burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

2 Jan 2017

Solo Thang: Sikuwa na nia ya kumdhalilisha Chidi Benz


Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Solo Thang amefunguka baada ya baadhi ya watu kumjia juu kwa kusambaza kipande cha video alichorekedi akiwa na Chidi Benz.

Akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV, Solo amesema kuwa Chidi ndiye aliyemtaka amshoot video wakati walipokutana ila hakuwa na nia kama watu wengine wanavyofikiria.

“Chidi ni mdogo wa rafiki yangu na nilimfahamu zamani sana kabla hata hajaanza kuimba. Hivyo tuna historia ndefu kidogo. Chid kwa sasa huwa hapigi picha na watu, lakini tulipoonana ni yeye mwenyewe ndiye alitaka tushoot ile video lakini sikuwa na nia ya kumchoresha,” amesema Solo.

Rapper huyo ameongeza kuwa watu waache kumlaumu Chidi kwa kile kilichomtokea na badala yake wanatakiwa kumpatia msaada bila ya kuchoka.

Wastara aandika ujumbe wakusikitisha kuhusu maisha yake ‘nahisi mauti yapo karibu yangu’

Image result for wastara sajuki
Msanii wa filamu Wastara Juma ameandika barua ya wazi kueleza jinsi anavyojisikia ikiwa ni miaka 5 toka ampoteze mume wake marehemu Sajuki Juma.
Muigizaji huyo amedai toka ampoteze mume wake huyo hajawahi kupata furaha katika maisha yake licha ya kujaribu kufanya kila awezavyo.

Yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya mwaka 2016 kumalizika, mrembo huyo kupitia facebook ameanda ujumbe huu.

Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu, Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza kesho. Ni miaka 5 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari .

Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwasababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo haikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu Sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo tarehe 31/12/2016 nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana, kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na Sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote sababu nitakufa siku yoyote tutumie muda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka.

Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hata moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipeleke baharini basi naupeleka uko ukisema nipeleke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitin naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need peace of mind,moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolote ili upumue hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumain unaishi kama uko dunia ya peke yako nimeongea haya ili muelewe hisia zangu kuwa hata ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kama na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani.

Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2017 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote
moyo wangu unahitaji furaha masikin mwaka 2017 uwe na neema kwetu sote ameen

Wabogojo alivyoisaidia Muziki ya Darassa kupaa kimataifa, soma maoni ya mashabiki nje ya TZ

Image result for darasa
Mwaka 2016 unamalizika ukiwa na historia ambayo haitosahaulika kwenye maisha ya muziki ya rapper Darassa. Rapper huyo amefanikiwa kutengeneza wimbo namba moja Tanzania kwa sasa huku pia umaarufu wa wimbo huo ukiendelea kusambaa kwa kasi ya ajabu katika nchi zingine.
Tunavyozungumza sasa, wimbo huo ni moja ya nyimbo kubwa Kenya na kinachofurahisha zaidi, Wakenya wameupenda kwakuwa una ladha ya muziki wa Kapuka na baadhi ya mashairi yake yamewafanya wafikirie kuwa ana asili ya Kenya
Lakini kuna mtu mmoja muhimu ambaye Darassa na Ben Pol wanapaswa kumshukuru kwa kusaidia kuupaisha wimbo huo nje ya mipaka ya Tanzania. Si mwingine ni mchekeshaji na mcheza sarakasi, Wabogojo. Wiki tatu zilizopita, mchekeshaji huyo alipost video akiwa amejifunga taulo la pinki na mswaki mdomoni akiucheza wimbo huo kwa mbwembwe nyingi.
Ndani ya muda mfupi, video hiyo ilisambaa mtandaoni hasa Facebook na Instagram na watu wengi nje ya Tanzania wakaiona. Umaarufu wa video hiyo uliwafanya watu waende Youtube kuutazama wimbo mwenyewe na kujikuta wakipenda walichokiona na kukisikia. Wengi wameeleza kwenye video ya Darassa kuwa wameenda kuitazama baada ya kuiona video ya Wabogojo ambaye wamempa jina ‘The Guy With A Pink Towel.’

Harmonize: WCB hakuna chuki wala ushindani kati yetu


Harmonize amedai kuwa hakuna ushindani ndani ya lebo ya WCB wala chuki tofauti na watu wengine wanavyodhania.
Hitmaker huyo wa Matatizo, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa ndani ya lebo yao hawajawahi kushindana wala wanapotoa nyimbo hawatoi kwa mashindano kati yao ila mashabiki ndio wanaowachukulia hivyo lakini kibiashara kwao inakuwa vizuri.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio yakwao waote.

Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kuda kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake waliopeana kuachia nyimbo zao.

New AUDIO | Hemedy PHD - Mkimbie | Download

Official VIDEO | Patoranking – God Over Everything | Watch



Official VIDEO | Angel Benard & Mercy Masika - Huyu Yesu | Watch