Ni miaka mingi tulikuwa tukilalamika kuhusu muziki wa Bongo Fleva lini utaweza kutambulika kwenye mataifa mengine huku nikikumbuka Salama Jabir alitumia nguvu kubwa kuponda video za wasanii ambazo zilionekana haziko poa.
Kiukweli ni ujasiri mkubwa aliufanya japo wapo baadhi ya wasanii wakubwa walimchukia kwa kitendo hicho lakini kwa asilimia kubwa amesaidia mpaka wasanii kuanza kutengeneza video nzuri na mpaka sasa tatizo hilo halipo tena.
Huo ulikuwa ni mwanzo nikikukumbusha kuhusu tulipotoka na muziki wetu japo kwa kidogo mpaka sasa tumefanikiwa kulifikia tobo tulilokuwa tunalitaka na hatimaye muziki wetu umepenya na kuanza kufanya vizuri kwenye mataifa mengine huku tukizidi kubarikiwa wasanii wenye uwezo mkubwa vipaji vikubwa kama Chemical, Ray Vanny, Darassa, Bill Nas, Barakah The Prince na wengine.
Hapa sitaki kwenda mbali sana ila nataka kusema kuwa kuna baadhi ya wasanii wanachukuliwa poa kwa sasa lakini endapo wakiangaliwa kwa jicho la tatu na wakipata support ya kutosha watafika mbali zaidi japo kwa sasa wameendelea kuchukuliwa kama ni wasanii wa kawaida tu.
Kati ya wasanii hao ni Darassa na Chemical. Wasanii haa wamekuwa wakichukuliwa kikawaida sana kwenye muziki lakini ni kazi kubwa wanaifanya hata ukifanikiwa kuangalia CV zao kwenye muziki tangu walipoanza kuachia ngoma zao wakiwa hawana zaidi ya miaka miwili tangu wafahamike lakini wameweza kuachia hit kibao na kuwashinda hata baadhi ya hao wasanii wengine wakubwa.
Hata ukiangalia kwa upande wa flow na style wasanii hawa wanatofautiana sana na marapper wengine ambao siku zote wamekuwa wakitumia style moja. Ukisikiliza nyimbo za Chemical kama ‘Sielewi’, ‘Kama Ipo Ipo Tu’ na ‘Mary Mary’ utaona kuna utofauti mkubwa zaidi upo kwenye hizi nyimbo zote tatu.
Vile vile kwa upande wa Darassa ambaye ameanza kuwanyima usingizi wasanii wengine wakubwa ukisikiliza ‘Sikati Tamaa’, ‘Tunaishi’ na ‘Muziki’ kuna utofauti mkubwa zaidi uliopo kwenye nyimbo zote.
Lakini pia ni ngumu kwa wasanii wengi kuachia hit tatu au zaidi mfululizo huku zote zikifanya vizuri kwa wati mmoja lakini kwa Darassa na Chemical imekuwa rahisi zaidi ndio maana wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la ziada kupitia hilo.
‘Kama Utanipenda’, ‘Too Much’ na ‘Muziki’ hizi zote ni hit za Darassa ambazo bado zinafanya vizuri zote kwa pamoja huku Chemical akiwa na ‘Forever (remix)’, ‘Am Sorry Mama’, ‘Kama Ipo Ipo Tu’ na ‘Mary Mary’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni