burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Mei 2017

Makala: Man Walter afaa kuvikwa taji La ”The Come Back King’


Staa wa muziki wa Bongo flava almaarufu kama Hussein Machozi, ambaye baada ya kimya cha kina kirefu hatimaye aliamua kukata kimya chake kwa kuachilia kichupa kikali kwa jina Nipe Sikuachi. Hii ni bayana shahiri kuwa kutokana na ukali na ubora wake kwenye kiwanda hiki cha sanaa ya muziki wa kizazi kipya chenye ushindani si haba basi alihitaji mtayarishi wa muziki mwenye haiba kubwa na uzoefu wa kusoma misimu ya muziki unavyo kwenda.

Na hapa ndipo nguli na mshindi wa tuzo za mtayarishaji bora wa muziki Africa Mashariki na Dunia kwasasa, nikisema hivi kwamaana sikuwa na mpandisha juu bure ila kwa kazi anazozifanya pia zimewafanya mastaa wa muziki kama Ali Kiba kutambulika Dunia kupitia mikononi mwake. Haya basi, kwanini tumuvike taji la Mfalme wa marejeo? Man Walter japo jina lake ni kubwa sana, lakini mdomo wake umekuwa finyu wa kutoa mtamushi kiholelaholela. Yeye amekua mtu wavitendo tu, huwaacha wengi wakaongea halufu yeye kupitia kemia yake na ujuzi wa miaka mingi kwenye kiwanda hiki kinacho kua kwa kasi cha Bongo Flava, akawajibu kwa mapigo ya kazi za mikono yake. Pengine naeza kuwa silijibi swali lililopo hapo juu, ila sasa naomba utulie maana jibu hili hapa linashuka asteaste.

Kuna wakati Staa wa Bongo Flava na mkali wa ngoma Aje nikimuzungumuzia Ali Kiba, aliamua kunyamaza ama kwenda mapumzikoni kimuziki kwa takribani miaka zaidi ya mitatu mfululizo. Nawakati akiwa mapumzikoni, huku nyuma vijana wenzake wenye tunu na tija za baraka za vipaji vya kuimba walikuja kwa kasi na kuiteka bahari ya Bongo Flava kwa fujo na mbwembwe na nusura jina la Alikiba kufunikwa na lisitajwe tena kabisa. Lakini ya Mungu nimengi, kati ya wale wasaanii wachanga, akaibuka kidedea mmoja wao ambaye ni Diamond Platnumz ambaye aliwafunika wote wasaani wa kuimba ambao kwa wakati huu walipachikwa jina la ”wabanapua”.

Nyota ya Diamond ilivyo ng’aa na kuzidi wengine, ilibidi mashabiki wamtafutie mtu atakaye weza kumkabili. Nahapo ndipo mashabiki wa upande mmoja wakajibandika jina la Team Kiba nakuanza kulalama kwamba Staa huyo wa Aje arudi studioni ili athibitishe kuwa yeye anaweza kumakabili Diamond. Hatimaye majibu ya mashabiki, nikimaanisha team Kiba ya kajibiwa. Ila Alikiba ilibidi amtafute mtayarishi wa muziki, si mkali tu bali anaye elewa muziki anaufanya Kiba ili aweza kutoa ngoma kali. Na karata hatimae zikamuangukia staa wetu na mfalume wa Come Back Man Walter.


Kibao Mwana kikazaliwa, na hakuna anayepinga. Kabla hata Video ya ngoma hiyo kutoka, Mwana ilifanya vizuri na kubadilisha taswira ya muziki wa kuimba si Tanzania tu bali Africa nzima. Na mtakubaliana na mimi kuwa wakati video ya Mwana ilipotoka, mashabiki wa upande wapili wa team Diamond walipata nafasi yakumuponda Alikiba kwa mara ya kwanza maana maudhui ya wimbo na video walidai kuwa yalikua hayaendani sambamba. Kwahivyo kwa upande mwingine walimaanisha kuwa, nyimbo ambayo ilitayarishwa na Producer Man Walter ilikuwa shwari ila muongozaji wa video hakuweza kuielewa nyimbo sababu ya lugha iliyotumika pale ilikuwa Kiswahili na ilihali yeye alikuwa Muafrika Kusini.


Sasa tena, Man Walter yule yule, aliyemrejesha Alikiba kwenye game, amefanya vilevile kwa Hussein Machozi. Hussein Machozi mwenyewe alijua fika kuwa, kurudi kwa game kama kitambo, basi alihitaji mtayarishaji mkali na mzoefu ambaye anaijua fika style anayotumia kimuziki. Na katika kuzicheza karata zake akiwa ughaibini nchini Italy, basi ramli yake ikamuangukia Producer Man Walter. Na matokeo yake ni kibao kikali, ambacho kimewagusa wengi tu. Wakati naandika makala haya hapa nchini Kenya, tayari kibao hiki kimesambaa kwa kasi maana wengi wa mashabiki wake staa huyu wako nchini humu haswa mjini Mombasa. Ama kweli mgala muue ila haki yake umpe, Man Walter japo wapo wengi watayarishi wa Muziki Africa ila yeye nafasi yake niyakipekee.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni