Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
23 Mei 2017
Riyama Ali kwa waigizaji wenzake – ‘Punguzeni kula bata’
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Riyama Ali amewapa makavu waigizaji wenzake na kuwataka wapunguze kula bata kwani hata hizo pesa ndogo ndogo wanazozipata zinaweza kuwafanya waishi vizuri .
Riyama Ali ambaye alikuwa nchini Kenya kwa muda mrefu kwenye shughuli zake za kibiashara amesema kwamba, ni kweli Wasanii wa Bongo Movie wanakosa kiasi kikubwa cha pesa kutokana na kukosa haki miliki na ongezeko la kazi haramu.
“Tupigie haki miliki kelele wasanii sisi masikini lakini tunakazi nyingi nzuri leo hii haki miliki zetu hazipo mikononi mwetu,Stori zetu kazi zetu tusiwe bendera kufuata upepo uchungu tuufanye kwa vitendo sio kwa kushinikizwa na mtu“, Alisema Riyama Ali .
Hata hivyo amewachana pia wasanii wenzake kwa kusema wapunguze kula bata kwani pesa hizo wanazozipata ingawaje ni ndogo lakini zinatosha kuendesha maisha yao ya kila siku.
“Nawapenda sana wasanii wenzangu ila tukumbuke kuwa tunajukumu kwenye jamii,Jamii inatudai na tusile sana bata,Tunakula sana bata, punguzeni kula bata…..na ifike sehemu tukubali kuwa kuna mahali tuliteleza,tulilie sana haki miliki“, Alisema Riyama Ali kwenye mahojiano yake na EATV.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake “Twiga Stars” kipo kambini tayari kwa michuano
Wachezaji wa Twiga Stars wanaendelea na Mazoezi kwenye uwanja wa Karume, wakiwa chini ya kocha Mkuu Sebastian Nkomwa.
Ushauri wa Young Killer kwa Dogo Janja
Baada msanii Dogo Janja kuwauliza mashabiki wake kupitia mtandao, wakipata fursa ya kumshauri watamshauri kuhusu jambo gani, Young Killer ameamua kuchukua jukumu hilo na kumshauri msanii huyo.
Young Killer amemshauri kwa kusema ‘Fanya kolabo na mimi nikukalishe but then nikutangaze kimataifa.
Yusuph Manji ajing’atua Yanga
Yusuph Manji amejiuzulu katika nafasi yake hiyo uwenyeketi katika klabu ya soka ya Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Manji amesema ameamua kuachia ngazi ya uongozi huo kwa ajili ya kuwapisha watu wengine waongoze ili wasifikirie uongozi katika timu hiyo upo kwa ajili ya watu wachache pekee.
Soma taarifa hiyo hapa chini.
Rihanna na Lupita kuigiza filamu ya pamoja
Tarajia kuwaona Rihanna na Lupita Nyong’o ndani ya filamu moja.
Mastaa hao wapo katika mazungumzo ya kuigiza filamu iliyopewa jina la “Netflix” ambayo itaongozwa na Ava DuVernayna mwandishi wake akiwa Issa Rae.
Elizabetch Taylor ndio alianzisha wazo la mastaa hao kucheza katika filamu moja ikiwa ni mwaka 2014 alipost katika mtandao wa Twitter picha ya wawili hao wakiwa wamekaa pamoja kwenye tamasha la Miu Miu fashion show.
“They look like they’re in a heist movie with Rihanna as the tough-as-nails leader/master thief and Lupita as the genius computer hacker,” aliandika Elizabetch. Hata hivyo Rihana na Lupita wote kwa pamoja walionesha kuvutiwa na wazo hilo.
Maua Sama ataja sababu ya kutoachia video ya ‘Sisikii’
Maua Sama amefunguka sababu ya kushindwa kuachia video ya wimbo wake ‘Sisikii’.
Akiongea na kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM ya Dodoma, muimbaji huyo ameitaja sababu ya kuchelewa ni video hiyo kuhitaji marekebisho makubwa ambayo yangempotezea muda zaidi.
“Muda ndio uliotutupa mkono halafu mwisho wa siku video ilikuwa inahitaji marekebisho mengi ambayo kimsingi isingeweza kutoka mapema, na mimi ingeweza kunigharimu gharama za video nzima na muda ulikuwa umeshakwenda wakati ambao nilikuwa natakiwa kutoka na wimbo mwingine,” amesema Maua.
Hitmaker huyo wa Main Chick, ametaja sababu ya kufanya kazi na Luffa badala ya Imma The Boy kama ilivyozoeleka kwa kusema, “Hata yeye mwenyewe alinishauri kubadilisha producer kwa sababu tulikuwa tunarekodi nyimbo na mwisho wa siku tuna sound the same, akaniambia ungebreak utafute producer mwingine nifanye naye. Mimi nikaona siyo vibaya hata uongozi wangu nao ukashauri nitafute producer mwingine, nimepata maproducer ambao kiukweli nafanya nao kazi kama hivyo Luffa na wengine”.
Simon Msuva,Abdulrahman Mussa washinda kiatu cha dhahabu
Baada ya kufanya vizuri msimu huu, Washambuliaji wawili Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Saimon Msuva wa Yanga wameibuka na tuzo ya wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/17 iliyomalizika wikiendi iliyopita.
Kutokana na wachezaji hao kufungana Idadi sawa ya magoli (14) wamepewa zawadi sawa ya ufungaji bora ambapo watapata Shilingi Milioni 5.8 za kitanzania.
Kwa kuwa vijana wetu Abrahman Mussa na Simon Msuva VPL wamefunga mabao sawa 14 wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa @Tsh 5.8m
4:00 AM - 22 May 2017
46 46 Retweets 210 210 likes
Twitter Ads info & Privacy
Sherehe za ugawaji wa tuzo hizo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 zitafanyika kesho kutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Naitamani sana nafasi ya Urais – Kala Jeremiah
Msanii wa muziki wa hip hop, Kala Jeremiah amefunguka kwa kusema kuwa hawezi kugombea ubunge kwani tayari ameshafanya kazi hiyo kwa miaka mingi na sasa anasubiri muda ufike aweze kugombea nafasi ya Urais.
Akiongea na umati wa watu uliojitokeza katika show ya ‘Wapo Tour’ya rapa Nay wa Mitego iliyofanyika Dar Live weekend hii, Kala atiwata mashabiki wake wajiamini katika mambo yao kama yeye anavyoamini siku moja anawekuwa Rais.
“Urais ndiyo ishu kwa sasa, kusema ukweli tayari nimeshakuwa mbunge kwa miaka mingi hata mashabiki wangu wanajua. Lakini kusema tena niende kugombea ubunge hapana siwezikufanya hivyo kwa hadhi yangu. Nafasi ya Urais ndiyo nayoitaka lakini siwezi kusema ni lini ila jua ipo siku mimi nitagombea nafasi hiyo,” Kala aliiambia Bongo5 muda mchache baada ya kushuka kwenye steji.
Rapa huyo amedai hakuna kitu kinachoshindikana kwenye dunia kama mtu akiamua kufanya jambo lake.
Tunamtafuta Ben Pol atueleze kuhusu zile picha za nusu utupu – BASATA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha za nusu za utupu za msanii wa muziki, Ben Pol ambazo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mngereza amewataka wasanii kufanya kazi nzuri ambazo zinaweza kuwaweka sehemu nzuri na siyo kutengeneza mazingira ambayo yanautia dosari muziki wao.
“Sisi kama BASATA tumeona hizo picha mtandaoni, siyo kitu kizuri, kwanza hakiendani na tamaduni zetu. Kwahiyo sisi tunamtafuta Ben Pol halafu tumsikilize, atueleze zile picha ilikuwaje mpaka zikasambaa mitandaoni. Tukiongea naye tunaweza kutoa kauli yoyote na kulaani matukio ya namna hiyo,”
Aliongeza,” Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol.”
Pia Mngereza amewaomba wasanii wa Tanzania kwa upande wa muziki wafanye muziki mzuri wasitegemee kiki.
Linex afunguka sababu za ukimya wake
Linex amesema licha yeye kuwa kimya hakuna mtu anaweza kumzuia kufanya muziki jinsi yeye anavyotaka au kuchukua nafasi yake kwa sababu muziki anaofanya yeye ni wa kipekee.
“Kwa hiyo ninaweza kurudi muda wowote, sisemi kuwa nitakaa muda mrefu bila kutoa wimbo kwa sababu kuna vitu nilitakiwa kuvifanya lakini sikuvifanya ambavyo ni mapumziko, nimefanya kazi zaidi ya miaka saba sijawahi kukaa nyumbani hata siku mmoja,” Linex amekiambia kipindi cha Twenzetu na kuongeza.
“Kwa hiyo nimejipa mapumziko huu ni mwezi karibia wannne sasa, nimekaa nyumbani nimepumzika, nimeandika kazi, kwa hiyo any time nitafanya kitu ambacho ni kikubwa,” amesema Linex.
Nay amjibu Mwakyembe ‘muziki na siasa vyote ni maisha ya watu’
Baada ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuwataka wasanii wa muziki nchini kuacha kufanya muziki ambao una uhusiano na siasa, rapa Nay wa Mitego amefunguka kuhusu kauli hiyo na kutuma ujumbe maalum kwa waziri huyo.
Waziri huyo aliyasema hayo mwezi huu Bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya Bajeti ya wizara yake.
Akiongea na g.lovetz Nay amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajaielewa kauli hiyo na mweshimiwa.
“Mimi sijawahi kuimba siasa huwenda hiyo kauli hainihusu, muziki wangu ni maisha ya watu ya kila siku, huwa siimbi siasa. Lakini nachoamini siasa pia ni maisha ya watu ya kila siku, muziki wa hip hop ni maisha ya watu ya kila siku na siasa ni maisha ya watu ya kila siku,” alisema Nay wa Mitego.
10 Mei 2017
NEW AUDIO I SINGLE SALLY & JOBFIRE WA MELODY I DOWNLOAD
CREW: WA MELODY CLASSIC PEPEZA PEPEZA
ARTIST: SINGLE SALLY & JOBFIRE WA MELODY
TRACK: CHARAMILLA
PROD: MESSEN SELEKTA
STUDIO: DEFERTALITY MUSIC
PHONE NOMBER
SINGLE SALLY - +255757517704
JOBFIRE WA MELODY- +255678614426
9 Mei 2017
BAADA YA UKIMNYA WA MUDA MREFU KUNDI LA WA MELODY CLASSIC LA RUDI KWA KASI YA AJABU
Baada Ya Ukimya Wa Muda Mrefu Kutoka Kwa Kundi La Wa Melody Classic Pepeza Pepeza Linalowakilishwa Na Wasanii Machachari Kutoka Kilimanjaro Hapa Namzungumzia Jobfire Wa MeLody Pamoja Na Single Sally Wa Melody
Kila Mtu Alikuwa Akiongea Lake Huku Tukiwasikia Wengine Wakisema Kwamba Hawa Jamaa Wana Bifu Zito Baina Yao Na Watu Hawategemei Kabisa Kuwaona Wakifanya Kazi Pamoja. Hayo Ni Maneno Yaliyokuwa Yakitoka Kwa Wadau Wa Mziki Huku Wakiongeza Kwa Kusema Kwamba Bifu Kubwa Ya Wasanii Hawa Ilipelekea Kuvunjika Kabisa Kwa Kundi Lao Na Kila Mtu Kuamua Kufanya Kazi Zake Peke Yake Na Kwa Wakati Wake.
Ila Cha Kushangaza Sasa Ni Kwamba Hivi Karibuni Zilianza Kusikika Tetesi Kwa Mashabiki Hao Hao Wakisema Kwamba Wawili Hao Single Sally Na Jobfire Wa MeLody Wamepatana Na Kuna Taarifa Kwamba Wamefanya Kazi Ya Pamoja Katika Studio Ya Defatality Music Chini Ya Mkono Wa Producer Mkali Messen Selector Tz. Baada Ya Uchunguzi Wa Kina Blog Yetu Imegundua Ukweli Na Kuthibitisha Taarifa Hizi Kwamba Ni Kweli Hawa Jamaa Wamepatana Na Soon Wanakuja Na Ngoma Mpya Inayoitwa #CHARAMILLA.
Kumbe Hawa Jamaa Hawakuwahi Kugombana Ila Ni Mipangilio Yao Tu Ya Kazi Waliamua Kuwapa Brake Mashabiki Wao Ili Wakirudi Kama Kundi Wakate Kiu Kwa Mashabiki Na Hii Ndio Ilikuwa Plan Yao Kwa Mujibu Wa Majibu Yao Wote Wawili Baada Ya Kuongea Na Blog Yetu. Daaaaaah. Haya Sasa Pata Mziki Mzuri Soon Kutoka Kwa Wamelody Classic PepezaPepeza Cc// Singo Sally & Jobfire Wa MeLody
Mbunge: TRA inamdai Diamond sh. mil 400
MBUNGE wa Kinondoni, Maulid Mtulia (Chadema), ameliambia Bunge kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’, anadaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) zaidi ya Sh. milioni 400.
Mbunge huyo aliyasema hayo bungeni jana wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Alisema Wilaya ya Kinondoni ina wasanii wengi maarufu na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mauzo ya kazi zao. Alidai Diamond Platinumz amemwambia kwa sasa anadaiwa kodi ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Kutokana na msanii huyo na wenzake kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kazi zao za sanaa, Mtulia aliiomba serikali kuhakikisha inaimarisha mapambano dhidi ya wizi wa kazi zao badala ya kutilia mkazo kwenye ukusanyaji wa kodi pekee.
Alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana kuzungumzia kauli ya Mbunge huyo, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Walipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema suala hilo liko kwenye uchunguzi.
“Hilo liko kwenye hatua ambayo hatuwezi kulizungumzia kwenye vyombo vya habari. Liko katika ‘investigation’ (uchunguzi),” alisema.
Chelsea wainyuka Middlesbrough 3 nunge
Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena Jumatatu hii ambapo vinara wa Ligi Chelsea waliinyuka Middlesbrough goli 3-0.
The Blues hao walishajitengenezea mazingira ya ushindi kwa kucheza kwa kujiamini muda wote wa mchezo.
Diego Costa aligeuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kugongewa pasi murua na Cesc Fabregas katika dakika ya ishirini na tatu ya mchezo na kuipachikia bao la kwanza timu hiyo.
Mchezo ulinoga zaidi baada ya Marcos Alonso alipopachika bao lingine kwa kuunyakua mpira miguuni mwa kipa wa timu ya Middlesbrough, Brad Guzan dakika kumi na moja kabla ya kipyenga cha mapumziko .
Naye Cesc Fabregas iliingizia Chelesea goli la tatu na la lala salama.
Diego Costa aligeuka kuwa nyota wa mchezo baada ya kugongewa pasi murua na Cesc Fabregas katika dakika ya ishirini na tatu ya mchezo na kuipachikia bao la kwanza timu hiyo.
Mchezo ulinoga zaidi baada ya Marcos Alonso alipopachika bao lingine kwa kuunyakua mpira miguuni mwa kipa wa timu ya Middlesbrough, Brad Guzan dakika kumi na moja kabla ya kipyenga cha mapumziko .
Naye Cesc Fabregas iliingizia Chelesea goli la tatu na la lala salama.
Mapokezi ya Darassa Kenya Ni Moto Wa Kuotea Mbali
Staa wa kibao, Muziki, Shariff Thabit alamaarufu Darassa, kwasasa hashikiki kwa jinsi alivyopanda chati kwa ghafla kwenye muziki wa kizazi kipya Africa. Darassa ambaye kwasasa ameachia kibao kingine kikali pamoja na video yake, amemwaga petroli kwenye moto uwakao. Niajabu kuwa Darassa bila ya kutumia kiki, ameweza kukubalika kirahisi kinyume kabisa na wasanii wengine wakali Africa Mashariki. Kupitia makala haya, nitakupa nafasi ya kubaini mwenyewe ukweli huu wa mambo ambao haufichiki ja kinga cha moto kilicho fichwa chini ya majani yaliyo kauka.
Takribani wiki mbili zilizopita, Darassa akiandamana na Ben Paul na AY ambaye Darassa amenukuliwa kusema yeye ndiye anayempa na kumuonesha njia zakupitia ilikuyafikia malengo yake kimuziki, waliitembelea nchi ya Kenya kwa ajili ya kupiga show mjini Nairobi na pia kufanya media tour yake ya kwanza nchini humu. Na kwakweli kupitia kanda za video ambazo ninakukonyezea hapa chini utakubaliana nami kuwa Darassa yuko katika level nyingine kabisa tofauti na wasanii wengine wa Tanzania na Africa Mashariki kwa jumla. Kati ya vyombo vya habari alivyowahi kuvitembelea, vilikuwemo viwili vikubwa si Kenya pekee bali humu barani Africa nikizungumuzia Citizen TV na NTV. Hebu jionee mapokezi yake kwenye runinga ya Citizen Tv kwenye kipindi maarufu cha burudani cha 10 over 10 kwenye kanda video ya kwanza pengine utaelewa ninini nachokisema.
ye kipindi maarufu cha Burudani #TheTrend, kinacho rushwa hewani kila siku ya Ijumaa na kinacho endeshwa na mtangazji maarufu Larry Madowa. Darassa pia alifunguka na kwa mara ya kwanza wakenya ama mashabiki wake walipata fursa yakujua kuwa Msanii mkali na staa wa Zigo Ambweni Yesaya aka AY pia ni mmoja ya wadau wanao masaidi kuzikwea ngazi za juu kimuziki. Hebu afatilie interview nzima ya Darassa akihojiwa kwenye kipindi cha #TheTrend kwenye runinga ya NTV ili uzidi kupata uhondo zaidi na uelewe kwa kina mktadha wa makala haya maalumu.
hi ya Kenya, aliwahi kuwaacha midomo wazi wengi pale alipoangusha burudani la kukata na shoka kwenye show yake nchini Burundi. Chakutia moyo na kufuhisha na kuburudisha zaidi, ni jinsi mashabiki wake wa nchini Burundi walivyoimba nyimbo zake pamoja naye alipokuwa jukwaani na kilichowagusa wengi ni pale mashabiki walivyopagawa na nyimbo ya Muziki pale Dj alipoiachilia hewani. Hiki sikitu cha kwaida, inamaanisha Darassa ameingia kwenye wasanii ”Extra-odinary”. Hebu tupia jicho na hii video ya Darassa akiwa Burundi, alivyojaza ukumbi huku mashabiki wakimshangilia kwa vifijo na nderemo.
ji chake si cha kupapasa. Maana kibao chake kipya Hasara Roho, alichokiachia wiki iliyopta hakika nakifananisha na bomu la nukilia la Nagasaki kule nchini Japani wakati wavita vya pili vya Dunia. Wakati jeshi la wanahewa la Marekani lilipofanya shambulizi lililoacha maafaa makubwa na madhara ya kiafya ambayo bado yanashudiwa mpaka sasa. Sitaki nikupoteze mwenzangu, ila mashairi ya wimbo Hasara Roho yanaua na kuumiza wasio mpenda na pia kufurahisha na kuburidisha wafuasi wake kwa wakati mmoja. Aisee huyu jamaa kwasasa ni level nyingine, na wala hahitaji kiki kukiki ja mashairi yake ya wimbo Hasara roho yanavyosema. Nikinukuu ” Kama uantaka kiki kwa Pikipiki, mara black mara white vipi, kama unatikisa kibiriti I am play no game am sorry rafiki.” Kweli Darassa si wamuchezomuchezo, na anastahili kongole.
Young Dee aeleza kisa cha kutimka MDB na kujiunga King Cash
Rapa kutoka King Cash, Young Dee amefunguka kueleza kilichosababisha akaondoka katika label yake ya zamani, Millian Dollar Boys (MDB) iliyochini ya producer Max Rioba.
Rapa huyo ambaye ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bongo Bahati Mbaya’ akiwa chini ya label hiyo mpya, ameiambia Bongo5 kuwa aliachana na label hiyo baada ya kushindwa kukubaliana baadhi ya mambo.
“Nikianza na watu ambao nilikuwa nikifanya nao kazi ni watu ambao nilikuwa nafanya nao kazi kama familia,” alisema Young Dee. “So lilivyokuja suala la kifamilia kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa ndipo ikaoneka kila mtu aanze kufanya kazi mwenyewe bila kumtegemea mtu mwingine,”
Aliongeza, “Mimi suala la kufanya kazi na Mr Ttouch ni suala la muda hata hapo awali tulikuwa tunafanya kazi kama washkaji. Kwahiyo baada ya kuona tunaweza kufanya kazi pamoja, akanikutanisha na uongozi wa King Cash, wakanisaini kama msanii wao wa kwanza,”
Rapa huyo alisema yeye pamoja na Mr TTouch wapo chini ya King Cash.
Fahamu : Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni
Watu wengi katika miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi.
Kinachowasumbuwa wanaume na hata wanawake siyo kitambi tunasema ni mrundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta mengi.
Hivi ni visababishi vya tumbo kwa kina mama:
Vyakula feki (Junk food)
Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
Kukaa masaa mengi kwenye kiti
Kutokujishughulisha na mazoezi
Mfadhaiko (stress)
Kula wali kila siku
Ugali wa sembe
Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, na vinginevyo vinavyofanana na hivi.)
Hivi ndio vyakula vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake
1. ASALI NA LIMAU
Tumia asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.
2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.
3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.
4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.
6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.
8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.
9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.
10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.
11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.
12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.
13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.
14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.
15. PARACHICHI
Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.
16. TUFAA
Kula tufaa maarufu sana kama ‘apple’ (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.
