burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

13 Jan 2017

G-Nako na Nick wa Pili ‘wamchenjia’ Young Killer baada ya kudai Joh Makini anabebwa

Image result for sinaga swaga
Ngoma mpya ya Young Killer, Sinaga Swagga ina utata mwingi. Mmoja wa mstari ambao tayari umeanza kumtokea puani rapper huyo ni ule usemao, wanasema Joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli
Joh Makini hana jibu lenye hasira kama wengi wanavyotarajia kwasababu kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, rapper huyo alisema,” Hiyo kamba, hiyo mbeleko hiyo toka 2005 mpaka mpaka 2015 basi hiyo kamba ngumu
Jibu lilikuwa tofauti kwa G-Nako aliyesema, “Sometimes watu kama hawa wanakuwa wanaongea tu kwasababu wanataka wasikike kwamba kuna vitu wanaviongea kwenye mistari, inabidi wakifika kwenye interview kama hapa muwe mnawachallenge, kwamba wewe umeongea hivi kwenye mistari yako, umeshafuatilia hiki na hiki? Maake sio mistari tu.”

Kwa upande wake Nick wa Pili alisema, “tatizo ninaloliona katika mstari kama huo ni kwamba unaharibu history sababu Joh amefanya kazi kubwa sana so tunategemea artist wadogo si lazima kumjua Joh Makini ila kuijua historia ya Joh Makini sababu pale ndo kuna mafunzo mengi ya kujifunza.”

Ameongeza, “Kwahiyo anavyokuja mtu akitoa neno kama hilo anaharibu ile historia sio kwa Joh, kwa mtu ambaye anakuja mdogo. Mtu ambaye anatakiwa kumjua Dullah hatakiwi kumjua leo, unatakiwa kujua Dullah alianzaje kufika hapa kwasababu kila mtu anaanza moja, unaweza ukarelate na hiyo story kikawaida.”

Joh alirejea tena kuelezea kwanini mambo kama hayo huwa hajibu akisema, “Katika historia ya interview yangu na jinsi ambavyo nafanya kazi, huwa sitoi nafasi kwenye vitu vya kipuuzi, navipaga tu mgongo naendelea na mambo yangu ya msingi sababu end of the day hata nitakachosema, hakitaleta maana sababu kama hawajui history.”

Ditto: Kundi la Mtu Pori lilishapita, ila tumebaki kama ndugu


Hitmaker wa Moyo Sukuma Damu, Lameck Ditto amefunguka kuhusu mipango ya kulirudisha kundi la Watu Pori.
Akiongea na mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touch, muimbaji huyo amesema kuwa kwakuwa hilo limepita hakuna mipango kama hiyo tena japo bado wanashirikiana kwa ukaribu na Afande Sele na MC Koba.

“Afande Sele na Koba ninaishi nao kama familia sio kwasababu kundi halipo hatushirikiani mambo yote, tunashirikiana sana. Kuhusu kulirudisha kundi la Watu Pori nadhani hilo limeshapita kwahiyo tunaendelea na mambo mengine lakini hilo halivunji undugu na ushirikiano tuliokuwa nao siku zote,” amesema Ditto.

Ditto ameongeza kuwa tayari ameshafanya nyimbo moja na Afande Sele lakini bado haijatoka.

Gabo awaka baada ya mtandao mmoja wa Kenya kudai yeye ni muigizaji wa nchi hiyo


Muigizaji anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Gabo Zigamba ameujia juu mtandao mmoja wa Kenya ambao umedai kuwa yeye ni raia wa Kenya.
Mtandao huo uliandika stori yenye kichwa cha habari “Gabo Kenyan-talented movie actor” .
Hata hivyo Ijumaa hii mtandao huyo uliamua kurekesha habari hiyo.


Jinsi kichwa cha habari hiyo kilivyokuwa kabla ya kubadilishwa

Muigizaji huyo baada ya kuona taarifa hiyo, kupitia instagram aliandika:

Kinachoweza kuondoa makucha haya ya majirani ni film tuu. Film is the best method of propaganda spreading. Na ili tufikie hapo ni kufanya kazi zenye ubora wa kidunia ili ziende duniani kufikisha ujumbe.. bado tuna deni kubwa la kuwavua nguo hawa wadhalimu.. hii vita ya nyenyenye za jirani viongozi wengi wana nafasi ya kuishiriki ila sioni ushirika wao. Nna hofu hata tukianza kutengeneza films za kuuambia ulimwengu juu ya machache yanayotangazwa na majirani mmh zisijeishia studio kisa ujirani mwema.. hio ni hofu yangu tuu.. kama trump anamuongelea Puttin on media vipi viongozi wa serikali yetu hawayaoni haya yote..? Mimi naamini serikali yetu inauwezo wa kuita press na media house za dunia na kuorodhesha yote yaliyodaiwa na wakenya kuwa yao na kuipa ujumbe serikali ya kenya . Mfano.. Tunajua mengi yatadaiwa kuwa ni raia tu binafsi na taasisi ndio zinajitamkia haya mambo. Yaani si kenyan government.
Lakini mimi najiuliz raia anapoongelea vitu kama Olduvai gorge ipo kenya mimi najiuliza darasani somo la historia kenya wanafundisha nini?
bado najiuliza wakenya wanafundishwa georaphia ya wapi mpaka waseme kilimanjaro iko kwao?
Mrisho mpoto miaka michache ilopita huko ughaibuni alishikishwa bendera ya kenya na wakenya,akaishusha bendera stegini. Hongera kwako mjomba. Sikupoteza nguvu zangu wakati wa kutoa mchango wangu kwako mjomba.. Ukitaka kuusimamisha moto nenda kwenye chanzo.. haya mambo ni ya history na geographia yaani namaanisha hutokana na elimu wanayopewa.. sasa swali ni kwamba kama oldivai na kilimanjaro ni viko kwao unashangaa nn wakisema Gabo ni wao au mpaka waseme Arusha nayo ni ya kwao😂

Seline atoa povu kwa wasanii wa kike Bongo


Msanii wa kike aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa label ya The Industry iliyo chini ya kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii Aika na Nahreel, Seline amefunguka kuhusiana na wasanii wa kike kutumia skendo kwa kujiongezea umaarufu.
Akizungumza na Mtangazaji Pk5tz wa kipindi cha Extra Fleva cha Uplands FM ya Njombe, Seline ambaye sasa yupo chini ya usimamizi wa Producer Mona Gangstar wa Classic Sound, amesema kitu anachokichukia kwa sasa ni wasanii wa kike kutumia skendo kwa ajili ya kupromote kazi zao.

Seline amedai wakati mwingine ni nzuri sababu zinamfanya msanii azungumziwe ingawa wakati mwingine ni vyema msanii akaamini katika kipaji alichonacho kwakuwa skendo zina changamoto yake.

Kwa upande mwingine, akizungumzia kuhusu uzoefu wa kuwa chini ya label, Seline amewatupia lawama wasimamzi wanaosimamia wasanii bila kuwa taaluma na hiyo.

Akothee afunguka tetesi za kumlipa Diamond milioni 36 kwaajili ya kolabo

Muimbaji wa Kenya, Akothee amefunguka tetesi zilizosambaa kuwa alimlipa Diamond Platnumz kiasi cha shilingi milioni mbili za Kenya ili ashiriki katika wimbo wake wa ‘Sweet Love’. Kiasi hicho ni takriban shilingi milioni 36 za Tanzania.

Akiongea katika kipindi cha runinga cha Talk Central cha K24, Akothee amekataa kuweka wazi lakini amedai kuwa fedha hiyo ni kitu kidogo kwa kuwa na kama wimbo huo usingekuwa mzuri wangeomba warudishiwe fedha yao.

“What is two million shillings? No! am not saying no but am not saying yes, am saying why 2 million. Is the song good, we don’t have to talk about price if the song is not good then if we have paid we will ask our money back,” amesema Akothee.

“And now the song is doing well let’s just talk about the song,’ ameongeza.

Mpaka sasa wimbo huo umefanikiwa kutazamwa mara 3,383,577 kwenye mtandao wa YouTube na umekuwa wimbo wa kwanza wa muimbaji huyo kutazamwa zaidi katika mtandao huo.

Ishu ya Joh Makini kubebwa sijaiongea kwa ubaya – Young Killer

Msanii wa muziki wa hip hop Young Killer anadaiwa kumdiss msanii wa Hip Hop Joh Makini kwenye wimbo yake mpya ‘Sina Swaga’ akidai kwamba anabebwa kisanaa.
Rapper huyo amedai kuwa hajasema hivyo kwa ubaya bali yeye amezungumza kile ambacho kimekuwa kikizungumzwa mitaani na baadhi ya watu pamoja na wasanii.
“Mimi sijaiongea kwa ubaya, nimeielezea kwa sababu hata Chidi Benz alishawahi kuizungumzia, lakini Joh kwangu ni msanii ambaye namkubali na kama nikisema nimweke kwenye list, tatu bora yupo,” Young Killer alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.Amedai aliamua kuyawakilisha baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakiongelewa na wasanii wengi ikiwemo Chid Benz ambaye aliongelea kwenye media na kutunga mistari inayoelezea jinsi gani Joh anabebwa kisanaa.Pia rapper huyo alidai kuwa kuna ushaidi mwingi wa picha kwenye blog tofauti zinazoonesha jinsi Joh anavyotuhumiwa kubebwa kisanaa na kusema hana tatizo na Joh Makini na hata akikutana naye atamsalimia.

Hili ni jambo ambalo wasanii wakongwe wanapaswa kujifunza toka kwa Dully Sykes


Muendelezo juu ya ubora fulani ambao mwanadamu anaweza kuwa nao katika kipindi fulani cha maisha yake ni jambo linalohitaji nidhamu,weledi, kujituma na utayari wa mtu kujifunza na kukubali kufanyia kazi mapungufu anayokuwa nayo.
Nchini kwetu suala la mtu kuweza kutunza ubora fulani aliokuwa nao katika jambo fulani ni mtihani mzito kweli kweli. Mara ngapi tumeona waigizaji, wanamuziki,wanamichezo, wanasiasa,hata watu wa kawaida,wakionyesha ubora fulani na baada ya kipindi kifupi tu wakashuka kwa kasi ya ajabu kama si kupotea kabisa?
Kwahiyo inapotokea kuna mtu kaonyesha kuutunza ubora wake kwa kipindi kirefu basi haina budi kutoka hadharani na kumpa sifa zake. Sote watu wa jamii ya muziki tunamfahamu Prince Dully Sykes, ukipenda mwite Mr Misifa. Ana kila sababu ya kusifiwa hasa ikikumbukwa ni mmoja ya watu wa mwanzo kuanza kufanya muziki lakini mpaka leo yupo anarindima kwenye ramani ya muziki.

Hii haitokei tu,Ila ni utayari wake wa kubadilika kulingana na mahitaji ya muziki kwa wakati husika,kukubali kujifunza hata kwa wadogo zake aliowakaribisha kwenye muziki. Lakini kujituma na ubunifu kila uchwao

Analowashindia wasanii wengi wakongwe wao kila kukicha ni lawama na maneno ya kuamini wasanii wa sasa wanaupoteza na kuuharibu muziki na kuamini wadau na media wanawabeba. Lakini Dully ameamua kuamini kua muziki unabadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Binadamu hata awe na ubora na kipawa kiasi gani mwisho wa kujifunza kwake ni pale pumzi yake ya mwisho inapokata. Ili uweze kudumu katika jambo lolote lazima uone msingi wa hayo yote ni kujifunza hata kwa wale unaowaona ni wadogo kwako.

Salute kwako Dully Sykes bila kuwasahau Lady Jaydee, AY, Fid Q, Mr Blue, Mwana FA na wengineo waliokuwepo juzi, jana na mpaka leo na wapo wanalisongesha game.