burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

11 Feb 2017

Profesa Jay awachana ‘wanaharakati’ wa hiphop wenye wivu kwa rappers waliotusua


Rapper mkongwe nchini Profesa Jay leo ametoa ya moyoni kuhusiana na rappers na wadau wanaokejeli harakati za wasanii wa hip hop za kubadilisha ladha ya muziki huo.
Kupitia Twitter Profesa ameandika:

Juzi tu dogo Nash Mcee aliuliza hivi SINGELI imeshakwenda international? nilitegemea angeuliza kwa nini HIPHOP Ya Bongo haivuki Boarder? Mkafurahia KISHABIKI bila kujiuliza HIPHOP ndio imezaa karibu aina zote za muziki wa kizazi kipya lakin mbona wasanii wake hawafiki mbali? Matokeo yake baadhi ya wasanii wanaojiita wa HIPHOP na mashabiki wao wanaichukia aina nyingine ya muziki kwa mafanikio wanayopata wenzao.

Badala ya kujiuliza tumekosea wapi sasa tunakuwa na WIVU wa kijinga na kuchukia mafanikio ya wengine waliopambana kufika hapo walipo sasa. Kupinga MTU aliyefanikiwa hakukupi uhalali wa wewe kufanikiwa, Tuna nafasi ya kujirekebisha na kupeleka HIPHOP Yetu mbali ila sio kwa WIVU.

MAPINDUZI yaliyofanywa na Kwanza unit, Saleh Jabri, Hbc, Sugu, Hashim, Majani, GWM, Solo, Afande, Jmo nk yalifanikiwa kwa UPENDO sio CHUKI. Hata wanaojitahidi kupeperusha bendera ya HipHop kama @FidQ @JohMakini watu wanawakatisha tamaa, I RESPECT YOUR HUSTLE my young brothers. Matokeo yake hao wanaopinga wenzao wanaoonyesha JUHUDI, wanaishia kuimbia washkaji zao kwenye vibanda vya kahawa,U NEED TO GROW Up.

Joseph Haule Kizazi hiki cha HIPHOP Kimekuwa kama Ukoo wa KAMBALE Baba, Mama na watoto wote wana NDEVU, Kila MTU akiambiwa mkali anajiona kweli KAMALIZA. Hii Heshima mliyoikuta kwenye HIPHOP tuliitafuta kwa Jasho na Damu kisha mnaichukulia poa tu, Badala ya kwenda mbele mnarudi nyuma kwa kasi. Wakati ule TANZANIA tulikuwa wa pili Africa tukishindana na SENEGAL ya kina DIDIER AWADI ila sasa hata Sudan wanatukimbiza, HAMJIULIZI tu? Tumebaki kujazana ujinga kwenye vijiwe vyetu na kujifanya REAL HIPHOP wkt hakuna chochote mnachokifanyia HIPHOP, Acheni WIVU fungueni AKILI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni