burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Mac 2017

Chanzo cha bifu ya Fid Q na Rado ni wimbo wa Chagua Moja, hiki ndicho kilichotokea


Moja ya bifu kubwa zilizowahi kutokea kwenye muziki wa Hip Hop nchini, ni kati ya Fid Q na Rado. Lakini unajua chanzo cha bifu hiyo ? Ni collabo ya Chagua Moja.

You see, kabla ya hapo rapper hao wote wanaotokea Mwanza walikuwa washkaji, lakini shetani alipita kati yao.

“Tayari nimepata label Bongo Records, naenda Bongo Records kurekodi Chagua Moja washkaji zangu wote wamewahi, kasoro Rado ndio amefika amechelewa,” Fid alimsimulia Lil Ommy wa Times FM kwenye kipindi chake cha The Playlist.

“Kaja katukuta tusharekodi, nikasema ‘mzee Majani, bado kuna verse moja ya Rado.’ Majani ananiambia ‘Mzee ngoma ishaisha hii, ushkaji na kazi ndio maana mnakuwaga mnafeli nyinyi, hapa ukiongeza verse inakuwa ndefu haiwi kiredio hii, hii ngoma ya redioni babu, kwahiyo kamwambie mwanao hii ngoma ishaisha.’ Hebu piga picha hapo nipo studio halafu nikamuambia Rado ngoma ishaisha, yupo getini.”

“Nikaenda getini, tena na tabasamu langu kabisa, ‘oyaa mwana amini usiamini nimejaribu kumfafanulia jamaa kwamba bado verse yako jamaa ananiambia ngoma ishaisha, I am sorry to say that sitapata verse yako katika ngoma yangu lakini if only wishes were horses, ningependa kuwa nayo lakini with all due respect jamaa kagoma na jamaa ndio kama music director wangu hivi sasa na mimi ndio niko Bongo Records inabidi nimsikilize yeye ndio kaamua hivyo, siwezi kugombana naye mimi naomba unisamehe.’

Fid anasema taarifa hiyo ilimkwaza Rado aliyeamini kuwa amebaniwa na mshkaji wake.

“Basi mimi nikajua mwanangu kanielewa sababu nimemfafanulia kihophop nini. Ameenda kule alikoenda ndio yakatokea yaliyotokea, ‘usiulize kama umeona pigia mstari’, ananichana kama snitch fulani na nini wakati si kweli.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni