Uhondo zaidi tazama video hii...
Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
27 Ago 2017
26 Ago 2017
BAISA MHELA AWAONYA WAIMBAJI WANAOKATA TAMAA
Mwimbaji Wa music Wa injili ambaye anakuja kwa kasi nchini Tanzania
Aliendelea kusema ukitazama sababu kubwa zinazowafanya watu kukata tamaa
Ni ghalama za studio
Ghalama za nauli
Na mengineyo kama mavazi kukatishwa tamaa na watu wanaowazunguka
Akaonya kwa kusema Waimbaji wanapaswa kujielewa kwamba wanafanya kazi ya Mungu na kikubwa na Mungu wetu ni tajili hakosi kitu wala hashindwi kitu hivo wakiomba kwa mwenye kazi yake hatawanyima
Aliongeza kwa kusema biblia inaeleza kabisa jinsi yesu alipowauliza wanafunzi wake kwamba JE MLIPUNGUKIWA NA KITU NILIPOWATUMA BILA KITU BILA MKATE BILA MAVAZI NA WANAFUNZI WALIJIBU HAPANA
Maana yake Mungu anapokutumia anakutumia kutangaza neno lake kama ulivo na hatokuacha atakulisha atakulipia na atakujaza na yote baada ya kuona hekima yako.
Aliwaaonya waimbaji wote na wainjilist mitume na manabii kutovaa sana ubinadamu Wa kulaumu au kulalamika bali wayapokee yote kama razalo mtumishi Wa Mungu katika bibilia
JUX AFUNGUKA KUHUSU NGOMA YA ‘UTANIUA’ KUYAZUNGUMZIA MAHUSIANO YAKE NA VANESSA MDEE
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Juma Mussa Mkambala a.k.a Jux ameyazungumzia mahusiano yake na muimbaji Vanessa Mdee na kwa namna ambayo wimbo wake mpya wa ‘Utaniua’ katika wazo la mahusinao yake na kupatikana kwa wazo zima la wimbo.
Akizungumza na G.LOVETZ Jux amesema kuwa ingawa maandalizi ya kufanya wimbo huo kupitia mdundo uliotumika katika wimbo yalikuwepo lakini kukamilika kwa wazo la wimbo umezungumzia zaidi hali ya kimapenzi na kuachana kwake na mpenzi wake wa zamani muimbaji Vanessa Mdee.
“Sasa hivi ni miezi mitano tangu tume-break up, …kitu ambacho nimekiimba kwenye ile nyimbo ni kitu ambacho nilikuwa katika ile hali ya hivyo, kitu ambacho nimekiongea nimekitoa moyoni kwangu yaani ni nyimbo ambayo nimeiimba kutoka moyoni na mtu aliyesababisha kuimba kwenye ile nyimbo ni Vanessa” Amesema Jux.
MASHABIKI WALIA NA PENZI LA JUX NA VANESSA MDEE
Staa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Juma Jux na muimbaji Vanessa Mdee kwa mashabiki imeonekana kuwa walipendezwa sana na uliokuwa uunganiko wao kama wapenzi na huku maoni ya wengi yakionekana kuwaomba warudiane na baadhi yao kujaribu kutuma maombi kwao.
Baada ya mahojiano ya Jux na G.LOVETZ maoni ya wini yameibuka wakiwataka wamelize tofauti yao na warudi kuwa wapenzi kama zamani kulingana na kile walichokisikia kutoka kwa Jux ambapo amebainisha kuwa wazo la wimbo wake mpya lilizaliwa kutokana yeye kuwa kayika panda shuka za kimahaba na Vanessa.
Hata hiivyo kwa maoni ya baadhi ya waliomsikia Jux katika maojiano imehisiwa kwamba waligundua kuwa bado kuna mahaba ya dhati kwa Jux, hivyo sio vyema kama hawatarudiana.
ASLAY BAADA YA ‘LIKIZO’ AJITOKEZA KAMA SIMBA
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Aslay baada ya kuzungumziwa sana kwa kasi yake ya kuachia nyimbo baada ya nyingine bila kuwaachia nafasi ya mashabiki kupumua, amedondosha nyingine ambayo mara hii iko katika maadhi na muonekana kama SIMBA.
Imani ya Rastafarian ni ya jamii ya Jamaica ambayo ndo muonekana wa ngoma mpaka miondoko yake, Aslay ameachia wimbo wake mwingine alioupatia jina la ‘Pusha’ uliyoko katika maadhi ya Reggae na katika kuweka msisitizo zaidi alivyoonekana unaweza kumuita Rastaman.
Hata hivyo kwa mahesabu ya haraka haraka ndani ya muda usiopungua miezi minne Aslay ameachia nyimbo zisizopungua sita ambazo zimetoka sambamba na video bila kujali kuwa ataweka msongamano wa nyimbo nyingi katika mzunguko wa uchezwaji katika vituo vya matangazo ndani na nje ya Tanzania.
Dayna Nyange aungana na A.Y, Diamond na Vanessa Mdee katika hili
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amezungumzia muonekano wake mpya baada ya kuweka meno ya gold.
Wasanii kadhaa wa Bongo Flava wameshafanya hivyo miongoni mwao ni AY, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Dogo Janja lakini katika mtindo wa kuweka na kutoa.
Muimbaji huyo amesema wasanii wengi walifanya hivyo lakini walikuwa wananunua yale meno ya kuweka na kutoa lakini alivyoweka yeye ni tofauti kwani huwezi kuyatoa hadi pale atakapoenda kwa wahusika ili kuyatoa.
“Niliwekea South Africa, unaweka booking for four days or one week, wanaenda wanakuchonga meno kidogo then wanaweka, kwa hiyo siyo kitu ambacho naweza kusema sasa hivi nataka kukituoa nikaweza,” Dayna ameiambia Bongo5.
“Sijajua kwa Wabongo kama naweza nikapata hiyo huduma kwa sababu nilishawahi kujaribu kuweka kikaja kikatoka wakati nafanya video ya Komela, kwa kuwa hakikua na utaalam,” ameongeza.
Dayna ameendelea kwa kusema alipoenda ku-shoot video yake mpya ‘Chovya’ South Africa ndipo alipotumia fursa hiyo kufanya hivyo kwa mara ngingine tena.
“Nikaona let do it, so nikawa nimeweka, ni gold huwezi kuweka bati mdomoni unaweza kuharibu utumbo. Thamani yake si kubwa sana, dola kadhaa tu,” amesema Dayna.
Afande aibuka baada ya kutajwa kwenye Zilipendwa ‘msiba hauwahusu’
Msanii mkongwe wa muziki wa hop hop, Afande Sele baada ya kujwa kwenye wimbo Zilipendwa wa WCB, amedai amependezwa na kitendo hicho kwa mpongeza Diamond Platnumz.
Wimbo ‘Zilipendwa’ uliowahusisha wasanii wote wa WCB, umeibua maswali mengi kwa baadhi ya mashabiki kutokana na maudhui ya wimbo huo kwa kuwataja baadhi ya mastaa wa zamani akiwemo Afande Sele.
Afande Sele amesema hajachukizwa na kitendo cha kutajwa kwenye ‘Zilipendwa’ na kuonesha kufurahia jambo hilo mbali na wengine huku akiwaambia walioupokea vibaya msiba hauwahusu.
“Sana mdogo wangu nyakati zinabadilika huu muda wa akina Damian sio nyakati za Burning Spear au Bob Marley , ndio maana nikawa Muhenga, wamuache Dogo afanye kazi zake #safiplatnumdiamond.,” aliandika Afande Instagram.
Wasanii wengine waliotajwa kwenye wimbo huo ni H Baba, Mr Nice pamoja na wengine wengi.
Wimbo huo umeachiwa muda mchache baada ya Alikiba kutoka RockStar4000 kuachia wimbo wake mpya, Seduce Me.
Ommy Dimpoz atuma dongo baada ya WCB kuachia ‘Zilipendwa’
Baada ya Ommy Dimpoz wiki hii kuandika ujumbe ambao uliichafua team nzima ya WCB na baadaye kuufuta, mkali huyo wa wimbo Cheche, Jumamosi hii amepost tena na kuufuta ujumbe mwingine ambao unaodaiwa kuwa ni dongo kwa WCB ambao wameachia wimbo mpya ‘Zilipendwa’
Wadau wa mambo wamedai Ommy Dimpoz ametuma ujumbe huo baada ya WCB kuachia wimbo mpya muda mchache baada ya mpinzani wao mkuu, Alikiba kuachia wimbo, Seduce Me ambao mpaka sasa unaongoza kupitia mtandao ya YouTube.
Muimbaji huyo wa RockStar4000 alipost picha ya tembo mtandaoni akimaanisha Alikiba akiwa amezungukwa na simba wengi ambao wanadaiwa kuwa ni team ya WCB
Picha hiyo alikuwa na ujumbe, “Watoto Wangu eeeh!! eeehh!! Mimi Baba Yenu eeeeh!! Sina Nguvu tenaaa Eeeeh za kuua Tembooo.
Watoto: Sawa Baba tunakuja kukusaidia Sema itabidi tutumie zilezile mbinu zetu za UJANJA UJANJA si Unajua sikuhizi hayuko peke yake kuna mwingine kajificha”
Ujumbe huo umetafsiriwa na wadau wa mambo kwamba Diamond alishindwa kupambana na Alikiba peke yake ndipo alipoamua kuachia wimbo akiwa na wasanii wake (WCB) ili kupamba na muimbaji wa RockStar4000.
25 Ago 2017
Fid Q afunguka kuchukizwa na Dimpoz, ‘Mimi siyo team Kiba wala Diamond’
Baada ya maneno kuwa mengi kuhusu ngoma yake ya Fresh Remix, Fid Q amefunguka na kusema hakujua kama mistari ya Diamond ilikuwa na lengo la kumdiss Alikiba kwa sababu yeye ni mtu wa hip hop na hajui chochote kuhusu Bongo Flava.
Rapper huyo ameeleza kuwa alikuja kujua hilo wakati wimbo umeshatoka hata hivyo hakuona kama kuna kibaya kilichofanyika kama inavyodai ila hajapendezwa na kitendo cha Ommy Dimpoz kuchukulia suala hilo binafsi zaidi na kuondoa maana ya burudani.
“Ok nyimbo imeshatoka na ndio imekuwaa hivyo nikaangali kama upande ule mwingine watasikia hii kitu na you know it entertainment industry, wataipokea kama biashara yenyewe ilivyo, huenda nao wakasema Fid na sisi tunataka hii beat because am cool both of side, mimi siyo tema Diamond, siyo team kiba nawapenda wote ningewagea beat,” amesema.
“Lakini niwe muwazi hiyo hope ilifutwa nilipokutana na post ya Ommy Dimpoz, kwamba ameweza kubadilisha ile burudani yote na kuipeleka katika kitu binafsi kabisa, imeniondolea lile vibe,” Fid Q ameiambia Clouds Tv.
Hata hivyo Fid Q ameongeza kuwa alichofanya Diamond siyo disrespect kwa Alikiba bali ni battle skills na siyo taarabu kwa watu wengi walivyokuwa wakidai katika mitandao.
“Hip hop majibizano yapo unakuwa unamgusia vitu vyako kwa kupitia muziki na msanii unashauriwa unapokuwa na ishu na mtu njia sahihi ya kuwasilisha ni kupitia muziki huo huo. Sitaki kusema Kiba alikosea kwa kujibu kwa tweet labda hakujisikia kuingia studio kufanya, yale ni maamuzi yake na menejiment yake hatuna budi kuyaheshimu,” amesema Fid.
Alipoulizwa mtazamo wake ni upi kuhusu beef ya Diamond na Alikiba, Fid alisema kila mmoja ana team yake ya mtandaoni ambayo ipo imara ila kilichomkuta ni kuoga matusi kutoka kwa team Kiba.
“Kuna mtu aliniambia Fid umefanya ngoma na Diamond tengemea matusi kutoka kwa team Kiba ya online, nimeoga matusi sana ambayo sijawahi kuyaoga. Watu wamenidhalilisha sana, nasikitika kwamba nimevisoma lakini kujibu mtu siwezi kwa sababu wengi wamenihukumu katika vitu ambavyo si vyangu mwenyewe kwa hiyo nimeamua kuwaacha muda utazidi kuwaponya zaidi ,” amesisitiza.
Fresh Remix ni ngoma ya Fid Q ambayo amemshirikisha Diamond na Rayvanny, kutokana mistari ya Diamond kuonekana inamlenga Alikiba, naye alijibu kupitia mtandao wa twitter. Siku iliyofuata Diamond aliachia audio clip katika mtandao wa Instagram ambayo inaaminika ilimlenga Ommy Dimpoz na Alikiba, ndipo Dimpoz alipochua uamuzi wa kuandika maneno makali kwa Diamond na familia yake katika mtandao wa Instagram.
Kesi ya Usher Raymond yafika patamu
Huenda kesi inayomuandama mwanamuziki Usher Raymond, ikafutwa wakati wowote endapo tu jaji wa mahakama akiridhia ombi lililotolewa na mwanasheria wa msanii huyo juu ya kutokumwambukiza mtu ugonjwa wa zinaa.
Usher Raymond alishutumiwa kumuambukiza ugonjwa wa zinaa mrembo Quantasia Sharpton. Kupitia mwanasheria wa mrembo anayedai kuambukizwa ugonjwa huo Lisa Bloom, aliiomba mahakama kumlazimu msanii huyo amlipe mteja wake fidia ili aweze kujitibu ugonjwa alioupata kutokana na kujamiia naye.
Hata hivyo mwanasheria wa msanii huyo amepinga madai hayo na kusema kuwa mteja wake hana na hajawahi kuwa na ugonjwa wowote wa zinaa na ni mtu anayejali afya yake kwa kuzingaztia matumizi mbalimbali ya kinga kabla ya tendo.
Pia zimeeleza kuwa kama msanii huyo hakuwa na ugonjwa wa zinaa hivyo basi huwenda mrembo huyo alikuwa nao na alitaka kumuambukiza Usher.
IDRIS SULTAN AJIALIKA MWENYEWE KWENYE UZINDUZI WA HEAVEN SENT YA WEMA SEPETU
Idris Sultan haishi visa. Mchekeshaji huyo amejialika mwenyewe kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Wema Sepetu, Heaven Sent wikiendi hii Mlimani City.
Ametumia karatasi kuandika mualiko huyo na kuweka picha yake Instagram akiandika,” Thank you ☺️ @wemasepetu ee jamani badae #RoadToHeavensentPremiere #Wakujialika #SioHabari.”
Utani huo wa Idris kwa Wema unazidi kuwaweka tena karibu mastaa hao waliowahi kuwa na uhusiano. Hivi karibuni Wema alimpongeza ex wake huyo kwa kuanzisha brand yake ya viatu, SultanXForemen. Uzinduzi wa viatu hivyo unafanyika wiki hii.
NIMENUSURIKA KUUAWA KWA BASTOLA – BOB JUNIOR
Msanii na mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Bob Junior ameiambia G.LOVETZ kuwa usiku wa kuamkia jana alitolewa na kutishiwa kwa bastola na watu wasiojulikana.
Amesema, ” Usiku wa saa nne maeneo ya Kinondoni Mwanamboka nilikuwa natokea maeneo ya Kinondoni napita Mwana mboka sheli kutia mafuta, so nilivyofika pale pale sheli kuna mambo fulani yalitokea,” amesema muimbaji huyo.
“Ndo wakatokea vijana wa kiarabu wawili wakanitolea bastola kwa bahati nzuri ni bado ilikuwa mapema na mimi nilikuwa na watu kwenye gari so nikanusurika,” ameongeza.
Amesema baada ya tukio hilo alilazimika kuripoti polisi ambao wanafanya uchunguzi. Hadi sasa hajaweza kujua nini lilikuwa lengo la watu hao.
RUBY AKANUSHA TETESI ZA KUWA MJAMZITO ‘SIJAWAHI KUWA NA MIMBA’
Ruby ametolea ufafanuzi tetesi za kuwa ni mjamzito. Akipiga story na Dizzim Online, mrembo huyo amasema tatizo la watanzania wengi wanapenda kujipa majibu wenyewe ambayo kwa asilimia kubwa yanakuwa sio ya kweli.
“Maneno wameumbiwa binadamu na huwezi kuyazuia,” amesema. “Ila kiukweli kabisa leo hii nathubutu kusema kuwa mimi sina mimba na sijawahi kuwa na mimba isipokuwa ile nguo niliyokuwa nimevaa ilikuwa inaonesha hivyo na hiyo siku nilikuwa nimetoka kula na pozi pia ambalo nilikuwa nimeweka so ikapelekea kuonekana nina mimba lakini nakanusha mimi sina mimba,” amesisitiza.
Kwa siku za karibuni Ruby alikuwa amewaacha njia panda mashabiki wake baada ya kupost picha kwenye mtandao wa Instagram akionekana kama ni mjamzito.
Sijawahi date na star na sitaki – Dayna Nyange
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hajawahi kutoka kimapenzi na star yeyote Bongo na hataki kufanya hivyo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’, amesema sababu ya maamuzi yake ni kufanya mahusiano yake kuwa binafsi zaidi.
“No siyo star, sijawahi date na star na sitamani ku-date na star na sitaki ku-date na star na sito-date na star,” Dayna ameiambia Bongo5.
Pia msani huyo ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano lakini anapenda kuyafanya siri sana kiasi kwamba hata mama yake mzazi hajui.
“Naogopa atakasirika ataniacha kwa sababu nampenda, ni mtu ambaye ana wivu, nilishawahi kusema sina mahusiano akachukia nikaoni ok, isiwe shida nipo kwenye mahusiano lakini hayatambuliki kokote hata mama hamjui,” amesema Dayna.
24 Ago 2017
Nay wa Mitego atoa ushauri kwa Diamond, Ommy Dimpoz na Alikiba
Nani kama mama? Rapper Nay wa Mitego ameonekana kuumizwa na silaha ya maneno mazito aliyoyatumia Ommy Dimpoz katika kumuangamiza adui yake.
Kupitia mtandao wa Instagram, Nay ameamua kuingilia kati kwa kuwataka wasanii hao Diamond, Ommy Dimpoz na Alikiba ambao kwa sasa vita yao inaonekana kuanza kufika mbali, wasiwaingize wazazi katika ugomvi wao huo.
Gombaneni, Loganeni Mpaka Muuwane… Napenda Kusikia Challenge Kwenye Game, Ila Tusiwaingize Wazazi Wetu🙏🏿 Please. Tutukananeni Matusi Yote Wenyewe Kwa Wenyewe Ikibidi Piganeni Kabisaaaa Atakae Kufa Tutazika na Itakua Historia Kama Big na Pac. Ila Kuwaingiza Wazazi ni U #Maku
Sipo Upande Wowote, Si #Kiba #Mond Wala #Ommy. Endeleeni na Vita yenu Kama Wanawake Mmechukuliana Mabwana. Ila Swala la Wazazi Mnavuka Mipaka #Maku nyie.!
23 Ago 2017
20 Ago 2017
EXCLUSIVE INTERVIEW Mr medical NA G.LOVETZ ADAI ANAMPANGO WA KUFANYA MAPINDUZI YA MUZIKI NDANI YA IRINGA NA TZ (Audio)
unajua muziki ninaofanya una ladha na vionjo tofati na wengine pia nna plani ya kuachia kichupa kikali ambacho kila mtu atasema yes kazi nzuri
Mapokezi ya ngoma yangu yako poa sana mana wengi hawakutegemea mimi kutoa kazi nzuri kiasi kile wengi walisema yess kazi nzuri
pia nawashukulu sana sana mafansi wangu kwa mchango mkubwa wanaonionesha
EBHANA NI MENGI SANA HUYU MCHIZI ALIYAONGEA ILA YOTE YAPO HAPO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI
KUSIKILIZA NA KUDAWNLOAD INTERVIEW YA
Mr medical
GUSA
SHILAWADU Watolewa Nduki na Mbwa Nyumbani kwa Alikiba.
Imebainika kuwa licha ya vijana hawa wa shilawadu kuwa na kipaji cha kunyapia umbea, wanakipaji kingine cha ziada cha kukimbia mbio fupi na hata zile ndefu kwa kasi kubwa zaidi hata kumshinda Usain Bolt.
Hayo yamebainika baada ya vijana hao kunyapia umbea nyumbani kwa Alikiba mda wa usiku na kukutana na bonge la mbwa jike aitwae rubi ambae hata hakuwabwekea lakini kutokana na uzoefu na kumbukumbu za hivi karibuni za kuingiliwa katika eneo lao la kazi na machine gun za kisasa waliamua kufunga turbo kwenye miguu yao na kukimbia mbio mithili ya mashindano ya olympic hali iliyopelekea kukosa umbea uliowapeleka kwa King Kiba, mzee wa Aje anayemiliki BMWX5 la kisasa kabisa...
16 Ago 2017
EXCLUSIVE INTERVIEW G.LOVETZ Vs SISTER RAHIMA AELEZA MENGI JUU YA MUZIKI WAKE (Audio)
akiongea na G.LOVETZ kwa njia ya simu SISTER RAHIMA amesema Kwa sasa video yangu ilipofika namshukulu mungu kwa kweli mana bila yeye nisingeweza kitu na pia kazi ikiwa nzuri ndo chanzo cha msanii kukubalika na watu
kwa upande wa kushoot video haikunisumbua sana sababu nilishajipanga na pia niliipania sana na location ilikuwa huku huku zenji ingawa watu hawaamini kwa jinsi ilivotokea
Na nimejipanga haswa katika usambazaji wa video yangu na hivi karibuni nakuja dar kwa ajili ya hii video yangu na baada ya hii kuna vitu vingine vinakuja siwezi kuvitaja mana nataka iwe zawadi ya ghafla kwa mashabiki wangu,alisema SISTER RAHIMA
kwa upande wa kushoot video haikunisumbua sana sababu nilishajipanga na pia niliipania sana na location ilikuwa huku huku zenji ingawa watu hawaamini kwa jinsi ilivotokea
Na nimejipanga haswa katika usambazaji wa video yangu na hivi karibuni nakuja dar kwa ajili ya hii video yangu na baada ya hii kuna vitu vingine vinakuja siwezi kuvitaja mana nataka iwe zawadi ya ghafla kwa mashabiki wangu,alisema SISTER RAHIMA
KAMA BADO HUJAKIONA KICHUPA CHA SISTER
BONYEZA
NI mengi sana alifunguka kuhusiana na muziki wa sasa
kumsikiliza na kudanwload
Barnaba, Gigy Money Wakana si Wapenzi...Picha Waliyopakatana Yawa Gumzo Mitandaoni
Baada ya Gigy Money na Barnaba kupiga picha wakiwa wamepakatana na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wakidaiwa kwamba ni wapenzi, Elias Barnaba ‘Barnaba’ na muuza sura Gift Stanford ‘Gigy Money’ wameibuka na kudai kuwa wao si wapenzi.
Awali kulikuwa na nyepesinyepesi zikidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana wakiwa wamepakatana katika maeneo mbalimbali, wakisema baada ya Barnaba kuachana na mkewe, aliamua kujiweka kwa mwanadada huyo asiyeishiwa matukio mjini.
kwa upande wake Barnaba, alisema Gigy Money ni dada yake kama walivyo madada wengine na katika maisha yake haishi kwa skendo hivyo wanaosema hivyo siyo kweli.
Kwa upande wake Gigy, alisema Barnaba ni kaka yake na pia shemeji yake, kwani ni rafiki wa aliyekuwa mpenzi wake, Mo J na hiyo picha walipigwa wakiwa kwenye shoo hivyo hakuna suala la mapenzi kati yao.
Barua yamchanganya Shilole, atoa neno
Msanii wa Bongo Flava, Shilole amejikuta akisisimuka mara baada ya kupokea barua kutoka kwa mtoto wake ‘Rahma’.
Kupitia mtandao wa instagram Shilole ameweka barua ambayo ameandikiwa na binti yake huyo na kueeleza kuwa haamini jinsi amekuwa lakini katika yote hajutii kuwa mama.
Rahma binti yangu umeniliza na hii barua yako Siamim km Mungu amenikuzia kiasi hiki mpk leo katoto kangu ka pili kananiandikia maneno mazito hivi. Nakupenda sn mwanangu wewe na dada yako ndio urithi wangu na furahayangu….Nikivurugwa hukoo na ya ulimwengu nikitud nyumban nyio ndio faraja yangu.
Simkufuru Mungu kwa kuishi maisha ya shida niliyopitia, sisikitiki kwa kukosa elimu bora na kutimiza ndoto zangu nyingi nilizokuwa nazo nachojua MIPANGO YA MUNGU SIO KAMA YA MWANADAMU….Namshukuru kwa kila alichonipa, jina, umaarufu, rizki, marafiki na ndugu wa kweli lkn zaidi WATOTO wangu ambao kila iitwapo leo ndio mnanipa nguvu ya kuamka kupambana kuvumilia matusi vikwazo na kila vipingamizi. Nataka msome mtimize mdoto zenu nizeeke nikiona mnakuwa mabinti wa kuigwa na mumpendeze Mungu na wanadamu.
KAMA KUNA JAMBO NINAJIVUNIA KULIFANYA SAHIHI DUNIANI NA SIJAWAHI LIJUTIA NI MIMI KUKUBALI KUWA MAMA. By the way ndugu zangu sijui kizungu nimekielewa vizuri.
Fid Q atoa Darasa kwa ma-director wa video Bongo
Msanii wa hip hop Bongo, Fid Q amewapa somo madirector wa video kutoka Bongo kwa kuwataka kutoamini katika kufanya kazi pekee yao.
Rapper huyo amesema kipindi cha nyuma madirector walikuwa wakilalamika kuwa wasanii hawawapi bajeti ya kutosha na ndio sababu ya kufanya video chini ya kiwango lakini hata pale walipopewa bado hakuna kilichobadilika.
“Kwa hiyo shida ikawa siyo bajeti suala ni namna wanavyofanya wao masuala ya quality ya picha na color grade. Sasa hivi madirector wa Bongo wapo vizuri na kama haitoshi siku hizi wamekuwa na DOP (director of photo) ambao wanachukua picha nzuri, kwa hiyo tumeanza kupata video kama za South Africa na sisi,” ameiambia Ladha 3600 ya E Fm.
“Wanasema give credit panapo husika, kwa hiyo naomba niwape pongezi hizo wanafanya kazi nzuri, cha msingi wasiamini katika kufanya kazi wao pekee yao bila hata kushirikiana,” amesema Fid Q.
Ameongeza kuwa “unajua kuna siri moja ya ndani kidogo watu hawajui, unajua GodFather hafanyi mwenyewe zile video yeye anadirect tu halafu anachagua nani ataenda kuedit, GodFather sio mnyama wa video yeye anajua nani afanye naye kazi”.
Fid Q kwa sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili mpya ambazo ni Fresh na Ulimi Mbili.
Usher Raymond hana mpango wa kumlipa mtu
Usher Raymond hana mpango wa kulipa fedha yoyote kwa watu waliomshtaki kwa madai ya kuwaambukiza ugonjwa wa ngono.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Usher, ameuambia mtandao wa TMZ, msanii huyo hana mpango wa kukutana na mtu yoyote kuhusu jambo hilo.
Hivi karibuni Usher alishtakiwa kwa kumuambukiza na kumlipa mtu ambaye alitambulika kama mbunifu wa mavazi yake kiasi cha dola milioni 1.1 Disemba 28, 2012 kwa kumuambukiza ugonjwa huo unaodaiwa kuwa wazinaa.
Mpaka sasa wanawake watatu na mwanaume mmoja wamejitokeza wakidai kuambukizwa ugonjwa huo na msanii huyo.
Dawa za kulevya zamtia Chid Benz mikononi mwa Polisi
Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema Chid Benz amekamatwa na watuhumiwa wengine saba kufuatia msako mkali uliofanyika August 12 majira ya jioni.
“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema.
Chid Benz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Muda’ aliyomshirikisha Q Chillah si mara ya kwanza kukutwa na tuhuma kama hizo kwani alishawahi kukamatwa na dawa za kulevya aina bangi mkoani Mbeya.
Diamond anahusika kufanikisha kolabo ya Madee na Tekno
Msanii Madee amebainisha kuwa Diamond Platnumz anahusika kufanikisha kolabo yake na Tekno.
Madee amesema haikuwa ngumu sana kumpata muibaji huyo kutoka Nigeria na pia si yeye aliyeangaikia kolabo hiyo na hata pale Tekno alipoangalia kazi zake hakuwa na pingamiza kuhusu kufanya hiyo ngoma.
“Nilimuelezea tu Babu Tale pamoja na Diamond, bwana naweza kufanya kazi na Tekno?, wakasema inawezekana ngoja tumuambie nakumbuka alikuwa hapa hapa Dar es Salaam, wakamwambia akasema nipeni kama lisaa limoja ili nimuangalie huyu Madee,” ameiambia Bongo5 na kuongeza.
“Nadhani katika hilo lisaa limoja ndio akawa anamuangalia Madee ni nani, amefanya nini na ana impact gani baada hapo akawajibu its ok tunaweza kufanya lakini production nafanya mimi kwa sababu yeye ana studio,” amesema.
Ameongeza kuwa, “kwa hiyo akapiga ile biti akafanya vocal akaja tena Dar es Salaam kwenye mishe zake akatupatia ile biti pamoja na vocal nikaweka vocal zangu akapewa tena alipoona ipo ok, ndio ikanyika mixing WCB,” amesema.
Roma arudi nchini kimya kimya, Aahidi kuweka wazi kila kitu kuhusu ‘Zimbabwe’
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki amewasili jana usiku akitokea nchini Zimbabwe alikoenda kikazi.
Roma Mkatoliki ambaye ameachia wimbo wake mpya wa Zimbabwe wiki iliyopita amejikuta akisakwa na vyombo vya habari kuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo lakini hakuwepo nchini na kumuachia jukumu hilo la kutambulisha wimbo huo kwenye Media, mke wake.
“Kiukweli nimechoka wanangu what i need ni kuona familia yangu, mke wangu na mtoto na ndugu, jamaa na marafiki”,amesema Roma Mkatoliki jana usiku alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, jijini Dar es salaam.
Alipoulizwa ni kwanini alimtuma mke wake aachie wimbo huo ile hali alikuwa nje ya nchi Roma Mkatoliki amesema alifanya hivyo kwa sababu muda ulifika wa kutoa ngoma hiyo na tayari alifanya booking na Media, lakini alikataa kuzungumzia wimbo huo wala kueleza alichoenda kufanya Zimbabwe huku akiahidi mashabiki wake kuwa kuanzia leo ataanza Media Tour kuuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo .
Wakazi, Stamina, Ndugu jamaa na Marafiki zake wa karibu wa Roma walikuwepo kwenye mapokezi hayo ambayo yalikuwa kimya kimya.
13 Ago 2017
11 Ago 2017
Mwanamke Chezea Pesa, Mshahara, Mali Hata Kazi Chezea ila Usicheze na Umri au Muda....
Kipindi nasoma sekondari tulikuwa na kijimsemo kuwa TIME IS MAKANGABILITY tukimanisha muda haupo upande wetu yaani tumechelewa.
Naomba nitoe onyo kwa akina dada hasa wasomi ambao ndiyo huwa wanajiona ukisoma kila kitu kimekwisha.
Kama kuna vitu mdada akikosea timing anaweza juta maishani ni pamoja na MUDA WA KUOLEWA (married is timing for girls). Sababu ni kama zifuatavyo hapa down.
Mosi, mdada huwa anaanza kuvutia kati ya umri wa miaka 15-25, kipindi hiki hutuvutia sana sisi wanaume reference(mimba za mashuleni hasa sekondari 14-18). Kipindi hiki 14-18 binti huwa kama UA WARIDI huku wanaume tukiwa VIPEPEO kumfuata kila aendapo, kwa mdada mjanja hapa huanzisha uhusiano kisiri na mkaka anaye mzidi kidogo (FORM ONE na FORM4). Hii ni ratio murua hapa binti kipindi anamaliza form six bfriend wake atakuwa namalizia chuo hivyo akiwa chuo ataolewa au akimaliza(kumbuka huwa kuna changamoto za kukosa kazi).
Pili, ni kwa kipindi hiki cha miaka 18-22, binti hufuatwa na wanaume wengi wazuri, wenye maono na nia ya kuoa, sababu huvutia na waoaji huwa kati ya miaka 25-28 ni wengi sana. Wasichana wengi katika umri huu huwa ndiyo wamekolea katika kula hujana, sababu huwa ni kipindi cha kupata uhuru(freedom gain) hapa achungwi tena na wazazi, walimu na watu wengine wanao mtakia mema. Wengi huona kuolewa km kifungo na huepuka ndoa.
Tatu, kati ya umri wa 23-25, hapa wengi wanaachana sana na bfriend wao wa zamani sababu ya kufuatwa na wanaume wengi ambao pengine wanasifa za ziada kuliko wazamani(kipya kinyemi walisema wahenga). Shida huibuka wanaume wengi wanaowafuata huwa wameshindwana na wadada wa type kama yao hivyo hujikuta wakitua kwa watu wale wale hivyo wakishaona hivyo ni kula na kuondoka bila kushukru ama kuosha vyomba sababu hapa mwanaume huona kila mdada ni malaya hana mapenzi ya dhati hivyo mipango ya kuoa siyo defined tena.
Nne, 25-28, hapa ni kipindi cha kujifariji "soon i will find me life partner" ila mambo huwa tofauti jamaa(wanaume) mchezo ni uleule kula na kusepa(eat and run) ghafla msichana hushutuka yuko 30 tayari, wachache km kwao wako vizuri kukimbilia shule(kufanya masters) wakidhani wakija maliza shule watakuwa wamepata wenza hali huwa tofauti wamalizapo shule bila kutimiza matarajio.
Tano, 30 onwards! Tunasema CONFUSION TIME, hapa mdada hajielewi tena hachagui tena, utamkuta ana elimu, kazi nzuri, wengine wana nyumba, na pesa za kutosha ila hawana MUME, uamuzi wa mwisho ni kuzaa bila mume, mara nyingi huzaa na waume za watu, au hujibamiza kwa masingle dady au janaume lolote ili watoe nuksi wakidhani wamemaliza kazi ghafla life husonga mbele mtoto akikua anadai baba ndipo mama hutambua alizaa na baba wa watoto wengine atajisikia upweke usio na kipimo kulea mtoto mwenyewe regardless she has everything.
ANGALIZO:
Wanaume 18-22_waoji ni wachache, wengi hapa wanaoa wasioenda shule.
23-25 waoaji wapo ila ni wachache wale wanaolipoliwa mahari na wazazi wao.
26-30 hapa waoji ni wengi mno na hulenga kuoa mabinti wa miaka 20- 24(most preferably).
30 onwards, hapa wanaume hupungua sana, wamechanganyika na WAGANE, MASINGLE DADS, MICHEPUKO YA KIUME .
ONYO KWA WADADA;
Chonde chode, ndoa ni mhimu sana siyo kama mnavyodhania, sababu ya upuuzi wenu wenda msione haya nisemayo but wahenga walishaniwahi na kusema UJANA MAJI YA MOTO FINAL UZEENI, siyo mbali hivyo at 30 yrs mtakuja na majibu hapa.
Fahamu: Faida za ulaji tunda la Tango
Leo tujifunze nakuzitambua faida za Tango katika miili yetu, ikiwa watu wengi tunakula bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku. Watu wengi tunapenda matunda fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida katika mwili.
Hizi ni faida za tango katika mwili wa binadamu na kiafaya
1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2. Tango huupa mwili na vitamin kwa asilimia 95 maji kuusaidia kuondoa sumu mwilini.
3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
4. Tunda hilo lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo husaidia kupunguza aina mbalimbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
5. Pia husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.
6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani pia hupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
7. Husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri, kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kamba kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari.
9. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
10.Tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.
Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani – Ebitoke
Mchekeshaji Ebitoke amedai si kweli penzi lake na Ben Pol limekufa bali wanafanya mambo yao kwa usiri zaidi.
“Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo,” ameiambia Times Fm.
Mchekeshaji huyo amesema mipango walionayo kwa sasa ndio inapelekea kutoonekana pamoja kwa sasa na kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.
“Tunamipango mingi, kwanza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote na ameniaidi lazima ahakikishe natimiza malengo yangu na ameona mimi bado ni mdogo ananifundisha kila kitu jinsi gani nikue kwenye hii tasnia na the way hii mitandao ya kijamii ilivyo na maneno ya watu yalivyo,” amesema.
Couple ya wasanii hawa imekuwa ikichukuliwa kama kiki kitu kilichochangiwa na uvumi kuwa mmoja wapo alilipwa ili kufanikisha hilo kitu ambacho wote wamekuwa wakikana.
Mwanamuziki akamatwa Saudia kwa kosa la kucheza ‘dabbing’ (Video)
Dabbing imepigwa marufuku katika taifa hilo la kihafidhina ambapo utawala unaifananisha na utamaduni wa utumizi wa mihadarati.
Kanda ya video ya densi hiyo ya bwana Al Shahani ilikuwa maarufu katika mitandao ya kijamii na maelfu wametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusu kisa hicho.
Inadaiwa kuwa dabbing inatoka katika muziki wa Hip- Hop katika jimbo la Atlanta, Georgia, Marekani, takriban miaka miwili iliopita lakini ikapata umaarufu baada ya watu maarufu , wanariadha na wanasiasa
Waziri wa maswala ya ndani anayehusika na kukabiliana na mihadarati nchini Saudia hivi majuzi alipiga marufuku densi hiyo kwa kuwa wanaifananisha na watumiaji wa bangi.
Chapisho lililowekwa na wizara hiyo linawaonya raia kuhusu hatari yake katika vijana na jamii na inaonya dhidi ya kuiiga .
Beka Flavour afichua ishu ya kuimba chini ya Polisi
Msanii wa Bongo Flavour, Beka Flavour amedai aliposhikiliwa kituo cha polisi kwa mashtaka ya kutapeli kupitia mtandao alikuwa akiwaimbia washtakiwa ‘mahabusu’ wenzake aliowakuta kituoni hapo.
Kati ya July 19/20 mwaka huu muimbaji huyo alishikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi Tabata Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli Tsh. milioni nane kupitia mtandao wa facebook ambapo baadae alitolewa kwa dhamana.
Beka amekiambia kipindi cha Leo Tena Cha Clouds Fm kuwa ilibidi awaimbie ili kuwaridhisha kwa sababu walitaka lakini kikubwa alichogundua kuna ambao wanatamani kufanya muziki na nyimbo tayari wapo nazo.
“Mule kunakuwa na wasanii wengine, anakuambia dah!, mimi mwenyewe naimba nikitoka humu tu nafanya ngoma yangu, kuna mmoja aliniambia mimi nimejifunza sana nimeshaandika ngoma kwa ajili ya mazingira ya huku ndani nikamuambia hongera ukitoka karekodi ukitoka inaweza ikakutoa,” amesema na kuongeza.
“Ukigoma wanaweza wakakufanya kitu kibaya kwa sababu wapo wengi halafu wote ni wahuni, kwa hiyo ukileta ubishi wanaweza wakakubadilikia wote,” amesisitiza.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)