burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Nov 2016

New Audio I Darassa Ft. Ben Pol - Muziki I DOWNLOAD

Official VIDEO | MwanaFA Ft. Vanessa Mdee – Dume Suruali


dume
djmwanga1bdownloadlogo

Ommy Dimpoz afunguka kisa cha kukosana na Diamond Platnumz

Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.
Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.
Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.
“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi, nikauchuna tu,” alisema Ommy.
Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.
“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.
Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe kualikwa.
Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.
“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”
Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa ‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”
Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo ameshaiwahi.
Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho yake.
Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.
“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.
Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana hakuchagulii tusi.’
“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”

Diamond atoa jibu la utata kufuatia interview ya Ommy Dimpoz

Inaitwa Tit for Tat! Baada ya Ommy Dimpoz kueleza kwa kina kuhusiana na sababu iliyopelekea wakakosana na Diamond, muimbaji huyo wa Salome, amejibu kupitia Instagram.
15056662_331170897262349_6840282975670632448_n
Majibu ya Diamond ni ya mafumbo kiasi na tayari yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki huku wengi wakichukizwa na kauli yake.
Ameandika:
Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue
Itazame hapo chini interview ya Ommy Dimpoz.


Ommy Dimpoz: Nilichangia kuandika Nasema Nawe ya Diamond

Ommy Dimpoz amesema alichangia kuandika hit single ya Diamond, Nasema Nawe – kipindi bado ni marafiki.
“Mimi nataka kusema kitu kimoja, sijawahi kusema sehemu yoyote hapa, mfano kwenye nyimbo ya mduara ya D Nasema Nawe, mimi nimechangia kwa asilimia kubwwa uandishi wa ile nyimbo. Sio kwamba D hajui kuandika, anaandika vizuri na nawaheshimu ni moja ya waandishi bora kabisa,” Ommy alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Alhamis hii.
Ametolea mfano mstari aliochangia ni wa verse ya pili usemao ‘zingifuli zingifuli usozinga mahala ukakaa.’ Muimbaji huyo amesema hata kwenye verse ya kwanza kuna maneno ameyaandika lakini hakuwahi kutaka apewe credit.
“Sikufanya vile kwasababu nilipwe au nipewe credit. Lakini nataka tu niseme kuwa mashabiki kuna vitu vingine vingi hawajui,” alisisitiza.

Wema Sepetu ampongeza Ommy Dimpoz

Baada ya hapo jana Ommy Dimpoz kufunguka kiundani kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kwa kuelezea kilichopelekea akosane na rafiki yake wa zamani, Diamond Platnumz – Wema Sepetu amempongeza kwa kile alichokifanya.
dimpozzz-25f2a
Malkia huyo wa filamu nchini, amempongeza hitmaker huyo wa Kajiandae kwa kumsifia kuwa ni mpole na mwenye busara ila alipenda kile alichokifanya kwenye mahojiano yake hayo.
Kupitia mtandao wa Instagram, Wema ameandika.
Busara, Upole, Hekma… Thats wat u r made of… Im very very Proud and Impressed kwakweli… Mnyonge mnyongeni haki yaki mpeni… Sasa sio mje muanze kusema sijui napick sides… Nooooo…!!! Sina side maana na mimi pia ni outsider tu… But kwa leo nimependa ulichofanya Ommy…. Forever Bae… 👌🏽Sometimes being the bigger person doesnt hurt… @ommydimpoz

Darassa adai muziki wake hauwezi kuchuja

Rapper Darassa amedai kuwa muziki anaofanya ni wa kuishi milele ndio maana nyimbo zake haziwezi kuchuja.
14583380_1795519663993381_1232498486868443136_n
Akiongea na Times FM, Darassa amesema, “Natengeneza muziki wa kuishi milele, ndio maana ‘Utanipenda’ na ‘Too Much’ hazichuji.”
Kwa sasa Darassa ni mmoja kati ya rapper wa kizazi kipya ambao wanafanya vizuri huku wimbo wake aliouachia siku chache zilizopita ‘Muziki’ aliomshirikisha Ben Pol ukionekana kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga.