burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

9 Mei 2017

BIRDMAN NA LIL WAYNE WAZUA MASWALI NA KUWAACHA MASHABIKI MIDOMO WAZI


Rapa anayefanya kazi chini ya lebo ya muziki inayomilikiwa na Jay Z ya Roc Nation Records, Lil Wayne amefanya tukio ambalo wengi waliomfatilia hawakutegemea kwa kipindi hiki cha kutoelewana kibiashara na lebo yake ya zamani ya Cash Money Records kabla kuingia rasmi katika mkataba mpya wa kiabishara na Rock Nation.

Katika Rolling Loud festival ilayoendelea huko Miami Florida rapa Lil Wayne aliwashangaza mashabiki waliokuwa na taarifa za kuwepo kwa bifu nzito kati yake na mfanyabishara na rapa nayemiliki lebo ya Cash Money Records baada ya kukubali kupiga picha na watoto wawili wa Birdman Bryan Jr. na Bria.

Aidha zengwe hilo haikuishia hapo kwenye kupiga picha pekee kwakuwa mara baada ya picha hizo za kumbukumbu za watoto wa mmiliki wa lebo ya Cash Money Records Birdman na Lil Wayne picha liliendelea kupitia akaunti ya Instagram ya Birdman kwakuwa alizipost kitendo ambacho kiliacha maswali na majibu ya kuwa inawzekana hakuna tatizo kati yao kwasasa.







Hata hivyo Lil Wayne tangu kuingia mkataba wake mpya na Rock Nation ameonekana katika kazi mpya ya DJ Khaled ya I’m the One iliyowashirikisha Justin Bieber, Quavo na Chance the Rapper inayoenakana kuwa na mapokezi makubwa sana kwakuwa imefikisha watazamaji zaidi ya milioni 78 ndani ya wiki moja pekee katika mtandao wa Youtube.


NICKI MINAJ AWALIPIA MASHABIKI WAKE ADA ZA SHULE, WALIMTUMIA AKAUNTI ZAO ZA BENKI TWITTER


Nicki Minaj amezijaza akaunti za benki za mashabiki wenye bahati kwa fedha za kulipia ada zao za shule. Ilianza kama utani Twitter baada ya kuwataka mashabiki wake washiriki kwenye shindano analoliendesha ambalo linawapa nafasi kukutana naye.

Hata hivyo, shabiki mmoja aliichallenge kauli yake kuwa anaingiza fedha za kutosha kuwasafirisha mashabiki wake kokote duniani, kwa kumuomba awalipie ada zao za shule.



Nicki alichukua ushauri huo lakini akaweka kigezo kuwa atawalipia wale tu wanaofanya vizuri darasani. “Show me straight A’s that I can verify w/ur school and I’ll pay it. Who wants to join THAT contest?!?!??♀️ Dead serious. Shld I set it up,” alitweet.

Mashabiki kibao walijitokeza wakiwa na maombi ya kulipiwa ada, vitabu na vitu vingine vya darasani. Wengi walimuonesha screenshot za matokeo yao. Wale ambao walikuwa na A za kutosha, aliwaomba wamtumie DM akaunti zao za benki.

Na sasa TMZ imebaini kuwa Nicki Minaj hakuwa akiongea maneno tu. Imesema kuwwa tayari ameanza kuwatumia fedha mashabiki hao. TMZ imezungumza na baadhi ya mashabiki hao ambao wamethibitisha kuwa wamepokea fedha hizo ambapo mmoja amesema amepokea, $800 na mwingine $500.

Rapper huyo amesema atakuwa na awamu nyingine ya kutoa mpunga kwa mashabiki wake baada ya mwezi au miezi miwili.

“Ok u guys. It’s been fun. Let me make those payments tmrw then see if I have any money left?. I’ll do some more in a month or 2,” alitweet.

MEEK MILL AKUTANA NA ZAWADI YA MAPOKEZI KATIKA SIKU YA KUZALIWA KWAKE


Rapa na mmiliki wa lebo ya Dream Chasers Records ‘Meek Mill’ kufuatia kusherehekea siku ya mfanano wa kuzaliwa kwake siku ya jana alipata mapokezi ya kipekee huko visiwa vya Bahamas ambapo alipotua na kukanyaga ardhi kutoka katika ndege iliyomleta akiwa na timu yake alikutana na bendi ilimpokea kwa nyimbo shangwe na mizuka ya kumtakia mafaniko na siku njema ya kuzaliwa kwake.

Mapema siku ya jumamosi asubuhi Meek alisafiri kwa ajili ya kuianza wikiendi ya kusherehekea kuzaliwa kwake mbali na mapokezi ya bendi pia katika ufukwe wa visiwa hivyo alikutana na kibendela cha rangi ya machungwa kilichokuwa na ishara ya kuheshimu uwepo wake lililopambwa kwa maneno mawili ambayo ni DC maneno yanayosimama kama Dream Chasers jina ambalo linawakilisha lebo yake.

Hata hivyo mbali na kuitumia wikiendi hiyo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pia atafanya matamsha kadhaa yanayoendeleza ziara yake ndogo iliyopewa jina la MeekEND ambapo jana mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa rap duniani kote waliwapatia zawadi ya mixtape inayokwenda kwa jina la Meekend Music yenye ngoma tatu kama zawadi.

YOUNG D ATOBOA SIRI YA TATTOO YAKE YA MWISHO


Rapa kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma Bongo Bahati Mbaya(BBM) Young D ametoa sababu za tattoo yake ya mwisho pindi atakapo amua kufanya maamuzi ya kuchora yake ya mwisho ya kumi na moja.

Akizungumzia idadi ya Tatoo kumi alizonazo mwilini Young D amesema kuwa atakapoongeza atachora tattoo ya mwane anayekwenda kwa jina la Tamali kama heshima kwake.

“nina tattoo kama kumi hivi, na bado moja ambayo nahisi nitafungia mwili ya Tamal ambayo bado sijafikiria nitaichora lini au wapi lakini bado nina plan” Alisema Young D kupitia The Playlist ya Times Fm.

Hata hivyo Young D kazi yake ya Bongo Bahati Mbaya imekuwa kazi ya kwanza tangu ilipofahamika kuwa ameachana na uongozi wake wa lebo ya muziki ya MDB na kuanza kufanya kazi chini ya Studio za Touch Sound na mtayarishaji Mr. T Touch.

NEW VIDEO | TANZANIA ONE SOUL - NI SALAMA | Watch

6 Mei 2017

JLo alinizingua kolabo, ila nitamtafuta Nick Minaj- Shilole


Zuwena Mohamed maarufu kaka Shilole ametoa ufafanuzi wa kushindikana kufanya kolabo yake na Jennifer Lopez(JLo) ambayo msanii huyo alitangaza kufanya nae.

JLo amesema kuwa alisha onana na meneja wa msanii huyo kutokea Marekani na kuongea nae kuhusu mpango wake wa kufanya kolabao, lakini baadae ilishindikana hivyo naye ameshindwa kwenda tena Marekani kutokana na kuwa busy.


“Nilishindwa kurudi tena Marekani kutokana na mambo niliokuwa nayo ikiwemo ya kifamilia na pia Jlo nae alikwa busy busy na nyimbo yake ya “Ain’t your mama” nikaona basi tusisumbuane sana mwache aendelee na mambo yake, ila nitamfuta Nick Minaj.


Baba yangu alinipa jina ‘Majuto’ akiwa gerezani – Ben Pol


Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol, amesema kuwa Baba yake mzazi alifungwa kifungo cha miaka miwili wakati mama yake mzazi akiwa na ujauzito wake.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘ Phone’, amesema baaada ya kuzaliwa alipelekwa na Mama yake gerezani na Baba yake kumpatia jina la ‘Majuto’.

“Baada ya 40, Mama akanipeleka gerezani akaniweka mimi pale kwenye dirisha la kuongea na wafungwa ndipo nikapewa jina pale, sijawahi kusema popote nikaitwa ‘Majuto’. Lakini baada ya kuja kubatizwa ndio nikaitwa Bernard,” Ben Pol alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM.

Pia alisema wakati baba yake yupo gerezani, Mama yake alimlea kwa biashara ya vitumbua pamoja na kuuza maji.

Ben amesema baada ya miaka miwili, Baba yake aliachiwa na kuendeleza gurudumu la maisha kama kawaida.