burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Jul 2018

Hii ndio show kali zaidi ya Diamond Platnumz kuwahi kutokea, awaimbisha kiswahili Wafaransa kisiwani Mayotte


Kwa sasa ukitaja majina ya wasanii 10 bora wanaofanya vizuri barani Afrika huwezi kuacha kumtaja Diamond Platnumz hii ni kutokana na kuongezeka kwa wigo mpana wa mashabiki wake.

Hili la kuongezeka kwa idadai ya mashabiki linajidhihirisha hata pale Diamond anapokuwa nje ya Tanzania hususani katika mataifa ambayo hayaongei Kiswahili.
Jana Julai 28, 2018 Diamond Platnumz alikuwa katika visiwa vya Mayotte nchini Ufaransa ambapo aliweza kutumbuiza nyimbo zake zote tena zile ambazo hajafanya kolabo na jambo la kufurahisha licha ya asilimia 99% ya wananc

7 Jun 2018

Muziki wa Diamond unakosha roho hata kwa sisi wazee – Mrema


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustino Mrema amesema msanii wa Bongo Flava anayemfuatilia kwa sana ni Diamond Platnumz.

Ameeleza sababu ya kumfuatilia muimbaji huyo ni kutokana na kujituma kwake na muziki wake unavutia.

“Namfuatilia sana Diamond, ni kijana mdogo, muimbaji mahiri, yaani Diamond asaidiwe naona hatima yake katika maisha yake na nchi yetu atatufikisha mahali pazuri. Kwa muziki wake unakosha roho, hata sisi wazee, mimi naridhika sana,” Mrema ameiambia Times FM.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa serikali kuwa karibu zaidi na wasanii, hata hivyo amesema anaziona jitihada za Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe za kukutana na wasanii kila mara hasa pale wanapopata matatizo na kuwasaidia.

Madee huwa simuelewi, anatoa biti sio wimbo tena – Belle 9


Msanii Belle 9 amesema moja ya wasanii asiyowaelewa katika Bongo Flava ni Madee.

Muimbaji huyo akipiga stori na JJ wa Jembe FM amesema kuwa kutokana anasikiliza wachanaji wengi wanaofanya vizuri anahisi kuna kitu anakikosa kutoka kwa Madee.

“Honesty, let me be honesty, Madee huwa simuelewi. I don’t know, ujue kuna wasanii inafika kipindi unasikiliza unasema huyo mtu ana-release beat sio wimbo tena,” amesema.

“Labda kwa vile nasikiliza rappers ambao wanajua sana au kuna kitu nakitegemea kutoka kwake kutokana muda mrefu yupo kwenye game, kuna kitu nakimisi, so naona kama nikimsiliza na lose,” amesisiza.

Belle 9 ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Dada, ameongeza kuwa mara nyingi ni vigumu mtu anayetoa kauli kama yake kueleweka ila yeye amesema kile ambacho anaona kipo sawa na kuwataka mashabiki wa Madee kuchukulia kawaida.