burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Jul 2017

Rihanna kurejea Afrika mwaka huu


Msanii wa muziki, Rihanna amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron, jijini Paris kwa ajili ya kutoa misaada kwa Bara la Afrika katika elimu.

Akizungumza na waandishi masanii huyo amelezea mipango yake ya kusaidia katika elimu kupitia tasisi yake. “Nilikuwa na kikao kizuri na Rais wa Ufaransa na mkewe.Wamenikaribisha na tumeongea kuhusu mada ya elimu tutatangaza tuliyoyafikia ifikapo Septemba mwaka huu,” amesema Rihanna.


Rihanna na mke wa Rais wa Ufaransa Bi.Brigitte Macron

Pia mrembo huyo ametangaza kurejea Afrika ifikapo Oktaba mwaka huu, kwa ajili ya kuendelea na mipango yake ya kusaidi Bara hilo katika elimu.

Mwezi wa pili  mwaka huu, msanii huyo alitunukiwa tuzo ya ‘Humanitarian of the Year’ na chuo cha Harvard kwa mchango wake katika elimu na afya.

NEW VIDEO | Msami Ft. Chemical - So Fine | Watch

Msami Ft. Chemical - So Fine


NEW VIDEO | Harmonize - Sina | Watch



NEW VIDEO | Bonge La Nyau Ft. Baraka Da Prince – Homa Ya Mapenzi | Watch


NEW VIDEO | Meda - Nawe | Watch

Meda - Nawe

26 Jul 2017

Nikki wa Pili ashusha ‘nondo’ kwa vijana


Rapper Nikki wa Pili kutoka kutoka kundi la Weusi amewataka vijana kujitengezea mfumo binafsi wa kujikwamua katika changomoto zinazowakabili.

Kupitia mtandao wa Instagram Nikki ameeleza kuwa ni vema vijana kuepuka mifumo ambayo haitawezesha ndoto zao kutimia bali wajaribu kufanya vyao hata ikiwa katika hatua ya chini.

“Kwa kijana uliyezaliwa Tanzania tambua kuna utamaduni mkubwa wa kuwapangia vijana cha kufanya, kusema, kuvaa, hata huko mashuleni au vyuoni sauti za vijana au wanafunzi hazina nafasi katika kuandaa mitaala wala namna ya kuendesha vyuo au shule kila kitu kinapangwa na walio wakubwa zaidi ndio mana kufanikiwa wengi wanaanza juu ya miaka 38,” ameandika Nikki.

“Kuna mifumo mingi ya kuwafelisha vijana, msifuate mifumo au mitizami isiyo akisi ujana wenu nguvu yenu na ndoto zenu, msisubiri vitoke juu kwa wakubwa kama msaada, anzieni chini jifunzeni kupitia nyie kwa nyie. Niamini mimi hata kwenye madarasa ya masters hakuna uhusishwaji wa sauti za wanafunzi katika lolote wewe lipa ada ingia darasani fundishwa pita hivi,” amesisitizi.

Nikki wa Pili kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Quality Time’ ambayo pia ni funzo kwa vijana katika kuzingatia muda ambao wanapaswa kuutumia kwa kufanya mambo yenye manufaa kwao.

Madrid na Man City kuingia vita ya dunia kwa Mbappe rekodi yake itachukua miaka mingi kuvunjwa


Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri wazi kuwa yupo katika vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji kinda wa AS Monaco ya Ufaransa, Kylian Sanmi Mbappe Lottin dhidi ya Mabingwa klabu bingwa barani Ulay klabu ya Real Madrid.

Pep Guardiola amesisitiza kuwa “chochote kinaweza kutokea”, kuhakikisha wanafanikiwa katika mbio zao za kumsajili, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18 na kuwazidi wapinzani wao Real Madrid.

Mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) klabu ya AS Monaco inatarajia kuweka rekodi ya dunia ambayo huenda ikachukua mihongo miwili ama mitatu mpaka kuvunjwa kwake hii ni kutokana na kuhitaji dau la pauni milioni 161 ikiwa ni sawa na Euro milioni 180 ili kumuachia mshambuliaji wao Mbappe.


Madrid kuvunja rekodi ya dunia

Vita ya klabu hizi sasa imeamia katika mchezo wao wakirafiki unaotarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi ya wiki hii katika dimba la Los Angeles Memorial Coliseum uliopo nchini Marekani.


Dimba la Los Angeles Memorial Coliseum uliopo nchini Marekani

Guardiola amesema vita yao ya kumsajili, Mbappe haija kwisha bado watapambana kuahikikisha wanafanikiwa.
“Mchezaji bado yupo na timu yake ya Monaco”. Guardiola ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari



“Chochote kinaweza kutokea bado tunaendelea kutafuta wachezaji watakao jumuishwa katika kikosi lakini Mbappe ataendelea kusalia katika mahitaji ya timu.”

City mpaka sasa imeshatumia zaidi ya pauni milioni 200 katika dirisha la usajili na Guardiola anawakingia kifua wapinzani wao wa Hispania kuwa hawatashinda katika vita hiyo.

“Madrid hawana zaidi ya vile Manchester City walivyo navyo”, amesema Guardiola.
Dirisha la usajili nchini Uingereza linatarajiwa kufungwa Agosti 31, huku Ligi kuu ya nchi hiyo (Premier League) ikitarajia kuanza Agosti 12 mwaka huu.

Shilole ‘ampuuzia’ Gigy Money


Baada ya choko choko za kila mara kutoka kwa Gigy Money kwenda kwa msanii Shilole, hatimaye msanii huyo ameonyesha kuchukulia poa choko choko za video vixen huyo.

Siku zilizopita Gigy Money alidai hawezi kufanya muziki na Shilole kwa sababu hamshabikii na hajawahi kupenda muziki wake, pia hivi karibuni alidai Shilole hajui kuongea kingereza vizuri.

Kupitia 5 Selekt ya EATV Shilole amesema ni kweli hajui kingereza vizuri, na anamchukulia Gigy Money kama mdogo wake.

“Ni mdogo wangu kwa hiyo lazima apite kwa dada yake, kwa hiyo watu kama hao wadogo zangu ninawachukulia poa tu, hamna tatizo,” amesema Shilole na kuongeza kuwa.

“Kingereza is not my language, kwa hiyo nikisema bado hainilazimishi kukijua sana lakini najifunza kuongea, na pale panapobidi nitaongea. Hiyo ni kweli hamna shida kama sijaenda (shule) ni sawa, kwani watu wangapi hawajaenda shule, ukiwa umeenda shule na hela uwenayo,” amesistiza.

Chemical azungumzia kivazi chake kilichoibua gumzo


Chemical amefunguka baada ya watu kuhoji kivazi alichovaa katika video mpya ya Msamii ‘So Fine’.

Rapper huyo amesema kuwa yeye ndiye bosi wa muziki wake na pia watu waelewe kuwa sanaa ni zaidi ya mavazi na shabiki anapaswa kujielekeza zaidi katika kazi ya msanii, lakini wale waliokosoa muonekano wake sio kitu kilichomkwaza.

“Hapana siwezi kuwa disappointment kwa sababu mimi nilivyojitambulisha kwa watu walinikubali jinsi nilivyo, kwa hiyo ningeamua kujitambulisha kwa namna ile watu walivyoniona na Msami pia watu wangekubali kwa sababu walikuwa hawajui the real me, kwa hiyo vyote vyote ningeamua kujionyesha kwa mashabiki wangenikubali,” ameiambia Daladala Bets ya Magic Fm na kuongeza.

“Kitu kingine nilitaka kuonyesha kuwa mavazi sio kitu kikubwa katika sanaa, naweza kubalika vyovyote ninavyotaka kuwa, mwisho wa siku unachatakiwa kupokea kutoka kwangu ni muziki,” amesisitiza.

NEW VIDEO | Joh Makini Ft. Davido - Kata Leta | Watch

NEW AUDIO I J- ONE - SAMBAMBA I DOWNLOAD

NEW AUDIO I EDANO NOVEMBER Ft LYDIA - HISIA ZANGU I DOWNLOAD




NEW VIDEO | Rich Mavoko Ft. Fid Q - Sheri | Watch


23 Jul 2017

NEW AUDIO I Betty Barongo & Walter Chilambo - Nijenge I DOWNLOAD


Weusi wajifunza mambo haya kutoka kwa Future: Waahidi pia kuachia kolabo yao na Sauti Sol

Image result for WEUSI
Kundi maarufu la Muziki la Weusi Kampuni limeahidi kuachia Kolabo yake ya kwanza kufanya na kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya.

Weusi wamesema kwa sasa wameshafanya kolabo na Sauti Sol kinachosubiriwa ni vitu vichache tu kumalizika ili waweze kuachia Kolabo hiyo.

Hata hivyo, Weusi wamethibitisha kuwa kuna Kolabo nyingine mbali na hiyo ya Sauti Sol ambazo wamefanya na Rapa Falz na YCEE wote kutoka Nigeria.

Kwa upande mwingine Weusi wanaotamba na single yoa ya ‘ Naliamsha Dude’ wamesema wamejifunza vitu vingi kikiwemo uzoefu wa kuperfom kwenye majukwaa ya kimataifa hii ni baada ya kuona Perfomance ya Rapa Future.

Weusi, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na Diamond Platnumz ndiyo Wasanii pekee kutoka Tanzania ambao walipata bahati ya kutumbuiza kwenye tamasha la Castle Light Unlocks lililofanyika jana usiku kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo Rapa wa kimataifa kutoka Marekani, Future alitumbuiza pia.

NEW New VIDEO: Flavour – Jaiye


“Fahyma anichungi” Rayvanny asema haya baada ya video yake akiwa na Gigy Money kusambaa mitandaoni

"Fahyma anichungi" Rayvanny asema haya baada ya video yake akiwa na Gigy Money kusambaa mitandaoni
Huenda Rayvanny anafuata nyayo za Diamond Platnumz – hii ni baada ya video yake na Gigy Money iliposambaa mitandaoni huku wakionekana kuwa na ukaribu usio wa kiurafiki tu.

Hata hivyo magnificent huyo wa tuzo ya BET 2017 ameiambia Times Fm kuwa yeye na Gigy Money ni marafiki tu na pia mpenzi wake Fahyma anafahamu haya. Aliendelea kuongeza kuwa yeye na Fahyma hawachungani kwa hivyo hili si jambo linaloweza kumletea shida na mama wa mtoto wake. Msanii huyo alisema,

“Hawezi kuchukia, halafu pia mimi sichungwi am live my life, president of own life, so nobody anaweza akaingilia akasema usifanye hiki, so Fahyma hana noma sometimes anaweza akafanya vitu vyake mimi simuingilii.”

Hata hivyo alidai kuwa video yake na Gigy Money ilikuwa ya utani lakini wambea waliona kuineza ilikumletea utata.

“It’s just a joke, Gigy ni mshikaji wangu na ni wa Mbeya pia, namjua before hajanza mbwembwe zake na ni mtu ambaye yupo happy muda wote mimi naona anaenjoy maisha yake”.

Vanessa Mdee: Mapenzi yangu na Jux hayakuwa ya kisela

Vanessa Mdee: Mapenzi yangu na Jux hayakuwa ya kisela
Wiki mbili zimepita sasa tangu Vanessa Mdee kuachia wimbo wake mpya wa kimapenzi ‘Kisela’ aliyomshirikisha Peter Okoye wa P Square.

Mdee, ambaye aliwachana na mpenzi wake Juma Jux, alifunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki huyo.

Mrembo huyo alieleza kuwa mapenzi yake na Jux hayakuwa ya kisela kwani walikua wako na mapenzi ya dhati ingawa iliisha katikati.

“Mapenzi yangu na Juma hayakuwa ya Kisela, lakini pia sitaki na ninakemea kwa nguvu mapenzi ya kisela. Kuhusu kuimba wimbo huu nikwamba nimewasaidia wanawake wenzangu ambao huwa wanaingia kwenye mahusiano bila kujua ni mahusiano ya aina gani waliyonayo. Lakini kwenye uhalisia mimi siishi maisha hayo,” Vanessa aliambia EATV.

Hutaamini alichosema Emmanuel Mbasha kuhusu mtalaka wake, Flora


Aliyekuwa mume wa Flora Mbasha ‘Madam Flora’ ambaye pia ni mzazi mwenziye, Emmanuel Mbasha ameibuka gumzo mitandaoni baada ya kuandika ujumbe wa ghadhabu unaodaiwa kuwa huenda ni dhidi ya mtalaka wake.

Mbasha aliandika ujumbe huo kama majibu, baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa ambazo si za kweli zilizodai kuwa Flora alifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Mbasha, akisema uvivu wake kitandani ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao, ambapo Flora alikanusha vikali taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Baada ya taarifa hizi kutua mezani kwa Emmanuel, alipiga kimya kwa muda kutokana na kuwa bize na msiba wa bibi yake, lakini baada ya mazishi, akaingia kwenye mahakama ya mastaa , Instagram na kuandika ujumbe huu.

“Sipendi ujinga kabisa kwani hamuwezi kuuza hicho kidaftari chenu mpaka mtafute kiki kwangu?, acheni hizo mnaniingiza kwenye upumbavu wenu ili mkiuze hicho kidaftari chenu, Mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri, sipendi kabisa mie naingiaje kwenye hizo ishu za huyo mwanamke miaka zaidi ya 3 siko nae, na ni mke wa mtu na wewe hembu tulia na mmeo huko tena ukome kunitajataja.

Huoni hata haya eti unakiita kidaftari jina langu si uite la mumeo huyo, kunitajataja tu, taja jina la huyo bwana ako sijui nani vile! asinihusishe, usinihusishe Mnikome mbona mie siwafatili na bwana ako kwa lolote lile, kila mtu apambane na hali yake, pambana na hali yako,” alisema Mbasha.

NEW VIDEO | Linex X Nashipai - Angejua | Watch

Linex X Nashipai - Angejua


Ruby adaiwa kunasa ujauzito



Ikiwa amekaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma wala video, kuna taarifa zimeibuka kuwa msanii wa muziki Ruby ni mama kijacho.


Hii ni moja ya picha ya msanii huyo aliyoianika mtandaoni

Kwa mujibu wa vyanzo vya yetu vimeeleza kuwa mkali kutoka Bongo amekuwa kimya kutokana na kuwa ni mama kijacho,na hata ukipita katika baadhi ya picha zake katika mitandao unaona amekuwa akiongelea kuhusu suala la kuwa mama na kuweka picha za ujauzito.


Husna Abdul, Tunda na Linah Sanga

Endapo kama kweli ni mama kijacho msanii huyo atakuwa ameingia kwenye orodha ya watu maarufu wenye vibendi, kama vile Tunda, Linah Sanga, Husna Abduli na wengineo.

Nina ofa ya ngoma 10 kutoka kwa Trey Songz – Ben Pol


Msanii wa RnB Bongo, Ben Pol ameweka wazi mipango yake ya kufanya ngoma na wasanii wa nje.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Bongo Flava Top 20 cha EA Radio kuwa kutokana na ngoma yake ‘Tatu’ aliyomshrikisha Darassa kufanya vizuri amejikuta akipata ofa mbalimbali za kufanya kazi na wasanii wakubwa wakimataifa kama Chidinma wa Nigeria na Trey Songz wa Marekani.

“Nina kolabo nyingi zinakuja, nimeshafanya moja na Chidinma wa Nigeria ipo tayari, pia nina ofa ya ngoma 10 kutoka kwa director wa msanii Trey Songz wa Marekani ambapo nitaweza kufanya kazi moja na Trey Songz,” amesema Ben Pol.

Cheko la Maromboso wa Yamoto Band na safari ya WCB

Muimbaji Maromboso ambaye alikuwa Yamoto Band anadaiwa kuwa yupo mbioni kuelekea kwenye label kubwa ya muziki ya WCB.

Tetesi hizo zilichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya muimbaji huyo kuonekana kuwa karibu zaidi na rais wa WCB, Diamond Platnumz hasahasa baada ya kuonekana kushiriki kwenye project ya Diamond Karanga.

Muimbaji huyo akizungumza na Bongo5 wiki hii alikanusha taarifa hizo licha ya suala hilo kuonekana lina ukweli ndani yake.

Hata hivyo watu wakaribu wa muimbaji huyo wanadai muimbaji huyo tayari ameshasaini mkataba na label hiyo na kinachosubiriwa ni wakati wa kutoka tu.

Huu ndio muda mzuri wa kuanza kazi – Enock Bella wa Yamoto Band

Image result for Enock Bella
Msanii wa Bongo Flava, Enock Bella amedai ukimya wake ukilinganisha na wasanii wengine wa Yamoto Band amesababishwa na kutafuta menejiment ila kwa sasa amepata na muda wowote kazi zake zitaanza kusikika.

Akipiga stori na g.lovetz ameeleza pia anashukuru kuona member wenzake wa Yamoto Band wakifanya vizuri  na kazi zao nzuri ambazo zimefika mbali na yote inatokana na wao kuanza kupata menejimenti.

“Kwa sasa nina menejiment mpya ndio tunapanga ratiba ilimradi kazi iende vizuri, ukimya wangu ulikuwa katika michato ya kutafuta menejiment iliyomadhubuti ya kusimamia kazi zangu, kwa hiyo sasa hivi ndio muda mzuri wa kuanza kazi ingawaje ndugu zangu wameanza kwa kuwa wao walianza kupata hizo menejiment,” amesema Bella.

13 Jul 2017

Kuhusu Ray C kukesha studio siku mbili


Msanii wa Bongo Flava na hitmaker wa ngoma ‘Unanimaliza’, Ray C inaelezwa kutokana na uwezo wake wa kazi si ajabu yeye kukesha studio siku mbili akifanya kazi.

Mmoja wa mameneja wake, T Fighter ameeleza kwa malezi aliyolelewa Ray C ni tofauti na wasanii wengine kwani amezoea kurekodi albamu na si single.

“Tukienda studio tunakesha hata siku mbili, mimi nishazoea nikienda studio nakaa lisaa limoja naondoka ila yeye akiingia studio anakaa siku mbili anarekodi nyimbo tatu au nne kali,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Ameongeza kuwa kutokana na uwezo wake wa kazi wimbo wa Unanimaliza ulirekodiwa ndani ya saa mbili tu.

Diamond Platnumz – Fire ( Behind The Scene part 1, 2 and 3)

PART 1
PART 2
PART 3

NEW AUDIO | Peter Msechu - Yakawa | Download

Peter Msechu - Yakawa

NEW AUDIO | Mesen Selekta – Sukari | Download

Mesen Selekta – Sukari

NEW AUDIO | Matonya - Nyumba Ndogo | Download

Matonya - Nyumba Ndogo

NEW AUDIO | Linex Sunday Mjeda - Got Me | Download

Linex Sunday Mjeda - Got Me


NEW AUDIO | Jimmy CHansa - Sijakusahau | Download


NEW VIDEO | Matonya - Nyumba ndogo (Nachelewa) | Watch


9 Jul 2017

KILA SIKU NAZIDI KUPATA MARAFIKI WAPYA NA NI WAZURI PIA -G.LOVETZ

Boss wa blog ya G.lovetz ameiambia blog yake kuwa kila siku hupata marafiki wapya na ni wazuri pia huwa anapenda sana kutembelea sehemu za kuosha macho yani kuburudisha nafsi

maneno hayo yalimtoka siku ya jana ambayo ilikuwa ni wikiendi nzuri sana kwake kwa kupata marafiki wapya wengi wao ni wachangamfu na wenye furahaa pia

pia anaongezea kwa kuwashukulu wote waliokuwepo eneo la tukio  na kuwapomgeza sana wote walifurahi mpaka mwisho wa siku nzima

Ebhnaa eehh nisiwe mchoyo nakupa full stori kwa njia ya picha