Dabbing imepigwa marufuku katika taifa hilo la kihafidhina ambapo utawala unaifananisha na utamaduni wa utumizi wa mihadarati.
Kanda ya video ya densi hiyo ya bwana Al Shahani ilikuwa maarufu katika mitandao ya kijamii na maelfu wametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusu kisa hicho.
Inadaiwa kuwa dabbing inatoka katika muziki wa Hip- Hop katika jimbo la Atlanta, Georgia, Marekani, takriban miaka miwili iliopita lakini ikapata umaarufu baada ya watu maarufu , wanariadha na wanasiasa
Waziri wa maswala ya ndani anayehusika na kukabiliana na mihadarati nchini Saudia hivi majuzi alipiga marufuku densi hiyo kwa kuwa wanaifananisha na watumiaji wa bangi.
Chapisho lililowekwa na wizara hiyo linawaonya raia kuhusu hatari yake katika vijana na jamii na inaonya dhidi ya kuiiga .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni