Artist from Tanzania II Best perfomer II Song Writter II G.LOVE TANZANIA ENTERTAINMENT Dar es Salaam Tanzania Mobile:0766065169 Email.ggodyan@gmail.com.
burudan
https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/
26 Jul 2017
Madrid na Man City kuingia vita ya dunia kwa Mbappe rekodi yake itachukua miaka mingi kuvunjwa
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri wazi kuwa yupo katika vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji kinda wa AS Monaco ya Ufaransa, Kylian Sanmi Mbappe Lottin dhidi ya Mabingwa klabu bingwa barani Ulay klabu ya Real Madrid.
Pep Guardiola amesisitiza kuwa “chochote kinaweza kutokea”, kuhakikisha wanafanikiwa katika mbio zao za kumsajili, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18 na kuwazidi wapinzani wao Real Madrid.
Mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) klabu ya AS Monaco inatarajia kuweka rekodi ya dunia ambayo huenda ikachukua mihongo miwili ama mitatu mpaka kuvunjwa kwake hii ni kutokana na kuhitaji dau la pauni milioni 161 ikiwa ni sawa na Euro milioni 180 ili kumuachia mshambuliaji wao Mbappe.
Madrid kuvunja rekodi ya dunia
Vita ya klabu hizi sasa imeamia katika mchezo wao wakirafiki unaotarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi ya wiki hii katika dimba la Los Angeles Memorial Coliseum uliopo nchini Marekani.
Dimba la Los Angeles Memorial Coliseum uliopo nchini Marekani
Guardiola amesema vita yao ya kumsajili, Mbappe haija kwisha bado watapambana kuahikikisha wanafanikiwa.
“Mchezaji bado yupo na timu yake ya Monaco”. Guardiola ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari
“Chochote kinaweza kutokea bado tunaendelea kutafuta wachezaji watakao jumuishwa katika kikosi lakini Mbappe ataendelea kusalia katika mahitaji ya timu.”
City mpaka sasa imeshatumia zaidi ya pauni milioni 200 katika dirisha la usajili na Guardiola anawakingia kifua wapinzani wao wa Hispania kuwa hawatashinda katika vita hiyo.
“Madrid hawana zaidi ya vile Manchester City walivyo navyo”, amesema Guardiola.
Dirisha la usajili nchini Uingereza linatarajiwa kufungwa Agosti 31, huku Ligi kuu ya nchi hiyo (Premier League) ikitarajia kuanza Agosti 12 mwaka huu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni