burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

10 Jun 2017

Madereva watakaovunja sheria kuchapwa viboko


Baraza la Taifa la usalama barabarani limeazimia kuanza mpango mkakati wa awamu ya pili ambao katika utekelezaji wake pamoja na mambo mengine, utahusisha kuwachapa viboko madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.

Hayo yameelezwa jana mjini Dodoma na Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuf Massauni wakati akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa kupunguza ajali barabani nchini kwa aslimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti 2016 hadi Januari 2017.

Massauni amesema kuwa baada ya kuona utelekezaji wa awamu ya kwanza umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali, baraza hilo limeamua kuanzisha awamu ya pili ambapo moja ya mikakati yake itawachukulia hatua kali wale wote watakaokiuka sheria hizo ikiwemo kuchapwa viboko.

Akizungumzia operesheni,usimamizi wa sheria na hatua zilizofikiwa katika kipindi hicho cha miezi sita katika awamu ya kwanza, amesema jumla ya madereva 1,596 walikamatwa, kuwekwa mahabusu na kupelekwa mahakani badala ya kulipa faini ya papo kwa papo kama walivyokuwa wamezoea.

Hata amesema magari 188,602 yalikamatwa kwenye Operationi hiyo kutokana na ubovu ambapo kati ya hayo magari 623 yalifungiwa kutembea kutokana na uchakavu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni