burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Apr 2018

NEW VIDEO | Harmonize Ft. Diamond Platnumz - Kwangwaru | Watch

NEW VIDEO | Lulu Diva – Homa | Watch

Nandy ashushiwa maneno mazito na mpenzi wa Bill Nass, ‘Unajua kuvaa nje, ndani hujui’


Bado ni drama tele kati ya Nandy na Bill Nass, safari hii mpenzi wa Bill Nass amemshukia vikali Nandy kwa kile kilichotokea.

Alice ambaye ndiye anadaiwa kuwa katika mahusiano na Bill Nass kwa sasa ameonyesha kutopendezwa kabisa na kile kilichotokea kwa mpenzi wake pamoja na Nandy. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Ujue wakati mwingine jitahidi kujiheshimu Nandy, Ulimpigia William simu ukimuomba akutumia picha zenu za wakati mnadating…. bila hiyana mume wangu alikutumia, lakini wewe uliposti zile picha hukuridhika ukaamua uachie video chafu kama ile halafu hapo hapo unakataa na kumlaumu mume wangu wakati iliyotumika ni simu yako.

Upande wako kama unaona umewin basi jua umetuharibia mimi na mume wangu sana na hata kwa watoto wetu huko mbeleni sijui watamjengea picha gani baba yao.

Cant you doing your fu*** music bila kiki?, au uliona mume wangu William ndo wa kutafutia kiki, naomba ukome tena haswa, kama ulikuwa naye ndio ishapita hivyo tuache na mahusiano yetu, sijui ni mwanamke wa dizaini gani wewe usiyekuwa na haya, unayejua kuvaa nje, ndani hujui, ile chu** ni ya kuvaa msichana kama wewe.

Hapo juzi, April 12, 2018 ilivuja video mtandaoni ya utupu ambayo iliwaonyesha Bill Nass na Nandy wakiwa faragha. Nandy ameshaomba radhi kwa mashabiki wake kutokana na tukio hilo na kueleza hajui nani hasa amevujisha video hiyo ila amekiri kuwa yeye ndiye aliirekodi.

NEW ALBUM COOMING SOON KUTOKA KWA RITHA KOMBA



Mwimbaji wa nyimbo za injili anaekuja kwa kasi hivi karibuni {siku za usoni} ataachia album yake itakayo kwenda kwa jina la RAFIKI 
yenye nyimbo zipatazo tisa  ambapo atazindua album yake na utapiata kwa mfumo wa audio na hivi sasa anamalizia nyimbo zake ambazo utazipata kwa mfumo wa video  

Akipiga  stori na g.lovetz RITHA KOMBA amesema Natarajia kuachia album yenye nyimbo 9 
mpaka sasa kuna video zipatazo 5 ambazo tayari zimeshakamilika ila album yangu kwa sasa itakuja kwa mfumo wa audio then video itakuja kivingine  


Pia RITHA KOMBA hakuishia hapo ameahidi kuachia  VIDEO&AUDIO kwa mpigo na hayuko pekee yake amemshilikisha RACHEL  MWAMTOBE 
Nyimbo itakwenda kwa jina la NGUVU YANGU
Pia namalizia kwa kuwashukulu wote wanao ni sapoti wanaonitia nguvu
watu wa media asanteni sana sana na MUNGU AWABARIKI NYOTE



Nipo katika wakati mgumu, naapa sihusiki na kusambaza video – Nandy


Baada ya hapo jana Nandy kuwaomba radhi mashabiki wake kutokana na kusambaa kwa video iliyomuonyesha akiwa faragha na aliyekuwa mpenzi wake. Leo, April 13, 2018, Nandy amesema hausiki na kusambaa kwa video hiyo.

Nandy amesema video imesambaa kutokana na kubadili simu mara kwa mara yeye pamoja na Bill Nass na ni kitu ambacho kinaweza kumkuta yeyote. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Kiukweli niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo nimeweza hata shika simu yangu najuaa matusi yote na fedhea kutoka kwa mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!! sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida!

Sitakiwi kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye ataamuaa kuendelea kuni hukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea! Mambo yetu wote ya private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani mwangu. ilaa Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!! nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake.

So hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi. Kanisaa langu, wazazi wangu, ndugu zangu, marafiki zangu wa karibu wameliaa sana sanaa mnoo!!! sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano na nilifanya kwa mapenz ila siwez weka public, Mungu anisamehe kwa niliyowakwaza. nimepoteza watu wa maana nahisi ku poteza vitu vingi ilaa nashukuru sana kwa watu wangu wa karibu waliolia na mimi mashabiki wanaoniamini Mimi na dhamira yangu ya kweli.

Marafiki walio liaa kwa ajili yangu nawashukuru sana mnoo yote naomba radhi sana sanakwa kilicho tokea haikuwa kusudio langu na naumiaa sana!!! asante sana basata kwa ushirikiano wenu kwakuwa na mm na kunipa moyo hii ni fundisho kwa wote nimejifunza kitu kikubwa sana!! mashabiki, kabisa langu, serikali yangu viongozi wenye imani na mimi, mashabiki zangu, ndugu jamaa na marafiki. naomba Nisameheni naamini na hili nalo litapita. Sitaongea tena kwenye vyombo vya habari kuhusu hili namwachia Mungu, pale roho yangu itakapopata wepesi tutaonana tena kwenye Sanaa. Naomba mniombee nipate wepesi wa kuvuka hili daraja.

Kwa upande wa Bill Nass hapo jana alieleza kilichotokea kwa upande wake kuhusiana na tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ila baada ya muda mfupi alifuta ujumbe huo ambao kwa asilimia kubwa ulitupa lawama kwa Nandy.

Nandy umetudanganya, umezidi kumpa ushindi Zari

Kwanza nitoe pole kwa Nandy na Bill Nass mara baada ya video yao ya faragha kuvuja mtandaoni, ni kitu ambacho unaweza kukichukulia kawaida ila usiombe yakukute.
Viatu walivyovaa Nandy na Bill Nass kwa sasa vinawapwaya katika miguu yao na pengine ni vizito, nitoe pole kwao kwa hilo lilowafika kwani ni tukio ambalo si vigumu kuja kufutika katika maisha yao kutokana na utandawazi uliopo sasa.

Fid Q katika ngoma yake August 13 alisema, ustaa ni mzigo wa mwiba, ukiubeba utaumia. Video ya Nandy na Bill Nass imesambaa kwa kasi kutokana na umaarufu wao, hivyo maumivu wanayopitia wanapaswa kuelewa ni kawaida katika tasnia yao ya burudani.

Nandy ameelewa hilo na ndio sababu hakuona aibu kuomba radhi kwa mashabiki wake kwa hicho kilichotokea. Kwa anayeelewa maana ya neno samahani atakuwa amemsamehe na maisha mengine kuendelea.

Kwanini Nandy

Baada ya video kusambaa, Nandy na Bill Nass kila mmoja amejitetea kwa upande wake. Nimzungumzie Nandy kwa ufupi; ameomba radhi na kueleza kilichotokea ila kuna jambo halipo sawa kwa upande wake.

Kwa mujibu wa post aliyoweka Bill Nass katika ukurasa wake wa Instagram jana na kuifuta baada ya muda mfupi alitupa lawama zake nyingi kwa Nandy kuhusu kuvuja kwa video hiyo. Ameeleza siku moja kabla, Nandy alimtafuta kumuomba picha za zamani kipindi wakiwa wapenzi ili azitumie katika kum-wish Happy Birth Day yake, hata hivyo alimueleza kuwa hana picha hizo.

Lakini baadaye alikuja kuona picha hizo mtandaoni kitu ambacho hakupendezwa nacho kutokana kwa sasa ana mahusiano mapya, hivyo Nandy alishindwa kuheshimu uamuzi wa mwenzake.

Katika Interview aliyofanya Nandy na MCL Digital alieleza kuwa walikuwa na mahusiano mwaka 2016, mahusiano yao walipanga kuwa private lakini ukifuatilia kwa makini kuna kitu ambacho hakipo sawa hapa.

Katika video iliyosambaa mtandaoni unasikika wimbo wa Bill Nass unaokwenda kwa jina la Sina Jambo. Wimbo huu ulitoka Augost 17, 2017, yaani miezi saba iliyopita.

Hivyo kueleza kuwa walikuwa na mahusiano mwaka 2016 na ndio video hiyo ilirekodiwa, bado haiingii hakilini kwa urahisi huo.

Kuhusu Zari

Sikupenda kumhusisha mrembo huyo katika suala hili ila kutokana na ujumbe ambao ningependa kuutoa nalazimika kufanya hivyo. Nitangulize samahani kwa yeyote nitakayemkwanza.

March 28, 2018 mwaka huu Zari alipata dila la kuwa balozi wa kutangaza nepi za watoto za Soft Care. Baada ya hapo kulizuka mjadala kuwa ni kwanini mastaa wa kike Bongo hawajapewa dili hilo au kupata dili kama hizo.

Muigizaji Faiza Ally alihoji; ” how stupid Tanzanian can be, mastaa wote watanzania, watu wote Watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya Zari ? Ina maana uhitaji Bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje?.

Baada ya kauli hiyo Shamsa Ford alimjibu Faiza kwa kumueleza kuwa hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua staa wa Bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara.

Aliongeza kuwa baadhi ya mastaa wengi wa Bongo wanajulikana kwa mambo ambayo si mazuri kitu ambacho si kizuri kwa brand za kibiashara.

“Maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika.kikubwa tujifunze, swala sio kujulikana ila swala ni kuwa unajulikana vipi!? Watu wanakutambua kwa lipi. Ni vizuri tumeumia sasa tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika,” alisema Shamsa.

Kwa mujibu wa posti ya Bill Nass, alieleza baada ya kumuuliza Nandy ni kwanini ametoa picha hizo za kitambo wakiwa katika mahusiano kwani ni kitu walipanga kuwa siri, Nandy alimjibiwa kuwa amepanga kiki yeye na team yake. Weka nukta hapo.

Twende pole pole; Kwa kile kilichotokea jana kwa Nandy naanza kuelewa kile alichoeleeza Shamsa Ford. Sielezi kwa kumhukumu Nandy, hapana!, ila ni ukweli ambao upo na utendelea kuishi. Hivyo maneno ya Shamsa yanasaidifu kile kilichotokea kwa asilimia kubwa na tukio lenyewe linatoa sababu ya kwanini Zari alistahili kupata dili lile. Asante.

Video ya utupu ya Nandy na Bill Nass yawawekea uzibe Harmonize na Diamond Platnumz


Kwa wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania, hususani kwa wale ambao wanamfuatilia Diamond Platnumz utagundua kuwa jana Aprili 12, 2018 aliahidi kuachia video ya wimbo wa ‘Kwa ngwaru’ ambayo amemshirikishwa na Harmonize lakini mpaka sasa hivi hakuna chochote kile walichofanya.

Diamond kupitia kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii jana aliahidi kuachia video ya Kwa ngwaru kwa kuahidi kuwa endapo angepata maoni (Comments) 10,000 kwenye posti yake aliyochapisha kwenye mtandao wa instagram, basi wangeachia video ya wimbo huo ambao umetokea kupendwa sana na mashabiki wa wakali hao lakini posti hiyo hadi sasa imefikisha comments elfu 13 na video hiyo bado haija achiwa.

Hii haina ubishi kuwa video ya utupu ya Nandy na Bill Nass imepoteza attention kwa mashabiki wengi wa muziki nchini Tanzania kutokana na ukubwa wa wasanii hao ambao kila Mtanzania alikuwa anaamini kuwa ndio zao jipya la wasanii wa kizazi kipya.

Hata hivyo, mpaka sasa hivi si Diamond wala Harmonize aliyetoa kauli yoyote ile kuhusiana na kuachia video hiyo ingawaje mashabiki wengi walitazamia kuona video hiyo kwa siku ya jana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Nandy na Bill Nass kuhusu video yao ya utupu iliyovuja siku ya jana hadi sasa bado haijajulikana ni nani aliyevujisha kwani wamekuwa wakitupiana lawama kila mmoja.