Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines siku ya February 1 2016 ni hii ya msanii wa Bongofleva na CEO wa record label ya Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platnumz kuweka wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika atanunua gari aina ya Rolls Royce.
Kupitia account yake ya instagram usiku wa August 30 Diamond Platnumz alipost clip video yaRolls Royce yenye kivuli cha sura yake, inawezekana Diamond akawa ametimiza ahadi yake ya kumiliki gari hilo kabla ya mwaka 2016 kumalizika, kama Diamond atakuwa kanunua gari hilo atakuwa ni mtanzania wa pili anayefahamika kumiliki Rolls Royce baada ya makamu mwenyekiti wa zamani wa Yanga Davies Mosha.
Baadhi ya mastaa Afrika wanaomiliki gari aina ya Rolls Royce ni Koffi Olomide na staa wa soka wa zamani wa Arsenal Emmanuel Adebayor ambaye kwa sasa anaichezea Crystal Palace, bado haijajulikana Rolls Royce aliyopost Diamond ni toleo la mwaka gani ila stori kutoka autoguide.com inaeleza kuwa Rolls Royce inauzwa zaidi ya dola laki 3 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600 pia inategemeana na toleo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni