burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Mac 2017

Asilimia 70 ya watumiaji dawa za kulevya ni wanawake


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga, amesema zaidi ya asilimia 70 ya waathirika wa dawa za kulevya ni wanawake.

Kamishna Siyanga alitoa kauli hiyo Jumatatu hii, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ya mwaka 2016.

“Zaidi ya asilimia 70 ya watumiaji wa dawa za kulevya ni wanawake, ndilo kundi lililoathirika zaidi, jambo hili ni kubwa si Tanzania tu, bali nchi mbalimbali duniani, tunahitaji ushirikiano kuhakikisha tunalimaliza.”

Aidha Kamishna huyu alisema pamoja na mambo mengine zipo njia tatu ambazo zinapaswa kufuatwa kuhakikisha vita dhidi ya dawa za kulevya inakomeshwa nchini ambazo ni pamoja na kuzuia uingizaji, kutoa elimu na matibabu kwa waathirika huku akisisitiza kuwa hawatachukulia hatua za sheria waathiriwa wa dawa za kulevya, badala yake watawasaidia kuwapatia tiba waweze kurejea katika hali yao ya kawaida huku wakiwahoji wanakopata dawa hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni