Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
2 Jan 2017
Wema Sepetu auaga mwaka 2016 kwa style ya aina yake
Nini tena kimemkuta malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu? Ama labda ameamua kutoingia mwaka 2017 kwa kumbukumbu za mwaka 2016?
Ni kwa sababu mrembo huyo ameamua kufuta picha zote kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram yenye followers milioni 2.5.
Japo haijajulikana sababu ya kuamua kufanya hivyo, uwezekano kwamba ameamua kuukaribisha mwaka mpya kwa kupost picha mpya ni mkubwa.
Professor Jay afunga mwaka 2016 kwa kumvalisha pete mama watoto wake
Mwaka uliopita rapper huyo akiwa katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, aliahidi na kusema kuwa mwaka 2017 atafunga ndoa na mpenzi wake huyo.
Dawa za kulevya zamtafuna mshiriki wa BBA The Chase, Nando
muonekano wa mwanzo wa nando
Staa aliyewahi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa – The Chase, Nando ameendelea kudhoofika kutokana na matumizi ya dawa za kulevy
hivi ndivo alivo sasa
Nando aliyewahi kudai kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, alikuwa kipenzi cha wasichana wakati anashiriki kwenye shindano hilo na alitazamiwa kushinda kabla ya kutimuliwa kutokana na kujihusisha kwenye ugomvi kwa kumtishia kumchoma kisu mshiriki wa Ghana.Mwishoni mwa wiki, picha inayoonesha muonekano wake wa sasa imesambaa mtandaoni na kuwashtua watu wengi.
Mwaka uliopita staa mwingine aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano hilo, Feza Kessy, alisema kuwa anaamini Nando amepatwa na tatizo au anaugua kwakuwa tabia anazozionyesha zinampa mashaka.
“Naamini Nando ana tatizo asaidiwe,” alisema Feza. “Sijui kwanini lakini naamini Nando ana something hayupo sawa, sio yule Nando ninayemfahamu, naomba atafutwe asaidiwe,” alisisitiza.
Feza ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Choice FM, alidai kuwa aliwahi kukutana na Nando na akampa noti ya shilingi elfu 10. Anasema badala yake yake staa huyo aliitupa chini kwa madai kuwa haiwezi kumsaidia kitu.
Kabla ya hapo Nando aliwahi kudai kuwa atatoa kitabu chake kiitwacho ‘Mhuni huyo Mwenye Akili.
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na peer pressure na watu niliokuwa nao wakati ule, na life niliyoishi mimi…ni yale maisha ya kujiachia,” Nando alikiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM kuhusu kilichomfanya ajiingize kwenye matumizi ya dawa hizo.
Sifikirii kwenda international kabla sijakubalika vya kutosha nyumbani – Young Dee
Rapper Young Dee amesema hafikirii kwa sasa kufanya jitihada za kwenda international wakati nyumbani bado hajapenya ipasavyo.
Dee anasema anachoamini ni kuwa msanii hawezi kufanya vizuri kimataifa kama nyumbani bado hafanyi vizuri.
“Kuna sehemu mimi sijafika bado Bongo nahisi, Tanzania ni nchi kubwa sana, kuna East Africa halafu kuna Africa halafu ndio kuna kimataifa. Lazima uanze huko,” Young Dee alimuambia mtangazaji wa Lake FM ya Mwanza, Haroun Tambwe.
“Kabla sijafikiria kujulikana kimataifa, lazima nianze kwanza East Africa ili Tanzania nihakikishe nimetoboa. Kule watakuwa na sababu ya hata kuniassociate na muziki wao kwasababu nitakuwa nakubalika nyumbani.”
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


