLOAD

19 Nov 2016

G.LOVE ni msiri sana kuhusu mahusiano yake hakuweka wazi alipokuwa kwenye Exclusiv interview ya magic FM

Msanii Godlove kilave alimaarufu kwa jina la G.love amekuwa msiri sana kuhusu mahusiano yake akidai kwa sasa bado mapema kufahamu kwa sas haijuikani kama g.love yupo kwenye mahusiano au laaaa!!!!
jana g.love alitambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la nimekuona hivi sasa ameanza kuifanya promo nyimbo yake mpya

Barnaba afunguka faida aliyoipata baada ya kuachia ‘Lover Boy’

Msanii na mtayarishaji wa muziki Barnaba ametaja faida aliyoipata baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Lover Boy’.
15043882_695331390634946_6717057194262528000_n
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Storm cha Clouds TV kuwa wimbo huo umekuwa ya kwanza kumpatia show nyingi kwa muda mfupi na dili nyingine za matangazo.
“’Lover Boy’ ni wimbo ambao umenifanya nipate show nyingi kwa muda mfupi zaidi pamoja na kupata dili kibao za matangazo ya makampuni mbalimbali pamoja na endossement nyingine nyingi,” amesema Barnaba.
‘Lover Boy’ ni moja kati ya nyimbo kali usiyochoka kuisikiliza huku ikiwa imeshatazamwa zaidi ya mara laki 5 kwenye mtandao wa Youtube tangu ilipotoka mwezi Septemba mwaka huu.