burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Feb 2017

Claudio Ranieri asema alikuwa ana ndoto ya kuendelea kuifundisha klabu ya Leicester City


Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri baada ya kufungishiwa virago wiki hii, amesema kuwa ndoto yake imepotea ya kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Ranieri mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Leicester kushinda taji hilo licha ya kuorodheshwa kuwa na nafasi moja kati ya 5000 kushinda taji hilo.

Leicester sasa iko pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja huku ikiwa imesalia mechi 13.

“Baada ya furaha ya mwaka uliopita na kushinda taji la ligi nilikuwa na ndoto ya kusalia na Leicester. Kwa bahati mbaya haikuwezekana. Fursa hiyo ilikuwa nzuri na itakuwa nami maishani,” alisema Ranieri

Aliongeza, “Ninamshukuru kila mtu katika klabu hiyo,kila mtu aliyeshiriki katika ufanisi ,hususan mashabiki. Muliniweka katika nafsi zenu kuanzia siku ya kwanza na kunipenda.Ninawapenda nyie pia nami. Hakuna mtu anayeweza kuchukua kile tulichofanikiwa kupata pamoja na natumai munalifikiria hilo na kutabasamu kila siku ninavyotabasamu,”

Steve Nyerere aikubali audio iliyosambaa mtandaoni, ni ile anayowazungumzia viongozi kuhusu sakata la Wema

Msanii wa filamu nchini na mchekeshaji Steve Nyerere amefunguka na kuizungumzia audio yake na Mama Wema Sepetu ambayo ilisambaa mtandaoni kuhusu sakata la Wema Sepetu na dawa za kulevya.
Aidha muigizaji huyo amedai hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii baada ya kada mwenzake, Wema Sepetu kuhamia CHADEMA siku ya jana, Steve amedai Wema Sepetu ndiye msanii aliyelipwa pesa nyingi wakati wa kampeni za CCM 2015.

“Kati ya wasanii waliolipwa fedha nyingi na CCM ni dada (Wema Sepetu), na hakuna msanii wa Mama Ongea na Mwanao anayeidai CCM-Steve Nyerere. CCM tulifanya kampeni na tulilipwa, hatukuingia mkataba kuwa baada ya kampeni ukikamatwa na unga, CCM itakulinda na kukutetea,” alisema Steve Nyerere.

Kuhusu audio ambayo ilisambaa mtandaoni akizungumza na Mama Wema kusuhu sakata la Wema na madawa ya kulevya na kuwahusisha baadhi wa viongozi wa serikali na wabunge, Steve amedai siyo kweli kwamba alizungumza na viongozi hao kama alisema kwenye audio kwani alikuwa kumlaghai mama Wema Sepetu ili kumtuliza.

“Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa. Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa,” alisema

Aliongeza, “Sijazungumza na Waziri yeyote kuhusu Wema kukamatwa, nilitaka kumtuliza Mama. Ni kama kumlaghai mtoto na pipi achomwe sindano. Niwaombe radhi wote niliowataja katika mazungumzo yangu, sikufanya kwa nia mbaya, nilitaka kukilinda chama na kumsaidia Wema. Niliombe radhi Bunge tukufu, nimuombe radhi Spika Ndugai kwa kudanganya kuwa nilishinikiza Wabunge wamjadili Wema Sepetu. Nimuombe radhi Rais Magufuli kwa kuwatumia Mawaziri wake aliowaamini katika hili, lakini sikufanya kwa nia mbaya,”

Hawa ndio wasanii wanaompa changamoto Country Boy


Country Boy amewataja wasanii ambao wanaonekana kumpa changamoto kwenye muziki.

Raper huyo amewataja wasanii wanne kutoka Afrika Kusini ndio wanaompa changamoto huku kwa Bongo akimuona Bill Nas pekee.

“Ukimsikia Bill Nas unamsikia Emtee anauza, kuna Nasty C, KO, kuna Cassper Nyovest. Kwahiyo ukimweka na Bill Nas hiyo ndio challenge yangu, nafanya muziki ambao unatakiwa kuwa kiinternational,” amekiambia kipindi cha FNML cha EATV.

Kwa sasa rapper huyo yupo chini ya lebo ya LFLG inayoongozwa na Petit Man na Chakoma na tayari ameachia video ya wimbo wake wa kwanza ‘Hakuna Matata’ akiwa chini ya lebo hiyo.

Wayne Rooney asema ataendelea kusalia Manchester United


Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anasema kuwa atasalia katika klabu ya Manchester United baada ya kuhusishwa na uhamisho wa China.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kuwa anatumai kwamba atashirikishwa kamili katika mechi zilizosalia za klabu hiyo msimu huu.

Mkufunzi wa United Jose Mourinho amekataa kukana kwamba Rooney huenda akaondoka klabu hiyo mwezi huu, ijapokuwa uhamisho huo huenda usikamlike kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho nchini China mnamo tarehe 28 Februari.

“Ni wakati wa furaha kubwa katika klabu hii na ningependa kusalia,” alisema Rooney.

Ajenti wake Paul Stretford, alisafiri kuelekea China kuona iwapo arafanikiwa kupata makubaliano, ijapokuwa haijulikani alizungumza na klabu gani.

Mbili kati ya klabu tatu zilizoonekana kuwa klabu m’badala Beijing Guoan na Jiangsu Suning, zilfutilia mbali uvumi kuhusu uhamisho huo.

Nicki Minaj ajibu mapigo, atuhumiwa kumdiss Remy Ma kwenye nyimbo 2

Nicki Minaj na Remy Ma mambo yameanza kuwaka moto. Nicki atuhumiwa kumdiss Remy Ma kwenye nyimbo mbili alizoshirikishwa.
Nyimbo hizo ambazo rapper huyo wa kike anadaiwa kumdiss Remy ni ‘Swalla’ ya Jason Derulo aliomshirikisha Nicki na Ty Dolla na mwingine ni ‘Make Love’ wa Gucci Mane aliomshirikisha Minaj.

Tukianzia kwenye wimbo wa ‘Swalla’ Minaj amerap, “I gave these bitches two years, now your time’s up. Bless her heart, she throwin’ shots, but every line sucks. I’m in that cherry red foreign with the brown guts. My shit sluppin like dude did Lebron nuts.”
Remy Ma aliachiwa gerezani Agosti 2014 ambapo mpaka sasa ni miaka miwili imepita na Nicki Minaj amekuwa kimya kwa takribani miaka miwili tangu alipoachia albamu yake ‘The Pinkprint’ Disemba 2014, kulingana ma mashairi ya Nicki yanaonekana mja kwa moja yamemlenga Remy Ma.

Wakati huo huo tukiangalia kwenye wimbo wa ‘Make Love’, Nicki amerap, “Go against Nicki, it’s gon’ cost ya. Cause now it’s fuck ya, intercourse ya. I rep Queens where they listen to a bunch of Nas. I’m a yes and these bitches is a bunch of nahs. Trying to win a gunfight with a bunch of knives. I win, get off the bench and give a bunch of fives. I don’t see her Bitch, I’m ‘The Greatest’, no Kendrick, and no Sia. I’m the iPhone, you the Nokia.”
“You the queen of this here? One platinum plaque, album flopped, bitch, where?,” ameongeza. Kulingana na mashairi hayo ya Nicki ni dhahiri amemdiss Remy Ma kutokana na rapper huyo wa kike wimbo wa ‘All The Way Up’ aliofanya na Fat Joe baada ya kutoka gerezani ndio umefanikiwa kufikia mauzo ya Platnum Plaque na albamu yake ya ‘There’s Something About Remy’ aliyoitoa kabla hajaenda gerezani ndio haikufanya vizuri sokoni.

Hata hivyo mwezi Disemba mwaka jana naye Remy Ma alituhumiwa kumdiss Nicki kwenye wimbo wa ‘Wait a Minute Remix’ alioshirikishwa na Phresher.

Sam wa Ukweli kuvunja kimya kirefu cha muziki hivi karibuni!


Staa wa Bongo Flava Sam wa Ukweli, anapania kuachia kibao kipya hivi karibuni. Sam ambaye amekuwa kimya kwa muda sasa anahisi ni wakati muafaka wa yeye kuikata kiu ya muziki kwa mashabiki wake.
Hata hivyo kibao hiki kwa jina Nawaona kinatarajiwa kuwa kibao kinachoeleza ugumu uliopo kwenye game ya muziki wa Bongo Flava kwa sasa. Hit maker huyo wa ‘Hata Kwetu Wapo’ alimtumia sample ya nyimbo hiyo mkali wa Muziki Majanga Dogo Rich ambaye walishawahi kufanya collabo pamoja awali ilikuisikiliza.

Dogo Rich hakusita kueleza ujumbe uliopo katika kibao hiki Nawaona kwani ujumbe uliopo kwenye ngoma hii unaonekana kushabihiana na ujumbe wa Muziki Majanga. Rich alitumia ukurasa wake wa Facebook kumwaga mtamaa kwenye kuku wengi kwa maneno haya yafuatayo.

Ndugu yangu Sam kanitumia nyimbo karibu inilize…yaani usidhani majanga yapo kwetu…wenzetu pia wanayapitiw japo wako kimya.. richie nimetoa hits kibao tu ..Naonaraha..sinaraha hayanamjuzi…yoyobah na baadae majanga eti natafta kiki …kwani nilikua cjulikani daaaa tafuta nyimbo ya sam itakugusa sana….

Kunani? Maneno haya yanavutia na yamewatia mashabiki wengi hamu ya kujua kibao Nawaona kimebeba nini. Je Sam Wa Ukweli atatumia fursa hiyo kuwataja mastaa wakubwa Bongo na maisha yao wakiwemo ma producer na waimbaji kama alivyofanya Richie ama bahasha hii mpya imebeba kitu gani ndani yake? Sisi letu jicho na masikio tayari tumeyafungua kuona na nini Sam Wa Ukeli anatuletea.

TID kumshtaki Steve Nyerere, ni baada ya kutuhumiwa kupokea milioni 2 za RC Makonda


Msanii mkongwe wa muziki Khalid Mohamed ‘TID’ ameahidi kuwachukulia hatua watu wanaosambaza taarifa kuwa alipewa pesa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kama kivuli katika sekeseke la kutaja majina ya wanaohusika na dawa za kulevya.

Muimbaji huyo alisema yeye alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na serikali ilimkamata kwa kosa la kutumia lakini ikaamua kumsaidia kwa kumfanya aachane na dawa hizo pamoja na kumpa nafasi ya kuelimisha vijana wenzake ambao bado wapo katika janga hilo.

“Watu wana ushahidi gani kama mimi Mh. Makonda kanipa mimi pesa au wanazungumza tu? mimi nataka huyo sijui Steve nani nani…..aseme kwamba aliniona nikipatiwa hizo pesa bila hivyo mimi nitamshtaki, unaituhumu serikali, bila ushahidi, hili ni kosa ambalo naweza nikampeleka mtu mahakamani,” TID alikiambia kipindi cha Selekt cha EATV.

Msanii anayedaiwa kutoa kauli hiyo ya TID kupewa pesa ni Steve Nyerere, kupitia sauti za simu zilizosambazwa tangu juzi, zikionesha mtu anayedhaniwa kuwa ni Steve Nyerere akiongea na mtu anayedhaniwa kuwa ni Mama wa msanii Wema Sepetu.

Willy Paul Msafi awatoa povu mashabiki kwa picha za harusi akiwa na Alaine wa Jamaica


Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya almaarufu kama Willy Paul Msafi, Ijumaa hii ya tarehe 24/2/2017 amezua gumzo kwenye mitando ya kijamii Kenya baadaya ya ku-post picha zinazoonyesha kua amefunga ndoa na mwanamuziki staa wa Dance hall kutoka Jamaica mrembo Alaine.

Willy Paul anatambulika kuwa mshndani wa karibu wa msanii mwenzeke wa muziki wa gospel, Kevin Bahati, ambaye hivi majuzi alitikisa nguzo za mitando ya kijamii Africa Mashariki kwa kutuletea Prayer Partner wake. Je Willy Paul analipiza kwa kumjibu Bahati na Alaine kama prayer partner wake ama ni project tu?

Alaine ambaye hivi majuzi alifanya collabo ya wimbo Addicted na mwanamuziki Edyy Kenzo kutoka Uganda, amekuwa akiitembelea nchi ya Kenya kufanya kazi zake za muziki. Na inafahamika kazi yake yakwanza kufanya na Mkenya ilikuwa Nakupenda aliyofanya na Wyre.

Hata hivyo mrembo huyo wa Jamaica hajasema lolote kuhusiana na kuwekwa kwa picha hizo za pamoja ya harusi na Willy Paul Msafi japo ametajwa mara zaidi ya mia moja kwenye tags na mashabiki lukuki wa muziki wa mwanamuziki Willy hali ambayo imefanya jina lake ku-trend kwenye mtandao wa Twitter nchini Kenya.

Mashabiki wengi wa Willy Paul na wale wa mpinzani wake kimuziki Bahati, wamekuWa wakitoa maoni yao tofauti tofauti huku wengi wakikataa kabisa kuwa Alaine anaweza kuolewa na Willy Msafi.

Soma hapa baadhi ya cheche zenye hisia tofauti kutoka kwa mashabiki nchini Kenya, Ambao wengi wamepigwa na butwaa maana hawakutarajia kama Willy Paul angechukua hatua kama hii, ambayo kwakweli haijulikani kama ni project ya wimbo ama wanamuziki hawa wawili wameamua kuzifunga pingu za maisha pamoja.

bil.jordan‏@bilojode:I repeat if Alaine x Willy Paul is anything other than a music video I’ll never listen to Alaine again

Melchizadek Olungur‏@melongur: hahaha….so Willy Paul was the Wafula Alaine was searching for That’s the world for you

ReplyLoki (ECCC-P14)‏@MisterLokiDoki: Quick drawings of my NPC Alaine from my DND campaign with @Dihuh @kikiinspace @GendoBrendo and @NavyBlueDude

Joshua Ndirangu: MoDon’t get me wrong folks, its not that I dislike Willy Paul, I fc***ng despise him. Alaine read my lips

IamConstato‏@ConstatoAsirvex: Now it’s Willy Paul and Alaine next will be Mbuci Bonoko with Nicki Minaj

Master_Ben‏@benhembb: so we shud just call Willy Paul #wafula as that’s what she came searching 4 & Alaine #mke_mwema coz that’s wat he prayed 4!

DJ PSKRATCH™‏@PSKRATCH1 MoAlaine is an SDA and Willy Paul is a Lejio Maria. I have no idea of how they are prayer partners #alaine

Replyremzilla‏@remzi_wemzi: Awww Alaine got married

Oscar pentium‏@Oscarpentium: I got no problem with willy paul marrying Alaine.My worry is,can our brother deliver ”D”effectively to alaine??Jst asking#ConcernedKenya

Its Gitz Bruh!‏@iGitz_ : Willy Paul Weds Alaine (Official Video)
FM

Chege‏@fmchege: If willy Poze can marry Alaine, then Jose Gatutura will marry Akothee
MANWARI‏@ReubenNyaribari: MorThe reason why you shouldn’t take this Willy Paul Alaine serious is that, the priest in this pic looks like a junior fuckboy. So I dont kno pic.twitter.com/JZgwIYo38N

Hii ndio ratiba ya michuano ya kombe la Europa


Ratiba ya michuano ya kombe la Uefa Ueropa League katika hatua ya robo fainali imetoka huku michezo ya awali ikitarajiwa kuchezwa Machi 9 na marudiano ikiwa ni Machi 16.

Mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa ni pamoja na Olympique Lyon ya Ufaransa iliyopangiwa kucheza na AS Roma ya Italia na mechi nyingine ikiwa ni Schalke 04 dhidi ya Borussia Monchengladbach (zote zinacheza ligi kuu ya Ujerumani).

Kutokana na kiwango kwa sasa kutoka kwa Manchester United inapewa asilimia kubwa ya kuingia katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo kutokana na kupangiwa timu ya Rostov kutoka Urusi ambayo inashika nafasi ya saba katika ligi ya kwao.

Wakati huo huo timu ya Mbwana Samatta KRC Genk imepangiwa kucheza na KAA Gent (zote kutoka Ubelgiji) ambayo iliitoa Tottenham Hospurs katika hatua ya timu 32 bora.

Wema Sepetu athibitisha kutolipwa na CCM fedha zake za kampeni 2015

Image result for wema sepetu kuhamia chadema
Malkia wa filamu nchini Wema sepetu amethibitisha kuwa japo amekihama Chama cha Mapinduzi lakini bado alikuwa anadai madeni yake yaliyotokana na kampeni za uchaguzi mkuu alizofanya mwaka 2015 akiwa na wasanii wengine.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama wa Chadema leo hii, Wema amesema walikuwa wanakidai chama hicho yeye na wasanii wenzake wengine lakini wamekuwa wakiambia madeni hayo wakamdai Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

“Kuna madeni kweli ambayo wasanii wenzangu wanadai nikiwemo mimi lakini cham kama chama kinajua chenyewe, nikianza kuongelea madeni nitakuwa kama nakumbuka shuka asubuhi,” amesema Wema.

“Madeni yapo kama hilo ndio swali na wasanii wenzangu wengi wanakidai Chama cha Mapinduzi lakini sasa tumekuwa tunaambiwa tumfuate tumfuate JK. Tumfuate JK tukamdai na maneno mengine mengi ambazo ni fununu tumekuwa tunasikia,” ameongeza.

Leicester City yamtimua kocha wake Claudio Ranieri


Kocha wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Leicester City, Claudio Ranieri ametimuliwa kwenye klabu hiyo.

Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville.

Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametoa kauli kuhusu kufukuzwa kwa kocha huyo huku akimpongeza kwa historia aliyoiweka katika ligi hiyo.

“CHAMPION OF ENGLAND and FIFA MANAGER of THE YEAR⚽️.sacked. Thats the new football claudio.keep smiling AMICO😀.nobody can delete the history you wrote.,” aliandika Jose kupitia Instagram.

Marry You ya Diamond yaingia kwenye Top 20 za Vevo Marekani

Diamond Platnumz anazidi kufikia malengo aliyojiwekea mwaka huu. Video ya wimbo wake, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, imeingia kwenye Top 20 za Vevo nchini Marekani. Chati hiyo inahusisha wasanii wapya wa Marekani.
Video hiyo sasa inapigana vikumbo na ngoma za rappers maarufu wakiwemo Desiigner na Lil Yatchy. “Kwahiyo @vevo ndio wameamua iwe hivyo? Top 20 New Artists Videos in the U.S na #MarryYou imo? Kwanini wanafanya upendeleo?,” ameandika meneja wake, Sallam.

Chuo kikuu cha Harvard champa Rihanna heshima hii


Rihanna ana mengi ya kusherehekea mwaka huu, ikiwa ni siku chache baada ya kutimiza miaka 29.

Muimbaji huyo ametajwa kama 2017 Harvard University Humanitarian of the Year, heshima ambayo inamweka kwenye ligi moja na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na muigizaji James Earl Jones.

Heshima hiyo imetokana na shughuli zake za kusaidia elimu katika nchi maskini kupitia taasisi yake ya Clara and Lionel Foundation.

Mkurugenzi wa taasisi ya Harvard, S. Allen Counter amemuelezea Rihanna:

Rihanna has charitably built a state-of-the-art center for oncology and nuclear medicine to diagnose and treat breast cancer at the Queen Elizabeth Hospital in Bridgetown, Barbados,” Counter said. “She has also created the Clara and Lionel Foundation Scholarship Program for students attending college in the U.S. from Caribbean countries, and supports the Global Partnership for Education and Global Citizen Project, a multiyear campaign that will provide children with access to education in over 60 developing countries.



Hivi karibuni Rihanna alitembelea nchi ya Malawi.

Alikiba alivyovutia mashabiki kwenye uzinduzi wa filamu ya Marekani, SA


Kama mtu ananidharau kusaini WCB, hajui biashara yangu – Rich Mavoko


Muimbaji wa Kokoro, Rich Mavoko amedai kuwa kama bado kuna watu wanaona uamuzi wake wa kusainishwa na label ya Diamond, WCB ni kujishusha sababu yeye ni msanii mkubwa, hawaijui biashara yake.

“Mimi nakutana vitu vingi, mtu mwingine nyuma ya pazia haoni,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.

“Tunashoot, tunatoa video, tunarelease ngoma inahit, mimi ndo nakuwa napata tabu.Mtu anayesema nimejishusha kimuziki kujiunga WCB anakuwa hajui biashara yangu,” aliongeza.

Rich alisainishwa na WCB mwaka jana na kuachia wimbo wake wa kwanza, Ibaki Story.

Kwa upande mwingine, Rich alidai kuwa asipofanya muziki atakuwa akiwaandikia watu wengine mashairi na kwamba Tanzania ina upungufu mkubwa wa waandishi wa Bongo Flava.

NEW AUDIO | Tunda Man - Simba | Download

NEW AUDIO | TID Ft. Tofy - Woman | Download

NEW AUDIO | TANZANITE x DEE PESA - USINIVUKE | Download

NEW AUDIO | Sam wa Ukweli - Nawaona | Download

NEW AUDIO | Pam D - DAFFA | Download

NEW AUDIO | Mesen Selekta - Mtoa Sadaka | Download

NEW AUDIO | Man Fongo - Nani Asiyependa | Download

wanapenda

NEW AUDIO | G Nako & Jux – Go Low | Download

NEW VIDEO | Country Boy Ft. Billnass - Hakuna Matata | Watch


NEW VIDEO | Pam D - Daffa | Watch


NEW VIDEO | Lumino Ft. Mohombi, Diamond Platnumz, Franko - Rockonolo (Remix) | Watch


NEW VIDEO | Eddy Kenzo - Jubilation | Watch


NEW VIDEO | Mimi Mars - Shuga | Watch


NEW VIDEO | G Nako & Jux - Go Low | Watch


NEW VIDEO | Man Kide - Ndoto | Watch



VIDEO | Lulu Diva - Usimwache | Watch


VIDEO | WYRE - LION | Watch


NEW VIDEO | Boneye Ft. Konkodi x Joh Makini x Owuor Arunga – APPETITE | Watch


NEW VIDEO | NEEMA MUDOSA x GOODLUCK GOZBERT - WASHANGAZE | Watch


VIDEO | MAKOMANDO - SAULA | Watch

VIDEO | Bonge La Nyau - Tusiachane | Watch

VIDEO | MB Doggy – UWE WANGU | Watch


18 Feb 2017

NEW AUDIO I YAMOTO BAND - KICHECHE I DOWNLOAD

Image result for yamoto band

NEW AUDIO | Timbulo Ft. Naytruboy- Niambie | Download

NEW AUDIO I T.I.D ft Fid Q - Maisha ya jela I DOWNLOAD

NEW AUDIO | Rose Muhando Ft. Oliva Wema - Lazima Wakae | Download

Image result for rose muhando

NEW AUDIO I Mr Nay - Muda Wetu I DOWNLOAD

Image result for MR NAY MUDA WETU

NEW AUDIO | MAKOMANDO - SAULA | Download

 DOWNLOAD

NEW AUDIO | Linex Sunday Mjeda - YAONGOZE (Bonus Track) | Download

Image result for linex mjeda

NEW AUDIO | Diamomd Platnumz Ft. Sporah - Kosa Langu | Download [Extended]

NEW AUDIO | Bonge La Nyau - Tusiachane | Download

NEW AUDIO | Alikiba Ft. M.I - AJE Remix | Download

Image result for Alikiba Ft. M.I - AJE Remix

VIDEO | QUEENDARLIN Ft. RAYVANNY - KIJUSO | Watch



VIDEO | Nandy - One Day | Watch