Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
6 Mei 2017
Makala: Asante Darassa kwa wimbo mpya, ila kumbuka CMG tunaidai
NI miaka zaidi ya sita sasa imepita tangu tumpokee kwa mikono miwili Ramadhani Shariff ‘Darassa’ katika muziki wa Bongo Fleva. Hatukumpokea hivi hivi bali mikononi alikuwa ameshikilia ngoma ijulikanayo kama ‘Sikati Tamaa’ aliyomshirikisha Ben Pol.
Vizuri sana, miaka inazidi kwenda muziki unazidi kukua. Darassa wa wakati ule sio wa sasa, amepiga hatua na muziki wake pia umepiga hatua.
Jana Darassa ametoa wimbo mpya ‘Hasara Roho’ na kukata kiu ya wengi waliokuwa wakimsubiri kwa hamu mara baada ya kufanya vizuri na wimbo wa Muziki. Maswali ya wengi sasa ni kama wimbo huu utafanya vizuri kuzidi ‘Muziki’, ila mimi kwenye hilo sina wasiwasi kwa sababau naujua uwezo wa Darassa.
Wasiwasi wangu ni namna Darassa anavyodondosha ngoma mpya kila kipindi, kabla hatujamsikia msanii yeyote wa lebo yake ya Classic Music Group (CMG), hapa twende pole pole.
Nimkumbushe hili Darassa
June 30, 2016, yaani mwaka jana Darassa alikuwa na mkutano na waandishi wa habari (press conference) katika ukumbi wa Habari Maelezo, Dar es Salaam. Katika mkutano huo Darassa alitangaza mipango yake mikubwa minne katika muziki wake kwa mwaka huo.
Mosi: Kutambulisha ‘style’ ya uchezaji ilijulikanayo kama ‘Zombi Walk’ ambayo atakuwa anaitumia katika ‘show’ zake akishirikiana na madensa wake.
Pili: Utambulisho wa ngoma yake mpya ambayo ilikuwa ‘Too Much’, alitangaza ngoma hii ingetoka June 12 mwaka jana na kweli akafanya hivyo. Pia alitoa dondoo kadhaa kuhusu ngoma hiyo, nilifurahi kwa kuwa alionyesha kujiamini na kuamini kile anachokifanya, kitu ambacho kilikuja kutokea.
Tatu: Alitambulisha ujio wa lebo yake ya CMG katika Bongo Fleva na kusema amelenga kuwainua wasanii wachanga na kuwapaisha kumuziki, ila kwanza CMG itaanza kwa kusimamia ‘project’ zake na ifikapo December itaanza kutoa kazi za wasanii wa lebo hiyo.
Aliwataja Mr Torch, Khabah, Dj Virus na Bastita kimbe kama watu wa karibu wa lebo hiyo ambao siku hiyo aliongozana nao, pia alimtaja na Director Hanscana ambaye alishindwa kuhudhuria.
Nne: Alitangaza kutoa historia ‘documentary’ siku chache zijazo ambayo itaelezea ‘hustle’ zake za miaka 15 kabla ya kutoka kimuziki.
“Lengo ni kuwatia moyo wasanii wachanga na vijana wanaotafuta maisha kwa ugumu, wengi walianza na Darassa ila wameshindwa kwa kukatishwa tamaa ila tunamshukuru Mungu kila tunapakatishwa tamaa ndivyo tunavyoinuka na kusonga mbele,” alisema Darassa.
Swali langu kwa Darassa
Kwenye mkutano huo, yote aliyozungumza Darassa binafsi nilivutiwa sana na suala la lebo kwani ni kitu kinachoonyesha kukomaa kwa masanii, kutaka kujitangaza zaidi na kuinua wengine. Nikaona asiondoke bila kumuuliza hata swali moja, au vipi?.
“Kwa sasa kumekuwa na muamko mkubwa kwa wasanii kusimamia wasanii wenzao (lebo), tumeona alianza A.Y, akaja Diamond, Ommy Dimpoz na sasa tunashikia Shilole naye anataka kufanya hivyo, pia Young Killer kupitia Matunzo Zero Unity, je hili la lebo wasanii mpo nalo serious au kwa sasa watu wanataka kufanya kama fashion?,”, niliuliza.
Jibu: “Mimi sifanyi vitu vya fashion na sipo katika dunia hiyo, ningekuwa naishi huko ungekuta tumeshakutana sana kwenye maisha ya fashion, am just to be a really. Sifanyi hiki kitu kwa kumuonyesha mtu yeyote au nataka fulani anione, na fanya hiki kitu kwa sababu nafeel.
“Nimekuwa na watu wengi nyuma yangu for years wakiamini kupitia mimi, siwezi kuwa mtu sawa kama sitowafanyia kazi hawa watu, nimeanza kufanya hivyo siku nyingi, mix tap yangu wa kwanza miaka mitatu iliyopita ilikuwa na wasanii ambao hawajulikani hata mmoja lakini nilifanya nao kazi ili wapate kusikika,” alijibu Darassa.
Kwa nini naandika haya
Naandika makala haya kama sehemu ya kumkumbusha Darassa katika ile mpigango yake minne. Kuna ambayo ametekeleza na kuna ambayo bado.
Ngoma ya Too Much kweli alitoa, alichosema nilikiona na ndio sababu ya kufanya vizuri, kwenye hilo hakuniangusha hata kidogo.
December ya mwaka jana niliyosubiria ngoma ya msanii kutoka CMG ilipita bila kusikia lolote, ilikuwa ni vigumu kuhoji wakati ngoma ‘Muziki’ imeshika kila kona. Hili deni ambalo Darassa anatakiwa kulilipa ili tuamni katika maneno yake vinginevyo swali langu daima litaishi kwake.
Kuhusu ‘style’ ya Zombi Walk bado sijaona hilo akilitendea kazi, ‘show’ zake nyingi bado naona anafanya mwenyewe licha ya kuwa anafanya vizuri. Kama angeishi katika maneno yake kwa kuifanyia kazi ‘style’ hiyo na kupandisha jukwaani madensa wake, ni wazi angeongeza dhamani kubwa katika muziki wake.
Diamond Platinumz anatoza mamilioni ya fedha katika ‘show’ zake, hii ni kutokana bidhaa anayokwenda kuuza jukwaa nje ya muziki wenyewe. Kwa wingi wa mashabiki alionao Darassa kwa sasa hashindwi kufanya hivyo, ni jambo tu la kujipanga.
Nafasi ya CMG
Binafsi niliamini katika CMG mara baada ya kueleza wazi mipango yao ambayo ni kuwa zaidi ya lebo. Licha ya kusimamia na kuwaibua wasanii wachanga walilenga kutoa ushauri kwa vijana kuhusu athari za utumiaji dawa za kulevya, pia ushauri wa kibiashara na uzalishaji wa kazi za sanaa.
Tuanze na hili la dawa za kulevya. Mwishoni mwa mwaka jana tulishuhudia ‘utitiri’ wa wasanii wakiripotiwa kutumbukia katika janga hilo, endapo CMG wangeanzisha mradi huo mapema walikuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kusikilizwa kwa kwao nao ni wasanii pia.
Sina maana kuwa wakati huu hawawezi kufanya hivyo, la hasha!, ila kwa wakati ule lingewapa maksi (credibility) zaidi na kuonekana kama watu waliojitoa zaidi kwa jamii. Zaidi ya hapo ni ule uwezo wa kuona mambo kabla ya wengine (intellectual), walijua wazi wasanii wanaathirika sana dawa za kulevya hivyo lebo yetu ikiwa na mpango wa kupiga vita hilo itakuwa wenye kuaminika zaidi.
Mambo haya yote yatawezeka iwapo timu CMG itasimama na kufanya kazi nje ya Darassa ambaya tayari ameshakuwa ‘brand’, CMG inahitaji watu wengine kutoka Darassa ili kukua, kujitangaza zaidi na kupanua wigo wa kibiashara.
Ajifunze mifano ipo wazi
Tangu kuanza kwa mwaka huu 2017, nimeona lebo tatu ‘changa’ zikionyesha uwezo katika muziki huu, naweza kusema lebo hizi zimeibuka baada ya Darassa kutangaza ujio wa CMG.
Lebo hizi zinamilikiwa na Fid Q, Navy Kenzo na Vanessa Mdee, hawa ni wasanii ambao wapo katika kiwango kimoja kimuziki na Darassa isipokuwa Fid Q aliyemtangulia. Lakini wamejaribu kwa muda mfupi na wameweza.
Cheusi Dawa Entertainment
Hii ni lebo ambayo anaimiliki Fid Q, hadi sasa inamsimamia msanii mmoja ‘Big Jah Man’ambaye kwa sasa anatamba ngoma itwayo Mabundi aliyompa shavu boss wake.
Awali Cheusi Dawa ilikuwa ni Tv Show yake ambayo iliwapa nafasi wasanii wengi wa hip hop nchini kuonyesha uwezo wao wa kuchana. Baada ya kusimama kwa ‘project’ hiyo, Cheusi Dawa ikawa sehemu ya kusimamia kazi zake hadi leo tunaizungumzia kama lebo.
Ngoma ya Big Jah Manambayo imetoka February mwaka huu mapokezi yake yamekuwa makubwa, bila shaka kilichopelea hilo ni uwepo wa Fid Q katika ngoma hiyo.
Mdee Music
Hii ipo chini ya Vanessa Mdee, hadi sasa ina masanii mmoja ambaye ni Mimi Mars. Msanii huyu kwa sasa anatamba na wimbo ujulikanao kama Sugar.
Huyu ni mdogo wake wa damu Vanessa Mdee ambaye ameshatengeneza ‘hit’ kibao kwenye Bongo Fleva. Mimi Mars akiwa kama msanii anayechipukia kazi yake imekuwa kifanya vizuri kwanzia kwenye radio na vituo vya runinga nchini na nje pia.
Kwa kipindi kifupi ameweza kutambulika, si kwamba ana bahati bali ni uongozi madhubuti alionao. Inaweza kuwa ni bahati ila haiwezi kufika kiwango hiki kwa ushindani uliyopo kwenye ‘game’.
Tumesikia vizuri wimbo huu (Sugar), na sasa anasiki katika wimbo wa mpya wa Quick Rocker ‘Down’.
The Industries
Lebo hii inamilikiwa na wasanii wawili, Nahreel na Aika ambao wanaunda kundi la Navy Kenzo. Hadi sasa wana simamia wasanii wawili, mmoja wapo ni Rose Ree.
Rapa huyu amekuwa akifanya vizuri tangu atoke na wimbo wake ‘One Time’. Kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Up In the Air’, kazi zote zake mbili zimetengenezwa na mmoja ya wamiliki wa lebo hiyo (Nareel).
Kwa mifano hii mitatu utaona kuna mafanikio yaliyofikiwa kwa muda mfupi na hawa wasanii wanaosimamia lebo hizi ambao hawajapishana sana kiuwezo na Darassa, hivyo CMG inaweza kufanya hivyo pia.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni