burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

1 Jan 2018

T-Pain aitaja albamu bora mwaka 2017


Msanii T-Pain ameitaja albamu yake bora kwa mwaka 2017.

Akiongea na mtandao wa Rap Up msanii huyo ameitaja albamu hiyo kuwa ni Heartbreak on a Full Moon ya Chris Brown yenye ngoma 45 ndani yake.



My favorite album of 2017 would probably be Heartbreak on a Full Moon. For sure. Chris Brown, definitely, guaranteed. There’s enough to pick from. You’re gonna like most of that album, but even if you don’t like most of the album, you’re gonna like an album’s worth of that album,” T-Pain ameuambia mtandao huo.

“There’s for sure 12 songs on there that you’ll like. You can’t go wrong. You cannot not like a big chunk of 45 songs. You’re gonna like an album’s worth of it so there’s no way to lose on that album. There’s no way to not like that album,” ameongeza.

Chris Brown aliachia albamu yake hiyo ya nane October 31 ya mwaka jana.

NEW AUDIO I KIVI CLASSIC - MAUMIVU I DOWNLOAD


NEW AUDIO I J KATA - NI WEWE I DOWNLOAD


Manchester City wapata pigo


Mshambuliaji machachari wa Manchester City, Gabriel Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na jeraha alilopata wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace Jumapili ambapo walitoka sare 0-0, meneja Pep Guardiola amethibitisha hilo.

Mbrazil huyo wa miaka 20 alionekana kuumia kwenye goti kipindi cha kwanza wakati wa mechi hiyo uwanjani Selhurst Park.

Aliondolewa uwanjani akitokwa na machozi.

Kiungo wao Kevin de Bruyne pia huenda akakosa kuwachezea kwa muda baada ya kuondoka uwanjani akiwa amebebwa kwa machela.

Mbelgiji huyo hata hivyo alionekana nje ya uwanja baada ya mechi, dalili kwamba huenda hakuumia sana.

“Nafikiri Gabriel atakuwa nje kwa mwezi mmoja hivi au siku chache zaidi, naye Kevin tutasubiri Jumatatu tujue iwapo aligongwa tu kidogo au ameumia sana,” alisema Guardiola.

Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Guardiola: Manchester City hawatamaliza ligi bila kushindwa
“Ni lazima ukubali ukali na ugumu wa ukabaji Ligi ya Premia, lakini waamuzi wanahitaji kuwalinda wachezaji, hilo ndilo naomba pekee.”

Jesus atakosa mechi dhidi ya Watford Jumane.

De Bruyne naye ambaye ameng’aa sana msimu huu na kusaidia ufungaji wa mabao tisa Ligi ya Premia msimu huu aliumia baada ya kukabiliwa na kiungo wa Palace, Jason Puncheon.

Barakah The Prince aeleza kilichomfanya avurunde mwaka 2017

Msanii wa muziki, Baraka The Prince amefunguka kueleza kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri kimuziki mwaka 2017.
Muimbaji huyo ambaye mwaka 2017 aliachana na label ya Rock Star4000 na kuanzisha label yake, Bana Music, amedai sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vizuri ni kukataa baadhi ya show ambazo alikuwa anapewa na mapromota.
“Mi nimiongoni mwa wasanii ambao nabagua sana show, mpaka nikifanya show mpaka promota afike bando ambalo nahitaji, na ninafaya hivyo ili kulinda brand yangu ambayo tayari nimeshaitengeneza,” Baraka alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aliongeza,”Na kama nimeyumba kimaisha nayumba kweli kwa sababu maisha ndivyo yalivyo, kuna kupanda na kushuka, mpaka mataifa mkubwa wanayumba kiuchumi mimi ni nani, sio kitu kibaya, kinaweza kumtokea mtu yeyote”,

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa maashabiki kuwa msanii huyo sio tu amefulia, bali hata uwezo wake kwenye kazi umeshuka, na kushauri kama inawezekana awe anaandikiwa kazi zake.

Mwaka 2017 ulikuwa mbaya kwangu – Nay wa Mitego


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amefunguka kwa kudai kwamba mwaka 2017 uliomalizika weekend iliyopita haukuwa mzuri katika muziki wake.

Rapa huyo ambaye haishiwi matukio, mwaka 2017 aliwekwa ndani na jeshi la polisi kutokana na kuachia wimbo ‘Wapo’ambayo ulidaiwa kuwa maneno ya kutengeneza chuki kwa wananchi na viongozi wao.

“Mwaka 2017 haukua mzuri sanaa. But niseme asante kwa pumzi na afya njema,” aliandika Nay wa Mitego Instagram.


Aliongeza, “Asante mungu kwa Kila Kitu. Asanteni mashabiki wangu ambao mmekua bega kwa bega na mimi kwenye kila jambo ata nilipo kosea hamjawai nitupa, Nawapenda sana. Shukrani kwa media zote kwa support mnayozidi kunipa mungu azidi kuwaongezea mwaka 2018. Happy New Year🔥#NiweDawa,”

Rapa huyo anajipanga kuachia wimbo mpya uitwao, Niwe Dawa.