17. MAFUTA YA SAMAKI
Huwenda yakakulera harufu yake ila mafuta ya samaki ni mbadala mzuri kabisa katika kuchoma mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe hulenga kuyachoma moja kwa moja mafuta yanayozidi tumboni.
18. SIAGI YA KARANGA
Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho kama ‘niacin’ ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo kwenye mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga badala ya mafuta mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi ya karanga kama mafuta yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika hata katika wali unaweza kutumia kama mafuta yako mbadala.
19. MAYAI
Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya kienyeji lakini) na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk. Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni. Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta mwilini. Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba kwa muda mrefu bila kuhitaji kula kula tena.
20. CHAI YA KIJANI
Chai ya kijani maarufu kama ‘Green tea’ hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Kunywa chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.
21. MTINDI
Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata hivyo mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku yasizidi kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya kutaka kula.
22. JUISI YA KOTIMIRI
Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka nyingine zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.Tumia kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda kulala.
23. NDIZI
Ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu na vitamini za aina mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara zinachofanya mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki (fast food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi kila siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.
24. MAJI YA KUNYWA
Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza uzito. Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu bali pia litafanya ngozi yako kung’aa na kukuwa. Nywele zako pia zitaonekana ni zenye afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.
Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na uendelee hivyo hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa nzima. Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni kipande kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au hamu ndipo unywe maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.
25. MAZOEZI YA KUTEMBEA
Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.Ili kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka ni lisaa limoja yaani dakika 60 bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja huamsha mwilini kimeng’enya kijulikanacho kama ‘lipase’ ambacho chenyewe huamka tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa (when it is activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfulululizo.
Jux ataja muda wa kumaliza masomo yake China
Mashabiki wa Juma Jux, wamekuwa na swali gumu ambalo wamekuwa wakijiuliza na kukosa majibu kuhusu kikomo cha masomo cha Msanii Jux nchini China.
Muimbaji huyo amefunguka kupitia kipindi cha Vmix cha Channel Ten kuwa, ifikapo mwezi wa sita mwaka huu ndio utakuwa mwisho wake wa masomo nchini humo.
“Nimekuwa nikisoma kwa muda mrefu nchini China na safari zilikuwa nyingi sana hapa kati mara kwenda kurudi kwenda tena kurudi. Ninachoshukuru ni kuwa hazijawahi kunifelisha kwa sababu nimekuwa mpangaji mzuri wa ratiba za masomo, muziki na maswala yangu binafsi. Kwa hiyo Mungu kabariki na mwezi wa sita mwaka huu namaliza masomo nchini china,” amesema.
Hitmaker huyo wa Umenikamata, amewataka mashabiki kusubiria vitu vizuri kutoka kwa kundi lao la Wakacha na kuongeza kuwa haliwezi kufa kwa kuwa wao ni kama familia.
Darassa afunguka kusinzia kwa ‘Hasara Roho’
Wimbo wa “Muziki” umeonekana kwenye masikio ya mashabiki kiasi ambacho inanonekana ni vigumu kwa ‘Hasara Roho’ kupenya kirahisi.
Darassa amefunguka kwa kudai kuwa kazi yake mpya ambayo ameiachia wiki iliyopita aliisikiliza kwa umakini akaona huu ndio muda muafaka wa kuiachia kwa mashabiki lakini wao walitarajia wimbo utakuwa kama ‘Muziki’.
“Kitu ambacho kinatokea ni wimbo wa muziki umewakaa sana na kuusikiliza sana kwa namna moja au nyingine,” amekimbia kipindi cha 255 kwenye XXL cha Clouds FM.
“Mimi mwenyewe nilikaa sana na huu wimbo na kuupima, nikaona kuwa ni project ambayo inafaa kufuata na ikawatosha. Kwa hiyo kwa watu kukaa na kutegemea kuwa uje wimbo kama “Muziki” hiko ndio kitu kinachorudisha sanaa yetu nyuma,” ameongeza.
EXCLUSIVE: QUICK ROCKA AFUNGUKA KUHUSU UMAARUFU WA BULLET, KUNDI LA ROCKAZ, KAJALA, SWITCH RECS NA KUPISHANA NA NAHREEL
Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Quick Rocka aligeuka kuwa jina maarufu kwenye Hip Hop ya Tanzania, thanks kwa hit single yake, Bullet. Wimbo huo ulimpa sifa ya kuwa rapper anayerap kwa kasi zaidi katika muziki wa Bongo – kama jina lake.
Quick anasema wimbo huo ulikuja katika kipindi ambacho alikuwa amejiandaa nusu, na nusu nyingine umaarufu ulimwijia kama upepo wa jangwani.
Maisha yalibadilika kwa kasi na kujikuta akiwa busy kila wikiendi kwa show ambazo hazikuwa zikikoma.
“Every weekend I was booked,” anasema Quick nilipozungumza naye kwenye kipindi changu, Chill na Sky: Reloaded. “Na kuna time nilikuwa nazunguka sana mpaka nachoka, mpaka sometimes kuna show nazibonyeza, yaani mwili unagoma. Bullet ilinifanya mtu ambaye niko leo,” amesema.
Pamoja na mafanikio ya mwanzo mwanzo akiwa mwenyewe, Quick alikuwa kwenye kundi la hip hop lililowahi kutamba sana, Rockaz. Kundi hilo liliundwa na members wanne, yeye, Chief Rocka, Dau Rocka na Mo Rocka. Anasema yeye na Chief walikuwa wakifahamiana kitambo kwakuwa ni mtoto wa dada yake. Ni Chief ndiye aliyewaleta pamoja kwakuwa alikuwa akifahamiana na Dau na Mo. Baada ya kundi lao kuundwa, lilibatizwa jina la MGT Fellaz kabla ya mtu mmoja aitwaye Kabwe kuwapa jina Rockaz kutokana na uwezo wao kuchana, jina ambalo lilipita na kila mmoja kuwa sehemu ya jina lake.
Ni Mo Rocka ndiye aliyewaunganisha members wenzake kwa Lamar aliyekuwa amesharekodi naye ngoma zake za solo ukiwemo Ninashine. Quick anasema baada ya siku kama tatu baada ya kutambulishwa walifanya kazi yao ya kwanza ya kundi, Rockaz Anthem iliyotamba vikali redioni. Hata hivyo kundi hilo halikuweza kudumu kwa miaka mingi.
“Hatukuwa tayari,” Quick anasema kuhusiana na sababu za kuvunjika kwa kundi lao. “We had this chemistry na tulikuwa tunafanya muziki as a hobby, as fun, tulikuwa tunaenjoy watu wanavyosikia, watu wanavyovibe, vitu kama hivyo. Kila tatizo huanza pale pesa inapoanza kuingia, hapo ndio kunakuwaga na mipishano. Then by the time mimi nikawa niko signed under MJ, kwahiyo mimi J alivyonicheki tu nikawaambia ‘there is this on the table, it’s an opportunity.’ Wengine walikubali, wengine walikataa, so pale kwenye kukubali kataa ndo kundi likasplit,” anakumbushia rapper huyo.
Quick amesema juhudi za kulirudisha tena kundi baada ya miaka kadhaa baadaye zilifanyika lakini hazikuzaa matunda. Amesema sababu ni kushindwa kutumia muda mwingi pamoja ili kutengeneza chemistry mpya.
“Kundi lilipovunjika, Chief alisafiri akaenda China kusoma for five years. Baada ya three years aliporudi ndio tukasema let’s bring it back, tukajaribu the chemistry wasn’t there. Tulijaribu sana, unajua tunachekiana tunaenda studio it’s trash so hauwezi ukalazimisha.”
Baada ya kukaa kwa muda MJ Records na kisha mkataba kuisha, alianza kufanya kazi na Manecky ambaye alitengeneza naye wimbo My Baby aliomshirikisha marehemu Ngwair. Uhuru wa kurekodi ngoma muda wowote aliokuwa nao MJ ulipotea.
“Kipindi hicho nafanya kazi na Manecky, nilianza kununua vyombo taratibu, ili kuepukana na hiyo – sipendagi kuombaomba, ndivyo nilivyo,” anaeleza Quick. “So nikawa nanunua vyombo taratibu mpaka nikawa complete navyo vyote lakini bado nafanya kazi kwa Manecky. Then there is this day nilikuwa naumwa, Manecky na Tudd wakaja kunicheck home. Wameingia chumbani kwangu wakakuta nina maspika, mixer, everything wakasema ‘yaani wewe unaumwa halafu una studio ndani!’ nikasema ‘bado nataka nipige building fulani’ wakasema ‘hizi hizi, usitafute hela zingine, hizi zitakuletea hela ujenge studio, ufanye nini so you have to start with this.’ Walinipush sana kusema ukweli na I have to thank them Manecky na Tudd na nakumbuka kompyuta ya kwanza ya Switch alinipa Manecky.”
Rapper huyo ambaye hujiita Switcher, anasema baada ya kuifunga vizuri studio yake alimtafuta Nahreel ambaye alimkabidhi kiti cha uproducer kwenye studio yake, Switch Records.
Hata hivyo baada ya kufanya kazi kwa muda, Nahreel aliondoka kwenye studio hizo na kwenda kuanzisha zake, The Industry. Kuachana kwao hakukuwa kwa amani na hivyo wakajikuta wamekuwa maadui kwa muda. “[Nahreel] hakuniweka wazi kwamba kuna moja mbili. Ujue unapofanya kazi na mtu, hata kama unaondoka kwamba ‘oi, mimi nasepa’ kiroho safi, hamna mtu tunashikana cause hatujui leo yako, kesho yangu ikoje, wote tunatafuta so aliondoka kimya kimya tu,leo kaja studio, kesho hayupo tena, hicho ndio kitu kilinikera.”
Pamoja na hivyo, Quick na Nahreel sasa ni marafiki tena na anaona ulikuwa uamuzi wenye faida. “Tulifanya kazi Switch ikasikika, then he went away which is a good thing akaenda kuintroduce The Industry ambayo sasa hivi ni label kubwa, studio nzuri, inafanya kazi.”
Pia hilo lilikuwa somo kwake kuwa hapaswi kumtegemea mtu katika kuhakikisha kuwa Switch Records inasonga mbele. Baadaye alikuja kumpata Luffa aliyeunganishwa na ndugu yake, japo mwanzoni hakuwa mzuri kama alivyo sasa na alipewa ujuzi zaidi na lundo la maproducer wazoefu walio karibu na Quick wakiwemo Bano, Dupy, Bob Manecky na Chizan Brain.
Kwa upande wa uhusiano Quick amewahi kuhusishwa kuwa na uhusiano na Kajala, kitu ambacho amekuwa akikikana hadi sasa licha ya kuwahi kujipost wakibusiana. “Hatukuwahi kuwa wapenzi,” anasema.
“Zile nyingi ukiangalia ni vitu ambavyo mtu mwingine alikuwa anashoot, ni sehemu ambapo tulikuwa tunafanya movie, tunafanya hivi, vipisi vinakatwa. Kuna movie ilitoka ilikuwa inaitwa Wake Up na vipisi vingi vilivyokuwepo viliondolewa, I don’t know why,” ameongeza Quick kwa kicheko.
Kwa sasa anadai ameweka mapenzi pembeni na anajikita zaidi kwenye kazi.
“I am building something on this music industry, haya mambo mengine yatafuata baadaye tukishakuwa na chapaa nyingi.”
Msimamo huo wa Quick haumaanishi kuwa hakuna warembo anaowakubali hasa wa nje. “Wapo wengi,” anasema kwa kicheko. “Mmoja ambaye nikimuona tu inakuwaga noma, kuna Keri Hilson na Ashanti. Ashanti nimewahi kuwa shabiki wake mkubwa sana, nilikuwa napenda sana anavyoimba, jinsi anavyojipresent na mpaka leo yupo kwenye form.”
Kwa upande wa mipango ya kuoa, Quick anasema, “Haipo kwenye ratiba yangu.”
STEVEN SEAGAL APIGWA MARUFUKU KUKANYAGA UKRAINE, ATANGAZWA TISHIO KWA USALAMA WA NCHI
Muigizaji mkongwe wa filamu za kipigo, Steven Seagal amepigwa marufuku kukanyaga ardhi ya Ukraine, lakini pia kutangazwa kuwa ni tishio kwa usalama wa nchi hiyo.
Taarifa kutoka nchini humo zimedai kuwa mamlaka za usalama zimechapisha barua kutangaza kuwa Seagal hatakiwi kuingia nchini humo kwa miaka mitano ijayo.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Seagal amefanya vitendo vya hatari kijamii ambavyo vinaingiliana na nia ya kulinda usalama wa Ukraine. Kosa la Seagal ni kuonekana akiwa pamoja na watu watata wakiwemo Alexander Lukashenko na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Sababu nyingine ni muigizaji huyo kupewa uraia wa Urusi na Rais Putin.
Urusi na Ukraine zimekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa tangia mwaka 2014 na tayari nchi hiyo imewawahi kuwazuia wasanii 140 wa Urusi kuingia.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)