burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Jul 2017

NILIANZA NA NYIMBO ZA MAPENZI NA ZA KIJAMII LAKINI BAADAE NIKAANZA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI NDIPO BARAKA ZA MUNGU NIKAZIONA JUU YANGU - BAISA MHELA


Baisa Mhela ni mwimbaji binafsi Wa music Wa injili anayeishi jijini dar es salam na ni mwumini wa kanisa la baptist pia mhitimu Wa mafunzo ya utabibu kutoka katika chuo cha Kampala university of dar es salam

Baisa Mhela aliiambia g.lovetz kuwa ana walezi pamoja wazazi wake waligundua kipaji chake cha uimbaji alipokuwa shule ya awali baada ya kuanza kutumika kwa kuongoza wenzake katika uimbaji na pia kuanza kuimba kanisan kwaya za watoto akiwa mdogo sana chini ya miaka kumi aliendelea na uimbaji Wa music kanisan lakin baadae akiwa na miaka 18 alikutana na shilika linalohusu vijana youth challenge intanational lililopo Canada likaanza kumtumia yeye na wengine ktk uelimishaji Wa maswala ya jamii ndipo akaanza kuimba nyimbo mbali mbali zinazohusu jamii mapenzi,magojwa anasa na burudani

Aliamua kuacha music huo baada ya kushauriwa na viongozi wake Wa kanisa walioko mkoani morogoro na kuanza rasimi kuimba injili katika matamasha mbalimbali na makanisani mwaka 2013 ndipo alipoacha rasmi japo alikuwa ameanza kuwa na umaarufu lakin aliskiliza ushaul Wa viongozi wake Wa kanisani

Baisa Mhela anasema kikubwa kinachomvutia katika music Wa injili ni jinsi neno la Mungu lilivo na nguvu katika matamasha huwa anapokelewa vizuri sana  mafanikio aliyoyapata mpaka sasa anasema ni jinsi anavyopata safar mialiko mbali mbali ndani na nje ya Tanzania hivo inamsadia kuinua kipato chake na anaweza kusaidia wanamusic wengine Wa injili wanaochipukia mpaka sasa ana nyimbo saba za injili alizozilekodi na zinapigwa katika redio mbalimbali Tanzania na Kenya

Anaongeza kwa kusema katika nyimbo zake wimbo bora kabisa anaoupenda ni mwimbie Mungu kwa kuwa ndio wimbo aliokuwa anauimba tangu akiwa mtoto bibi yake ambaye ameshafariki anaitwa Mahuyemba ndie aliye mfundisha hivo anaupenda kwa kuwa unamkumbusha bibi yake kipenzi mpaka sasa amefanya video tatu katika album yake anaomba watanzania na watu Wa Mungu kuendelea kumpokea vizuri katika nyimbo zake zote.

Maoni 2 :

  1. Glory To God, Mungu Ambariki sana kaka Baisa kwa Huduma nzuri aliyopewa na Mungu.

    JibuFuta
  2. Glory To God, Mungu Ambariki sana kaka Baisa kwa Huduma nzuri aliyopewa na Mungu.

    JibuFuta