August 17 2016 Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imewahoji wasanii wanne wa kundi la sanaa ya uigizaji Orijino komedi akiwemo kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.
tumefanikiwa kumpata Kaimu kamishna wa jeshi la polisi Dar es salaam Hezron Gyimbi ambaye ametusogezea taarifa za awali kwa kusema…>>>’Wamekamatwa jana saa 10 jioni ambapo wamehojiwa na wamekaguliwa sehemu wanazokaa kuona kama wana vitu zaidi ya uniform‘
‘Tunakamilisha hatua za kiupelelezi, makosa yanadhaminika wakipata watu wanaweza wakawadhamini sababu dhamana ni haki ya mtu‘-Hezron Gyimbi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni