Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
27 Mac 2017
Hawa ni watangazaji watano wa vipindi vya burudani redioni wanaokubalika zaidi Kenya
Kupitia utafiti wangu mwenyewe nilioufanya, niliingia mitaa mbalimbali ya hapa nchini kukusanya takwimu juu ya watangazaji wanaokubalika zaidi kupitia ubora wao. Hakijatosha, niliwahusisha na pia wadau kutoka pande nyingine za nchi kwa ajili ya kupata takwimu sawa.
Utafiti huu ulihusisha idadi kubwa ya vijana na nimeifanya kuanzia January hadi mwisho wa February. Hii hapa Top 5 ya vipindi vya burudani.
1. Mzazi Willy M. Tuva
Kabla ya kubatizwa jina la Mzazi, Tuva alianza kazi ya utangazaji mwaka 2006 fresh kutoka masomoni. Alianza kusikika ‘on air’ kupitia kipindi maarufu nchini cha Mambo Mseto cha Radio Citizen. Kwa raia wote waliohusika katika shughuli hii, Tuva ndiye aliyezungumziwa sana. Kinachowavutia wengi kusikiliza kipindi chake ni kwamba ‘he is creative in his activities and he is natural’. Anatumia sauti yake yenye nguvu na ubunifu hivo ilivyo.
Kipindi chake ambacho ni cha burudani na pia kimekaa kwa mfumo wa habari ina mantiki ya kihamasisho na kielimu kwa vijana, kitu ambacho ni kivutio kikubwa uraiani. Mzazi Willy Tuva ni maktaba ya muziki wa Afrika Mashariki na uelewa wake wa muziki huu humzidishia zaidi idadi wasikilizaji wa kipindi hicho kinachoangazia miziki ya kutoka sehemu zote za Africa Mashariki.
Hakijatosha, mahojiano anayofanya kwenye kipindi huleta msisimko usio kifani uraiani.
Huyu ni mtangazaji ambaye mchango wake kwenye hii sanaa unadhihirika kwa sababu amechangia katika kulea vipaji na amekuwa daraja la mafanikio kwa wasanii wa nyumbani na pia wa kutoka pande nyingine za kanda hii yetu. Ukubwa wa jina lake umeongezeka kwa sababu ya hiyo.
Ameendelea kuwa ‘creative in his activities’ na ndio maana yupo kwenye orodha ya watangazaji wanaoingiza mkwanja mrefu nchini Kenya kwa sababu ya ubora wake.
2. MBUSII
Huyu hapa ndiye aliyekuwa wa pili kwenye orodha hii. Kwa upande wa muziki wa reggae, jina la mtangazaji huyu sio geni kwa mashabiki wa aina hii ya muziki. Kwa miaka sasa amekuwa ‘powerhouse’ ya muziki wa reggae. Kwenye kipindi cha ‘The Drive Show’ kinachoruka kupitia Radio Jambo, Mbussi huwaburudisha idadi kubwa ya wasikilizaji wanaopenda ‘style’ yake ya utangazaji.
Matumizi ya slang ya mitaani na weledi wake kwenye hii fani ni kivutio cha vijana si haba.
Uelewa wake wa muziki wa reggae humfanya kuwa hatua mbele ya wenzake wanaofanya vipindi kama chake hiki cha reggae na siku zote wa kumfikia hajapatikana maana Waswahili wakasema mzoea punda farasi hapandi.
Siku zote amekuwa mstari wa mbele kuleta mijadala inayowahusu watu mitaani na ni kitu kinachofurahisha wengi wa wasikilizaji wake. Mbusii ana uwezo wa kuja na mijadala na mada nyingi kwa kutumia ‘angle’ tofauti tofauti unaovutia umati mkubwa nchini Kenya.
Pamoja na hayo yote, huyu ni miongoni mwa watangazaji wa redio nanaoingiza hela nyingi mno.
3. Amina Abdi
Huyu ni miongoni mwa vipaji tulivyojaliwa nchini kwa upande wa watoto wa kike. Mtangazaji huyu ambaye pia ni muimbaji na muigizaji mzuri ana uwezo mkubwa sana kwenye hii fani. Kupitia show yake ya ‘Hits not Homework’ inayoruka hewani kupitia Capital fm, ameweza kupata ufuasi mkubwa nchini. Ubunifu wake katika uendeshaji wa kipindi chake na ubora wake wa kufanya ‘interviews’ ni kivutio kikubwa. Mwanadada huyu ni mpambanaji anayewawakilisha vizuri wenzake wa kike katika hii tasnia ya utangazaji.
4. Mwende and Clemmo
Kila unapoisikiliza sauti ya Mwende kupitia kipindi cha ‘Connect’ cha radio Maisha akiwa na mwenzake Clemmo bila shaka utaipenda. Wawili hawa wana chemistry fulani hivi ya kishua inayowavutia watu wengi mitaani. Combination yao huwawezesha kuiendesha show yao kwa ubora wao. Kila kitu kwenye kipindi chao kuanzia kwa chaguo la nyimbo wanazochezesha na vitu kama hivyo ndivyo huwafanya watu kibao kutune kwenye iyo show yao.
5. Jeff Mote
Kijana huyu alipata umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha asubuhi cha ‘Jeff, Linda and Chipukeezy’ cha Kiss fm. Mtangazaji huyu ameendelea kuvutia wasikilizaji wengi hususan vijana kwenye kipindi cha muziki cha ‘The Hot 30’ hapo hapo Kiss fm. Katika hii orodha ya nyimbo 30, aina zote za nyimbo huangaziwa na zile bora zaidi kulingana na maoni ya wasikilizaji hupewa nafasi.
Hii ni show inayopendwa sana nchini na vijana wa vyuo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni