burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

Fahamu: Panya wanaokunywa pombe


Panya kutokea Mashariki mwa nchini India katika jimbo la Bihar, wameripotiwa kunywa pombe ambazo ziliwekwa kutumika kama ushahidi na polisi.

Hayo yamebainishwa na Maafisa wa polisi katika jimbo hilo. Kupitia afisa mkuu wa polisi katika mji wa Patna, Manu Maharaj amesema kuwa, aliarifiwa na inspekta mkuu wa polisi hapo siku ya Jumanne kuwa, pombe zilizoweka kama ushahidi zimenywewa na panya.



Waziri kiongozi wa jimbo la Bihar, Nitish Kumar, alitangaza kupiga marufuku unywaji, uundaji na uuzaji wa pombe, mara baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka jana.

Tangu wakati huo maafisa wa polisi wamenasa zaidi ya lita 900,000 ya pombe haramu.Pia wamewatia mbaroni zaidi ya watu 40,000, kwa kuhifadhi pombe haramu manyumbani na madukani mwao.

Baadhi ya vituo kadhaa vya polisi pia hukodi maghala ya kibinafsi ili kuhifadhi viwango hivyo vikubwa vya pombe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni