burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

22 Okt 2016

Msaga Sumu adai yeye ndiye mwanzilishi wa Singeli

Muimbaji nguli wa muziki wa Singeli, Msaga Sumu amedai kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa muziki huo hapa nchini.
msaga
“Mimi ndiye mwanzilishi wa singeli, nimeipigania sana toka enzi za vigodoro kabla havijapigwa marufuku. Nilikuwa naloop beat za taarabu hadi akina Mzee Yusuph walitaka kunishtaki, nimepigana hadi leo hii imefikia hapa,” amekiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.
“Nilikuwa nikipata kazi nashirikisha wanangu kibao ili nao waonekane. Kwa mara ya kwanza mimi ndiye nilimtambulisha Sholo Mwamba, nilikuwa na kazi fulani, nikampigia simu, nikampa nafasi akashika kipaza akafanya mambo na watu wakaanza kumjua,” ameongeza.
Muimbaji huyo ameachia video yake mpya ya ‘Iga Tena’ ambao amedai kuwa wimbo huo hajamlenga mtu yeyote.

Diamond Platnumz afungukia collabo yake na Lady JayDee

diamond-platnumz

Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona Diamond Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali hao wa bongo fleva huenda wakaja na ‘collabo’ ya hatari, siku chache zijazo.
Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna sababu yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na ratiba zao kubana.
lady-jaydee
Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za EATV, na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani  ‘collabo’ yao.
“Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana”
Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika  ‘collabo’ hiyo inakuja.

New AUDIO I Dogo D x Sajna - HABARI I DOWNLOAD


New AUDIO I ManuvaTZ ft Barakah Da Prince-SIWEZI COVER I DOWNLOAD

Kijana anayedaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu afunguka, adai hamjui Idris Sultan

Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na malkia wa filamu Wema Sepetu, Calisah amefunguka na kuzungumzia tetesi hizo ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.
wema-sepetu
Kijana huyo ambaye tayari ameshaonekana mara kadhaa katika baadhi ya video za mastaa wa muziki nchini, amemmwagia sifa malkia huyo wa filamu huku akishindwa kuweka wazi kama ni kweli anatoka naye kimapenzi au la!.
“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe,” Calisah alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri,”
Pia kijana huyo alidai kuwa hamtambui Idris Sultan na hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika.
“Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?,” aliuliza kijana huyo.
Malkia huyo wa filamu toka aachane na mshindi huyo wa Big Brother Afrika 2014, hajaweka wazi mahusiano yake mapya.

Juu ya Vanessa na Jux yaingia kwenye playlist ya The Beat London FM ya UK

Wimbo wa Vanessa Mdee na Jux ‘Juu’ umeingia kwenye playlist ya kituo cha redio cha The Beat London FM ya Uingereza.
14717556_1155079124586248_382814176008994816_n
Baada ya taarifa hiyo kupitia mtandao wa Instagram, Vanessa Mdee ambaye yupo nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la One Africa Music, ameandika, “Mad love to ALL THE DJs AROUND THE WORLD bumping #Juu ðŸ’œAsante Sana. Na bado tunaenda Juu baby. #London is switched on.”
14712431_692500844253202_2890857476649910272_n
Kwa sasa imeonekana ni hatua kubwa muziki wa Bongo Fleva umepiga kwa kuanza kupata tobo lake ikiwa ni mwezi moja umepita tangu kituo cha redio cha BBC Radio 1Xtra kuutangaz\a wimbo wa ‘Kidogo’ wa Diamond kuingia kwenye playlist ya kituo hicho.

JB anusurika kifo katika ajili ya gari

Mwigizaji wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ Ijumaa hii amenusurika kifo katika ajali ya gari.
bongo
Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni alikuwa mkoani Arusha katika shindano la Mama Shujaa, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba anaendelea vizuri pamoja na wanzake ambao walikuwa kwenye gari hilo.
Asanteni wote mlionipa pole kwa ajali ya jana,” aliandika JB instagram. “Hakika Mungu ni Mwema, nipo poa mimi na wenzangu wote. Namshukuru sana Mungu.Thank you JESUS,”
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya vizuri na filamu yake, ‘Kalambati Lobo’.
Ajali za barabarani nchini Tanzania zinatajwa kuwa ni moja kati ya matukio ambayo yanasababisha vifo vingi nchini.