burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

11 Feb 2017

Sugu alaani uamuzi wa TCRA kuzizuia TV za mtandaoni

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi amelaani kitendo cha mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA kuzizuia online TV kuendelea kufanya kazi kama TV za kawaida hadi pale itakapotolewa muongozo na sheria za kuziendesha.

Katazo hilo itaziathiri baadhi ya TV za mtandaoni zenye umaarufu ikiwemo Ayo TV ya Millard Ayo. Akiongea bungeni leo mjini Dodoma, Mbilinyi amedai kuwa uamuzi huo unaliingiza taifa gizani.

“Tunakuwa North Korea kwa spidi ya ajabu sana,” amesema.

“Tunaonekana wa ajabu kwenye international community kwa maamuzi kama haya. Kwasababu wananchi wana haki ya kupata habari kutoka upande wa pili, mfano jana Askofu Gwajima na mfanyabiashara Manji walipata nafasi ya kujibu kwa haraka sana tuhuma dhidi yao zilizotangazwa kwenye TV pendwa za serikali lakini wao wasingeweza kupata nafasi ya live kusingekuwa na online TV wakaweza kujitetea kwa haraka sana,” ameeleza.

“Wananchi sasa wamekuwa wakitegemea online TV kupata habari za bunge kwahiyo ni wazi suala la kuzuia kwa namna yoyote online TV ni mwendelezo wa kuzuia wananchi kupata habari za bunge, ni mwendelezo wa kuliweka taifa gizani.”

Sugu amependekeza kazi za online TV ziendelee hadi pale sheria hizo zitakapotungwa kwasababu uwepo wake hakuvunji sheria yoyote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni