burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

14 Nov 2017

Ndikumana afariki dunia ghafla baada ya mazoezi


Mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda na beki wa zamani wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla.

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza kuwa Hamad Kataut kabla ya kufikwa na umauti alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Katauti alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, enzi za uhai wake na aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus.

Ndikumana alikuja nchini siku ya Simba Day Agosti 8 mwaka huu akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kufungwa bao 1-0.

Mchezaji Ndikumana Hamad amewahi kuwa mume wa muigizaji filam maarufu nchini, Irene Uwoya.

10 Nov 2017

Bright awashangaa wanaomfananisha na Belle 9


Msanii wa Muziki Bongo Bright amesema kuna utofauti mkubwa kati yake na Belle 9.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ni Wewe’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wapo wanaowafanisha lakini kiuhalisia hawafanani na walishafanya hata ngoma pamoja ili mashabiki kuona utofauti wao.

“Hapana, mimi nimeingia studio kwa mara kwanza mwaka 2006 sidhani kama Belle 9 alikuwa amefahamika lakini kutokana amefahamika na mimi nimekuja kufahamika baadaye yeye ameshapata nafasi lazima mtu awe anaongea hivyo” amesema Bright.

Ameongeza kuwa kutokana na watu kuwafananisha ndio sababu ya kufanya kazi kwenye menejiment moja kipindi cha nyuma ambapo hata uongozi wao ulikuwa unawafanisha lakini kila mmoja ana kitu chake.

Kesi ya Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond Platnumz yafutwa na Mahakama


Dar es salaam, Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.

Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.

Mobeto anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

New Video: Jennifer Lopez ft. Wisin – Amor, Amor, Amor

Related image

NEW VIDEO | Queen Darleen - Ntakufilisi | Watch


1 Nov 2017

Barakah The Prince alia kufanyiwa hujuma akose views YouTube


Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Barakah The Prince amedai kuwa YouTube account yake inafanyiwa mchezo mchafu ili ishusha idadi ya views.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sometimes’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa views za ngoma yake hiyo zimekuwa zikishuka na kupanda na hata muda mwingine comment kufutwa.

“Kwa upande wa YouTube kuna mchezo mchafu unafanyika kwa sasa hivi, kwa mfano wimbo wangu kama jana ulikuwa ni namba saba kwenye trending ukiangalia video za watu wengine ni namba 40 lakini views wake ni milioni 4.4, nyingine inasoma namba 10 ukiangalia views zake ni laki 5.8 lakini mimi ambayo nina views elfu 20 ninasoma namba saba kwa nini iwe hivyo?” alihoji.

“Kuna mchezo mchafu unafanyika wa ku-block views wangu hata Mx kaniambia kuna mchezo mchafu unafanyika” ameongeza.

Amesema kuwa kuna baadhi ya nchini ikiwemo China mashabiki wake wamekuwa wakilalamika haiwapati video yake lakini video za wa wasanii wengine zinapatikana.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa watu wenye access ya kuendesha account yake hiyo ni Mx Carter na Seven Mosha wa RockStar4000 kutokana na makubaliano ya hapo awali, pia ameeleza kuwa yupo katika utaratibu wa kufuta account hiyo na kufungua nyingine.

Ngoma ya Barakah ‘Sometimes’ video yake ilitoka October 28 mwaka huu lakini hivi sasa haipatikani YouTube (imeondolewa).

Anachojivunia Feza Kessy kwa sasa


Msanii wa muziki Bongo na Mtangazaji wa Choice Fm, Feza Kessy amefunguka anachojivunia kwa sasa ni mafanikio yaliyofikiwa na ngoma yake ‘Kaa Kijanja’ ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili.

Muimbaji huyo amesema ngoma hiyo imeweza kumpeleka katika hatua nyingine kabisa ukilinganisha na hapo awali.

“Nafikiri imeniweka katika position nzuri kama female artist wa Tanzania, so I thanks my supporter, am very happy, am very great full kwa sababu imenitoa from one level to another, sasa hivi nipo kwenye  level nzuri naweza kusema kwa sababu ya Kakaa Kijanja” amesema Feza.

Feza kwa sasa ametajwa kuwania tuzo za Afrima katika kipengele cha Best Female Artiste in Eastern Africa, tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 10 hadi 12 mwaka huu Lagos nchini Nigeria.

Nyomi la mashabiki la kwamisha mazoezi Al Ahly


Timu ya Al Ahly ya Misri hapo jana imeshindwa kufanya mazoezi katika makao makuu ya klabu hiyo huko Cairo baada ya mashabiki kujaa Uwanjani.

Mamia ya mashabiki waliingia Uwanjani kuitazama timu hiyo hali iliyosababisha wachezaji kushindwa kufanya mazoezi na hivyo kughairishwa.

Wamisri wanatazamia kuweka rekodi ya kutwaa kombe la Afrika mara ya tisa endapo wataifunga timu ya Wydad Casablanca siku ya Jumamosi huko Morocco.

Katika mchezo wa awali uliyofanyika Alexandria timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Ahly itahitaji kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wao wa nyumbani kabla ya kusafiri siku ya Jumatano kuifuata Wydad Casablanca huko Morocco.

Ahly wamekutana na klabu hiyo ya Afrika Kaskazini 2006 kwenye mechi ya CAF Super Cup.


Timu hizo zimekutana mara nne kwenye michuano hii awali. Wydad wakiing’ang’ania Ahly kwa sare ya 3-3 mnamo 2011 mjini Cairo na 1-1 mjini Casablanca na 2016 sare ya bila kufungana mjini Alexandria na hatimaye Ahly kushinda 1-0 Morocco, kabla kukutana tena na nakutoka sare ya 1-1 Alexandria mwaka huu.

Msimu huu timu zote zilikuwa kwenye kundi moja, kila moja ikishinda 2-0.

Al Ahly ambao wanatafuta ubingwa wa tisa, waliifunga Etoile du Sahel 7-2 nyumbani na ugenini kutinga fainali.



Licha ya kupata kipigo  cha 2-1 Sousse, Mashetani Wekundu walibadilika katika ardhi ya nyumbani kwao Misri na kushinda 6-2. Walid Azaro akifunga hat-trick kwa timu hiyo ikiwa nyumbani.

Kwa upande wa Wydad, walishinda 3-1 mjini Casablanca baada ya sare waliyopata mjini Algers dhidi ya USM Alger, katika harakati zao za kutwaa ubingwa wa pili Ligi ya Mabingwa tangu waliposhinda 1992.

Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani milioni 2.5 na atapata tiketi kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa duniani mwezi Disemba falme za kiarabu.

NEW AUDIO | Mr Nice - Yaya | Download

NEW Audio | Rocky – Nimwambie | MP3 Download

Baada ya Jux, Vanessa Mdee atua kwa Cassper Nyovest


Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee amezidi kuonyesha uwezo wake kwa upande wa ‘video queen’ mara baada ya kuonekana katika video ya rapper Cassper Nyovest kutoka nchini Afrika Kusini.

Hii si mara kwanza kwa Vanessa kufanya hivyo, utakumbuka January 2015 alitokea kwenye video ya Jux katika ngoma ‘Sisikii’, baada ya hapo waliweza kutoka ngoma ya pamoja inayokwenda kwa jina la Juu.

Hata hivyo kuna uwezekana mkubwa Cassper Nyovest akapita katika nyayo za Jux kwa kuja kuachia ngoma na Vanessa. Akizungumza na Dj Show ya Radio One Vanessa amesema kuna muendelezo wa kazi kati yake na rapper huyo.

“Ni project endelevu tumeanza kwanza na video yake ya ‘Baby Girl’ ambayo nimecheza, so next msubirie kidogo itakuja very soon” amesema Vanessa.

Sunderland yamtimua kazi kocha wake Simon Grayson



Meneja wa klabu ya Sunderland muingereza, Simon Grayson ameachishwa kazi baada ya kuihudumia timu hiyo katika michezo 18 pekee toka kuteuliwa kwake.

Grayson ametangazwa kuachishwa kazi dakika 17 tu kupita baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bolton Wanderersdraw.

Simon Grayson raia wa Uingereza alichukua mikoba ya David Moyes mwezi Juni wakati akitua Sunderland.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema “Sunderland AFC jioni ya leo kwa kushirikiana na meneja Simon Grayson, imeamua kuachana nae na kumpatia shukrani yeye na benchi lake la ufundi kwa jitihada zao kubwa walizofanya katika klabu hii.” Imesema taarifa kutoka Sunderland.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu toka akabidhiwe nafasi hiyo.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Glynn Snodin alishaondoka bila klabu hiyo kutoa maelezo ya nani atarithi nafasi yake wakati ikikabiliwa na mchezo wa derby siku ya Jumapili dhidi ya Middlesbrough.

Baada ya mapenzi kung’oa warembo MJ Records, Idris na Wema watajwa


Wakati mjadala ukiendelea baada ya wasanii wawili wa kike, Haitham Kim na Nini kutimuliwa katika label ya MJ Records na producer Daxo Chali, suala hilo limechukua sura mpya mara baada ya Idris Sultan na Wema Sepetu kutajwa.

Taarifa za awali zilieleza kuwa kutimuliwa kwa wasanii wao ni kutokana na mmoja wapo kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii Nay wa Mitego kitu ambacho kilidaiwa kinaweza kuchafua brand ya label hiyo.

Hata hivyo Haitham Kim amefunguka mambo mengine kwa kile kilichokuwa kikidaiwa anatoka kimapenzi na Idris kitu kilichopelekea pia kutimuliwa MJ Records. Akizungumza na E-Newz ya EATV Haitham amesema jambo hilo halina ukweli wowote bali ni watu tu wanazusha.

 “Ni watu tu wametengeneza kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya Haitham na Idris kwa sababu ukiangalia Wema pia ni mtu ambaye hakusapoti hiyo kazi ya Play Boy, so watu wanaendelea kujiuliza kwanini Wema hakusapoti, hivyo sababu inaweza kuwa ni hiyo lakini yule siyo sababu” amesema.

“Mimi nina mpenzi wangu na Idris ana maisha yake, so siwezi kumuingiza Idris kwenye maisha yangu ya mahusiano kwa sababu I have a boy friend, nishamposti hata kwenye social media fans wangu wanamjua” Haitham ameongeza.

Chini ya MJ Records Haitham ameweza kutoa ngoma mbili official, ya kwanza ikiwa ni ‘Fulani’ aliyomshirikisha Mwana FA na Play Boy ambayo sauti ya Wema Sepetu inasikika ndani yake.