burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

10 Jun 2017

Barakah The Prince amjibu Ben Pol


Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol kusema Baraka The Prince anabeza wimbo wake mpya ‘Tatu’ kutokana walimpunguza kwenye show, Barakah amesema hakuna kitu kama hicho na hawawezi kufanya hivyo.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa yeye hapunguzwi bali alijitoa mwenyewe kutokana Ben Pol na Jux hawakutaka kufuata utaratibu wa uogozi wake.

“Mimi sipunguzwi, nilijitoa nikawaambia nina menejiment ambayo ina utaratibu wake, ninapofanya kazi lazima kuwe na makubaliano na mkataba kwa sababu wao walishindwa kufuata utartibu nikajitoa kwenye hiyo show yao,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Hatukuwa na muungano wowote kusema kwamba tulikuwa na tour, tulifanya show moja tu ile, show iliyofuata uongozi wangu ukataka utaratibu wa hizo show waliposhindwa nikawaambia mimi sitaweza kufanya. Sema nyimbo yake ni mbaya asitafute sababu ya kujitetetea… utovu wa nidhamu yule (Ben Pol) baba yangu?,” ameongeza Barakah.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni