burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Jun 2017

NEW VIDEO | Ray C - Unanimaliza | Watch


Sehemu hizi za kutembea siku ya Sikukuu ukiwa Dar es Salaam


Kama upo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na umesha maliza pilika piliaka za kuweza kula katika Siku kuu ya Eid basi si haba kuweza kutafuta sehemu ya kupumzika na kufurahia siku hiyo pamoja na familia.

1. Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni

Kama unapenda historia na unataka kujua zaidi kuhusu historia na utamaduni ya Tanzania, Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni ndio sehemu ya kutembelea. Makumbusho haya yanaonyesha mengi yakiwemo urithi wa kikabili, ufundi wa kitamaduni, vifaa vya muziki, sanaa ya kitanzania, historia ya kikolony na ya kisiasa na zaidi.

2. Kijiji cha Makumbusho – Kijitonyama

Makumbusho, kama inavyoitwa kwa kifupi, itakupeleka ndani ya Tanzania vijijini kwa kuonyesha tofauti ya vijiji vya Tanzania, kabila kwa kabila. Wanabaadhi za nyumba za kiasili ambazo unaruhusiwa kuingia. Kwa kifupi, Kijiji cha Makumbusho itakupa uzoefu wa utamaduni ya Tanzania.

3. Kisiwa ya Mbudya

Kama unataka kupumzika fukweni ukiwa Dar, Kisiwa ya Mbudya ndio pakwenda. Njia rahisi kufika mbudya ni kwa kupanda boti kutoka Jangwani Sea Breeze Resort iliyopo Mbezi Beach, na kawaida hakujai. Kwa hiyo, unaweza kutulia hapo kwa raha zako.

4. Coco Beach

Fukwe ya Coco ambayo ipo Msasani Peninsula sehemu hii ni maarufu pia kwa kuza vitu kama mishkaki na muhogo wa kuchoma. Fukwe ya Coco inapendwa sana na familia au marafiki wa aina zote.

5. Kijiji ya Wamakonde, Mwenge

Kama unatafuta sanaa, nguo, viatu, begi, vifaa vya jikoni, chochote kile, utavikuta kwenye Kijiji ya Wamakonde. Eneo lote limetengwa kwa ajili ya kukuza sanaa ya kitanzania. Zaidi ya hapo, mara nyingi wauzaji ndio wasanii wenyewe kwa hiyo wanaweza wakakutengezea kitu chakipekee.

Alikiba na Diamond wananiumiza sana kichwa – Z Anto


Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo Binti Kiziwi,  Z Anto amesema siku  yoyote kuanzia sasa anaachia ngoma yake mpya na video huku akidai watu anaowawaza na kuwafikiria sana kuwa ni Alikiba, Diamond Platnum pamoja na Vanessa Mdee.

Z Anto ameiambia Enewz ya EATV kuwa ujio wake mpya katika muziki wa bongo fleva unakuja kuleta heshima tena ya muziki huo na kusema kipindi yupo kimya alikuwa anajifunza mengi kupitia wasanii wa sasa na kusema ameona mapungufu yao hivyo yeye anakuja kuwafundisha sababu tayari amewasoma na kufanya kitu kupitia makosa yao hivyo watajifunza kupitia yeye.

“Kuna wasanii wengi wanafanya vizuri lakini ambao naweza kusema wanaoangaliwa na wengi ni Diamond na Alikiba pamoja na Vanessa, hawa ukitaka kwenda mbali zaidi au kimataifa unatakiwa kushindana nao na ndio kitu ambacho nakiandaa,”

Muimbaji huyo amedai ukimya wake kwenye game, umeutumia kuisoma tasnia ya muziki ili akirudi asimuache mtu.

Manji aitema Coco Beach


Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kesi aliyoifungua akidai kupewa haki ya uwekezaji katika eneo la Coco Beach lililopo jijini Dar es Salaam.

Manji alishinda zabuni iliyotangazwa na Manispaa ya Kinondoni mwaka 2005, kwa ajili ya uwekezaji wa eneo la Coco Beach karibu na Bwalo la Maofisa wa Polisi lililopo Oysterbay.

Manji ameeleza hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema licha ya kampuni yake kupitia kampuni ya Q-Consult kuingia makubaliano na Manispaa ya Kinondoni Desemba 21, 2007 kulikuwa na ucheleweshaji wa mradi huo.

“Hali hiyo ilisababisha kampuni yetu kutafuta njia ya sheria katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Desemba 17, 2007 na kufungua kesi ya ardhi namba 334 ya 2009 ambapo baada ya miezi sita Mahakama Kuu iliagiza Manispaa ya Kinondoni kutekeleza ahadi yake,” alisema Manji.

“Kwa kutambua maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano tunatii agizo na kuacha eneo hili liendelee kwa matumizi kama ambavyo linatumika sasa.Ninaomba radhi binafsi kwa Rais John Magufuli na Serikali yake kwa sintofahamu yoyote iliyojitokeza wakati wa ufuatiliaji wa jambo hili.”

Hata hivyo Manji alisema wamewaagiza mawakili wao kujitoa kama wapinzani katika rufaa iliyowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutodai gharama zozote walizoingia au hasara ya mapato kwa kuwa masilahi yao sio halali ukilinganisha na manufaa ya jamii.

“Quality Group Limited inatambua na kuunga mkono juhudi zote za Rais Magufuli za kizalendo katika kusimamia rasilimali za nchi yetu,” alisema Manji.

Tuwe wasafi wa roho na mwili – Elizabeth ‘Lulu’ Michael


Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameoneshwa kukasirishwa na vitendo vya uchafu kwa baadhi ya waumini makanisani.

Lulu amesema waumini wawapo makanisani na hata nje wanatakiwa kuzingatia usafi wa mwili na roho kwani kuna muda huwa wanasalimiana wanapokuwa kwenye ibada hivyo kama hawatazingatia usafi huenda ikaleta taabu katika kukamilisha misa au ibada.

“Mnaowekaga Vidole Puani Kanisani,Hamjui kama kuna ule muda wa kupeana mikono au Mnatakaga kugundua nini? Tuwe Wasafi Wa Roho Na Mwili Pia,“ameandika Lulu kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo mrembo huyo ameongeza kuwa kuna siku moja alimuona muumini mmoja akishika pua na leo ameamua kumpa makavu kwa kumuelimisha.

“Wallahy kuna Mmoja alifanya hvyo Pembeni yangu leo Sijampa mkono bali Nimempa UKWELI,“ameandika Lulu.

Unaweza kuwa na akaunti mbili za whatsapp kwenye simu moja


Utumiaji wa simu za smartphone umeweza kusababisha kuanzishwa kwa app nyingi zaidi duniani, hivyyo kupeleka watumiaji kutamani kuongeza application hizo kila kukicha.

Application ya whatsapp ni moja ya app inayotumiwa zaidi kwa sasa, kwa kuzingatia hilo wameamua kuongeza whatsappna kuwa mbili kwenye simu yako. Hivyo basi unaweza kufuta maelekezo ilikuweka whatsapp hiyo katika simu.

Hatua ya kwanza

Download App inayoitwa parallel space kwenye play store

Hatua ya pili

Kama simu yako ni line moja basi weka line nyingine ambayo unataka iwe whatsapp yako ya pili

Hatua ya tatu.

Install application uliyo download kwenye Step 1(parallel space ), kisha ifungue.

Hatua ya nne

Utakapofika kwenye kipengele kinachotaka kuweka number ya simu hapo utaweka namba yako ya pili ili uweze kuwa na whatsapp mbili

Hatua ya tano.

Utaendelea na Steps za kawaida utakazo onyeshwa kama ulivyojiunga na whatsapp ya kwanza.

Hitimisho:

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka na kuanza kutumia whatsapp mbili kwenye simu moja, nakutakia kila la kheri.

BET Awards 2017: Remy Ma amchakaza Nicki Minaj,Beyonce,Chance The Rapper wakwara tuzo (Orodha Kamili)

2017 BET Awards - Show
Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na sherehe za ugawaji wa tuzo za BET jijini Los Angeles nchini Marekani, Tuzo ambazo watu wengi walikuwa wakisubiria kwa hamu kujua mshindi wa kipegele cha Best Female Hip-Hop Artist ambapo kulikuwa na majina makubwa kama Nicki Minaj, Remy Ma,Cardi B Missy Elliott na Young M.A ambapo Remy Ma ameibuka mshindi na kumnyamazisha hasimu wake Nicki Minaj.

Washindi wengine ni mama wa mapacha wawili, Beyonce ambaye ameibuka na tuzo 5 kutoka kwenye vipengele vya Muimbaji bora wa kike wa RnB/Pop, Album bora ya mwaka (Lemonade), Video bora ya mwaka (Sorry) , Muonozaji bora wa video wa mwaka ambapo tuzo wamegawana na Kahlil Joseph kupitia video ya wimbo wa (Sorry) na tuzo yake ya tano kachukua kwenye kipengele cha Viewers’ Choice Award .

Chance The Rapper

Msanii mwingine aliyeibuka kidedea kwa kukwara tuzo nyingi ni Chance The Rapper ameibuka na Tuzo tatu kutoka kwenye vipengele vya Best New Artist,Best Collaboration ambapo ngoma yake ya ‘No Problem’ aliyomshirikisha 2 Chainz ndiyo imechukua tuzo na kipengele cha  Humanitarian Award tuzo hii ya heshima amepewa baada ya kutoa misaada kwenye shule za umma huko Chicago.

Wasanii wengine walioshinda tuzo usiku wa jana ni Bruno Mars, Kendrick Lamar, Solange,Mchezaji wa Kikapu Steven Curry na mcheza tenesi Serena Williams.

Tazama Orodha kamili ya washindi wa tuzo za BET hapa chini.

Best Female R&B/Pop Artist: Beyonce Knowles
Best Male R&B/Pop Artist: Bruno Mars
Viewer’s Choice Award: Beyonce Knowles, “Sorry”
Best Group: Migos
Best Collaboration: Chance the Rapper Ft. 2 Chainz, “No Problem”
Best Male Hip-Hop Artist: Kendrick Lamar
Best Female Hip-Hop Artist: Remy Ma
Video of the Year: Beyonce Knowles, “Sorry”
Video Director of the Year: Kahlil Joseph and Beyonce Knowles – “Sorry”
Best New Artist: Chance the Rapper
Best Actress: Taraji P. Henson
Best Actor: Mahershala Ali
Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award: Lecrae, “Can’t Stop Me Now (Destination)”
Youngstars Award: Yara Shahidi
Best Movie: “Hidden Figures“
Sportsman of the Year: Stephen Curry (II)
Centric Award: Solange Knowles, “Cranes in the Sky”
Album of the Year: Beyonce Knowles, “Lemonade”
Best International Act Europe: Stormzy
Best International Act Africa: Wizkid
Humanitarian Award: Chance the Rapper
Lifetime Achievement Award: New Edition

Gabo amzungumzia Kanumba na Wema Sepetu

Image result for gabo zigamba
Msanii wa Filamu Tanzania, Gabo amesema si kweli tasnia ya filamu imeshuka baada ya kifo cha Steven Kanumba.

Muigizaji huyo ameeleza kuwa watu wengi wanaamini kutokuwepo Kanumba kumedhoofisha soko kutokana alikuwa wenye kuleta changamoto ambayo kwa sasa haipo.

“Sio kweli industry ipo vile vile, kwa hiyo jamaa alikuwa analeta changamoto kwa wacheza sinema wengi sana hivyo baada ya kuondoka ule ushindani ukawa umeshuka, hicho ndio kitu ambacho wanakikosa,” Gabo ameiambia Bongo Dot Home ya Times FM na kuongeza kuwa

“Lakini mimi nisema waendelee kuwa na mapenzi ya dhati ila wasiste kutoa malalamiko yao na kukosoa pale ambapo wanahisi pameenda tofauti kwa sababu changamoto za watu pekee ndio zinabadilisha.Tunajua hapo tunakosea inabidi tufanye hivi, kwa hiyo tunaenda tunabadilika kutokana na mawazo ya watu,” amesema Gabo.

Katika hatua nyingine Gabo amemuelezea muigizaji Wema Sepetu ni mtu wa namna gani katika ufanyaji kazi hasa pale walipokuwa wakishoot filamu yake mpya ‘Kisogo’.

“Ni dada mmoja ambaye yupo na utaratibu wake, ukiufuata na kuusikiliza utafanya nae kazi vizuri sana na atakuwa yupo poa sana. Ukiwa nje ya huo utaratibu unaweza kumuona ni msumbufu na ukamuona kero kwenye kazi,” ameeleza Gabo.

Saida Karoli atoa ya moyoni kwa Darassa na Ray C


Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amewamiminia sifa kibao wasanii wa Bongo Fleva, Ray C na Darassa.

Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya Orugambo, amesema hit song ya Darassa ‘Muziki’ ni vigumu kuja kushuka na kuwataka wasanii wengine hasa wa hip hop kuchukulia hilo kama somo.

“Wimbo wa Darassa utaendelea kuhit, utaendelea kuwa shule kwa waimbaji wa hip hop. Nitapenda watumie akili alizotumia Darassa, mimi naamini wimbo wa Darassa hauwezi kushuka hata siku moja na Watanzania wengi walikuwa hawapendi muziki wa hip hop lakini Darassa kuonyesha njia kwa sababu sasa hivi hadi kwenye harusi wanaimba acha maneno weka muziki, hadi Bungeni,” Saida ameiambia Clouds FM.

Kwa upande wa Ray C Saida amesema licha ya msanii huyo kupitia matatizo mengi bado uwezo wake upo pale pale na kuna baadhi wamejaribu kumuiga ila wameshindwa.

“Kwa kweli Ray C nampenda sana kutoka moyoni tangu zamani, sauti yake ni nzuri haina mpinzania, wasichana wengi wamejaribu kuiga kuimba kama yeye, wanapenda mvuto wake na muonekano wake lakini wameshindwa,” amesema Saida na kuongeza.

“Na ukiangalia Ray C amepitia matatizo makubwa sana hapa katikati lakini napenda kumshukuru Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipomsaidia Ray C, na ningependa Rais wetu wa sasa, Dkt. John Magufuli afanye hivyo ili tuweze kunyanyuka sisi tuliokwama,” ameeleza Saida.

10 Jun 2017

NEW VIDEO | Christina Shusho - U Mwema Wakati Wote | Watch


Picha ya utupu ya Amber Rose yafutwa


Mtandao wa kijamii wa Instagram wenye watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani umefuta picha ya utupu ya mwanamitindo Amber Rose.

Picha hiyo ambayo Amber aliiweka kwenye mtandao huo, ilifutwa kutokana na kukosa maadili. Mara nyingi mtandao huo huziondoa picha ambazo zinaripotiwa kutokuwa na maadili.

Baada ya kufutwa picha hiyo ya utupu ambayo imewatoa udenda vidume wengi mitandaoni, Amber ameandika ujumbe mwingine kwenye mtandao huo unaoonyesha masikitiko yake baada ya kufutiwa picha hiyo huku mashabiki wakimuunga mkono kwa kitendo hicho.



“When IG deletes ur fire ass feminist post but you really don’t give a fuck because everyone picked it up already #amberroseslutwalk #bringbackthebush 😍,” ameandika mrembo huyo kwenye picha hiyo hapo juu.

Hizi ni baadhi ya comment za mashabiki wakimuunga mkono Amber Rose.

mosebjadi_d@lesliefinesse3: stop telling feminists what to do and what not to do.

k.mad:I knew they were going to delete it fuck them

isaacaboagye5:May I join you

laratrv:💓💓

dalanez:So hot

bonniielynn:I got the screenshot boo, fire af 🔥🔥♥️

golfwangfook:I love u😘😘

justveeveekins:I LOVED it

Shaa aeleza sababu ya kufanya kolabo kiurahisi na chipukizi


Shaa afunguka sababu ya kukubali kufanya kazi na wasanii wachanga kiurahisi.

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo Flava ambao hushirikina kwa ukaribu na wasanii chipukizi katika kufanya nao kazi bila hata ya kuwadai fedha.

Akiongea katika kipindi cha FNL cha EATV, Shaa amesema, yeye wakati anaanza muziki akiwa msanii mdogo aliweza kupata nafasi ya kumshirikisha AY kwenye wimbo wake ‘Pambazuka’ bila hata ya kudaiwa hela na msanii huyo, hilo ndio limempelekea kuvutika kufanya kitu kama hicho.

Baadhi ya nyimbo ambazo muimbaji huyo amefanya na wasanii hao chipukizi ni ‘Nikilewa’ wa Nasi kutoka Mbeya, na ‘Mali ya Mungu’ wa Biznea kutoka Mwanza na nyingine.

Madereva watakaovunja sheria kuchapwa viboko


Baraza la Taifa la usalama barabarani limeazimia kuanza mpango mkakati wa awamu ya pili ambao katika utekelezaji wake pamoja na mambo mengine, utahusisha kuwachapa viboko madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.

Hayo yameelezwa jana mjini Dodoma na Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuf Massauni wakati akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa kupunguza ajali barabani nchini kwa aslimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti 2016 hadi Januari 2017.

Massauni amesema kuwa baada ya kuona utelekezaji wa awamu ya kwanza umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali, baraza hilo limeamua kuanzisha awamu ya pili ambapo moja ya mikakati yake itawachukulia hatua kali wale wote watakaokiuka sheria hizo ikiwemo kuchapwa viboko.

Akizungumzia operesheni,usimamizi wa sheria na hatua zilizofikiwa katika kipindi hicho cha miezi sita katika awamu ya kwanza, amesema jumla ya madereva 1,596 walikamatwa, kuwekwa mahabusu na kupelekwa mahakani badala ya kulipa faini ya papo kwa papo kama walivyokuwa wamezoea.

Hata amesema magari 188,602 yalikamatwa kwenye Operationi hiyo kutokana na ubovu ambapo kati ya hayo magari 623 yalifungiwa kutembea kutokana na uchakavu.

Nicki Minaj amdiss tena Remy Ma


Acha movie iendelee – Ni moja ya kibwagizo kinachopatikana katika wimbo wa Number One Remix wa Diamond aliomshirikisha Davido. Sasa kama ulijua bifu la Nicki Minaj na Remy Ma limeisha utakuwa umechelewa.

Mafahari hao wawili wamekuwa katika beef ya maneno tangu mwezi Disemba mwaka jana, baada ya Remy kuanza kumchana Nicki katika wimbo wake wa ‘SHETHER’ lakini alijibiwa na mrembo huyo wa Young Money alijibu mapigo kupitia nyimbo mbili alizoziachia mwezi Februari mwaka huu.

Niki amedaiwa kurudi tena na kumchana Remy kwenye wimbo alioshiikishwa na 2 Chainz’s “Realize”, “I’ve been winning eight years consistently, at least respect it,” amerap mrembo huyo. “Papoose wrote that ‘Ether’ record, but I broke Aretha record / See this is chess, not checkers / You cannot check the checkers / Did Nas clear that ‘Ether’ record? / Nah, but I will complete the record.”

Mwezi Machi mwaka huu Remy alipohojiwa kwenye kipindi cha Another Round, alionekana kulimaliza bifu lake na Minaj huku akiwachana waliokuwa wakishangilia vita yao hiyo, je kwa kuchanwa tena kwenye wimbo huo ataendelea kubaki kimya au Nicki ndio kachkoza nyuki?

Barakah The Prince amjibu Ben Pol


Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol kusema Baraka The Prince anabeza wimbo wake mpya ‘Tatu’ kutokana walimpunguza kwenye show, Barakah amesema hakuna kitu kama hicho na hawawezi kufanya hivyo.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa yeye hapunguzwi bali alijitoa mwenyewe kutokana Ben Pol na Jux hawakutaka kufuata utaratibu wa uogozi wake.

“Mimi sipunguzwi, nilijitoa nikawaambia nina menejiment ambayo ina utaratibu wake, ninapofanya kazi lazima kuwe na makubaliano na mkataba kwa sababu wao walishindwa kufuata utartibu nikajitoa kwenye hiyo show yao,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Hatukuwa na muungano wowote kusema kwamba tulikuwa na tour, tulifanya show moja tu ile, show iliyofuata uongozi wangu ukataka utaratibu wa hizo show waliposhindwa nikawaambia mimi sitaweza kufanya. Sema nyimbo yake ni mbaya asitafute sababu ya kujitetetea… utovu wa nidhamu yule (Ben Pol) baba yangu?,” ameongeza Barakah.

NEW VIDEO | B GWAY Ft. NAY WAMITEGO - SIJACHUKIA | Watch

B GWAY and NAY WAMITEGO - SIJACHUKIA

NEW VIDEO | RAYVANNY - MBELEKO | Watch

RAYVANNY - MBELEKO