Kampuni ya mtandao wa Facebook imesema kuwa wameanzisha upelelezi ili kubaini akaunti feki zilizoanzishwa na watumiaji kupitia mtandao huo.
Tayari imeshaanza kuwatumia wafanyakazi kutoka nje ya kampuni hiyo watakaoweza kugundua kompyuta zinazotumika mara kwa mara ambazo zinahusiana na akaunti hizo feki. Mara kadhaa kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa na watumiaji wa mtandao huo kushindwa kuchukua hatua juu ya wale wanaotoa taarifa feki kwa kutumia akaunti hizo.
Inadaiwa kuwa baadhi ya watu hutumia akaunti hizo feki walizofungua kupitia mtandao huo kwa ajili ya kuweka habari ili wapate watazamaji wengi ili kuzidi kujipatia fedha nyingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni