burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Feb 2017

Je wajua kwanini kila unachokionja baada ya kupiga mswaki huwa na ladha mbaya


Toka ukiwa mdogo mpaka unazeeka umekuwa ukijiuliza kwanini kila kitu unachokula au kukionja huwa kinakuwa na ladha mbaya mara tu baada ya kusafisha kinywa chako kwa kutumia mswaki ulioweka dawa ya meno.

Dawa nyingi za mswaki huwa zinakemikali zifuatazo Sodium lauryl sulfate, sodium laureth sulfate (SLS) and sodium lauryl ether sulfate (SLES) ambazo hupunguza nguvu ya ukinzani ili kutengeneza povu (foaming action) kwenye dawa ya meno ili kusaidia katika kuondoa mabaki ya vyakula kwenye kinywa chako.

Lakini pia kemikali hizi hukinzana na utendaji kazi wa taste buds (huhusika na utambuzi wa ladha) kwa kuvunja vunja phospholipids kwenye ulimi wako. Matokeo yake husababisha ladha ya uchachu (bitter tastes) nahii ndo sababu kila unachokionja na kukila huonekana kibaya mara baada ya kusafisha meno yako.

Lakini hali hii huondoka mara tu baada ya mda mfupi. Niwatoe hofu watumiaji wa dawa za meno kuwa hali hii ya kuhisi uchachu haina madhara yeyote kiafya.

NEW AUDIO | Ray C - Upepo (Cover) | Download

Image result for Ray C - Upepo (Cover)

VIDEO | AT – Sili Feel | Watch



VIDEO | Baghdad - Nipe Namba | Watch

VIDEO | Diamond Platnumz Ft. Ne Yo - Marry You | Watch


1 Feb 2017

Navy Kenzo watajwa kutumbuiza kwenye Hipipo Awards 2017 Uganda


Kundi la Navy Kenzo limetajwa kutumbuiza katika sherehe za utoaji tuzo za Hipipo Music Awards 2017 za Uganda.
Wasanii wengine ambao watawasha moto katika jukwaa hilo ni pamoja na Navio, Bebe Cool, Ziza Bafana, Maureen Nantume, Sauti ya Africa, Charlyand Nina na wengine.

Tuzo hizo zinatarajia kutolewa Jumamosi hii ya Februari 4 katika ukumbi wa Kampala Serena Hotel.

Dayna Nyange atoa somo kwa wasanii wanaoandikiwa nyimbo zao


Dayna Nyange ametoa somo kwa wasanii ambao hawana uwezo wa kuandika nyimbo zao.
Hitmaker huyo wa Komela, amekiambia kipindi cha E News cha EATV Jumanne hii, wasanii wajifunze kuandika kwani wanaweza wakapata bahati ya kufanya kazi na msanii mkubwa duniani wakaanza kuhangaika.

“Siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali kwa kuwa hujui kuandika,” amesema Dayna.

Dayna ameongeza kwa kumpongeza Maua Sama kutokana na uwezo wake wa kuandika nyimbo zake ambazo zimeonekana kumfurahisha zaidi.