burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

22 Okt 2016

Msaga Sumu adai yeye ndiye mwanzilishi wa Singeli

Muimbaji nguli wa muziki wa Singeli, Msaga Sumu amedai kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa muziki huo hapa nchini.
msaga
“Mimi ndiye mwanzilishi wa singeli, nimeipigania sana toka enzi za vigodoro kabla havijapigwa marufuku. Nilikuwa naloop beat za taarabu hadi akina Mzee Yusuph walitaka kunishtaki, nimepigana hadi leo hii imefikia hapa,” amekiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.
“Nilikuwa nikipata kazi nashirikisha wanangu kibao ili nao waonekane. Kwa mara ya kwanza mimi ndiye nilimtambulisha Sholo Mwamba, nilikuwa na kazi fulani, nikampigia simu, nikampa nafasi akashika kipaza akafanya mambo na watu wakaanza kumjua,” ameongeza.
Muimbaji huyo ameachia video yake mpya ya ‘Iga Tena’ ambao amedai kuwa wimbo huo hajamlenga mtu yeyote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni