Kokoro umekuwa wimbo wa kwanza katika career ya Rich Mavoko kuchezwa na vituo vya redio vya nchini Uingereza vikiwemo BBC Radio 1Xtra na Capital Xtra.
Rich ameiambia G.lovetz kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwake.
“Katika ndoto zangu nilikuwa nafikiria nije kufanya kitu ambacho kitatoka nje ya mipaka, kufika west, kufika south, kufika sehemu ambazo nawaona wasanii ambao nawatamani wanafanya kazi kubwa wanafika,” amesema.
Mavoko amesema Kokoro ambao amemshirikisha Diamond, ni wimbo wenye ladha ambazo hajawahi kufanya lakini risk aliyoifanya imezaa matunda.
“Namshukuru Mungu nimeona matunda yake, BBC sijawahi kuchezwa haki ya Mungu. Nimetumiwa nikiwa huku Marekani nikasema noma noma,” ameongeza Mavoko kwa furaha kubwa.
Muimbaji huyo amesisitiza kuwa kwa sasa ana hasira kubwa zaidi ya kuhakikisha anafika katika masoko ambayo hakuwahi kufika kwa kuachia kazi kali zaidi.
“Nataka niingie kwa nguvu,” anasema. “Nataka niingie nikiwa nachop muziki wa aina tofauti tofauti. Bado nitastick kwenye Bongo Flava kwasababu ndio muziki wa nyumbani, ndio maana Kokoro home itafanya vizuri, nje itafanya vizuri kwasababu naweza nikafanya vitu vingi kwenye wimbo mmoja.”
Naye Diamond ametumia Instagram kumpongeza Mavoko kwa hatua hiyo.
Ameandika, “Congrats @richmavoko naona malengo yanaanza kutimia… Inshaallah Mungu aendelee kukuongoza, kukupa ubunifu na roho ya kuthubutu zaidi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni