Akiongea na g.lovetz Dudu amedai TID alitaka kukataa kushiriki kwenye wimbo huo baada ya kusikia wimbo huo unazungumza masuala ya kijamii.
“TID nilikutana naye Unyamani baadaye nikaenda naye studio Tawanyika Record. Lakini wakati nampigia chorus TID alijua ni ngoma ya club inuka inama. Lakini wakati namchania verse pale nikamwambia muda huu tunahitaji meseji kwa jamii kwa sababu jamii imemiss meseji kwa sababu wasanii wametoa ngoma nyingi za kucheza, TID akasema No No tupige ngoma yakuchezeka,,”
Aliongeza, “Nikamwambia ngoja sikiliza kwanza verse nikapiga verse ya kwanza ya pili ndo akasema jamaa una akili sana, akaingia kwenye chorus ngoma na ikatoka,”
Pia rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa video ya wimbo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni