burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Mac 2017

Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings washtakiwa na FA


Mchezaji wa klabu ya Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki wa Bournemouth Tyrone Mings wamefunguliwa Mashitaka na chama soka cha England (FA) kwa Mchezo usio wa kiungwana.


Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings wameshtakiwa na FA kwa vitendo vyao walivyofanya katika mchezo wa ligi Jumamosi iliyopita. Ikiwa watapatikana na hatia huenda wakafungiwa mechi zisizopungua 3, kwa maana hiyo Zlatan hatocheza mchezo wa FA Cup vs Chelsea na mechi nyingine mbili za ligi.

Kwa mujibu wa Kanuni za FA, Mchezaji kumpiga Kiwiko na Kumkanyaga mchezaji mwezake makusudi ni faulo ambazo zinastahili kutolewa kadi nyekundu na pia Kifungo cha kusimamishwa kucheza Mechi 3.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni