burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

27 Mac 2017

Rais Magufuli aagiza Nay wa Mitego aachiwe huru, wimbo wake uchweze redioni na auboreshe zaidi kwakuwa ameupenda


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amedai kuwa Rais Dkt John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa Mitego.

Dkt Mwakyembe aaedai kuwa Rais amemuambia amuelezee Nay auboreshe zaidi wimbo huo kwakuwa umegusa masuala muhimu.

“Yaani asiondoe kitu chochote, ila aongeze kwasababu unaelezea changamoto zilizopo kwenye jamii halafu wanaitikia watu ‘wapoo’” amesema Dkt Mwakyembe kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.

“Rais amesema [Nay] amesahau vitu vingine vingi, wakwepaji kodi, aongeze mambo kama hayo, wabwia unga na mihadarati wapo, wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wapo, watanzania wanaopenda tangu asubuhi hadi jioni wao ni kwenye vijiwe tu hakuna kufanya kazi wavivu waitikie tena wapoo. Kwahiyo anasema itatusaidia sana maana ni muziki mzuri na BASATA walikuwa wameshafanya mpaka uamuzi usipigwe kokote pale, wao siwalaumu walitekeleza wajibu wao, ila leo tu nimetoka kuwaomba kipindi ambacho mimi naongoza hii wizara naomba wafanye consultation zaidi kabla ya kuchukua hatua ili katibu mkuu ajue, naibu waziri ajue tunaweza kubadilishana mawazo sababu haya mambo yanahusu haki za msingi ambazo zipo kwenye katiba ya jamhuri ya muungano,” amesisitiza Dkt Mwakyembe.

“Kwahiyo nimechukua hatua kama waziri mwenye dhamana kuwaagiza polisi wamwachie yule kijana, hebu waache kumhoji huyu kijana, badala ya kujitetea mimi ningemshauri hata aje Dodoma naweza kumuona kesho, nimwelekeze vizuri hata namna ya kuongeza wimbo utakuwa mzuri kweli kweli. Na mimi mwenyewe nimeisikiliza hii beat nakubaliana na mheshimiwa rais, rais najua anapenda muziki, lakini hata mimi mwenyewe napenda muziki kwakweli ile beat ni kali.”

Nay alikuwa tayari akichukuliwa maelezo na polisi jijini Dar es Salaam. Kwa uamuzi wa Rais Magufuli hiyo ina maana kuwa hana tena shtaka lolote la kujibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni